Mkoa wa Chato na siasa za Kanda ya Ziwa nyuma ya pazia

Chato haina sifa ya kuwa mkoa!!!
 
Umefafanua vizuri. Tumejua kuanzishwa mkoa wa Chato ni ndoto ya zamani ya mwendazake iliyosukumwa na ukabila.
 
Uko sahihi!
 
Walau, huenda kauli hizi zikatunusuru.


"Iwapo kuunda mkoa no kusogeza huduma jirani na wananchi, ni busara mkoa huu kuundwa kwa kuweka makao makuu Biharamulo au Nyakanazi.
Sioni maana/mantiki ya wakazi wa wilaya za Ngara na Kakonko kuvuka wilaya ya Biharamulo wakienda Chato.
Makao Makuu ya mkoa hui mpya yatakuwa pembeni mwa mkoa huu mpya.

Mkoa huu badala ya kuwanufaisha wakazi wake wengi, utawaumiza.

Pia sioni manufaa atakayoyapata mkazi wa Buseresere na Katoro kwa kuwa ataongeza umbali wa kwenda makao makuu ya mkoa.

Nashauri serikali badala ya kuwaza kuongeza mikoa na wilaya, ijikite kupunguza ukubwa wa vijiji na kata.
Hili liende sambamba na kuwarahisishia utendaji wa kazi zao viongozi wa vijiji na kata kwa kuwapa usafiri, vifaa vya kazi kama kompyuta mpakato, simu zinazoweza kupata matukio[picha] vema nk.

Hapa Ngara kwenye kata ya Muganza, umbali kutoka Kitongoji cha Nyakafandi hadi makao makuu ya Kijiji chao cha Mukubu ni km.15.
Kutoka kitongoji hicho hadi makao makuu ya kata ni zaidi ya km.30.

Mtendaji wa kata na wa kijiji hawana usafiri wowote.
Wanatumia usafiri wa kudandia au kukodi.
Huko hakuna umeme wa TANESCO.
Wangeweza kusaidiwa kupewa umeme wa jua kwenye ofisi zao ili wachaji simu zao ambazo kwa sehemu kubwa zinafanya kazi za ofisi.

Wananchi hatuna hitaji la mikoa na wilaya.
Tunahitaji zaidi huduma bora za vitongoji vijiji na kata.

Ikumbukwe miaka michache iliyopita ukubwa wa vitongoji uliongezwa badala ya kupunguzwa.
Kuna sehemu mitaa/vitongoji vitatu viliungwa kuwa kimoja.
Mzigo uliongezeka."

Wasomi nendeni mtafiti/mjiulize au muwaulize wananchi wa kawaida wanakwenda mkoani na hata wilayani kwa ajili ya nini?
Wengi wao, maisha yao yote hawatakuwa na shida yoyote mkoani.

Ikumbukwe kuwa kuanzisha mkoa Kuna gharama nyingi na kubwa mno.
Gharama za kuanzisha mkoa au wilaya zikielekezwa vijijini au katani zitaleta tija.

Kazi iendelee.
 
mhn! ni mguno sina ninachonusa!
ninachokiangalia kwangu ni rasilimali zilizowekezwa Chato jinsi gani zinaweza kuisaidia taifa na watu wake; vinginevyo tukubali kuwa tumepoteza kila kitu.
busara na maamuzi yenye tija yatumike ili yale yaliyojengwa yanufaishe nchi yote.
kazi kwenu watawala! ndo mjifunze na muache ubinafsi
 
Ni kwamba Chato haina sifa ya kuwa mkoa huo ndio ukweli acha kuzunguka muanzisha mada.Ni ukweli ulio wazi mwenda zake alikuwa mbinafsi kupitiliza ukitaka kujua zaidi ya hilo kwanini ajenge uwanja wa ndege Chato asijenge mkoani Geita ambapo ni makao makuu ya mkoa?.Kibaya zaidi alitoa maamuzi bila kupitia bungeni.

Mwenda zake alikuwa na chuki za wazi kwa baadhi ya mikoa hasa mkoa wa Kilimanjaro alikuwa na dhana kwamba ni wezi.Ni waambie ndugu zangu baadhi ya maendeleo ya Tanzania,Kenya,Uganda na sehemu zingine zilisababishwa na athari ya mkoloni.Mkoloni alivyokuja Kilimanjaro,Wakikuyu na Wabaganda kwa Uganda aliona hali ya hewa ya kule ilifanana na kwao ulaya na akapiga hesabu kupanda mazao ya cash crops kwa vyovyote vile sehemu hizo alianza kujenga makanisa na shule kwa vyovyote hawa watu lazima waonekane wako mbele kuliko sehemu zingine.

Hakuna kabila ambalo tunaweza sema wana akili kuliko wengine wote wako sawa na mtu akitangulia ametangulia tu.Nenda mkoani Mbeya na Bukoba mashule yalijengwa siku nyingi.

Pamoja na yote kila utawala una zama zake na kitabu chake huwezi kuwa raisi au kiongozi wa ngazi yeyote hata ya kata usiwe na mazuri yako na mapungufu yako hayo ni mapungufu yake kama binadamu wengine.Nyerere alikuja alileta mazuri yake na mapungufu yake.Hali kadhalika kwa Mwinyi,Mkapa na Kikwete nao ni binadamu wana nyama na damu.

Ila ni ukweli ulio wazi toka tupate uhuru hatujawahi pata kiongozi aina ya mwenda zake kipindi kifupi alileta mabadiliko makubwa mno na aliwazidi watangulizi wake tujiulize je mungu asingeamua kumchukua watanzania tungefikia wapi?Raisi wa zamani wa Bukina Faso marehemu capt Thomas Sankara alipata kusema wakati mwingine ukitaka kuleta mabadiliko lazima uwe na level flani ya wehu alimaanisha kuna mahali inabidi ukengeuke utumie nguvu.

Mhe wetu Mwenda zake aligundua tumechezewa mno mno na nidhamu ya kazi ilikuwa haipo na ubadhirifu wa mali ya uma ulikidhiri ndio maana akawa anatumia misimamo mikali kwa hapa kwa kweli hatutamtendea haki kumpa pongezi zake kipindi chake kulikuwa hakuna tofauti ya mnyonge na mtu aliye nacho aliyenacho akikosea anafungwa sawa na asiye nacho katika kipindi chake ndio haki zilizokuwa zinafinywa kwa wanyonge alizifungua.


Mungu ambarikia amlaze pema mhe wetu.Sio vyema kuhesabu mabaya yake ila tuyaenzi mazuri yake na pale alipokosea turekebishe.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Mzizi wa hii yote ni "Ubinafsi tu"
Uko sahihi kabisa. Kwanza nimebaini kwamba hao wahamiaji kutoka usukumani, wamevamia mkoa wa wenzao na kulazimisha uwe wa kwao na kutaka kufuta historia ya wenyeji na kuleta za kwao. Pili hapa Tanzania kuna mambo mengi ya ajabu sana, imagine mwendazake, ambaye amevamia mkoa wa watu akashawishi mpaka jimbo likagawanywa ili eti yeye ashinde uchaguzi. Yaani badala ya jimbo kugawanywa for public interest likagawanywa ili fulani ashinde uchaguzi!!!
 
Yaani umeanza vizuri lakini kwenye hitimisho umejichanganya... Jifunze kwamba unapojenga hoja yako hakikisha conclusion ina support your original arguments... Huwezi kuwa na paragraph tatu za mwanzo unaelezea mapungufu ya mwendazake ikiwemo ubinafsi, ukabila na upendeleo halafu umalizie tofauti...
 
Shida siyo ukubwa wa maeneo ya kiutawala bali tuna tatizo la utawala bora, Nchi ambayo tuna watendaji mpaka ngazi ya Kijiji,hatuhitaji kuongeza mikoa Zaidi tunahitaji utawala bora tu.
 
Huo mkoa uundwe lakini makao makuu ya mkoa yasiwe Chato yawe Runzewe
 
sawa bro ila kumbuka upande mmoja wa shillingi unakuwa na upande mwingine pia huwezi ukawa mzuri kwa yote sasa mimi nimeeleza mabaya yake na mazuri pia usije dhani hayapo yapo pia ukifanya hivyo unanilamisha kukandia kitu au unanilazimisha kuwa na mawazo yanayofanana.
Hata wewe uliyenkosoa una mazuri yako lakini pia una mapungufu yako kama binadamu mtu akikuambia usimlazimishe ataje mabaya yako tu na mazuri yako pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…