Mkoa wa Geita wavunja rekodi,wagombea ubunge wawili ni wahitimu wa darasa la saba B

Ndio wa kukenua tuu Bungeni!
 
Waja jamaa kachelewa sana kuwa mbunge hapo Geita ni msomi na mchapa kazi sana
Shule yake na hospital zimeipamba Geita kama huduma Bora za jamii kwa mda mrefu
 
Hawa wasomi wa kukalili madesa wanna tufauti gani na wahitimu wa std seven.....halafu unamchukuliaje MTU aliyekaa darasan miaka saba bado unamchukulia kuwa ni tabulalasa!!!!
 
Geita hatutaki Mbunge atakayeongea kiingereza Bungeni, mara Ofcoz sijui nini hatutaki. Kasheku anatosha
 
Ndio maana pamoja na rasilimali zote bado umetopea kwenye Lindi la ufukara
 
Degree iwe kiwango cha chini cha Elimu, ndiyo wanapitisha mikataba ya nchi.
 
Kwamba akina sisi tusiosoma hatuna haki ya kuwa viongozi?

Kwanza nyie mnaojiita wasomi ni mafisadi na wakwapuzi wa mali na rasilimali za nchi yetu

Acheni ubinafsi nchi ni yetu sote
 
Kwamba akina sisi tusiosoma hatuna haki ya kuwa viongozi?

Kwanza nyie mnaojiita wasomi ni mafisadi na wakwapuzi wa mali na rasilimali za nchi yetu

Acheni ubinafsi nchi ni yetu sote
Mimi naona hawa ambao hawajasoma wanapitisha mikataba na kuisaini bila kujua kilichoandikwa humo.
 
Hawana baya ilimradi mbunge wao awe anajua kuwasimanga wasomi tu.
 
Kwamba akina sisi tusiosoma hatuna haki ya kuwa viongozi?

Kwanza nyie mnaojiita wasomi ni mafisadi na wakwapuzi wa mali na rasilimali za nchi yetu

Acheni ubinafsi nchi ni yetu sote
Tatizo lenu mnajidai hamtaki usomi ila cha ajabu tukiwapa tu ubunge mnaenda kuununua udaktari UDOM.
 
Kigezo kikubwa cha kuwa mbunge Tanzania ni kujua kusoma na kuandika. Swali langu ni hili kwako, hao wa la saba B huko Geita, hawajui kusoma na kuandika???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…