Mkoa wa Iringa utolewe Nyanda za Juu Kusini na kupelekwa Kanda ya Kati iwe Pamoja na Dodoma na Singida

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko pamoja na Waziri wa Masuala ya Nishati wa Zambia, Mhe. Peter Kapala leo wamefanya kikao kilicholenga kujadili nia ya Serikali ya Tanzania na Zambia kuanza ujenzi wa bomba la inchi 24 la kusafirisha mafuta safi kutoka Tanzania kwenda Zambia.

Kikao hicho kimefanyika tarehe 29 Januari, 2024 jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, Makatibu Wakuu wa Wizara za Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, (Tanzania) na Dkt. Chisangano Zyambo (Zambia) pamoja na watendaji mbalimbali kutoka Wizara hizo na Mashirika yanayosimamia Mafuta.

Dkt. Biteko amesema, majadiliano hayo ya Mawaziri yanatokana na ziara ya Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoifanya nchini Zambia mwezi Oktoba mwaka 2023 ambapo katika mazungumzo yake na Rais wa Zambia, Mhe. Hakainde Hichilema walijadiliana kuhusu kuongeza uwekezaji kwenye Bomba la Mafuta la TAZAMA kwani bomba hilo kwa sasa halikidhi mahitaji kutokana na kuwa na ukubwa wa inchi 12.

“Kulingana na maendeleo makubwa katika nchi zetu mbili, mahitaji ya mafuta yamekuwa makubwa ndio maana inabidi kujenga bomba jingine jipya kubwa ambalo litasafirisha mafuta kutoka Tanzania kwani kuna Bandari, bomba hili litakalojengwa pembeni ya Bomba la Mafuta la TAZAMA litasafirisha mafuta pia kwenda mikoa ya kusini mwa Tanzania na hivyo kupunguza gharama za usafirishaji na kuwapatia wananchi mafuta ya gharama nafuu.” Amesema Dkt. Biteko.

Ameeleza kuwa, bomba hilo litakuwa na urefu wa kilometa 1,710 na uwekezaji wa Dola za Marekani Bilioni 2.5 na kusisitiza kuwa, kwa uwekezaji huo kunahitajika umakini kwenye utekelezaji wake na bila kuuchelewesha.

Ameongeza kuwa, bomba litakuwa na matoleo ya Mafuta katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Morogoro, Makambako, Mbeya na Songwe na kupunguza suala la mikoa hiy
 
kesho utakuja hapa utasema na Morogoro nayo iko kanda ya kati. Bora ibaki hivyo ilivyo hii mikoa miwili Mbeya na Iringa watu wake wameingiliana sana kuliko Dodoma nikiwa na maana kuoana ndio maana utakuta koo zake zinafanana kwa mfano Kalinga /Mwakalinga ,Lutengano pande zote wapo hizi ni chache tuu nawasilisha
 
Acha ibaki huko huko nyanda za juu kusini kijiografia zaidi maana ukitoka Dodoma ukifika Mtera unaanza mdogo mdogo kupanda juu alafu ukipita Migori unapanda mlima Nyang'olo alafu ukifika juu inakuwa tambarare kuonyesha umetoka chini upo ukanda wa juu, vivyo hivyo ukitoka Dar ukipanda Kitonga yaani kuna action ya kupanda sio kushuka na ukitoka Iringa kwenda Dom au Dar kuna action ya kushuka na sio kupanda na hiyo ndio maana halisi ya Nyanda za Juu

Btw, sehemu ndogo sana ya Iringa inafanana na Dodoma yaani kuanzia Mtera, Migori, Isimani, Kihorogota, Kising'a mpaka Nduli ila ukiingia mjini kuanzia Kihesa Kilolo, Kihesa kuanza kuitafuta Mafinga hali ya hewa ni tofauti yenye ujazo ya uoto wa asili na vijito visivyokauka hata kama ni kiangazi tofauti na Dodoma, achilia mbali hapo hujaenda wilaya ya Kilolo ambayo utaunganisha mpaka Kidabaga, Mwatasi unatokeza wilaya ya Mufindi vijiji vya Usokami, Kibengu, Mapanda na Kipanga ambapo napo huku kupo juu kabla ya kuanza kushuka kuitafuta Morogoro tarafa ya Chita - Bwawa la Kihansi mpaka Mlimba
 
Ukiacha Mufindi kwingine kote ni sawa na Dom lakini pia Iringa Iko karibu na Dom kuliko Mbeya na Ruvuma.

Kilolo Haina tofauti na Mpwapwa.
 
Acha uongo we kada wa chama cha mafisi. Kilolo asilimia kubwa ipo Milimani. Inayofanana na Morogoro na Mpwapwa ni tarafa ya Mahenge yenye kata za Mahenge, Ruahambuyuni na Nyanzwa ila ukipandi Kitonga tu na ukifika huko Dabaga anaposemea jamaa ni tofauti na Mpwapwa. Ni pure nyanda za juu kusini.
 
Acha ibaki huko huko nyanda za juu kusini kijiografia zaidi maana ukitoka Dodoma ukifika Mtera unaanza mdogo mdogo kupanda juu alafu ukipita Migori unapanda mlima Nyang'olo alafu ukifika juu inakuwa tambarare kuonyesha umetoka chini upo ukanda wa juu, vivyo hivyo ukitoka Dar ukipanda Kitonga yaani kuna action ya kupanda sio kushuka na ukitoka Iringa kwenda Dom au Dar kuna action ya kushuka na sio kupanda na hiyo ndio maana halisi ya Nyanda za Juu

Btw, sehemu ndogo sana ya Iringa inafanana na Dodoma yaani kuanzia Mtera, Migori, Isimani, Kihorogota, Kising'a mpaka Nduli ila ukiingia mjini kuanzia Kihesa Kilolo, Kihesa kuanza kuitafuta Mafinga hali ya hewa ni tofauti yenye ujazo ya uoto wa asili na vijito visivyokauka hata kama ni kiangazi tofauti na Dodoma, achilia mbali hapo hujaenda wilaya ya Kilolo ambayo utaunganisha mpaka Kidabaga, Mwatasi unatokeza wilaya ya Mufindi vijiji vya Usokami, Kibengu, Mapanda na Kipanga ambapo napo huku kupo juu kabla ya kuanza kushuka kuitafuta Morogoro tarafa ya Chita - Bwawa la Kihansi mpaka Mlimba
Unapajua hadi huko mwatasi na Mapanda mkuu? Umetembea sana kaka.
 
We ngumbaru una shida Kwa kweli.

Makao Makuu yapo ndio maana Huwa unasikia Hospital za Kanda,Ofisi za Kanda za Huduma Fulani nk ila sio rasmi kwamba Kuna Mkuu wa Kanda wa Serikali hapana ila Meneja wa Kanda wa banks, kampuni nk wapo.
Wewe ndiye Ngumbaru kweli, wakazi wa Mufindi na Mafinga zinawezaje kuwa karibu na Dodoma kwa huduma??
 
Back
Top Bottom