Mkoa wa Iringa utolewe Nyanda za Juu Kusini na kupelekwa Kanda ya Kati iwe Pamoja na Dodoma na Singida

Sijui Kuhusu hayo mengine ila mimi nahisi sababu za kijamii na kiutamaduni ndio hasa zinazounganisha mikoa hii ya nyanda za juu kusini. Kwa ufahamu wangu nafikiri wahehe wanafanana zaidi na watu wa Njombe na Mbeya kuliko wwnavyofanana na watu wa Dodoma na Singida. Kwa hiyo mtoa mada unataka kusema idadi ya wagogo waliopo Iringa inazidi idadi ya wabena na wakinga?
 
Hapana wale omba omba waendelee kukaa wenyewe ukiwachanganya na wachapakazi watawaambukiza uvivu, Acha waendelee kulelewa na serikali.
Iringa Kuna Wagogo Kwa hiyo wanajuana na ndio maana nasema Iringa iende Kwa ndugu yake.
 
Mkoa wa Iringa Kwa Sasa uko Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Ingefaa Kwa Serikali kuiondoa Iringa Nyanda za Juu Kusini na kuihamishia Kanda ya Kati Kwa sababu zifuatazo

Sababu yako ya kijiografia haina maana, kuitwa nyanda za juu kusini kulitazama jiografia ya eneo husika toka usawa wa bahari...

Huo ukanda hata hali yake ya hewa ipo tofauti sana na maeneo ya kati ya nchi kama Singida, Dodoma na Tabora...

Ukitumia kigezo cha kupakana na Dodoma zaodo, nami nitakwambia umepakana na Njombe zaidi hivyo tuufanye tu uendelee kuwa nyanda za juu kusini...
 
Unatakiwa kuwa na heshima kidogo. kwahiyo unataka kuiunganisha iringa na singida na dodoma? unaelewa maana ya nyanda za juu kusini? iringa ni nyanda za juu (milimani), dodoma kuna nyanda? singida kuna nyanda? wamekuchosha nini?
 
Habari mkuu, serikali ipo mchakatoni na hilo, nilisikia kuanzishwa kwa kanda ya kati ambayo itakua na mikoa ya singida Iringa dodoma na Babati kama sikosei.
Lakini sio mbaya, kama wanataka kuchanganya kidogo sura za kihehe na kinyaturu na wambulu kidogo. pengine mhehe atatokapo na kasura kengine.
 
Kwani ukibaki maali ulipo kipi kinakosekana au ukihamia huko kipi kitaongezeka kwa huo mkoa.
 
Hilo ni gumu Sana. Mkoa wa iringa mwanzoni ulikua unapakana na Ruvuma na Mbeya mikoa yenye Hali ya hewa sawa. Mikoa hiyo ilikua na sifa sawa yaani umbali kutoka usawa wa bahari na Hali ya hewa. Baada ya Njombe kujitenga mkoa wa iringa bado eneo kubwa linapatikana katika nyanda za juu(kilolo, iringa mjini na mufundi) hivyo haitakuwa sawa kuwekwa Kanda ya kati.

Kuhusu watu, mkoa wa iringa una kabila kuu la wahehe ambao wengi wanapatikana Mbarali, makambako na Mbeya mjini Kwa kiwango kidogo. Lakini mkoa huo una idadi kubwa ya wabena na wakinga kuliko wagogo.

Kuhusu mwingiliano wa watu kati ya iringaa na mikoa ya nyanda za juu kusini na Dodoma. Idadi ya watu toka Njombe na mbeya wanaoingia na kutoka mkoa wa iringa huwezi fananisha na Ile ya Dodoma. Kutoka iringa kwenda Njombe Kuna mabasi Kama Mwafrika (Iringa- makete,ludewa) mgumba trans( iringa -njombe) Mwenda mseke (iringa -njombe), Chula (iringa - Madibira) na coaster nyingine za route hiyo. Wakati iringa- Dodoma Kuna gari chache ambazo huondoka Kwa interval kubwa na Kuna basi Moja hupiga go and return maana yapo machache.

Kuhusu upatikanaji wa huduma za Kanda. Hilo ni kawaida Kwa maeneo yaliyombali na ofisi kutumia huduma za karibu. Rejelea maeneo ya mipakani mwa nchi kupata huduma nchi jirani, mikoa kupata huduma mikoa jirani n.k hivyo haiwezi kutumika Kama kigezo Cha kuhamishia mkoa, ingekua hivyo basi watu wa Mbozi wangehamia nchi jirani kitambo maana huduma wanafuata Dodoma.
 
Mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmhhhhhhhhhhhhhhh
 
wawaweke tu pamoja na wagogo. si unajua mkwawa alitawala hadi parts of Dodoma, ukienda mpwapwa, asili kubwa ya watu ni wahehe na wabena, nawezasema majority na hao walienda wakati wa utawala wa Mkwawa. aliteka maeneo yote hayo wakawa chini ya utawala wake.
 
Naunga mkono hoja, Iringa iwe kanda ya kati inasound zaidi kuliko huko iliko sasa.
 
Naunga mkono hoja, Iringa iwe kanda ya kati inasound zaidi kuliko huko iliko sasa.
zamani ilikuwa sahihi kwasababu wilaya ya ludewa, njombe na makete ambazo zote zipo mkoa wa njombe, zimesambaa hadi kusini na upande mwingine kuungana na mbeya. lkn sasaivi, iringa inaishia tu pale mafinga kurudi nyuma. ukiondoa Kilolo (dabaga) iringa ni kavu kama singida na dodoma tu. sio mbaya kama wataiondoa kusini.

Pamoja na kwamba utakuwa umewatenga sana na watumwa wao (wabena, wakinda na wapangwa). kihistoria, wabena, wakinga na wapanga hawana historia ya kutawala, wao walikuwa subordinates tu wa Mkwawa hadi usangu huko. na wameendelea kujifanya wahehe hadi kesho kwasababu kwao kuitwa mhehe ndio anatambulika zaidi kuliko akijiita mbena au mkinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…