Mkoa wa Kagera na Ufukara

Kuna wachangiaji waliwahi kufika vijijini huko na si wahaya ndo wanatoa uhalisia wa mkoa wa Kagera na Wilaya zake.

Kuna wachangiaji hawajawahi kufika kwa hiyo wanaongea kwa hisia +ve na -ve.

Kuna waliofika stand wakaona nyomi ya mabasi lakini kwa kuwa stand ni ya udongo basi wakahitimisha wanavyojua

Wapo wanaoenda kwenye viwanja na mahoteli kuona totoz hao ukiwaambia Kagera ni maskini hawakuelewi.

wanaosema Kagera ni maskini hawaongelei maafa yaliyowahi kuikumba lakini wenyeji hujitegemea bila kuomba wala kupelekewa msaada. (Vita ya Kagera, matetemeko, mnyauko wa migomba, siasa kwenye zao la kahawa n.k).
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Hatari sana eti kuna mlala hoi pale Dar nae anahesabiwa anapata milioni 5 kwa mwaka wakati hana pa kulala
Nenda kariakoo usiku kwenye corridors za maduka watu wanalala mzungu wa nne asubuhi anaonekana kachomekea alafu anajisifu mkoa wangu tajiri! Utajiri wa mkoa husika sawa unaweza kutokana na juhudi binafsi lakini utashi wa kisiasa kuusaidia ni muhimu! Mfano: Arusha/Kilimanjaro: utalii na mbuga za wanyama na mlima Kilimanjaro na Headquarter ya East Africa community, na ujirani wa maingiliano na Kenya kiuchumi vimewabeba na vile vile kushika nyazifa za juu serikalini kumewasaidia pia! Kagera majirani zake wote ni vita na mahuaji DRC Congo, Burundi, Rwanda, Uganda! Hawa majirani hawana msaada zaidi ya kuleta majambazi na kupora watu hela! Misafara ya magari kutoka inland Tanzania inazuiwa na majambazi! Mawasiliano na mikoa jirani ya mwanza na msoma yanachangamoto ya ziwa Victoria! Msiwabeze wahaya! Asilimia kubwa ya shule binafsi za Dar ni za wahaya! Wanawekeza kuinua maharifa ya watanzania ili waje hapa jukwaani kuwabeza? Shwaini hamna adabu!!!! Mwenye mtandao pendwa hapa nchini na Africa pia ni mhaya! Shikeni adabu zenu na mkome kuwabeza wahaya eboooh!
 
Geographical location ya mkoa wa Kagera na rasilimali zake haziuruhusu uchangie pakubwa kwenye pato la taifa. Hakuna viwanda, nani ajenge kiwanda kipo more than 1000km kutoka bandarini? Malighafi zitafikaje na finished products zitafikaje.
Hakuna migodi wala utalii wa maana sasa kodi serikali ipate kutoka wapi.

Mkoa umezungukwa na nchi maskini Rwanda, Burundi na Uganda ambazo nchi hizo zina mazao yaleyale yanayopatikana mkoa huo. Hakuna exchange ya products.

Mkoa hauna miradi ya uzalishaji ya serikali. Hutosikia kimejengwa kiwanda cha kahawa, wala mazao ya mbao, wala soko la mataifa jirani.

Serikali haitaki kuona mkoa unaendelea kwenye kilimo. Ikitokea fursa yoyote ya kilimo serikali inaona wivu, hivi Tanzania hii kuna zao linaloshushwa bei mara 10 kama ilivyo kwa vanilla? Leo kilo ni 100,000 mwakani kilo 10,000 na wanunuaji hamna. Hilo zao lingekuwa kubwa huko kuliko mkoa wowote.
Mikoa inayolima mahindi na mpunga haizuiliwi kuuza nje hata kama inapandisha gharama ya chakula kwa soko la ndani ila Kagera kuuza kahawa nje ni jambo gumu sana, wakati nchi ikikosa kahawa haina hamna kinachobadilika.

Mkoa unapakana na nchi nyingi hivyo ni hatarishi kwa magonjwa ya kuambukiza, vita na uhamiaji ikitokea machafuko kwa majirani. Hayo yote yanatokea na hakuna jitihada za serikali kupunguza madhara, kwanini baada ya vita ya Kagera tulilipwa reparations na Uganda. Kwenye hiyo hela kuna iliyoenda mkoa ule kufidia athari? Majengo, madaraja, shule na vifo vingi vilitokea kule ila hela ya fidia haikwenda.
Tetemeko lilitokea michango jamaa akaipeleka anakojua yeye.

Kuna tofauti ya eneo kuwa maskini na watu wa eneo kuwa maskini. Wapemba wana maduka Kariakoo na wamejaa nchi nzima wakinunua na kuuza bidhaa, ambaye hajawahi kwenda kwao hawezi amini ukimwambia hawana hata vyoo wanajisaidia baharini na vichakani.

Serikali ikiwa na wivu na eneo haliwezi endelea. Pwani inapewa kila kitu na haijulikani kwanini. Shinyanga ina umaskini sana na matukio ya kutisha ukiachana na migodi ya wazungu. Morogoro imejaa wageni kuna fursa za kutosha ila kuna makabila uko wakimaliza mavuno wanapiga sherehe mazao yanaisha wanasubiri msimu mwingine. Hii nchi distribution kwa mikoa ya mbali ni ndogo.
 
Ulishawahi hudhuria harusi za watu wa mkoa huo? Au ulishawasikia wanavyojigamba?
 
Sasa mkuu hicho kilimo nani atalima wakati wote wamekimbilia marekani kusaka ajira kutokana na elimu zao
 
Hawana akili Istanbul
 
Buloo....per capita income vs kukusanya kodi ni vitu viwili tofauti kabisa, rudi kwa class.
 
Buloo....per capita income vs kukusanya kodi ni vitu viwili tofauti kabisa, rudi kwa class.
Hata hiyo Kodi wanayokusanya Iko ndani ya hesabu za GDP ambazo huzaa per Capita against their population so hakuna pa kukwepea
 
Wahaya wanaojiuza huko Dar ni matajiri?

Wahaya wa huko Kagera Wana pesa zipi zaidi ya kuongeza idadi ya maskini Tanzania?
 
Hii dhana Yako Iko sawa kabisa Kwa muktadha wa Mikoa ambayo Ina migodi mikubwa kama Shinyanga,Geita na Mara.

Hata hivyo Mkoa kama Kagera una Hali ya hewa nzuri Kuliko Mikoa Mingi Kwa nini Watu wake wasijihusishe Kwa kilimo kama Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambayo Haina Cha migodi Wala uwekezaji wowote wa Serikali lakini Iko Juu kwenye list Kwa kazi za Kilimo tuu.

Kwa hiyo hakuna excuses hapa,nyie ni wavuvi mdomo umezidi.

Mwisho kabisa Serikalini iwe na formula ya kugawa rasilimali za Taifa Kwa usawa,hii tabia ya kujenga Dar,Dom,Arusha na Mwanza pekee Kwa pesa za Mikoa mingine ikome mara Moja.Mimi Huwa naandika mada za kupinga hili ila Huwa mnaniona mjinga.
 
Watu wanajua ukifika Muleba na Bukoba basi ndio Kagera wakati Kuna Wilaya choka mbaya huko hazitamaniki.
 
Wewe acha ujuaji wananchi wa Shinyanga wana kipato kikubwa kuzidi nyinyi! Chukulia kwa mfano Wilaya ya Kahama na Msalala ambayo ina watu wengi zaidi ya asilimia 50% ya wakazi wa shinyanga unaweza kulinganisha kipato chao na wananchi wa wilaya gani hapo Kagera! Mnapenda sana sifa za kijinga! Mji wa Kahama unaizidi mpaka Bukoba makusanyo ya TRA na unawafanya biashara wengi kuliko Bukoba mjini! Migodi midogo midogo na biashara Kahama ni ya wananchi wa Kawaida na wengi ni Wasukuma! Kama mnasingizia migodi vipi kuhusu Kilimo? Mbona mikoa wenye hali ya hewa kama nyinyi iko juu kuliko nyinyi? Mfano mna mji gani wa Kibiashara hapo kagera wa kulingana hata na Katoro Geita?
 
Shinyanga hii ambayo nyumba za tembe zimetapakaa au kuna Shinyanga nyingine??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…