Supu ya kokoto
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 4,194
- 7,602
Nilipoona tu "ukatili wa kijinsia" nkajua lazima uitaje MARA.
Horrible....!!
Horrible....!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mtoto ni asset ya mzazi, wacheni wazazi wawazoeshe watoto wao kazi hususani kilimo wangali bado wadogo, ilikusudi kwa miaka ijayo na ya baadaye wawe wakulima bora na wasio tegemezi "practise makes perfect"Mkoa wa Kigoma ukatili waongezeka, "madanga" kutoka Congo DRC na Burundi waingia Kasulu
Mkoa wa Kigoma umetajwa kuwa na kiwango kikubwa cha vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana kitendo ambacho kimeelezwa kusababisha kurudisha nyuma shughuli za maendeleo katika mkoa huo.
Mkoa huo ni kati ya mikoa 10 nchini yenye kiwango kikubwa cha vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana.
Mkoa huo una kiwango cha asilimia 61 ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimekuwa vikifanywa kwa wanawake na watoto.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za wanawake na wasichana la mkoani Mwanza la KIVULINI YASSIN ALLY.
Yassin amesema hayo wakati wa maadhimisho ya siku 16 ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana yaliyofanyika katika viwanja vya umoja wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma
Amesema mkoa huo hususani wilaya ya Kasulu, imekuwa na idadi kubwa ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu ambao wengine wametelekezwa na wazazi wao.
Yassin amesema inahitajika mpango maalumu wa kuwatambua watoto hao ambao wengi wao wanafanyiwa vitendo vya ukatili baada ya migogoro ya familia na wengine kutelekezwa na wazazi wao.
Amesema jamii nyingi katika wilaya ya Kasulu, wamekuwa na utaratibu ambao sio rasmi, katika kipindi cha kilimo kwa kuwapeleka watoto wao kwenye shughuli za kilimo.
Pia amesema wazazi wengi katika kipindi hicho wa kilimo, wamekuwa wakiwatelekeza watoto wao nyumbani wakijilea wenyewe jambo ambalo linachangia kuwepo kwa wimbi kubwa la watoto wa mtaani.
"Watoto unakuta wamekaa miezi sita hawajaenda shule kutokana wazazi wao kuwapeleka kwenye shughuli za kilimo na hali hii inapaswa Serikali ichukue hatua za haraka kuondoa tatizo hili.
"Ukiachana na hayo, katika wilaya hii kuna wimbi kubwa la wanawake wanaojiuza "madanga" wanaingia ijumaa na kutoka Jumatatu kuja kuuza miili yao na hii inaleta athari kubwa kwenye jamii.
"Tatizo hili la wanawake kutoka Congo DRC na Burundi, kuja hapa Kasulu kutokana na hilo Polisi kuingilia na kuangalia suala hili ambalo linachangia familia kutelekezwa kutokana na hao "madabga", amesema Yassin.
Afisa dawati la Jinsia na watoto Polisi wilaya ya Kasulu ,Maimuna Abdul amesema Wilaya ya Kasulu ni kinara kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika mkoa huo.
Abdul amesema Januari mpaka novemba 2020, wamepokea kesi 153 za watoto waliofanyiwa ukatili ambapo amedai wamefikisha mahakamani kesi 20 na kesi nyingine 133 zipo katika hatua ya upelelezi.
Amesema katika wilaya hiyo, Januari - Novemba kesi za ndoa za utotoni zimelipotiwa ndo saba, mimba za utotoni zilikuwa 42 ambazo zilisababishwa na janga la Corona.
"Kesi za watu wazima ambazo zimelipotiwa Polisi kuanzia kipindi hicho 333 ambapo kesi zilizofikishwa mahakamani ni 43 na zilizopo kwenye upelelezi ni 190," amesema Abdul.
Makamu Mwakilishi wa Shirika la umoja wa mataifa linalojihusisha na masuala ya wanawake (UN - WOMEN), Julia Broussard amesema Shirika hilo limekuwa likifanya kazi na Serikali kuhakikisha vitendo vya ukatili vinapungua nchini.
Pia amesema Shirika hilo linafanya kazi kukuza vituo vya utoaji wa elimu ikiwemo madawati ya Jinsia la Polisi nchini ili kusimamia kesi mahakamani zinazohusu wanawake na watoto.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, mkuu wa Polisi wilaya ya Kasulu Iddy Kiyogomo amesema ukatili wa kijinsia hususani watoto wa kike unasababisha watoto hao washindwe kutimiza ndoto zao.
Amesema vitendo vya kutelekeza familia unasababisha kurudisha nyuma shughuli za maendeleo katika jamii, kitendo ambacho wananchi wanapaswa kukemea na kutokomeza vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na haki za binadamu na sheria za nchi.
Kiyogomo amesema Serikali ya awamu ya tano bado inaendelea na jitihada za kupambana na vitendo ukatili wa kijinsia kwa kutunga miongozo, sera na sheria za kupambana na ukatili wa kijinsia katika jamii.
Mikoa inayoongoza kwa kuwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia ni Mara asilimia 66.4, Shinyanga, Kigoma, Geita na Kagera.
Mwisho
Kwa sehemu na kuunga mkono ukipiga hesabu ya gharama ya masomo hasa kwa shule hizi zinazoitwa za kisasa za kulipia,za binafisi ni bila maandalizi ya mzazi kumuwezesha tena baada ya kupata elimu aweze kujiajiri ni hasara tupu.mtoto ni asset ya mzazi, wacheni wazazi wawazoeshe watoto wao kazi hususani kilimo wangali bado wadogo, ilikusudi kwa miaka ijayo na ya baadaye wawe wakulima bora na wasio tegemezi "practise makes perfect"
Hao wanaotaka watoto wakasome wasiwapangie watoto na wazazi wao, kwani hawajawazaa, yawapasa wapambane na watoto wao, waache watoto wa watu wafanye kazi.
Wasomi wengi wapo mtaani na ni tegemezi, wasomi hao hao wanaambiwa wakalime, wasomi hao hao wanaambiwa wajiajiri, na Elim walioipata ni ya nadharia(theory) sio ya vitendo (practical) hivyo kutokana na mfumo mbovu wa elim ya Tz wanashindwa yote hayo wanayoambiwa wayafanye then wanaishia kuwa tegemezi na matapeli.
Mwisho; wawaache hao watoto waendelee kulima na kufanya kazi nyingine za maendeleo ktk jamii kwani hii huwanoa watoto mapema katika masuala ya kujiajiri na kujitegemea, mara tu wafikishapo umri wa mwanafunzi wa chuo huwa ni watu waliopiga hatua ya kimaendeleo ktk jamii na wengi wao hujitegemea mapema wangali wadogo na wakiwa na stadi nyingi na kubwa za maisha ktk jamii tofauti na hawa wa vyuoni waliopelekeshwa na serikali kusoma huku ikitambua kabisa ajira ni changamoto.