kudraty
Senior Member
- Mar 4, 2018
- 142
- 189
Ambiele Kiviele, Bora umemuelewesha
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji1] [emoji2] [emoji3] umekosea wanasema ipere thikindu kindu ni mshombeThamaki thi kindo, kindo nyi mthombe.
Kuna vijiji ugweno wanaongea kipare na hawajui kigwenoWasangi ni kabila dogo sana Ugweno wengi wao wapo Usangi ambapo ndio upareni
Nina mashaka na level ya elimu yako, exposure na umri wako sitaki kubishana na wewe.
Hii ni ramani ya makabila ya Tanganyika ya mwaka 1956.Kuna watu ukiwatajia kuwa unatoka mkoani Kilimanjaro wanajua wewe ni Mchanga!
Si kweli na kuna baadhi wanajua yakuwa Kilimanjaro kuna Wapare na Wachaga tu ngoja nikusanue.
Kilimanjaro kuna makabila matatu;
1, Wachaga
2, Wapare
3, Wagweno.
Leo nazungumzia wagweno kwa ufupi;
Wagweno wanapatikana katika milima ya Ugweno mkoani Kilimanjaro na kwa bahati mbaya wengi wamekuwa wakiwachanganya na wapare na wengine wakiwafananisha na wachaga kimuonekano:
1. Ni warefu sio wafupi kama wapare
2. Wanaongea lugha yao waiitayo kigweno isiyofanana kabisa na kipare japo inafanana na kichaga cha Rombo.
3. Majina yao Mshana, Msangi, Kimaro, Shirima, Mfinanga, Mbaga nk ukitumia majina unaweza kumwita mchaga au Mpare.
Kigweno ni kleori yani mchanganyiko wa lugha mbili yani kichaga na kipare japo kichaga ni dominant ktk lugha ya kigweno ambapo kihistoria baada ya wagweno kutoka Kenya kupitia Taveta kipundi hicho wakiwa makundi mawili ya wapare na wachaga walivyokutana ktk milima ya ugweno walikuwa wanaongea lugha mbili tofauti ambapo mkanganyiko huo ulipelekea kutokea kwa lugha mpya waliyoiita Kigweno yani ni mfano wa Kibantu na Kiarabu kupatikana lugha adhimu ya kiswahili.
Kwanini nasema kuwa Wagweno ni kabila?
Sifa za kabila;
1, Kuwa na Lugha ___Kigweno
2,Kuwa na tamaduni __ Kutambika
3, Kuwa na eneo ____ Ugweno kifula, Msangeni, Vuchama, Raa, Masumbeni nk
4, Shughuli za kijamii; Ufuaji wa vyuma bila kusahau kuwa Washana ndio watu wa kwanza weusi kufua vyuma duniani ambapo ilisaidia shughuli za kilimo, uwindaji nk
Hii mada ni ndefu sana japo kuna waliopotosha kuhusu mila na tamaduni za Kigweno kama Prof Kimambo katika kitabu chake "The History of Tanzania" but mlio tayari kujua kuhusu hili nakuja na full package ya Kitabu ambacho ni full of reseach kikikamilika nitawajuza namna ya kukipata kwa wale watakaopenda.
Wito wangu ni kwamba tusiishi kwa kukariri Waafrika tupende kujifunza.