Mkoa wa Tabora kugawanywa na kuwa mikoa miwili

Ukiuangalia mkoa wa Tabora utagundua ni mkubwa mno kieneo hata kiwilaya kuna Urambo, Kaliuwa, Nzega, Igunga, Manonga, Sikonge, Uliankuru na kadhalika, itafaa ukigawanywa.

Na mimi labda nitabahatisha ukuu wa mkoa.
Kuna faida gani ya kuugawa wakati kodi yoote inayokusanywa inaenda dodoma?
 
Mindset is everything
 
Ukiuangalia mkoa wa Tabora utagundua ni mkubwa mno kieneo hata kiwilaya kuna Urambo, Kaliuwa, Nzega, Igunga, Manonga, Sikonge, Uliankuru na kadhalika, itafaa ukigawanywa.

Na mimi labda nitabahatisha ukuu wa mkoa.
Jiografia darasa la ngapi kufundisha kuwa mkoa wa Tabora kuna wilaya zinazoitwa Manonga ama Ulyankulu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kama unataka kuona faida ya kugawa Mikoa nenda kaone Chato ambako hata vipofu wameona, hebu fikiria wakti ule Bariadi ilivyokuwa wilaya ndani ya Mkoa wa Shinyanga ni jinsi gani watu walipata shida kufuata mahitaji ya kiutawala?

Au fikiria mtu wa Bukene/Nzega anapataje kutatua shida za kiofisi Tabora mjini au chukulia mfano wa mtu aliyeko Igunga anasafirije siku mzima kufika Tabora na kutatua mambo yake ya kiofisi?
 
Mkoa wa Tabora 76,150 km² hakuna mpango wa kuugawa, Geita 20,054 km² tunagawa

Huenda kuna mahali tumefungwa kamba.
 
Tabora likubwa jinga haliendei, sijui kwanini serikali imekaa kimya, why wasimege nusu ya eneo ikawapatia Shinyanga/Kahama na Singida!!!
 
Mkuu hatugawi kulingana na km squire bali ni population density ya eneo na demographic distribution data.
 
Mkuu usiusahau mkoa wa Morogoro, nao ni balaa. Ukubwa wa mkoa wa Morogoro ni sawa na Burundi+Rwanda.
 
Haya maujinga yalianzishwa na mwenda zake hata kama vigezo havikuwepo jamaa alitaka tu kulazimisha ndiomaana alianza na uwanja wa ndege kabisa
 

Naufahamu mkoa wa Tabora...

Ni kweli ni Mkubwa, lakini sehemu kubwa ni mapori yasiyokuwa na wakazi...

Ni ukweli kwa ujumla ni mkoa wenye wakazi milioni 2.5 (labda)..

Hata hivyo watu hawa wengi wako mijini. Sehemu kubwa ya eneo la mkoa wa Tabora ni wazi likiwa na misitu na mapori tu..

Hakuna haja ya kuugawa mkoa. Haukidhi vigezo...
 
2,091,863 / 2= 1,045,932 ndio idadi ya watu kila mkoa wanaotarajiwa kudogezewa huduma.
Gharama ni kubwa kuliko faida, ikizingatiwa kuwa hakuna vyanzo vya mapato vinavyoeleweka
 

Wakate nusu wapewe Shinyanga/Kahama na Singida. Tabora ilitakiwa wawe na eneo dogo sana kulingana na poulation na uchachu wa maendeleo.

Dar kwa eneo ni dogo sana kwa tbr na population yao ni kubwa may be mara tatu ya tbr, akili kweli hii!!! Mwanza eneo dogo kwa tbr na population yao iko juu + maendeleo,akili kweli hii!!! Mbeya pia eneo dogo kwa tbr akili kweli hii!!! Serikali wafanye kila namna wakate nusu ya eneo wapewe Shinyanga/Kahama na Singida.
 
Kuna mikoa midogo kieneo lakin huduma za wananchi HAKUNA.. Kwahiyo nayenyewe waigawe? Mi nadhan wilaya zote ziitwe mikoa na tarafa ziwe wilaya... Na kata ziwe tarafa, na vijiji viwe kata, na vitongoji viwe vijiji Ili mfurahi... Maana ni upumbavu mnatuletea kila wakati... Eti kuwasogezea wananchi maendeleo..MAENDELEO YANAKUJA KWA KUFANYA KAZI KUWA WABUNIFU NA KUWATUMIKIA WANANCHI..

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…