Hizi bangi hizi za mtu mweusi,hakuna tija ya kiuchumi ya kugawa mkoa,Kwanza haiingezi kipato kwa nchi, zaidi inaongeza matumizi tu, RC, DED.
Cha muhimu mungewaza kwamba viwanda vya kutengeneza matairi ya gari, au viwanda vya nondo au saruji, au sukari havitoshi, tuongeze viwe vingi, ili tutengeneza mapato, nyie mnawaza kuteuliwa. Bora kuongeza hospitari, vyuo vya Elimu ya juu, au kufungua campus ya UD mkoani Tabora, au Bora mseme, hatuwezi kutegemea mvua kwa kilimo, sasa tuje na mpango wa kutumia maji ya ziwa victoria kufanya umwagiriaji.
Mkoa wa Tabora, unatumia maji ya victoria, lakini na yenyewe ni mgao,maana mkoa hauna mapato ya kuwezesha kutembwza pump 24/7.
Hakuna faida ya kuongeza mkoa, ukisema unasogeza huduma kwa jamii, kwani eneo linaongezeka? Geographical area ipo vile vile, kuongeza mkuu wa mkoa. Kuna msaidia vipi mwananchi wa kawaida, sie hatutski kuona sura, tunataka huduma, vituo vya polisi, barabara, Elimu, afya.