Al Watani
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 21,237
- 31,811
Angeshauri kuigawa wilaya ya Uyui ningemwelewa sana ile wilaya ni kubwa kibaya zaidi kufika makao makuu ya wilaya kuna baadhi ya kata lazima uvuke makao makuu ya mkoa.
Kugawanywa mikoa Tanzania, haipeleki huduma yoyote karibu na wananchi. Secretariat za mikoa hazina kazi kivile. Wananchi hupata huduma nyingi katika ngazi ya halmashauri na kidoogo kwa DC.
Hatuhitaji tawala za mikoa Tanzania. Ni matumizi mabaya ya Rasilimali fedha na watu. Tugawanye halmashauri kadri ya uwezo wetu lakini siyo mikoa. Hata kwa watoa huduma wakubwa Kama polisi, Tanesco na TRA, wanaweza kujiorganize kiwilaya pia.