Mkoa wa Tabora kugawanywa na kuwa mikoa miwili

Mkoa wa Tabora kugawanywa na kuwa mikoa miwili

Kugawanywa mikoa Tanzania, haipeleki huduma yoyote karibu na wananchi. Secretariat za mikoa hazina kazi kivile. Wananchi hupata huduma nyingi katika ngazi ya halmashauri na kidoogo kwa DC. Hatuhitaji tawala za mikoa Tanzania. Ni matumizi mabaya ya Rasilimali fedha na watu. Tugawanye halmashauri kadri ya uwezo wetu lakini siyo mikoa. Hata kwa watoa huduma wakubwa Kama polisi, tanesco na tra, wanaweza kujiorganize kiwilaya pia.
Tunapogawa mikoa, kikubwa kinachoangaliwa ni kuongezeka kwa utendaji kazi ambao utapelekea kuleta tija katika nyanja zote, kiuchumi, kiutawala(kisiasa) na kijamii
 
Kuugawa mkoa hakuongezi maendeleo bali mzigo kwa taiafa, huu mkoa ulishataka kugawanywa lakini ilishindikana sijui kwa nini ila walishaliongea hili bungeni, Tabora ina semekana ina mita za mraba 76,151. Licha ya kuwa na madini na kilimo cha tumbaku lakini ni mkoa maskini, shida itakuwa kwenye uongozi sio ukubwa maana una rasilimali za kutosha tu.
 
Tabora sehemu kubwa ni hifadhi ya misitu tu.
Hakuna haja ya kuigawanya eti papatikane mkoa usihadaike na ramani boss.
 
Mawazo yako mazuri mkuu, lakini bado haujatazama mfumo wa utawala wa nchi yetu, unaweza kufanikiwa kama ukibadilisha mfumo mzima wa utawala
YES ila mfumo huu ni sisi wenyewe tumeuweka,maana toka day one ya uhuru wetu tumeruhusu status ago iendelee,kweli kulikuwa na umuhimu wa nchi yetu iwe na mikoa zaidi ya 30?ya nini yote hii,mimi nimetokea makete Iringa ,je kulikuwa na umuhimu wa kuigawa wilaya ya Njombe mara Tatu?yaani Ludewa,Njombe,Makete?je tumeendelea zaidi ya kuwa na wilaya hizi tatu badala ya kuwa na Njombe pekee?je pesa zinazolipwa kwa watumishi wa makete,ludewa kuanzia ma DC hadi DED zisingeweza tumika kujenga mashule na hosp nzuri zaidi?halafu hadi leo kuna mtu ambaye ni middle class bado ana mawazo kama haya ya kugawanya nchi eti kuwa ndio kichocheo cha kuleta maendeleo!!,nimetulia huku Lingusenguse ninavua tu.
 
Kwenye tija hapo utoe mkoa wa Njombe,weka hiyo simiyu na Katavi
Kwa maana ya Jiografia, mikoa ya Tabora, Morogoro, Ruvuma na Lindi inastahili kugawanywa. Lakini tunaweza kufanya makosa kama yaliyofanyika kugawa mikoa ya Rukwa na Iringa. Mikoa mipya ya Njombe na Katavi zimeshindwa kuleta tija kiuchumi na kijamii. Na hii ni kwa sababu ya nature ya tawala za mikoa Tanzania. Utawala wa Tanzania tunahitaji kuwa na Halmshauri siyo mikoa wala wilaya.
 
Hili ni kwa ajili ya kuharakisha maendeleo, je kuna haja ya kuugawa mkoa wa Tabora tukapata Mikoa miwili, Nawasilisha hoja
Toa takwimu za mkoa kuhusu eneo lake, idadi ya watu, miundombinu ya usafiri (barabara, relic na ndege)na maeneo ya hifadhi (misitu na wanyamapori) kupata ulinganifu na mikoa mingine yenye sifa kama mkoa wa Tabora.

View attachment 1249710
Toa takwimu za mkoa kuhusu eneo lake, idadi ya watu, miundombinu ya usafiri (barabara, reli na ndege) na maeneo ya hifadhi (Misitu na wanyamapori) kupata ulinganifu na mikoa mingine yenye sifa kama za mkoa wa Tabora
 
Hili ni kwa ajili ya kuharakisha maendeleo, je kuna haja ya kuugawa mkoa wa Tabora tukapata Mikoa miwili, Nawasilisha hoja

View attachment 1249710
Tena hiyo Sikonge imekuwa wilaya miaka si zaidi ya kumi...Yaani hiyo toka Uhuru ilikuwa ni Tarafa ndani ya Wilaya ya Tabora Vijijini ambayo makao makuu yake yalikuwa Tabora Mjini.

Tabora ni kati ya mikoa iliyosahaulika sana kimaendeleo pamoja na kuwa kitovu ama kambi ya CCM ya kuzolea kura miaka nenda rudi.

Ni kati ya mikoa inayohitaji Maombi kwa kweli...maana jitihada za kawaida zilishindikana toka Uhuru enzi za Mwalimu...Maji safi na salama hasa wilaya ya Sikonge ni ndoto tena ya mchana..Umeme ndiyo umewaka miaka mitatu hivi tena vijiji vingi vya wilaya hii bado viko gizani.

Kwa sasa hivi ndiyo kwanza wanachi wa Wilaya hii wanapata barabara ya lami kuunganisha Wilaya hii na Tabora Mjini...ni kama mm 72 tu, lakini wameisubiri kwa miaka 58.

Yaani tangu Uhuru hizo km zilikuwa ni za kiwango cha matope...sasa as we speak lami hata bado haijakamilika 100% hadi Sikonge.

Wilaya ya Sikonge ni kati ya wilaya maskini mno hapa Tanzania; ina shida nyingi mno hata sijui hawa wananchi wake walimkosea nini mola wao. Hapo sijagusia Uchumi wa mwananchi mmoja mmoja, Elimu na Afya...utatoa chozi msomaji wangu.
 
Upeo wetu wa kufikiri ni wa ajabu kubwa,watanzania wanahitaji service delivery sio wingi wa mikoa au wilaya,elewa hili linasababisha kuwa serikali kubwa mno na gharama za kuiendesha zinakuwa kubwa,nikiwa Rais for one day ,nitahakikisha kufikia saa 4pm nchi nzima tumebakiwa na mikoa sita tu,na maamuzi yote makuu yatakuwa chini ya serikali hizi za majimbo,serikali kuu itaangalia maswala ya Fedha,ulinzi na usalama,home affairs tu,mambo mengine yataishia huko huko kwenye serikali za majimbo,kuanzia leseni za biashara,magari,udereva,majengo,etc etc .
Santeeee na majimbo yatakuwa
1.jimbo la kusini (utajumuisha mikoa mingapi kuunda jimbo hili ? )
2.jimbo la kaskazini (utajumuisha mikoa mingapi ili kuunda jimbo hili ?)
3.jimbo la mashariki(utajumuisha mikoa mingapi ili kuunda jimbo hili ?)
4.jimbo la magharibi(utajumuisha mikoa mingapi ili kuunda jimbo hili ?)

Hii inapunguza ukubwa wa serikali kwa kuwa na utitiri wa wakuu wa mikoa
Nalog off
 
Tena hiyo Sikonge imekuwa wilaya miaka si zaidi ya kumi...Yaani hiyo toka Uhuru ilikuwa ni Tarafa ndani ya Wilaya ya Tabora Vijijini ambayo makao makuu yake yalikuwa Tabora Mjini.

Tabora ni kati ya mikoa iliyosahaulika sana kimaendeleo pamoja na kuwa kitovu ama kambi ya CCM ya kuzolea kura miaka nenda rudi.

Ni kati ya mikoa inayohitaji Maombi kwa kweli...maana jitihada za kawaida zilishindikana toka Uhuru enzi za Mwalimu...Maji safi na salama hasa wilaya ya Sikonge ni ndoto tena ya mchana..Umeme ndiyo umewaka miaka mitatu hivi tena vijiji vingi vya wilaya hii bado viko gizani.

Kwa sasa hivi ndiyo kwanza wanachi wa Wilaya hii wanapata barabara ya lami kuunganisha Wilaya hii na Tabora Mjini...ni kama mm 72 tu, lakini wameisubiri kwa miaka 58.

Yaani tangu Uhuru hizo km zilikuwa ni za kiwango cha matope...sasa as we speak lami hata bado haijakamilika 100% hadi Sikonge.

Wilaya ya Sikonge ni kati ya wilaya maskini mno hapa Tanzania; ina shida nyingi mno hata sijui hawa wananchi wake walimkosea nini mola wao. Hapo sijagusia Uchumi wa mwananchi mmoja mmoja, Elimu na Afya...utatoa chozi msomaji wangu.
Mkuu sio sikonge tu, umeisahau wilaya ya Uyui, Urambo,Nzega yaani hadi unaona sasa Tabora imekosea wapi?
 
Kuugawa mkoa hakuongezi maendeleo bali mzigo kwa taiafa, huu mkoa ulishataka kugawanywa lakini ilishindikana sijui kwa nini ila walishaliongea hili bungeni, Tabora ina semekana ina mita za mraba 76,151. Licha ya kuwa na madini na kilimo cha tumbaku lakini ni mkoa maskini, shida itakuwa kwenye uongozi sio ukubwa maana una rasilimali za kutosha tu.
Kweli mkuu, ni mkoa ambao unaweza hata kujiendesha wenyewe kiuchumi, lakini kwanini unasahaulika? Tabora ukilima Tumbaku, Pamba, Alizeti lakini pia kuna madini. Hapa ndio tuangalie shida ipo wapi
 
tabora ugawanye nini sasa..ukame au?
Mkuu kwa karne hii mtu anapozungumza kwa akili iliyoelimika hawezi kumaliza mazungumzo bila kugusia teknolojia, Ukame sio shida , shida ni tunatatua vipi hii changamoto kwa kutumia teknolojia
 
Tabora sehemu kubwa ni hifadhi ya misitu tu.
Hakuna haja ya kuigawanya eti papatikane mkoa usihadaike na ramani boss.
Mkuu mara ya mwisho kufika Tabora ni lini? maana inawezekana hata ulifika au haujatembelea mkoa wote
 
Kwa maana ya Jiografia, mikoa ya Tabora, Morogoro, Ruvuma na Lindi inastahili kugawanywa. Lakini tunaweza kufanya makosa kama yaliyofanyika kugawa mikoa ya Rukwa na Iringa.

Mikoa mipya ya Njombe na Katavi zimeshindwa kuleta tija kiuchumi na kijamii. Na hii ni kwa sababu ya nature ya tawala za mikoa Tanzania. Utawala wa Tanzania tunahitaji kuwa na Halmshauri siyo mikoa wala wilaya.
Njombe hapana. Ni moja ya mikoa inayofanya uzuri kiuchumi.
 
Back
Top Bottom