Hili jamaa tuliambiwa kwamba lilikuwa bado na umri mdogo kushika pale mahali sisi tukafikri mwalimu alikuwa namaanisha umri wa kuzaliwa!! Kwa ufupi mwalimu alikuwa anamaanisha huyu bwana tulimfanyia upasuaji wa kumwekea kichwa na kwa vile hatukupata kichwa cha binadamu tulimwekea Koroma la nazi, hana akili ya kuongoza, hivyo hawezi kuwaongoza ninyi wadanganyika!! Sisi tukapuuza tukamwaga kula kwa wingi sasa tunayaona machungu yake!!
Anyway, asante Yesu bado miezi 7 tuondokane na huu udhia, hatutarudia tena, tumekoma!! Mkoa wa Pwani unastahili kupigwa Ban kwenye kinyang'anyiro cha kiti hicho maana tumejionea wenyewe! Hawa wabaki kushabikia tu vigodoro haya mambo makubwa hawawezi!! Hivi wanaposema kuboresha huduma huwa wametathmini kuona unapoongeza mkoa au wilaya huduma zinaboreshwa kwa kiwango gani? Hiyo fedha inayoenda kugharamia hizo ofisi ingepelekwa moja kwa moja kwa wananchi si ingesaida pa kubwa? Fikria gharama ya majengo yanayojengwa kwa ajili ya ofisi na nyumba za maafisa wa serikali, magari ya maana yanayonunuliwa (maana hili Punda lilishamshinda, mbona kila uchao tunaona Ma-VX). Mishahara ya watumishi wapya (maana hapa kunakuwa na duplicate ya ule mkoa wa zamani). Sasa hizi gharama jamani tunaziweza sisi? Au kumbebesha mwananchi mzigo asiostahili? Wa-Tz tujifunze kutokana na haya makosa!