Mkoa wa Tabora kugawanywa na kuwa mikoa miwili

Mkoa wa Tabora kugawanywa na kuwa mikoa miwili

Liwale nayo sasa itakuwa mkoa wa wanyama pori kwani ina eneo kubwa.
Aibu sana.
Hata kuiweka Tanzania kwenye ramani inakua sheeeder!!
Ukiwajengea watu fikra za kujigawa gawa kwa maana kuwa ndio maendeeo kuna siku Lindi ,Mtwara na Songea , Kigoma Katavi na Rukwa nao watadai ziwe nchi kamili ili wapate maendeleo.
 
Hili ni kwa ajili ya kuharakisha maendeleo, je kuna haja ya kuugawa mkoa wa Tabora tukapata Mikoa miwili, Nawasilisha hoja



tabora ramani.png
 
Kwa maana ya Jiografia, mikoa ya Tabora, Morogoro, Ruvuma na Lindi inastahili kugawanywa. Lakini tunaweza kufanya makosa kama yaliyofanyika kugawa mikoa ya Rukwa na Iringa.

Mikoa mipya ya Njombe na Katavi zimeshindwa kuleta tija kiuchumi na kijamii. Na hii ni kwa sababu ya nature ya tawala za mikoa Tanzania. Utawala wa Tanzania tunahitaji kuwa na Halmshauri siyo mikoa wala wilaya.
 
Ungeweka km2 maana kwa asiyeifahamu Tabora hiyo ramani haina ukubwa wowote!
 
Kugawanywa mikoa Tanzania, haipeleki huduma yoyote karibu na wananchi. Secretariat za mikoa hazina kazi kivile. Wananchi hupata huduma nyingi katika ngazi ya halmashauri na kidoogo kwa DC.

Hatuhitaji tawala za mikoa Tanzania. Ni matumizi mabaya ya Rasilimali fedha na watu. Tugawanye halmashauri kadri ya uwezo wetu lakini siyo mikoa. Hata kwa watoa huduma wakubwa Kama polisi, Tanesco na TRA, wanaweza kujiorganize kiwilaya pia.
 
Upeo wetu wa kufikiri ni wa ajabu kubwa,watanzania wanahitaji service delivery sio wingi wa mikoa au wilaya,elewa hili linasababisha kuwa serikali kubwa mno na gharama za kuiendesha zinakuwa kubwa,nikiwa Rais for one day ,nitahakikisha kufikia saa 4pm nchi nzima tumebakiwa na mikoa sita tu.

Maamuzi yote makuu yatakuwa chini ya serikali hizi za majimbo,serikali kuu itaangalia maswala ya Fedha,ulinzi na usalama,home affairs tu,mambo mengine yataishia huko huko kwenye serikali za majimbo,kuanzia leseni za biashara,magari,udereva,majengo,etc etc .
 
Upeo wetu wa kufikiri ni wa ajabu kubwa,watanzania wanahitaji service delivery sio wingi wa mikoa au wilaya,elewa hili linasababisha kuwa serikali kubwa mno na gharama za kuiendesha zinakuwa kubwa,nikiwa Rais for one day ,nitahakikisha kufikia saa 4pm nchi nzima tumebakiwa na mikoa sita tu,na maamuzi yote makuu yatakuwa chini ya serikali hizi za majimbo,serikali kuu itaangalia maswala ya Fedha,ulinzi na usalama,home affairs tu,mambo mengine yataishia huko huko kwenye serikali za majimbo,kuanzia leseni za biashara,magari,udereva,majengo,etc etc .
Mawazo yako mazuri mkuu, lakini bado haujatazama mfumo wa utawala wa nchi yetu, unaweza kufanikiwa kama ukibadilisha mfumo mzima wa utawala
 
Kwa maana ya Jiografia, mikoa ya Tabora, Morogoro, Ruvuma na Lindi inastahili kugawanywa. Lakini tunaweza kufanya makosa kama yaliyofanyika kugawa mikoa ya Rukwa na Iringa. Mikoa mipya ya Njombe na Katavi zimeshindwa kuleta tija kiuchumi na kijamii. Na hii ni kwa sababu ya nature ya tawala za mikoa Tanzania. Utawala wa Tanzania tunahitaji kuwa na Halmshauri siyo mikoa wala wilaya.
Wazo zuri mkuu
 
Back
Top Bottom