Mkong'oto wanaotembezewa wastaafu wanaotumia mafao kuanzisha biashara ni funzo kwamba uzoefu ni muhimu, Biashara zinabuma stress zinawamaliza wazee !

Mkong'oto wanaotembezewa wastaafu wanaotumia mafao kuanzisha biashara ni funzo kwamba uzoefu ni muhimu, Biashara zinabuma stress zinawamaliza wazee !

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Wafanyakazi wa serikalini na baadhi ya makampuni huwa wanakatwa pesa kila mwezi kwenye mishahara yao kwa ajili ya malipo yao ya mafao ya kujikimu wakistaafu.

Mafao wanayopewa kwa mkupuo moja huwa ni fedha nyingi sana mfano milioni 200, 150, 100, 50, 30, n.k. kulingana na kazi walizofanya.

Wengi wanapopata pesa hizi, matumizi ya mwanzoni hununua gari, kujenga / kukarabati nyumba, kujaza fenicha, n.k. Baada ya hapo wazo linawajia la kufanya biashara lasivyo pesa zitaisha.

Biashara ni kitu kipana, Mbali na fedha za mtaji biashara inahitaji Ujuzi, Uzoefu, Maarifa, Connections na Taarifa za Kutosha, kuvipata vitu hivi kwa inabidi uwe na biashara miaka takribani 10 wakati upo kazini kusudi ukistafu tayari una experience ya kutosha, Ukipewa mafao huendi kuanza, unaenda kujipanua.

Tatizo linapokuja ni kwamba wastaafu wengi walizoea mishahara na posho hawana uzoefu wa Biashara, Hapo ndipo ukikosea step mkong'oto haukwepeki.

Mzee anaona anunue bajaji / bodaboda bila kuzijua stress za vijana walivyo wasumbufu, Mzee anafungua duka kubwa bila kujua ushindani ulivyo, Mzee anafungua biashara bila kujali location, wengine wanaugulia maumivu kimya kimya ya kuingizwa chaka na watoto wa mjini kama ilivyo kwa wafanyabiashara wengi wageni, n.k.

Mafao yote yamedumbukizwa kwenye biashara ambazo hawana uzoefu nazo, stress zinaanza kuwatafuna kwa speed ya 4g kuanzia changamoto za wafanyakazi wezi, hawajakaa sawa taskforce ya Tra wanachomoa kodi zao kwenye account za benki, washindani wanauza mzigo kwa bei chee, n.k.
 
Wengi wao maisha yao yote walikuwa wanategemea mishahara ama kuwa na zile biashara za kutesti .

Matokeo yake wanapostaafu wakiwa kwenye 50s au 60s inabidi waanze kujitaufta upya kwa mafao wanayopewa.

Kwa wastani wengi huwa wanaambulia mafao milioni 20 hadi 50

Hapo kichwa huwa kinawaka moto wafanye biashara ipi, huwa waan utofauti mdogo sana na wanachuo wanaoingia mtaani kwa mara ya kwanza kuanza biashara, walichotofautiana ni mitaji tu.

Mzee anaona anunue bajaji / bodaboda bila kuzijua stress za vijana walivyo wasumbufu, Mzee anafungua duka anaweka mtaji wa milioni 50 bila kujua ushindani ulivyo, Mzee anaingizwa mjini na watoto wa mjini, n.k.

Biashra zikifiliska, presha na stress huwatafuna bila huruma
Tatizo lao wazee wetu wabishi sana
Kuna mtu wa karibu alilamba 100m nikampa mpango kazi akasema Jane anataka kunitapeli
As am typing ndani ya miaka minne hii hana hata ela ya kula
 
Mmh hapana nliona mambo ni mchanganyiko asee nikimpigia sijui alikua anahisi nataka hela zake, anapokea hasemi halooo akipokea "eeh unasemaje" nikaona hapana.....

Mi mbona sitoleagi mate mali ya mtu yoyote nkaamua kukaa kimya kwanza.
Bi mdashi alishajiona billionaire hivyo akawa anawagwaya wanaye anahisi mtqmfirisi
 
Back
Top Bottom