Mkong'oto wanaotembezewa wastaafu wanaotumia mafao kuanzisha biashara ni funzo kwamba uzoefu ni muhimu, Biashara zinabuma stress zinawamaliza wazee !

Hivi hizi hasira zote juu ya wastasfu za nini? Ni wivu au ujinga wenu? Je mtu hana haki ya kutumia atakavyo pesa itokanayo na jasho lake? Mbona nyie mnaanzisha biashara na zinabuma? Kwani na nyie ni wastasfu.
Mbona na ninyi mkipata hela mnahonga ?Kila mtu ashinde mechi zake .Wastaafu wana haki ya kutumia watakavyo hela zao.Ninyi hamna haki ya kuwapangia nini wafanye kwakiwa sio nyie mliozisotea hizo hela.
Mstaafu mbona povu.😄
 
650.000/- kwa kila Mwezi kwa uwekezaji wa mil 50 si haba. Ni kama unajilipa mshahara. Nadhani wastaafu wanaopata mafao ya mil 90-100 unawafaa sana hii. Kwa sababu pia huwa wanapata ile penshion ya kila miezi 3; maisha yanaenda kuliko kuishi kwa stress
Wengi wanafanya hivyo siku hizi... Mtu anapata 150m zile za mkupuo, anaigawa 3 x 50. Halafu inawekezwa kwa namna hiyo. Mtu akiongeza na monthly pension, anaishi vizuri sana
 
Ulaya unafananisha na Africa ambayo wananchi wake asilimia 80% masikini wanatafuta pesa Kwa jasho na damu yaani ulaya mpaka wanapata na pesa za kutoa misaada Africa inamaana maisha ya raia wao ni mazuri sababu pesa zinazoletwa kama misaada ni Kodi za wananchi wa nchi husika hivi unaakili timamu kweli
Nataka tufike huko. Tuna kila kitu cha kuweza kuwafikia na hata kuwazidi, kasoro yetu ni uongozi bora ambao ndiyo tatizo nililolijadili hapa. Upo?
 
650.000/- kwa kila Mwezi kwa uwekezaji wa mil 50 si haba. Ni kama unajilipa mshahara. Nadhani wastaafu wanaopata mafao ya mil 90-100 unawafaa sana hii. Kwa sababu pia huwa wanapata ile penshion ya kila miezi 3; maisha yanaenda kuliko kuishi kwa stress
Shida ni pale ukizikamata. unaona 150M ni pesa nyingi sana. yaani unachanganyikiwa. Ukiweka 100M kwenye hati fungani hukosi 15M kwa mwaka. Hapo ni 1.25M kwa mwezi on average. Hiyo pesa ukiiwaza wakati ukiwa na 150M mkononi unaona kama hela ya karanga. ...mzee hiyo 150M ikiisha, hiyo 1.25M utaitafuta kwa tochi bila mafanikio.
Mstaafu wa kijijini ukiwa na gurantee ya kupata 1m kila mwezi mbona utaishi vizuri tuu?
 
Si wastaafu peke yao. Kuna vijana wanauza nyumba za urithi na wengine hupata hata milioni mia moja.
Hizi pesa zinawarusha akili. Wenyewe wanasema anasafisha nyota. Atanunua gari. Matumizi yanafikia laki nne kwa siku. Baada ya miezi sita mpaka mwaka pesa ishakwisha. Anauza gari, luninga na vyengine kwa robo ya bei.
Kweli kabisa
 
Katika yote kuna Mambo Kadhaa dhahiri
1.Mtu ambaye amekuwa kwenye Ajira,akiingia biashara tofauti na Ajira yake,anatakiwa awe na Ujuzi,Maarifa na Taarifa za Kutosha Juu ya Biashara.Mtaji ni kitu kipqna Sana,mbali na fedha.Ikiwezekana awe ameanza Biashara Miaka 5 Hadi 10 Wakati akiwa kazini.Kusudi akistafu tayari anajua Moto wa Biashara
2.Watu wengi hata waliochangia mada Hawana Ufahamu wa Fedha.Yaani Elimu ya Fedha (Tofauti na uhasibu au finance).Elimu hii unatakiwa uwe nayo toka utotoni,uizoee Fedha,ujue kuweka akiba na yote yanayohusu Fedha.Ndiyo maana hata ungepewa 10b kama huna Elimu hii zitaisha.
3.Unapostafu mwili na akili huwa imechoka.Mikikimikiki ya biashara inahitaji akili fresh,Biashara zina dynamics nyingi Tofauti na Ajira.
4.Kuna Maeneo Salama ya Kuweka Fedha baada ya kustaafu Mfano UTT au Dhamana za Serikali.Lakini pia Nyumba za a Kupangisha zimekuwa Maeneo ya Msaada Kwa wastafu.
5.Ni Vema Mtu anapostafu kufanya biashara Katika Eneo analolimudu na aanze mapema,Mfano kama taaluma yako ni Kada ya Afya,usicheze mbali na hapo.Binafsi ni Mfamasia na nishaendesha Biashara ya Pharmacy Miaka 7 Miaka ya Nyuma na Nina Leseni,hivyo hiyo ndiyo Biashara Hadi Kufa.Kama ni Mwalimu asione haya kuanzisha hata nursery au Kindergarten.Mhasibu afanye uhasibu hata kama ni consultant.Mwanasheria asione aibu Kubeba begi afanye uwakili.Mbona Msajiri wa Zamani wa Vyama vya Siasa alichukua begi na koti lake akaingia Kortini tena.Watu hawajui hii hata Nyerere alianzisha Mwalimu Nyerere Foundation ili awe anaitumia uzoefu wake kwenye Sasa Kuendelea Kupiga Kazi.Nikiwa JKT nilikuwa Kambi ambayo tulikuwa na hukumu la kumjengea Nyumba pale Butiama.Kuna siku alikuwa akienda Shamba Kulima na Wasaidizi wale,kisha Mkutano ikija anapotea kama wiki Kadhaa.Chezea ndani ya Eneo Lako la competency.
6.Kuna ajali ya Makazi,wale ambao hawajakuwa na Makazi Pesa zinakwenda huko.Ingekuwa Vema Miaka 10 kabla ya kustaafu Nyumba iwe ishaisha.Usihangaike na Nyumba tena.
Mwisho hii ni yangu:Waisraeli Hawana msamiati wa kustaafu,ila unabadili Kazi au Shughuli.Ndiyo maana ukisoma Biblia hujawahi Kuona nabii au Kuhani au wafalme wanastafu.Usione aibu kufanya kitu kurahisisha maisha yako.Kama kuna Shamba au Mifugo itunze.Mbona babu zetu hawakuwa na pesheni na wameishi Hadi kuwa wakongwe.
NB:Kama Wewe ni kijana tumia Changamoto hii unayoiona Kuepuka hayo makosa ya watangulizi wako.Wala usikae kusimulia madhira Yao.Usije kukaa kihasara unasubiri mzazi wako akupe portion ya pensheni wala usianze kumpangia,achilia mbali kumshauri maana Wewe Siyo financial advisor wake.
 
We mjinga nini unataka mtu alipwe pesa inayokaribia mshahara Ili sisi wananchi tuhenyeke yeye awe anapata hela kirahisi tu boya wewe unafikiri hizo hela wanatoa ccm au raia Hali ya chini ndio Kodi zinapelekwa Kwa hao wazee
Kama huelewi kitu ni bora kunyamaza.
Wafanyakazi wote wa umma na private hukatwa pesa kila mwezi kwenye mishahara yao kwa ajili ya malipo yao wakistaafu.
Kwa hiyo kodi yako haitumiki kuwalipa waastaafu pension zao za kila mwezi.
 
Ni comment iliyoshiba sana, umemaliza kila kitu hapa
 
We mjinga nini unataka mtu alipwe pesa inayokaribia mshahara Ili sisi wananchi tuhenyeke yeye awe anapata hela kirahisi tu boya wewe unafikiri hizo hela wanatoa ccm au raia Hali ya chini ndio Kodi zinapelekwa Kwa hao wazee
Wastaafu wanalipwa hela yao walioiwekeza miaka yote waliokuwa kazini
 
Back
Top Bottom