Mkong'oto wanaotembezewa wastaafu wanaotumia mafao kuanzisha biashara ni funzo kwamba uzoefu ni muhimu, Biashara zinabuma stress zinawamaliza wazee !

Mkong'oto wanaotembezewa wastaafu wanaotumia mafao kuanzisha biashara ni funzo kwamba uzoefu ni muhimu, Biashara zinabuma stress zinawamaliza wazee !

Sijawahi Kutoa Mawazo Kwenye Hii APP ila Kutokana Na Uzito Wa Huu Ujumbe Ngoja Niweke Neno...✍️

Asilimia Kubwa Tumejifunza Maisha Ya Wastaafu Kupitia Watu Wetu Wa Karibu Inaweza Kuwa Mzazi Wako Au Mzazi Wa Rafiki Yako Au Jirani Yako N.k...✍️

Mawazo Ya Wadau Ni Mazuri Ila Na Mimi Nitaorodhesha Sababu Zinazofanya Wastaafu Wayumbe Baada Ya Kustaafu...👇👇👇

1.Wastaafu Wengi Baada Ya Kustaafu Wanataka Watengeneze Faida Katika Biashara Zao Zinazolingana Na Vipato Vyao Vya Kazini Yaani Mfano Alikua Analipwa Milion 1 Au 2 Au 3 Basi Atalazimisha Kufanya Biashara Zenye Mfanano Wa Faida Na Vipato Vyao Vya Kazini...

2.Tamaa Ya Faida Kubwa Tena Ya Haraka Na Hii Inasababishwa Na Kutaka Kuaminisha Watu Kwamba Sio Mjonge Yaani Amestaafu Ila Biashara Anayoifanya Niya Hadhi Ya Kazi Yake...

3.Baada Ya Kupambania Biashara Isimame Wao Wanapambana Kuaminisha Jamii Kuwa Yuko Vizuri Kwahiyo Hapo Analazimika Kuishi Maisha Ya Bajeti Ya Juu Asionekane Mnyonge...

4.Wastaafu Wengi Hawakubali Kuwa Wameshastaafu Na Wameingia Kwenye Maisha Mengine Bado Wanalazimisha Kuishi Maisha Yaleyale Ya Kazini Kwahiyo Hawezi Kubali Kujishusha Ili Apande Wao Wanataka Kubakia Kiwango Kilekile Cha Maisha Atakama Wanajifirisi...

5.Kwa Kumalizia Wastaafu Wengi Hawana Nidhamu Ya Pesa Yaani Kama Vile Walivyokua Wanaishi Maisha Ya Mikopo Kazini Yaani Anachukua Pesa Na Kuimaliza Huku Akiamini Bado Nafasi Ipo Ya Kusawazisha Akili Hiyo Hiyo Wanakuja Kuitumia Kwenye Pesa Ya Mwisho Ambayo Haina Marekebisho Hapo Ndio Wanajikuta Baada Ya Pesa Kuisha Hawana Amani Tena Maana Washajikatia Tamaa Kwa Kuona Hawana Njia Nyingine Ya Kupata Pesa Kwa Mkupuo Ndio Maana Wanaishia Kurudi Kwenye Kukopa Kupitia Pensheni Zao Wakiamini Maisha Yatarudi Kuwa Sawa Kumbe Ni Kujiongezea Mzigo Juu Ya Mzigo...

NB: AYA NI MAWAZO YANGU KWAHIYO NIMECHANGIA KAMA WADAU WENGINE...
 
Back
Top Bottom