Mkono wa Edward Manyama wasababisha mchezo kuvunjwa

Soloma TV Online

Senior Member
Joined
Jun 26, 2023
Posts
104
Reaction score
291
Mchezaji wa Azam FC Edward Manyama amevunjika mkono kwenye mchezo wa kirafiki wa Kimataifa dhidi ya Stade Tunisien uliochezwa huko Tunisia.

Katika mchezo huo Refa alishindwa kuumudu kwa mujibu wa Afisa Habari wa Timu hiyo Hasheem Ibwe ambaye kaenda mbali zaidi kwa kudai kuwa haukuwa mchezo wa kirafiki. Na mpaka unavunjwa tayari Stade Tunisien walikuwa mbele kwa magoli 4 dhidi ya 1 la Azam.

Goli la 4 ndiyo chanzo cha mzozo kwani Azam FC hawakukubaliana.
 
Aloooooooooo
azam tantalila nyingi utendaji sifuri
walitaka kututambia na preseason yao uturuki ila wameufyata fyuuuuuu
 
Genta njoo uone jamaa zako wamechukua mpira wao wamesepa.
 
Bakhresa bora akaichukue Simba tu
 
Ushauri wangu waachane na Mchezo ujao dhini ya CA, watavunjwa MIGUU haswa.
 
Azam wangeendelea na mchezo wangepigwa zaidi ya bao 20 - 1
Kocha Dabo aonyeshwe mlango wa kutokea kabla mambo kuharibika zaidi
 
Kocha amefeli pakubwa,mchezaji aliyeumia angetolewa nje....Game uendelee...hiyo sio picha nzuri mbele ya macho ya watu mechi ya kirafiki sio ligi.

Ila Azam sijui wanafeli wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…