Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
SALUM ABDALLAH NA CUBAN MARIMBA CHACHA BAND
Kuna wakati huwa kuna mambo nayajua lakini huogopo kueleza kwa hofu kuwa wasije watu wakaniita muongo.
Naogopa wataniita muongo kwa sababu inawezekanaje mtu mmoja akawa kila mtu yeye anamjua, kamuona na anajua historia yake?
Ukimtaja Frank Humplick mimi namjua na nikienda hadi nyumbani kwake Lushoto, Peter Colmore namjua nk. nk.
Frank Humplick alikuwa mwanamuziki mkubwa akiimba na dada zake katika miaka ya 1950 na mtu aliyejenga carrier yake ni Peter Colmore kama alivyojenga za wengine mfano wa Eduardo Masengo.
Salum Abdallah alikuwa rafiki ya baba yangu Said Salum Abdallah.
Nyimbo ya Salum Abdalla, "Mkono wa Eid," ndiyo ilikuwa ikipigwa TBC siku ya Eid tulipokuwa watoto tukiusikia imewekwa tunajua kumekucha Eid imeshaingia.
Nyimbo hii inaanza kwa kupulizwa tarumbeta zilizotiwa ''mute,'' chombo kinachobadili sauti ya tarumbeta kuifanya iwe ''sharp.''
Naamini mpiga tarumbeta hii ni wanafunzi wa Father Canute mmeshionari aliyewafundisha muziki na kupuliza tarumbeta vijana wengi wa Morogoro.
Baba yangu alipata kunihadithia historia ya Father Canute.
Ukisikiliza muziki wa Morogoro Jazz wa miaka ya 1950 utakuta umetawalisa sana na tarumbeta zilizokuwa zikipulizwa kwa ufundi mkuwa.
Nimemuona kwa macho yangu Salum Abdallah mwaka wa 1964 Mtaa wa Aggrey na Nyamwezi huku Mtaa wa Swahili ilipokuwa Cuban Marimba Branch.
Nilikuwa napita nje ya club na Salum Abdallah alikuwa ndani milango ilikuwa wazi na yeye na mtu mwingine walikuwa wako pale wanapiga magitaa na Salum Abdallah akiiimba.
Sikubanduka hapo.
Mwaka wa pili 1965 Salum Abdallah akafariki.
Iko siku nimekwenda likizo Tabora kwa babu yangu.
Niko uani na bibi yangu Bi. Zena bint Farijala radio inapiga nyimbo ya Salum Abdallah.
Bibi akaniona nimetulia namsikiliza Salum Abdallah na Cuban Marimba kwa utulivu mkubwa.
Bibi akaniambia, "Salum Abdallah alikuwa rafiki ya baba yako na alikuwa kila akija Tabora na bendi yake lazima aje hapa kumsalimia baba yako."
Hii ilikua miaka ya 1950.
Nimekuwa nikimsikiliza Salum Abdallah udogoni kwangu wakati huo akirekodi na kampuni inaitwa, "Mzuri."
Kampuni hii ndiyo ikirekodi bendi nyingi za Tanganyika pamoja na Kiko Kids ya Tabora.
Ilitokea katika miaka hii ya karibuni kutafutwa na wamiliki wa kampuni hii hivi sasa wako Ujerumani wakitaka taarifa za Salum Zahoro na wakati ule alikuwa yu hai.
Hawa Wajeruamani ndiyo walionunua hati miliki ya kampuzi ya Mzuri.
Niliwaeleza kile nilichojua.
Baada ya kukamilisha walichokuwa wakifanya waliniletea album la "vinyl" yaani muziki uliorekodiwa katika santuri si CD ukiwa kwenye nembo ya "Mzuri."
Hii nembo ilinirudisha nyuma mwaka wa 1957 nikiwa na umri wa miaka mitano na nikimsikiliza Salum Abdallah katika gramophone iliyokuwapo nyumbani kwetu.