Mkopo kwa dhamana ya nyumba, Msaada wenye Nyumba

Ni kweli kabisa hata sisi wenyewe yalitaka kutufika hayo. Tulinunua nyumba kumbe hati ameichukulia mkopo benki na akatuahidi pindi tungempa asilimia 30 angekwenda kumalizia mkopo ili tumaliziane nyingine na kutukabidhi nyumba. Basi hapo ndipo kimbembe kilipoanza, tulilipa ile asilimia 30 zikaenda na kumi nyingine sita jamaa ameingia mitini hataki kulipa. Mwisho ilikuwa kuwekana ndani mahabusu na kwa vitisho vikubwa ndio alimalizia deni lile na kutukabidhi hati (tuliandikiana kwa mwanasheria).

Kwa hivyo mambo hayo uyasikie tu nje lakini mtu asiwahi kujaribu kufanya hivyo hata kwa ndugu yake mwenyewe, labda akubali kuitoa kafara hiyo nyumba.
 
Bank hawataki dhamana ya nyumba ya mtu asie familia yako kwahiyo wameikataa nyumba na kusema ni lazima nyumba iwe ya Baba,mama,mtoto,mke,mume. na si nnje ya hapo.
Nakubaliana na Bank maana ukiweka ya MTU BAKI hutoona uchungu wa kulipa lakini kama ya NDUGU yako itakulazimu tu kulipa.
 
Samahani naomba kuuliza kiwango Cha mwisho Cha mkopo wa bank ni kiasi gani ..
Pia ni vigezo gan hivyo muhimu walivyokutajia.
Na je kama una nyumba Ila hivyo vigezo vyengine huna inatosha kukopea??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…