Mkopo kwa dhamana ya nyumba, Msaada wenye Nyumba

Mkopo kwa dhamana ya nyumba, Msaada wenye Nyumba

Yule Mbunge mwenye PhD huku akiwa na elimu ya darasa la 7 aliwahi kumfanyia ndezi mmoja kule Mbezi DSM kitu cha aina hii hii. Kilichompata yule ndezi, hatokuja kukisahau kamwe.

Jamaa alivuta mkopo benki kwa kutumia hati ya nyumba ya ghorofa moja Ndezi kule Mbezi! Halafu baada ya kuvuta mkopo akawa harejeshi marejesho. Benki ikaja kupiga mnada nyumba, Ndezi akajikuta ameduwaa tu na kushindwa cha kufanya.
Ni kweli kabisa hata sisi wenyewe yalitaka kutufika hayo. Tulinunua nyumba kumbe hati ameichukulia mkopo benki na akatuahidi pindi tungempa asilimia 30 angekwenda kumalizia mkopo ili tumaliziane nyingine na kutukabidhi nyumba. Basi hapo ndipo kimbembe kilipoanza, tulilipa ile asilimia 30 zikaenda na kumi nyingine sita jamaa ameingia mitini hataki kulipa. Mwisho ilikuwa kuwekana ndani mahabusu na kwa vitisho vikubwa ndio alimalizia deni lile na kutukabidhi hati (tuliandikiana kwa mwanasheria).

Kwa hivyo mambo hayo uyasikie tu nje lakini mtu asiwahi kujaribu kufanya hivyo hata kwa ndugu yake mwenyewe, labda akubali kuitoa kafara hiyo nyumba.
 
Bank hawataki dhamana ya nyumba ya mtu asie familia yako kwahiyo wameikataa nyumba na kusema ni lazima nyumba iwe ya Baba,mama,mtoto,mke,mume. na si nnje ya hapo.
Nakubaliana na Bank maana ukiweka ya MTU BAKI hutoona uchungu wa kulipa lakini kama ya NDUGU yako itakulazimu tu kulipa.
 
Habari zenu wana jamiii, ni matumaini yangu mu wazima wa afya tele.

Nina Shida ya Pesa ya dharura nimejaribu kukopa kwa watu binafsi hawana, katika taasisi nao wanahitaji dhamana (hasa nyumba).

Nimefika Bank CRDB nimewambia hitaji langu,wakaniambia mahitaji kwa mfanyabiashara kama mimi, Vyote walivyo taja ninavyo na vinapatikana 100%

Kitu ambacho mpaka sasa kinanikosesha huu Mkopo ni DHAMANA ya nyumba.

Kiwanja ninacho lakini hawataki kiwanja ambacho hakijaendelezwa na mimi sijajenga.

Hivyo wameniambia nitafute mdhamini atakaeweza nidhamini mwenye Nyumba.

Nimekileta HAPA JamiiForums nikiamini kuja watu wengi ambao mpo mtaweza nisaidia katika hili.

Nina uhitaji wa Mil.10 lakini CRDB wameangalia Account na kusema wanaweza nipa up to 20Mil.

Kwa atakae nidhamini nilikua nimepanga Kumpa 3m (kama asante) hiii nitampa yeye na hatoirudsha.

Kurudisha mkopo Aniachie Mimi nitaurudsha wote.

Au

Nichukue 20m tugawane 50/50 lakini kurejesha turejeshe wote "tusaidiane"

Naomba kwa yeyote anaeweza nisaidia nitashukuru hata kama Si kwa nyumba basi mtu atakae weza nisaidia mahali naweza jidhamini kwa biashara yangu na mali zangu zingine nikapata huo mkopo nitashukuru pia.

Hitaji Langu kubwa ni 10m TU. Asante kwa yeyote atakaeweza nisaidia fanikisha hili jambo.

MREJESHO :

Si kila mtu ana mashaka kuna watu wana nia ya kusaidia wenye uhitaji. Nimefanikiwa kupata mtu wa kunipa Nyumba yenye HATI lakini kikwazo kikawa BANK tena.

Bank hawataki dhamana ya nyumba ya mtu asie familia yako kwahiyo wameikataa nyumba na kusema ni lazima nyumba iwe ya Baba,mama,mtoto,mke,mume. na si nnje ya hapo.

Asante kwa Aliejitoa na Asante kwa waliotilia shaka.
Samahani naomba kuuliza kiwango Cha mwisho Cha mkopo wa bank ni kiasi gani ..
Pia ni vigezo gan hivyo muhimu walivyokutajia.
Na je kama una nyumba Ila hivyo vigezo vyengine huna inatosha kukopea??
 
Back
Top Bottom