Mkopo milioni 1

Mkopo milioni 1

Sawia

Senior Member
Joined
Feb 9, 2013
Posts
129
Reaction score
40
Waungwana naomba mwenye kukopesha kwa riba nafuu anikope mil. 1 niwekeze kwenye biashara ya duka la chakula. Nina uwezo wa kurejesha laki 4 kila mwezi kutoka kwenye mshahara wangu, pia napata vi safari vya hapa na pale kazini ambavyo vinanipatia posho itakayosaidia kumaliza deni haraka huku nikizungusha pesa ya mkopo kwenye biashara. Nataka nilipe deni lote na riba ndani ya miezi 4. Sina dhamana isiyohamishika wala gari isipokuwa mshahara wangu tu na pia biashara bado mpya hivyo siwezi kukopa benk wala taasisi za fedha kwa sasa. Yeyote anayeweza kunikopesha aniPM. Nipo Magomeni DSM.
 
Kama unaweza kurejesha laki nne kwamwezi,kwanini uangaike namkopo utakao kunyima usingizi? Balance matumizi yako ili uweze kuwa na saving yalaaki tatu nanusu kwamwezi ndani yamiezi mitatu tu utakuwa umepata mtaji.
Hayo maoni yangu tu
 
Kwa mujibu wa maelezo yako hiyo pesa waweza ipata ndani ya siku 60 sasa kwanini uhangaike na mikopo? Riba ya chini siku hizi ni laki 3 kwakila million 1

~~~Hiyo biashara una uzoefu nayo? Una vitendea kazi tayari? Fremu/chumba, mizani friji, mirija na vipimio, mshahara wa kwanza wa mfanyakazi, vibali kama leseni nk, umeme maji nk! Hapo bado mzigo wa kuanzia kazi na usafiri pia

Milioni moja kwa maisha haya ni pesa ya kufungua genge na si duka LA vyakula kwa muktadha wako
 
Maoni yako ni mazuri mkuu. Ila ajira yangu ni ya part time kwenye project ambayo bajeti yake inatumwa kwa miezi na baada ya hiyo miezi ripoti inaandikwa na kusubiri bajeti nyingine ya miezi 4 inayofuata iidhinishwe.

Changamoto ni miezi ya kusubiri kutumiwa budget nyingine maana mfadhili wa huu mradi anachelewa sana awamu iliyopita tumesubiri miezi 5 na pesa inapoingia tunaanza kusaini upya hiyo miezi ya kusubiri haimo kwenye hesabu za malipo japo tupo kwenye mkataba wa miaka 3. Wakati wa kusubiri nilitumia akiba yangu yote sasa hivi hofu imeniingia hali ikijirudia. Naona bora nianze kupata mahali pa kuzungusha huo mshahara na kujishikiza mapema.
 
Kwa mujibu wa maelezo yako hiyo pesa waweza ipata ndani ya siku 60 sasa kwanini uhangaike na mikopo? Riba ya chini siku hizi ni laki 3 kwakila million 1

~~~Hiyo biashara una uzoefu nayo? Una vitendea kazi tayari? Fremu/chumba, mizani friji, mirija na vipimio, mshahara wa kwanza wa mfanyakazi, vibali kama leseni nk, umeme maji nk! Hapo bado mzigo wa kuanzia kazi na usafiri pia

Milioni moja kwa maisha haya ni pesa ya kufungua genge na si duka LA vyakula kwa muktadha wako

Ajira yangu ni ya part time kwenye project ambayo bajeti yake inatumwa kwa miezi 4 na baada ya hiyo miezi 4 ripoti inaandikwa na kusubiri bajeti nyingine ya miezi 4 inayofuata iidhinishwe.

Changamoto ni miezi ya kusubiri kutumiwa budget nyingine maana mfadhili wa huu mradi anachelewa sana, awamu iliyopita tumesubiri miezi 5 na pesa inapoingia tunaanza kusaini upya, hiyo miezi ya kusubiri haimo kwenye hesabu za malipo japo tupo kwenye mkataba wa miaka 3. Wakati wa kusubiri nilitumia akiba yangu yote, sasa hivi hofu imeniingia hali ikijirudia. Naona bora nianze kupata mahali pa kuzungusha huo mshahara na kujishikiza mapema.

Fremu ya duka ninayo pamoja na friji na mizani. Jamaa yangu alikuwa akifanyia biashara hapa kabla hajajenga na kuhamia kwake Kimara ambapo amefungua duka lingine huko huko karibu na anapoishi na kuhamisha bidhaa zake za dukani. Wakati akiishi hapa nilikuwa nikimsaidia kuuza dukani na hata nilipopata hii ajira yangu ambayo nina miezi 10 sasa nimekuwa nikiendelea kumsaidia kuuza kuanzia alasiri nikitoka kazini hadi usiku. Hivyo ameniachia vitu vichache vya kwake vya kuanzia. Kinachohitajika ni bajeti ya kununua bidhaa za biashara tu kwa uchache ili mzunguko wa biashara ukae sawa wakati naendelea kuongezea kidogo kidogo kutoka kwenye kujibana na posho zangu kidogo za safari nitakazokuwa nikipangiwa huku mshahara ukilipia deni. Uzoefu ninao ila in a long run nitahitaji msaidizi kipindi nipo kazini ama safarini.
 
Hapo sawa kwa 1m unaweza kujibana ukaanza
 
Back
Top Bottom