HOJA Mkopo unanitesa sana, si jambo rahisi kama wengi wanavyofikiria

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Mikopo si jambo rahisi kama watu wengi wanavyofikiria.

Nilichukua mkopo na kuanzisha biashara nikiwa na matumaini makubwa. Hata hivyo, nilitumia fedha nyingi kwenye maandalizi, biashara haikufanikiwa kama nilivyotarajia, na baadaye nikapatwa na majanga yaliyoteketeza hata mtaji uliokuwa umebaki.

Kwa sasa sina kazi, lakini bado ninawajibika kulipa marejesho ya mkopo kila mwezi. Ni presha kubwa sana. Kila siku ni mawazo, msongo wa mawazo na hofu. Wakati mwingine nahisi kukata tamaa kabisa. Natafuta kazi kila sehemu lakini sipati.

Nimegundua kuwa msongo wa mawazo (depression) ni jambo la kweli. Unapokuwa na madeni, huna kipato, na huoni njia ya kutoka, maisha yanakuwa magumu sana.

Ninaendelea kutafuta kazi na fursa nyingine kwa matumaini kwamba siku moja hali itabadilika, lakini kwa sasa siwezi kuficha kwamba ninapitia kipindi kigumu sana. Sijui nifanye nini.
 
Ulitakiwa upate elimu ya mkopo kabla hujachukua..!!

Mkopo sio wa kuanzishia biashara.
Pesa za mkopo ni kwaajili ya kuongezea uhitaji wa bidhaa unazouza au unazozalisha kwa wateja..!!
 
Mikopo si jambo rahisi kama watu wengi wanavyofikiria.

Nilichukua mkopo na kuanzisha biashara nikiwa na matumaini makubwa. Hata hivyo, nilitumia fedha nyingi kwenye maandalizi, biashara haikufanikiwa kama nilivyotarajia, na baadaye nikapatwa na majanga yaliyoteketeza hata mtaji uliokuwa umebaki.

Kwa sasa sina kazi, lakini bado ninawajibika kulipa marejesho ya mkopo kila mwezi. Ni presha kubwa sana. Kila siku ni mawazo, msongo wa mawazo na hofu. Wakati mwingine nahisi kukata tamaa kabisa. Natafuta kazi kila sehemu lakini sipati.

Nimegundua kuwa msongo wa mawazo (depression) ni jambo la kweli. Unapokuwa na madeni, huna kipato, na huoni njia ya kutoka, maisha yanakuwa magumu sana.

Ninaendelea kutafuta kazi na fursa nyingine kwa matumaini kwamba siku moja hali itabadilika, lakini kwa sasa siwezi kuficha kwamba ninapitia kipindi kigumu sana. Sijui nifanye nini.
Unadaiwa kiasi gani nione kama naweza kukusaidia
 
Back
Top Bottom