Mkopo wa benki za Tanzania ni biashara au hisani?

Incredible

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,031
Reaction score
1,603
Najiuliza swali hili kwamba wafanyakazi kwenye mabenki yetu Tanzania wanaelewa kwamba benki kutoa mkopo kwa mtaje ni biashara kwa hiyo benki?

Sababu za swali hili ni kama ifuatavyo:

1. Wateja huwanyenyekea sana maafisa mikopo kama kwamba pesa watakayokopa haitorudishwa, tena kwa riba kubwa

2. Maafisa mikopo asiponyenyekewa basi mteja huyo aweza nyimwa huo mkopo

3. Watu wa kitengo cha mikopo wanapokea rushwa na kuna kipindi wanataka wapewe pesa yao kabla hata mteja hajapewa mkopo

4. Hata pale ambapo afisa mikopo hajaomba rushwa lakini utakuta ana mtail-gate mteja siku hela inapoingizwa kwenye akaunti. Mpaka mteja anashindwa kuondoka bila kumpa pesa

5. CEOs kwenye mabenki yetu, nao wanakula rushwa hasa pale ambapo mkopo ni mkubwa

Ikumbukwe kwamba riba za Tanzania ni kubwa na hii inatokana na kwamba mfumuko wa bei pia ni mkubwa. Na wateja mara nyingi wanatakiwa kuanza rejesha malipo ya mkopo hata kabla ya pesa waliyokopa kuzaa. Mfano mteja anaenda Uturuki kununua bidhaa, wakati mzigo upo melini unaletwa yeye ameisha rejesha malipo ya miezi miwili.

Lakini swali langu ni kwa bankers wetu. Je wanaelewa kwamba wakopaji ni wateja? Na je wanajua kwamba Interest Income itokanayo na mikopo ndiyo inayolipa mishahara yao, matibabu yao na familia zao?

Wanajamvi hebu tusaidiane kufikisha ujumbe.
 
... Mkuu, kwenye namba 3. Sio rushwa ya pesa tu inayoombwa. Akinamama/dada wanaombwa sana rushwa ya ngono - kabla na baada ya kupata mkopo!

Ni ukweli usiofichika, Loan Officers ktk Benki nyingi hapa ni vi-mungumtu, vijambazi na vibaka fulani hivi!

Pathetic!
 
Mim binafsi nimeomba mkopo lakin cha kustaajabu jamaaa wanataka niwape 10% ya mkopo wangu ili mambo yaende haraka haraka. Inauma sana
 

nenda NBC/CBA wanashika watu milangoni wakakope

pili usiombe mkopo wakati unashida utatukana watu wote bank

tatu kukopa ni porcess anaza na mkopo mdogo ukijenga profile yako wajuwe una kopesheka

nne, sheria na mashariti ya mikopo ni ile ile kwa bank zote, procedure za kukupa huo mkopo ndio zaweza differ
 

Mm ni mfanyakaz wa serkal ktk hospital.nataka kukopa je utaratbu wake ni upi kwa mfanya kaz wa serkal, msaada plz
 
Mm ni mfanyakaz wa serkal ktk hospital.nataka kukopa je utaratbu wake ni upi kwa mfanya kaz wa serkal, msaada plz

nenda stanbic, bancABC, wanawatafuta watu kama nyiewatakupokea vzuri sana upatapo huo mkopo rudi utujulishe na wenzio
 

Nadhani hapa kuna knowledge gap. I know all the procedures na huko nyuma niliwahi kufanya kazi benki kama tatu japo siyo idara ya mikopo. Nilicho kiandika ninakijua vizuri. Nadhani tusaidiane kufikisha ujumbe kwa jamii ili benki zijirekebishe badala ya kuzitetea.
 

hapana siku hizi ni nafuu sana, most banks ukiondoa zile za wahindi kama I & M or habib bank wanaoangalia sura kabla hawajakuhudumia. zingine zote zinafwata procedure, kama umetimiza mashariti yao yote gonga meza lazima mkopo wakupatie.

nilijaliwa mkopo wangu wa kwanza bank year 2005, niliwaomba tshs 50m wakanipa 30m year 2007. but know I enjoy up to tshs 1b zao.

so I know kuwa hali kwa sasa imebadilika.
 
Hiyo ni kweli kuna jamaa Yangu alikwenda Banc ABC alitoa laki mbili ndio akapata mkopo,hii bank kwa rushwa ndio inaongoza kwa sasa
 
Nimewahi kukopa standard chatterd benk millioni 14 kwa riba kama sikosei ya 17% hata hivyo katikati wakadai sababu kadhaa wakaongeza riba ikawa 20% sijui walidai kuna inflation etc,waliendelea kukata kila mwezi na hakuna mwezi nilipitisha bila kulipa,mwisho wa mkopo nilipiga hesabu na kukuta jumla hela nilyowalipa ni Milioni 21.5 niliwapigia simu kwa nia nzuri wanipe ufafanuzi wa kwa nini mwisho wa deni riba ianonekana ni 50% lakini hakuna jibu lolote walilonipa.Sijui na kwa benki nyingine ikoje,lakini kuanza siku hiyo nilisema mikopo basi
 
Mimi nafanya kazi private sector pia bank nayotumia no crdb hivi naweza pata mkopo kweli. Mwenye kujua tafadhali anijuze
 
Ni Kweli Mkuu, Benki Nyingi Sana Hapa Nchini Wanatumia Kigezo Cha Uelewa Mdogo Wa Watz Kwny Masuala Ya Mikopo Kufanya Suala La Mikopo Liwe Kama Huduma Badala Ya Biashara Na Kupelekea Mazingira Ya Rushwa Kuwa Mengi.

Loan Officers Wengi Wamegeuza Rushwa Kama Sehemu Ya Procedure Katika Kutoa Mkopo Kwa Kigezo Cha Kukuwahshia Kupata Na Wengine Wamejipangia Hadi Viwango Kabsa Kama Vle Ni Halali, Hata Kama Umefuata Process Zote Bdo Wataendelea Kukusumbua Njoo Kesho Mara Keshokutwa Hadi Wapate Kitu Kidg.

Tatizo Pia Lipo Kwny Hyo Mikopo Yenyewe Kwani Ukiachana Na Interest Rate Kuwa Kubwa (20%) Pia Uelewa Wetu Mdg Umepelekea Watu Wengi Kushindwa Kunegotiate Na Benki Kupewa Grace Period Hata Ya Miezi Sita Ili Kugenerate Faida Na Kurejesha Mkopo, Hali Inayopelekea Mzigo Kuwa Mkubwa Kwa Mkopaji Kwani Ndani Ya Mwezi 1 Atatakiwa Kuanza Kurejesha (Principal + Interest) Kitu Ambacho Co Kizuri Kwa Mtu Anayechukua Mkopo Kuanza Biashara.
 
Riba ni kubwa kiasi gani?

Msiishie kulalamika tu chukueni hatua

1. Kwenye mabenki kuna masanduku ya kutoa maoni ambapo si lazima mtaje majina yenu. Watajeni maofisa mikopo wanaokula rushwa.

2. Washikisheni na hela za moto kupitia vyombo vya kuzuia rushwa

3. Undeni umoja wenu wa watumiaji wa mikopo na mpeleke kilio chenu kwenye vyombo vinavyohusika kama ile tume ya kuzuia na kusimamia ushindani haramu

4. Wakati huu wa kutengeneza Katiba ya nchi, ndiyo kipindi chake kuhakikisha kuwa katiba inatamka haki ya kupata mikopo yenye riba ambayo ni 'fair'. Pelekeni hiki kilio kwa wajumbe wenu wa Bunge la Katiba
 
Changamoto kubwa kwa wakopaji wengi ni kukosa mpango madhubuti wa matumizi ya mkopo. Hili linatokana na kutoandaliwa kwa business plan pamoja na financial projections ambapo makisio ya mapato na matumizi unakuwa nayo hata kabla ya mkopo wenyewe. Laiti ukifanya hivi suala la kutoa takrima au rushwa linakuwa sehemu ya gharama hivyo linapunguza faida au kuongeza hasara ya ujasiriamali husika. ukichukulia takrima au rushwa kama gharama kwa biashara utapingana nayo kwani utagundua pamoja na kuongeza gharama hata riba ya mkopo inakuwa imeongezeka (effective interest rate)
 
Hapo BANC ABC kuna wadada wanashughulikia mikopo bila laki mbili kutoa mkopo utaupata baada ya week 4,majina yao nitayaweka hewani ili muwajue,naomba mwenye number ya cim ya mkurugenzi wa hiyo bank anipatie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…