Ndugu zangu, nimefikiwa na watu wanahitaji shilingi milioni tano (5,000,000) kwa shughuli za kibiashara. Wanasema wako tayari kulilpa mkopo huo kwa riba ya miezi miwili. Nilipowahoji, ili kuwasaidia, wakasema
1) Wanamazao yao ya biashara wanatakiwa kuyaweka sawa na kuyafikisha sokoni kabla mvua haijakolea.
2) Wanahitaji shilingi milioni tano kwa mpigo na kwa haraka.
3) Wana mtu mmoja anayewaelewa na hivyo ametoa nyumba yake iwadhamini katika mkopo huo.
4) Wamejaribu kutafuta kwa wakopeshaji binafsi wanaambiwa wanatakiwa kuwa na dhamana ya gari ambapo ili wapate huo mkopo, hitaji ni kwamba wapeleke gari la dhamana lika paki kwa mkoopeshaji na hati ya gari, na waandikishiane kwamba gari hilo wamemuuzia mkopeshaji, eti ili kama wasipolipa auze chapu chapu. Bahati mbaya hawana mtu mwenye gari miongoni mwao. Mazao hayo wanategemea yawasimamishe.
Kwa kuwa mimi sina uwezo wa kuwakopesha, nimeona nilete hapa jamvini. Kama kuna mtu mwenye nia ya kutoa mkopo huo bila hila, kwa utaratibu wa wazi kwamba miezi 2 alipwe na riba yake, la sivyo nyumba ya dhamana iwe halali yake, naomba ani inbox, ili nimuunganishe na hao wateja.
Natanguliza Shukrani.