Asante kwa maelezo yako ingawaje yamejaa hofu na jazba hasa pale unapodhani nimetoa mada kwa kutumwa na lapf pengine kwa sababu nimewataja.
Nadhani wewe ni muhusika na hapo pspf basi na mimi ni mwanachama wa pspf kwa miaka 5 sasa.sasa basi mnapo tangaza huduma zenu mjitahidi kutuelewesha yote ili tujue habari kamili sio tunakuja huko na kukutana na butwaa,
Najua hizi ni huduma za ziada zitolewazo na mifuko ya hifadhi ya jamii na wala sio lazima,basi muwe wa wazi kwa wanachama wenu,nakumbuka mwaka juzi nilipokuja kufuatilia mkopo wa nyumba kama tangazo linavyosema nilichoka baada ya kuambiwa hadi mwanachama uwe na umri wa miaka 55 !!,mambo kama hayo ndio yanayo tukera na tunaona haina maana na hayo mambo mnayotutangazia.
Kumbuka:sio kila anaye wakosoa ni mpinzani wenu kama unavyodhani kwamba nimetumwa na lapf kwa hilo umekurupuka na huwezi kupiga hatua kama unaona kila anayekukosoa anataka kukurudisha nyuma.