Mkopo wa piki piki ya hesabu au pesa ya kununulia piki piki

Mkopo wa piki piki ya hesabu au pesa ya kununulia piki piki

Comrade Liu Yang

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2023
Posts
206
Reaction score
326
Nakuja kwenu wafanyabiashara na watu wenye uwezo wa kunisaidia shida yangu ya Mkopo wa kupata PikiPiki kwa ajili ya kufanyia DELIVERY kwenye biashara zangu

au

Kiasi cha Pesa chenye thamani ya piki piki husika ili niende nunua mwenyewe Piki Piki hiyo MPYA dukani.

Piki Piki ninayohitaji ni BOXER X CC 150 ambapo bei yake dukani sasa imefika 3.7 to 3.8,Nahitaji pikipiki hii inisaidie katika kufanya delivery ya bidhaa zangu kwa wateja.

Mimi sio BODA BODA wala sitoitumia pikipiki hii kama BODA BODA itakaa ofisini ikitumika kwa ajili ya DELIVERY TU.

JINSI YA KULIPA DENI :

Kama ilivyo kwa MIKATABA YA BODA BODA mtu atakae ninunulia hii piki piki atanipa mkataba wa miezi anayo ona yeye inafaa kulingana na Piki PIKI husika.

Miezi inaweza kuwa michache HESABU ikawa kubwa (15,000) kwa siku au Miezi ikawa mingi hesabu ikawa ndogo (10,000) kwa siku. Ni swala la makubaliano kati yetu wawili.

Ukininunulia Piki Piki utanikabidhi na KADI ya piki piki ORIGINAL utabaki nayo
Ukinipa Pesa bado ni sawa na Umeninunulia piki piki Hesabu yako ni kwa siku

MKOPO HUU marejesho yake ni KWA SIKU kulingana na tutakavyokubaliana, Siku au WIKI (Utakavyoona)

UTHIBITISHO WA UAMINIFU WANGU :

Nina Wadhamini
Nina Biashara Physicaly ambazo BOSS utafika uzione Uzihakiki
Biashara zangu zimesajiliwa/Zinalipa Kodi
Nina Makazi ya Kudumu

KAMPUNI YA "WATU CREDIT" wanatoa mikopo ya piki piki lakini sitaki piki piki za TVS ambazo ndio WATU wanazitoa.

wanatoa TVS na HONDA hawatoi BOXER X (NYEKUNDU)

Kama kuna anaejua wanapokopesha Hizi piki piki za BOXER X tafadhali naomba muongozo,mawasiliano yangu,yapo PM

KWA yeyote atakae hitaji kwa msaada zaidi naomba.

NOTE :

Boss utakaenipa PIKI PIKI kama una kijana wako muaminifu anaweza endesha Piki Piki namuomba,Piki Piki utakayonipa ataiendesha yeye mimi nitamlipa mshahara tu kwa mwezi.

hivyo kama utanipa Piki Piki na utakua na kijana ndugu yako hana kazi na anaweza endesha piki piki naomba niunganishe nae awe dereva wa hii piki piki.

Maana natafuta piki piki ila kijana sina bado sijapata.

ukinisaida MIMI kupata Piki Piki utakua umemsaidia na kijana mwingine kupata AJIRA kwani mimi si ambae nitaiendesha hii Piki Piki.

Natanguliza SHUKURANI kwa yeyote atakaeguswa na OMBI LANGU.

ASANTE.

NAPATIKANA : DAR ES SALAAM
 
Chukua pkpk ya kununua cash
Au Nunua pikpk ambayo, mtu ameshindwa mkataba, ambayo Bado haijafunguliwa Engine, Ingawa pkpk za sasa hiv ni Tofauti na Boxer ya mwaka 2008/2010 Vipuri vyake hizi za sasa hivi wamechakachua sana, yaani Boxer inamiezi 6 Tu inaanza kutoa moshi hata kama kijana amezingatia uwekaji wa oil
 
Tatizo kuu ni CASH mkuu ningekua na hiyo pesa ningefanya hivyo,na katika piki piki hutakiwi nunua used ni piki piki unayokuja itumia kufanyia kazi.

piki piki ya kununua used labda kama utaitumia kutembelea na matumizi yako binafsi,90% YA PIKIPIKI USED zinauzwa sababu watu washazitumia vyakutosha
 
boxer mpk itoe moshi nadhani ni uzembe wa kutozingatia OIL naielewa sana hii pikipiki hasa 150 ktk kutenda kazi ngumu
 
Tatizo kuu ni CASH mkuu ningekua na hiyo pesa ningefanya hivyo,na katika piki piki hutakiwi nunua used ni piki piki unayokuja itumia kufanyia kazi.

piki piki ya kununua used labda kama utaitumia kutembelea na matumizi yako binafsi,90% YA PIKIPIKI USED zinauzwa sababu watu washazitumia vyakutosha
Poa, pole ila Biashara ni Kamali Anza na ulichonacho utafanikisha tuu.
Pia usiogope kuwekeza, ktk hilo wazo lako.
 
Back
Top Bottom