Mkopo.

M.E.M.A

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2013
Posts
1,373
Reaction score
472
Habarini ndugu zanguni.
Ninatafuta kampuni/taasisi inayotoa mikopo. Mm ni mfanyakazi wa taasisi binafsi. Nilicho nacho mkononi kama dhamana ni magari mawili. Nilishauriwa kwenda NMB lakini sikupata lolote lenye tija. Tafadhalini naomba mawazo yenu. Naamini.. problem shared=problem solved.
(Inaelekea niliipost kwenye wrong forum, hapa labda nimepatia)
 
Mikopo ni balaaa. Kwa nini usiuze gari moja ili upate hiyo pesa? Ukikopa ili kuhudumia gari mbili itakula kwako maana kiasi kitakachobaki watakapoanza kukata chao ni kidogo sana.
 
Mikopo ni balaaa. Kwa nini usiuze gari moja ili upate hiyo pesa? Ukikopa ili kuhudumia gari mbili itakula kwako maana kiasi kitakachobaki watakapoanza kukata chao ni kidogo sana.

Sikopi ili kuhudumia gari. Gari zinajiendesha zenyewe, na kulipa nitatumia mshahara wangu. Nikiuza moja kwa haraka hivi lazima nitapata hasara..na hela haitafikia kiwango ninachokitaka.
 
Sikopi ili kuhudumia gari. Gari zinajiendesha zenyewe, na kulipa nitatumia mshahara wangu. Nikiuza moja kwa haraka hivi lazima nitapata hasara..na hela haitafikia kiwango ninachokitaka.
Unataka mkopo kiasi gani na kwa muda gani???
 
Ndugu yangu kaa kwanza chini ufikirie sana.
naangalia concept yako ya kukopa 10m halafu unataka miaka 3? does it make sense?

Hapa ndio nakubaliana na jamaa aliesema kwamba uza gari moja hatakama kwa hasara,maana hata kama utapata mkopo haitakuwa chini ya riba ya 10% ambayo ni sawa na hasara ya kuuza gari.

Kimfaacho mtu chake,we uza tu kama una malengo pesa itarudi.Watu wameuza Maghorofa kwa malengo na leo wamejenga tena.

Halafu inakuwaje una magari mawili na hauna nyumba?,halafu unasema magari yanajiendesha yenyewe?.

Mienilifikiria nimkopo wa dharura wa 10 m na inarudi kama miezi mitatu au miwili hivi ila ni Miaka mitatu.Kweli unamalengo mkuu?

Kama kweli una gari uza,na kama umeweza kumiliki magari mawili na huna nyumba basi usikope itakuwa huna malengo mjini.

Ni hayo tu
 
Mkuu magari yenyewe sio ya kutisha..moja ni tax, nyingine binafsi baloon ya 1996. Nikiziunganisha zote haraka haraka naweza kupata M6 tu. Ila bila papara nitapata M10 kwa yote mawili.

Nyumba kweli sina, ila kiwanja kipo..mwez wa 10 ndio mkakati unaanza kupandisha nyumba..na ndio hapo hasaa target yangu ya mkopo huo.

Nikizipata hizo 10 nazitumbukiza saccoss ambapo nitapata 30M. Kwa hizo nikirudisha nilikopewa 10, nitabakiwa na deni moja kwenye saccoss. Hapo mchezo nitakuwa nimemaliza.
 
Miaka mi3 nimeweka iwapo favourable terms zitakuwepo, basi nitazirejesha kwa installment kama kawaida...kwa kuwa nitazitumia kuimarisha biashara ya tax (boda boda) included. So izo zinalipwa kwa biashara. Za mshahara zinaenda saccoss taratibu at the same time nyumba inapanda. Hivi ndivyo ambavyo nimepanga draft langu.
 
Hapo nimekuelewa,sio mbaya ni Idea nzuri mkuu.
Ila sijaelewa.
Mwanzo ulisema kwamba 10m kwa miaka mitatu then unasema kwamba 10m unazipeleka Saccos unapewa 30m na unarudisha 10m kwa mhusika.
Hapo kama sijaelewa vizuri huu mkanganyiko
 
Ni kweli mkuu. Hata mm nimeona haijasomeka vizuri ndio nikaifafanua kwa post iliyofuatia. So kwa upande wa marejesho mchanganuo ndio huo hapo mkuu.
 
Zanzibar Spices
 
Last edited by a moderator:

Mkuu kama uko Dar nenda Survey mita chache kutoka mlimani city kuna baa inaitwa BULLS PUB then kuna frem nyingi pale nimewasahau jina ila unaweza ulizia wao wanakopesha kwa dhamana ya MAGARI tu,watembelee upate maelekezo zaidi, ila na mimi nifafanulie kidogo kuhusu Saccos jinsi ya kuweka na kupata mkopo wao,Asante.
 
Ndessa please fafanua kidogo zaidi, unamaanisha nini unaposema wanakopesha kwa dhamana ya magari? Wanachukua reg card au wanabaki na gari kabisa? Maelezo yako ya kina yatawasaidia wengi I'm sure.
 
nenda azania bank,hakikisha plot ina title hati halali, tengeneza ramani ya hiyo nyumba,rekodi za biashara yako kwa miaka mitatu nyuma,hati zako zote ulipaji wako wa kodi variate go!
 
Wanaitwa Nyumbani Microfinance kama sijakosea.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mkuu nikiangalia vizuri jinsi ambavyo unaielezea hii biashara unayotaka kuiimarisha ili hela yake uitumie katika ujenzi sina hakika sana kama ina return nzuri namna hiyo (correct me if am wrong).
Stream yake ya income iko reliable kiasi hicho?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
nenda azania bank,hakikisha plot ina title hati halali, tengeneza ramani ya hiyo nyumba,rekodi za biashara yako kwa miaka mitatu nyuma,hati zako zote ulipaji wako wa kodi variate go!

Jino la Mamba pliz ongeza maelezo kidogo, you mean Azania bank wanatoa mikopo ya ujenzio wa nyumba?
 
Ndessa please fafanua kidogo zaidi, unamaanisha nini unaposema wanakopesha kwa dhamana ya magari? Wanachukua reg card au wanabaki na gari kabisa? Maelezo yako ya kina yatawasaidia wengi I'm sure.

Sure Bobby umeuliza swali la msingi sana mana kama wanazuia mkoko ni balaa lingine tena...unless haina jinsi mana mzee mzima kama maji yamevuka shingo yako kidevuni..haina jinsi ni kupiga TZ 11.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…