Ndessa please fafanua kidogo zaidi, unamaanisha nini unaposema wanakopesha kwa dhamana ya magari? Wanachukua reg card au wanabaki na gari kabisa? Maelezo yako ya kina yatawasaidia wengi I'm sure.
Sure Bobby umeuliza swali la msingi sana mana kama wanazuia mkoko ni balaa lingine tena...unless haina jinsi mana mzee mzima kama maji yamevuka shingo yako kidevuni..haina jinsi ni kupiga TZ 11..... Ndessa inabidi adadavue zaidi au atusaidie contact if possible
Mkuu Saccoss inategemeana na katiba yao. Kuna ambao ukiweka hela yako ndani ya miezi mitatu unakuwa na haki ya kukopa x2 au hadi x3 ya akiba yako. Mimi natumia ya walimu ipo vizuri sana.
Duh..sasa hapo miez 6!! Halafu tatizo sipo dar.
Mkuu hizi saccoss kwa sisi ambao siyo member kabisa unaruhusiwa kuweka hela kwa muda wanaotaka then wakakukopesha?
Nashukuru sana mkuu. Ngoja tuone..
Ukikopa M10 kwa miaka 3 utalipa si chini ya asilimia 25% ya mkopo uliopewa (25%=2.5M). Ukiweka chama cha akiba na mikopo (CAM) 10M watakupa 30M, Kwa riba ya wasatani wa 30% kwa mwaka utailipa CAM 9M, kumbuka umerudishiwa 10M yako na CAM wamekupa 20M tu. Ukweli utakua unalipa 45% CAM 20M kwa 9M, huu ni upande wa pili wa shilingi, unaobidi kutazamwa.Nikizipata hizo 10 nazitumbukiza saccoss ambapo nitapata 30M. Kwa hizo nikirudisha nilikopewa 10, nitabakiwa na deni moja kwenye saccoss. Hapo mchezo nitakuwa nimemaliza.