Reference ya hayo maandiko umeorodhesha please.
1: Bidii
Mithali 12:27
Mtu mvivu hapiki mawindo yake;Bali mwenye bidii anazo mali za thamani.
2: ASubuhi na mapema. Mambo Mengi ya maana karibu warmtu wote waliamka mapema sana.
Yoshua 3:1
Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, nao wakatoka Shitimu, wakafika mto wa Yordani, yeye na wana wa Israeli wote, wakakaa hapo kabla ya kuvuka.
3: Kutunza hesabu na usimamizi wa hesabu kidogokidogo
Mithali 13:11
Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; <br>Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa.
4: Connections.
Soma story yote luka 16, huyu jamaa alisifiwa na Yesu kwa sababu alikuwa na connections ambazo alipofukuzwa kazi zingemsaidia,
Luka 16:5
Akawaita wadeni wa bwana wake, kila mmoja; akamwambia wa kwanza, Wawiwani na bwana wangu?
5: Afya: Ipo kwenye ulaji wa vyakula vya asili kutoka ardhini.
Mwanzo 1:29
Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;
Na mengine mengi niishie hapo mkuu.