Mkristo ambaye hufungi na kuomba unatumia mbinu gani kujilinda na wachawi kwenye Biashara na maofisini?

Kula kitimoto sana,mama mdogo hawana ujanja.
 
Waislamu
Waislamu, hv mkuu kuna watu katika dini Yao wanaongoza kurogana Hadi kuuana Yani unamroga mtu Hadi afe sio apate mikosi labda, tena ni viongozi was juu ndo wanalogana.

Hapa nilipo wawili wameshazikwa, viongozi Hao... Wa tatu ni Msunni Mmoja mke wake alikuwa anaumwa, jamaa kaenda Hospitali kumpima mkewe.

MAJIBU ikawa Mwanamke haumwi popote, jamaa kurudi nyumbani kamdai mke Hela alotumia kulipa vipimo Hospitali, Siku ya tatu Mwanamke kafa.

Pia nimeshuhudia Mchungaji mlokole alilogwa na wachungaji wenzake...
 
Ni hiyo unayofanya unapata faida duniani na mbinguni.
 
Reference ya hayo maandiko umeorodhesha please.
1: Bidii
Mithali 12:27
Mtu mvivu hapiki mawindo yake;Bali mwenye bidii anazo mali za thamani.

2: ASubuhi na mapema. Mambo Mengi ya maana karibu warmtu wote waliamka mapema sana.
Yoshua 3:1
Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, nao wakatoka Shitimu, wakafika mto wa Yordani, yeye na wana wa Israeli wote, wakakaa hapo kabla ya kuvuka.

3: Kutunza hesabu na usimamizi wa hesabu kidogokidogo
Mithali 13:11
Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; <br>Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa.

4: Connections.
Soma story yote luka 16, huyu jamaa alisifiwa na Yesu kwa sababu alikuwa na connections ambazo alipofukuzwa kazi zingemsaidia,
Luka 16:5
Akawaita wadeni wa bwana wake, kila mmoja; akamwambia wa kwanza, Wawiwani na bwana wangu?

5: Afya: Ipo kwenye ulaji wa vyakula vya asili kutoka ardhini.
Mwanzo 1:29
Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;


Na mengine mengi niishie hapo mkuu.
 
Tunatumia MO Xtra kubwa
 
Pata muda binafsi wa maombi (omba katika Roho na sio kwa lugha yako pekee) na kula (chakula cha kiroho).

Taa yako ya rohoni iwe na mafuta, uone yaliyo sirini.
 
Yani Mungu mnayedai ana upendo, mwema sana na mwenye huruma,

Anafanya njia ya waovu iwe na wengi?

Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?
Ndugu hii dhambi kubwa sana jitahidi kutubu isije kukutafuna wewe na kizazi chako
 
Ndugu hii dhambi kubwa sana jitahidi kutubu isije kukutafuna wewe na kizazi chako
Dhambi haipo.

Sin is an imaginary disease invented to sell you an imaginary cure.

Hakuna Mungu wala dhambi.

Kwanza kama dhambi ipo, Mungu ndio mdhambi namba moja.

Mungu huyo amehusika na mauaji ya watu wengi sana.
 
Fungu la kumi ,malimbuko ,sadaka za ujenzi ,sadaka kwa baba wa kiroho,sadaka ya umisheni,sadaka kwa masikini ,Toa mahitaji ya familia yako,angalia wazazi wako FANYA HAYA KWA MUENDELEZO hauitaji maombi hapa ni kutoboa tu .
 
Dhambi haipo.

Sin is an imaginary disease invented to sell you an imaginary cure.

Hakuna Mungu wala dhambi.

Kwanza kama dhambi ipo, Mungu ndio mdhambi namba moja.

Mungu huyo amehusika na mauaji ya watu wengi sana.
Sema ndugu ujasili ulio nao sijui unaupata wapi maana wengi waliokuwa kama wewe waliishia kupata matatizo makubwa
 
Uchawi unakuzwa upo overrated.

In fact uchwi upo na science ya uchawi ipo Ila mchawi huwa haendeshi bali anaendeshwa yupo driven .

Na katika layer uchawi unaishia layer ya tatu.

Maisha ni kuwa innocence -mnyongofu hiyo pekee inatosha kuwa salama hakuna MTU wa kukugusa.

Huwa nasikitika kuona watu wanashindwa kutumia hadhina yao waliyonayo wanabaki kuogopa uchawi au kukimbilia kwenye uchawi.


Binadamu Ana infinite treasure , ni swala la kuichimba tu hadhina yake na Ku-manifest katika kazi zake na MAISHA.
 
Sema ndugu ujasili ulio nao sijui unaupata wapi maana wengi waliokuwa kama wewe waliishia kupata matatizo makubwa
Wengi wangapi?

Kina nani?

Matatizo yapo kwa sababu Mungu huyo ameshindwa kuumba Dunia isiyo na matatizo.

Mungu huyo ni Mkatili sana kwa kuumba Dunia yenye matatizo ilhali uwezo wa kuumba Dunia isiyo na matatizo alikuwa nao.

Otherwise, Mungu huyo hayupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…