Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Declaration of Interest.
Naomba kuanza uzi huu kwa ku declare my interest kuwa Mimi Pasco wa JF, naunga mkono maandamano na mikutano ya UKUTA nchi nzima na siku ya siku, nitajitokeza kushiriki na nitatoa wito wale wote wenye mapenzi mema na taifa hili, tujitokeze kwa wingi! .
Kijiweni au vijiweni ni wapi na kina nani
Niko kwenye kijiwe fulani hapa mjini kati, jijini Dar es Salaam. Kwa kawaida watu wanaokaa kijiweni, ni watu wasiokuwa na kazi, au wenye kazi zao lakini muda huo, wanakuwa ama wameishatoka kazini. Kazi kubwa inayofanyika kijiweni ni kuongea tuu, kuzungumza au kusikiliza.
Aina Mbalimbali za Vijiwe.
Kuna aina nyingi za vijiwe. Viko vijiwe vya watu wasio na ajira, wale ma jobless, vijiwe hivyo huitwa jobless corner, baadhi ya wakaji hao husubiria kazi yeyote au kitabarua chochote. Viko vijiwe vya madereva taxi, madereva wasio na magari huja hapo kubahatisha daywaka zozote. Viko vijiwe vya mateja, viko vijiwe vya wakereketwa wa vyama, na viko vijiwe vya heshima watu wenye kazi zao wametoka kazini hukutana hapo kubadilishana mawazo, hivi ni vijiwe kama vya gahawa, viko vijiwe vya watu wa class tofauti kukutana mahala tofauti, washabiki wa mipira na vijiwe vyao, walevi na vijiwe vyao vya baa mbalimbali. Wengine vijiwe vyao ni Clubs kama kijiwe cha Saigon, Kijiwe cha Tanzania Legion, hata hapa jf ni kijiweni kwetu wanabodi etc. Nyerere na Karume walikaa vijiweni, Nyerere akicheza bao, Karume akicheza dhumna. Hivyo wakaa vijiweni sio wahuni tuu au watu wasio na maana, bali ni watu wa aina mbalimbali kutoka makundi tofauti na kazi tofauti.
Reliability ya Taarifa za Vijiweni
Kufuatia watu wa aina mbalimbali kukutana vijiweni, sometimes vijiweni ni source ya taarifa muhimu, news tip za ukweli, ila pia nakiri vijiweni pia ni source ya habari nyingi za kutunga, uongo, zengwe, fitna na majungu haswa kwa vijiwe vya watu wasio na kazi, majungu huyafanya ni mtaji kws kutunga uongo na kuupeleka kijiweni.
Kufuatia vijiweni kuwa na mikutano iko ya watu wengine, hii hupelekea watakavyo habari kutembelea vijiwe mbalimbali kunisalimia habari. Sifa Kuu ya mwanaharakati yoyote ni kuwa na "nose for news " yaani kuwa na puani ya kususia habari, pia wako watu wanaokuja vijiweni kwa ajili ya kunusa tuu ndogondogo, hata wale 'jamaa zetu' hushinda vijiweni kama vituo vyao vya kazi, hata info za ile kesi ta uhaini ya 1982 ziliibukia kijiweni, hivyo info za kijiweni sio za kupuuzwa hata kidogo.
Tetesi za Mwk wa Chadema Safarini.
Wakati chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema, kiko kwenye maandalizi ya maandamano na mikutano nchi nzima kuhamasisha UKUTA, siku ya Tarehe 1 September 2016, habari kutoka kijiweni ambazo hazijathibitishwa, zimeeleza kuwa, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe, na familia yake, yuko kwenye maandalizi ya mwisho mwisho kuanza ziara binafsi ya Ulaya na Marekani kupitia Dubai. Ziara hiyo umeelezwa kuwa pia itahusisha matibabu, uchunguzi wa afya na mapumziko mafupi mjini Dubai. Mtoaji wa taarifa hiyo isiyothibitishwa, imesema ziara hiyo ni binafsi ya kimatibabu, ya kifamilia na ya kibiashara binafsi.
The Confidentiality of the source.
Mtoa habari huyu alijitambulisha rasmi kama mkereketwa wa Chadema, na kutaja majina yake halisi, lakini kufuatia habari hizi kuwa bado hazijathibitishwa rasmi na uongozi wa Chadema, naomba nisilitaje jina la mtoa habari wangu chini ya kinga ya kihabari iitwayo "the confidentiality of the source " mpaka habari hizi zitakapothibitishwa au kukanushwa. Kuna habari nyingi source anahifadhiwa hata kwenye ile scandal kubwa ya Watergate nchi Marekani iliyomg'oa madarakani rais wa Marekani, iliibuliwa kijiweni na mleta tip hakutajwa, mhariri wa gazeti la Washington Post alikubali kwenda jela kuliko kumtaja source baadaye uchunguzi ukathibisha ni kweli, rais akapigwa chini, mwandishi akawa shujaa! . Hivyo msidharau habari yoyote!.
Kwa nini ni Tetesi? .
Kufuatia source wa habari hii kuwa ni kijiweni tuu na sio a trusted source ndio maana habari hii ina lebo ya tetesi, tetesi inaweza kuwa kweli, ikiishatibitishwa, neno tetesi litaondolewa! . Ila pia tetesi inaweza kuwa ni uongo, ikithibitika tetesi fulani ni uongo, thread husika hufungwa, hii sio mara moja wala mbili kwa tetesi mbali mbali kushuka humu jf na baadae zikathibitishwa kuwa ni kweli au kukanushwa na thread kufungwa.
Ukweli au Uongo wa Tetesi Hii ni Precedence.
Ukweli au uongo wa taarifa fulani hutegemea kitu kinachoitwa "the reliability of the source" na precedence ni jambo ambalo liliwahi kutokea nyuma katika mazingira yale yale, likijirudia, linakua sio jambo jipya hivyo inafanyika kile kile kilichofanyika mwanzo. Kufuatia tetesi hii, kijiweni, mimi kama mwandishi makini, nilipaswa kuipuuza tuu kama soga za kijiweni, nyingine ni furahisha genge, lakini kwa vile tayari kuna precedence ya tukio kama hali, sikuipuuzia kwa sababu hii sii mara ya kwanza kwa kiongozi Mkuu wa Chadema kuanzisha maandamano lakini siku ya siku haongozi harakati hizo na badala yake huwa safarini kikazi au kibinafsi hivyo kuwaachia wengine waliopo kuongoza.
Lengo Kuu la Taarifa Hii, ni jf be the first to know! ".
Lengo kuu la kuileta habari hii humu jf hata kabla haijathibitishwa ili ile jf spirit ya "be the first to know! ".
Hata ikitokea ikathibitika habari hii sii ya kweli bali ni uzushi tuu, bado nitamuomba mode, asiufute uzi huu bali aufunge tuu kusubiria hiyo tarehe 1 September tuthibitishe this time around, Mwenyekiti atakuwepo kuongoza maandamano hayo.
Lengo la kuomba uzi usifutwe bali ufungwe tuu, ni kufuatia posibility ya Chadema kuikanusha taarifa hii kuwa sii kweli lakini siku ya siku ikaelezwa Mwenyekiti amepata safari ya dharura.
Lengo za Ziada.
Kwa vile tayari kuna a bad Precedence ya Mwenyekiti kuanzisha maandamano lakini siku ya siku haongozi harakati hizo na badala yake huwa safarini, let's assume, safari ya kwanza ilitokea tuu kwa Mwenyekiti kuwa safarini genuinely bila kupanga kuyakimbia maandamano, lakini hili likijirudia katika mazingira yale yale, this time around hakuna atakayeamini imetokea tuu, kwa Mwenyekiti kuwa safarini!, this time tutaamini kuwa hiyo ndio mipango ya Mwenyekiti Mbowe! .
Umuhimu wa Taarifa Hii.
Hivyo leakage ya taarifa kama hii ikafanya hata kama ni kweli imetokea na tarehe za maandamano haya zimegongana na safari binafsi ya Mwenyekiti, kumtamfanya Mwenyekiti kulazimika kubadili tarehe za safari yake ili kwanza aongoze maandamano, ndipo aendelee na safari zake binafsi.
Safari Binafsi Vs Safari za Kikazi.
Miongoni mwa haki za binaadamu ni pamoja na uhuru mtu kwenda anakotaka, hivyo Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe naye kama binaadamu wengine wowote, yuko huru kupanga safari binafsi ya kwake na familia yake bila kuingiliwa na mtu kwa kanuni ya "right to privacy " ila pia Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe kama Mwenyekiti wa Chadema Taifa, then ana surrender his public life na his private conduct kwa the public, na sometimes kutakuwa ku sacrifice his family na private life needs for the public, pale ambapo mahitaji ya kumuhitaji Mbowe kuitumikia public kupitia uenyekiti wa Chadema Taifa yanapokuwa muhimu kuliko kumhudumia familia yake hivyo kui sacrifice family kwa mahitaji ya public, hivyo hata kama kuna mgonjwa nyumbani anayehitaji urgent attention ya kupelekwa kwenye matibabu Ulaya na huku mtu huyo huyo kuhitajika na chama kuongoza maandamano, kutegemea lipi kwake ni muhimu zaidi kati ya kumhudumia familia au kukitumikia chama. Mwalimu Nyerere alitanguliza taifa kwanza familia baadaye, na kinachotokea kwenye familia ya Mwalimu sote tunazijua. Sasa tusubirie hiyo tarehe ifike ili tujue kwa viongozi wa Chadema nini kwanza na nini baadae.
Pasco.
Update 1.
Wanabodi
Post 110 nimepata uthibitisho toka kwa trusted source from Chadema Mkuu Ben Saanane.
Hivyo kwa ujumbe huu toka Ben Saanane, inawezekana tetesi hizi ni uzushi, jee tuchukulie tangazo hili ndio taarifa rasmi ya Chadema tuufunge huu uzi, au tusubirie official response from Chadema office bearer na kusubiria kama Mwenyekiti atakuwepo mwenyewe physically hivyo, Tarehe 1 September .
Pasco
Update 2.
Hivyo uzi huu sasa unaweza kufungwa hadi
hiyo tarehe 1 September ambapo Mwenyekiti akiishaonekana tuu kuongoza maandamano, then uzi huu ufutwe rasmi.
My Take.
Hii ni genuine tip niliyoisikia toka nilikosikia. Mimi sio ndiye aliyetunga uzushi huu bali nilikuwa natimiza wajibu wangu kwa jf, be the first to know! , ila pia kama ni kweli safari ilikuwepo na sasa imefutwa, then bandiko hili limesaidia!.
Kama ni uzushi mwanzo mwisho, basi nachukua fursa kumuomba radhi Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe, wanachama, wafuasi, wapenzi wa Chadema na wana JF kwa ujumla kwa taarifa hii.

@WanaJamvi,
Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe.Freeman Mbowe hana mpango wowote wa kufanya safari nje ya nchi siku za hivi karibuni
Katika Hotuba yake ya Leo kwa vyombo vya habari hapa Arusha ameeleza kuwa atakua mstari wa mbele kwenye mapambano kama ilivyo siku zote.
Hivyo kwa ujumbe huu toka Ben Saanane, inawezekana tetesi hizi ni uzushi, jee tuchukulie tangazo hili ndio taarifa rasmi ya Chadema tuufunge huu uzi, au tusubirie official response from Chadema office bearer na kusubiria kama Mwenyekiti atakuwepo mwenyewe physically hivyo, Tarehe 1 September .
Pasco
Update 2.
Mode : Naomba tuchukulie taarifa hii ni rasmi kutoka Ofisi ya Mwenyekiti Taifa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema. Hivyo habari nilizozisikia kijiweni ama ni uzushi, ama safari ilikuwepo lakini kufuatia leakage hii, mipango imebadilishwa hivyo this time around, hiyo tarehe 1 September, Mwenyekiti atakuwepo kuongoza maandamano hayo yeye mwenyewe in person physically .USAHIHI KUHUSU SAFARI YA MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA MHE.FREEMAN MBOWE:
Usiku wa Leo Tarehe 22/08/2016 imesesambazwa Taarifa kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe.Freeman Mbowe amepanga kusafiri nje ya nchi tarehe 28.08.2016 yaani siku 3 kabla ya Maandamano na Mikutano ya Kisiasa iliyopangwa kufanyika kuanzia Tarehe 01.09.2016 kutetea na kulinda katiba na sheria za nchi
Taarifa hizo zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii ziliambatanishwa na Tiketi na Ujumbe Feki ili kuongezea uzito wa habari iliyosambazwa.
Ofisi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa Inakanusha Taarifa hizo za Uongo na Uzushi uliosambazwa kwa makusudi na kwa nia ovu(Maliciously) hasa kipindi hiki ambacho Watanzania Wamejiandaa kikamilifu kutekeleza haki yao ya Kikatiba ya kukusanyika na kupaza sauti zao kupinga Uvunjaji wa katiba na sheria za nchi ifikapo Septemba 01,2016.
Aidha,Watunzi wa Uongo na Uzushi huu wameendelea kuonesha dharau kwa Watanzania kwa kudhania kuwa hawawezi kutofautisha kati ya Tiketi ya Ndege na "Boarding Pass" iliyotengenezwa kwa njia ya Kompyuta kisha kuisambaza na kuupotosha Umma kuwa ni Tiketi ya Ndege.
Kwa kawaida "Boarding Pass" hupatikana siku ya Safari.
Mwenyekiti Wa Taifa Mhe.Freeman Mbowe yupo mstari wa mbele na anaendelea kutekeleza Majukumu yake kuhakikisha Maazimio ya Kamati Kuu juu ya Uanzishwaji na Utekelezaji wa Operesheni ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania(UKUTA) inafanyika kwa ufanisi na kwa kiwango cha juu.Hadi sasa Mwenyekiti anaendelea na vikao vya Kimkakati ndani ya Kanda ya Kaskazini kama ilivyopangwa kwa na pia viongozi wenzake ambao ni wajumbe wa Kamati Kuu waliotawanyika nchi nzima wanaendelea kuongoza vikao vya Kimkakati katika Kanda,Mikoa na Wilaya zote Nchini
Mwisho,Sambamba na Jeshi la Polisi kufanya Uenezi wa Operesheni UKUTA kwa kutojua kama umma ulivyoshuhudia kwenye vyombo vya habari jioni hii,Ofisi ya Mwenyekiti Taifa inapenda kuutahadharisha Umma juu ya Propaganda chafu zinazofanywa na Serikali na Chama Tawala kwa Kushirikiana na Vyombo vya Dola katika jitihada za kuupotosha Umma baada ya kuona Vitisho vilivyotolewa na Viongozi wa Serikali hasa Rais Magufuli na hata Jeshi la Polisi kwa kuwakamata na kuwatisha Viongozi Wetu na Wananchi wasio na hatia vimeshindwa kuonesha Dalili za Kuwarudisha nyuma Watanzania katika kutetea Katiba na Sheria za Nchi
Tunawatakia Maandalizi mema katika Ulinzi wa Katiba na Sheria za Nchi
Ahsanteni.
Imetolewa Na:
Ofisi Ya Mwenyekiti Taifa-Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).