Tetesi: MKT wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Kuanza Ziara ya Ulaya na US Kupitia Dubai 28/08/2016? !.

Kuna jamaa aliwahi kupost humu jinsi mwanaume mmoja wa Dar anayejiita AT alivyomsuta Peter Msechu.. Ila Dar kuna wanaume wasutaji na wazushi sana..! Utamwambiaje mwanaume mwenzako eti ana tumbo kama kameza Vitz??
Mkuu mada iliyopo mezani ni mwenyekiti kuanza ziara tarehe 28......
 
Naona pasco anajitahidi kufiti kwenye mfumo...unaoamini unafiki,uzandiki,uongo,ukurumbembe,fitna,majungu,umbea-uchwara,uandishi uchwara na kikampuni uchwara na kuzurura masokoni na magulioni kuhoji umbeya.
U-DC wa miaka hii
 
Pasco. Unaunga mkono UKUTA? Nimekuona na kukusikiliza leo Asubuhi kupitia Jicho letu ndani ya hahari cha Star TV. Ulichoongea kule ni opposite.
Nilikuwa nakuheshimu. Sijui lengo lako ni nini hapa ila kumbuka kuna usemi wa kuogopa watu wenye ndimi mbili
 
Nilikuwa namuheshimu sana huyu Pasco, ila kwanzia Leo nimekudharau kuliko neno dharau. Heshima yote uliyojijengea apa Jf umeibomoa kwa ajili ya sifa za kijinga.

Sijui haya majungu yanawasaidia nini
Huyu mganga njaa hua unamheshim kwa sababu ipi mkuu? Huyu huishi kwa kufata upepo ka bendera.
 
Kinyonga akijibadiri rangi habadiri ukinyonga wake. Pasco ni kinyonga ki hoja HAACHI.

Tetesi nilizo nazo ni jumba kuu kupanga safari, ajali za viongozi wa CHADEMA hata taarifa bandia na potofu kabla ya September 1.

Uhakika nilionao ni UKUTA upo pale pale.

Hofu yangu ya baada ya September 1 Je bado tutakuwa taifa la amani na tulivu?
 
Yeye aende tu si wapo misukule waliogeuza vichwa vyao kuwa vitalu vya kuoteshea nywele.

Hao makamanda uchwara wasiojielewa ndo wataangushiwa jumba bovu.

Machar naye kakinukisha Juba halafu kaenda kutalii DRC.
 
Inatumika kila mbinu kuzoofisha UKUTA watu wapo kazini wanazoofisha wananchi wasitokee siku iyo wanaogopa nguvu ya Umma siyo Pasco tu wengi watakuja kupotosha umma ili ukuta usifanikiwe UKUTA ndiyo unaowasumbua kwa sasa
 
Wanabodi,

Naomba kuanza uzi huu kwa ku declare my interest kuwa Mimi Pasco wa JF, naunga mkono maandamano na mikutano ya UKUTA nchi nzima na siku ya siku, nitajitokeza kushiriki na nitatoa wito wale wote wenye mapenzi mema na taifa hili, tujitokeze kwa wingi! .

Niko kwenye kijiwe fulani hapa mjini kati, jijini Dar es Salaam, nikainasa ndogondogo kuwa wakati chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema, kiko kwenye maandalizi ya maandamano na mikutano nchi nzima kuhamasisha UKUTA, siku ya Tarehe 1 September 2016, habari ambazo hazijathibitishwa, zimeeleza kuwa, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe, yuko kwenye maandalizi ya mwisho mwisho kuanza ziara binafsi ya Ulaya na Marekani kupitia Dubai. Ziara hiyo umeelezwa kuwa pia itahusisha matibabu, uchunguzi wa afya na mapumziko mafupi mjini Dubai. Mtoaji wa taarifa hiyo isiyothibitishwa, imesema ziara hiyo ni binafsi, ya kifamilia na ya kibiashara.

Mtoa habari huyu alijitambulisha rasmi kama mkereketwa wa Chadema, na kutaja majina yake, lakini kufuatia habari hizi bado hazijathibitishwa rasmi na uongozi wa Chadema, naomba nisilitaje jina la mtoa habari wangu chini ya kinga ya kihabari iitwayo "the confidentiality of the source " mpaka habari hizi zitakapothibitishwa au kukanushwa.

Kufuatia source wa habari hii sio a trusted source ndio maana habari hii ina lebo ya tetesi, ikiishatibitishwa, neno tetesi litaondolewa! . Sii mara moja wala mbili kwa tetesi mbali mbali kushuka jf na baadae zikathibitishwa au kukanushwa! .

Hii sii mara ya kwanza kwa kiongozi Mkuu wa Chadema kuanzisha maandamano lakini siku ya siku haongozi harakati hizo na badala yake huwa safarini kikazi au kibinafsi hivyo kuwaachia wengine waliopo.

Lengo la kuileta habari hii humu jf hata kabla haijathibitishwa ili ile jf spirit ya "be the first to know! ".

Ikitokea ikathibitika habari hii sii ya kweli bali ni uzushi tuu, nitamuomba mode, asiufute uzi huu bali aufunge tuu kusubiria hiyo tarehe 1 September tuthibitishe this time around, Mwenyekiti atakuwepo kuongoza maandamano.

Lengo la kuomba uzi usifutwe bali ufungwe tuu, ni kufuatia posibility ya Chadema kuikanusha taarifa hii kuwa sii kweli lakini siku ya siku ikaelezwa Mwenyekiti amepata safari ya dharura.

Pasco.
AKIFANYA HIVYO BASI ATAKUWA AMEIUA CDM , afadhali awe hapa lakini asishiriki kwa namna na sabau yoyote kuliko kwenda nje!
 
Uko

Upo sawa Pasco
 
Back
Top Bottom