Mkubwa Fella awaita wandishi wa habari kuwaonyesha majumba aliowajengea Yamoto Band

Hao watu ndio walivyo hivyo, dereva anaendesha basi kutoka Dar mpaka Mwanza hata hawamwambii asante, bali wanamshukuru Yesu kwa kufika salama, kama Yesu alijua kuendesha gari vile.
Ipo siku!
 
Ni jambo jema sana kawafanyia hawa madogo...atakaeponda ajichunguze
 
Hata mi sijapenda hiyo saresare maua.

Utadhani nyumba za kota...

Halafu sasa haya makundi huja kuvunjika. Likivunjika hilo kundi sijui ndo itakuwaje..

Ila kwa ujumla wake ni jambo jema.
Hamna mkuu hii ni kambi, wanachukuliwa vijana wanaendelezwa vipaji vyao (Kumbuka wengi huwa wanachukuliwa kutokea familia masikini au mikoani) akiwa msanii mkubwa atapata show nyingi na pesa hivyo kumuwezesha kujenga nyumba anayoitaka. Sema madogo huwa wanakuja hawana kitu, wakiwa mastaa wanaendekeza starehe nakujikuta kuhisi wananyonywa.
 
Mtu asiye na jazba anisaidie anieleweshe, kwa nn kawajengea sehem moja? Je wanaruhusiwa kutumia nyumba hizo kama vitega uchumi? Ningependa kujua , nani ana hati miliki ya nyumba hizo? Kama huna jibu then futa huo uzi ukapate majibu coz ukishaleta hapa umelikoroga utalinywea tu! Vp akiamua kutoka kwenye kundi leo,?
 
Hata mi sijapenda hiyo saresare maua.

Utadhani nyumba za kota...

Halafu sasa haya makundi huja kuvunjika. Likivunjika hilo kundi sijui ndo itakuwaje..

Ila kwa ujumla wake ni jambo jema.

Miafrika Ndivyo Tulivyo
 
Ni nguvu zao ila nadhani anawasaidia kuwa manage kwa kuwekeza vipato vyao mahala sahihi akiwapa mapato yote watawekeza kwa wema, wolper na kwenye heineken.
Hata wa kishuka walau watakuwa na pakujihifadhi nahisi aslay hii itakuwa nyumba yake ya pili.
Well said
 
Kumbe kambi sio kwamba ni nyumba zao
Ni nyumba jamani,ndio maana kasema hata wakija kupata wake zao wataishi hukohuko ila kwa ndani kuna vimilango vidogo kama wakitaka kusalimiana
 
Hata kama anawapiga pesa,kwa alichofanya,anastahili pongezi,kwa huu muziki huu usiodumu muda mrefu na soko lisilo na uhakika ni jambo jema sana kuwa na kibanda,kwani kuna wasanii walikuwa juu sana kisanaa mfano Mr Nice,wakajisahau bata kwenda mbele,sasa hivi kwisha mbaya...
 
Hapo kapata faida mara nne ya gharama za izo nyumba
All in all respect to you...kwa afrika maisha ni nyumba
 
Afute uzi? Tuambie wasema hayo kwa mamlaka ya nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…