GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Siku nyingi sana na hapa JamiiForums ( walio wengi watashuhudia kwa akina Tomaso waliojazana ) GENTAMYCINE nilisema kuwa kama kuna Mchezaji ambaye si tu ninammudu bali pia namjua ndani nje kwakuwa kakua namuona ni Jonas Gerald Mkude.
Na ndiyo maana baada ya Leo kusikia kuwa ana Uwezekano wa kwenda Yanga SC niliwashangaa mno wana Simba SC ambao wameogopa na Kuhoji kwanini Kaachwa.
Leo GENTAMYCINE nitasema hapa Mambo Mawili tu kumhusu Mkude ambayo nina uhakika nayo kwa 100% na nayaandika hapa huku nikijiamini nayo kabisa.
1. Jonas Gerald Mkude ni mwana Yanga SC 100% ila alikuwa ni mwana Simba SC kwa Usoni tu na Kumridhisha Rafiki yake mkubwa Mwekezaji Mo Dewji ( kutokana na Kumfanyia Biashara moja hivi yenye Utajiri wa haraka ) miaka ya nyuma na pia Kumridhisha Kocha aliyemuibua Utotoni na mwana Simba SC Selemani Matola na Meneja Patrick Rweymamu.
2. Kwa tuliokuwa na mpaka leo tunashinda na Kukutana nae mara kwa mara Maskani za Kawe kwa Rafiki yake mkubwa Pazi, Kinondoni Kanisani Kwao kwa Rafiki yake mkubwa Chata na Tandale kwa Masela wake akina Dula, Zubery na Taita tukisikia uwezekano wa kwenda Yanga SC hatushangai kwani kila Akilewa Pombe na Mjiti wake husema kwa Sauti Kubwa kuwa lazima kabla ya Kustaafu kucheza Soka akacheze Yanga SC ili amfurahishe Mama yake Mzazi ambaye ni mwana Yanga SC lia lia.
Kwa faida yenu Jonas Mkude Siku nyingi ( Miaka mingi ) alikuwa akitaka kwenda Yanga SC ila aliyekuwa akimuogopa ni Marehemu Baba yake Mzazi ambaye alikuwa ni mwana Simba SC kindaki ndaki.
Kipindi Marehemu Baba yake anaugua wakati anakaribia Kufariki akiwa Mkoani Morogoro alimuita Mwanae Jonas Gerald Mkude pamoja na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Simba SC kipindi hicho Godfrey Nyange 'Kaburu' na Mmoja wa Waanzilishi wa Kundi la Friends of Simba Marehemu Zackaria Hanspoppe ambapo Marehemu Baba yake mbele yao alimwambia Mwanae Jonas kuwa aiheshimu sana Simba SC, wana Simba SC na Viongozi wa Simba SC kwani wamemjali mno japo hana Elimu Kubwa, wamemjengea Nyumba, wamempa Gari na wanamtunza Yeye Baba yake kipindi ambapo anaumwa hivyo Asante yake kwa Simba SC ni kwa Jonas Gerald Mkude kuendelea Kuichezea tu Simba SC na si kwenda Kwingineko.
Akienda Yanga SC laana hazimuachi.