Mkude gangwe!

Mkude gangwe!

kaah! nimepitia posts zote hizi sijaona sehemu mkude amejibu hata moja? KWELI NIMEAMINI MKUDE NI TOZI, YAANI NI ZAIDI YA GANGWE. ha ha ha ha ha ha ha!
 
Mkude bwana, gwange hasa. Yupo kweye ATM anataka kutoa pesa. Pembeni kuna kibaka anachungulia nambari ya siri ya Mkude.
MKUDE: Wewe unajihangaisha bure, katu huwezi kuijua nambari yangu ya siri, ninaijua mwenyewe tu.
KIBAKA: Mwongo Mkude, hata wewe mwenyewe huijui, hebu itaje niamini kama unaijua kweli.
MKUDE: Nambari yangu ni 8905671234 na hakuna mtu anayeijua isipokuwa mimi. Potelea mbali huko!
 
Mkude gangwe,katumwa na mzungu akalete 'meat' kilo 5,yeye akaenda porini kukata miti mitano akamletea mzungu!
 
Mangi analalamika kwamba mswaki una brush ngumu unamuumiza fizi,Mkude akamwambia;Ja! unalalamika nini Mangi,huo mswaki wenye brush ngumu ndo mzuri utadumu muda mrefu!
 
Mjomba mkude kweli gangwe kadondoka juu ya mti mpaka chini kaulizwa umeumia kasema hapana kapelekwa hospitali karudi na magongo...
 
Mkude Gangwe kwelikweli, kamdindia Katibu Kata kulima shamba la kijij

Mkude Gangwe kweli, kapanda Mabasi mawili (IKARUS) kalipa shilingi......

Mkude Gangwe kweli, kapanda basi kutoka Morogoro badala ya kushukia Ubunge, kashukia Kariakoo, kamkomoa Dereva.
hahaaa......Mkuu umesahau, huyo wa mwisho alikuwa wa kuliboma (mpogoro) katoka zake Mahenge na dawoyi (Dar oyeee) anakwenda Dar, ubungo. kufiki ubungo akaanza kumsimulia mwenyeji wake; ''Leu nimimkomeshi dereva kwelikweli, darwoyi limifika ubungu kondakta kasema ubungu ubungu mi nikabashi, ubungu ubungu nikabanisha, mpaka tumifiki kariikoo mi nikashuki nikachukui taxii mpaka ubungu. Mi gangwe kwelikweli si mchezu''.
 
Mke wa mkude gangwe kaenda dukani kununua vitu,akatupa kikapu jalalani ili akapewe paper bag ya bure!
 
Mkunde ni zaidi ya noma, amnamsimulia mwenzake kisa cha kuwa na chongo. akasema alikuwa amejilaza chuni my miti wa minyaa huku akimchungulia ndege aliyekuwa juu ya mnyaa huo kwa bahati mbaya utomvu wa minyaa ukawa unadondoka akaona uvivu kufumba macho na utomvu ukaingia jichoni hatimae akawa na chongo!!
 
Mkude Gangwe kweli, nae ni Great Thinker ..............
 
Mkude akajaribiwa na kibaka katika ATM..wewee nimeona pin yako.ni nyota nne..yaani **** mkude akacheka sana na kumuambia umenoa...ni 5865.
 
tehe tehe very funnny...........................
 
Mkude alikwenda hospitali kawekewa kipima joto kinywani akakimeza. Nesi kumuuliza kiko wapi kajibu ameshameza anangojea dawa ingine
 
Mkude alikwenda hospitali kawekewa kipima joto kinywani akakimeza. Nesi kumuuliza kiko wapi kajibu ameshameza anangojea dawa ingine
Buhahahahaaaaaah!
 
Mkude gangwe kaona mkewe hataki kuacha kuvaa suruali za kubana,akaamua kumkomoa mkewe na yeye akaanza kuvaa mini-skirt.
 
Loh, kweli Nkude gangwe, siku 1 alintembelearidhika na hali ya Nkude kuvaa viatu vya kulalia, yaani kutembelea rim. Akampa buku jero akanunue ndala pale MoroStores. Massawe akamwambia kuwa bei ya ndala ni moja tu; buku unusu. Sasa Nkude yeye anavaa saizi namba 7, lakini kwa ugangwe wake akamwambia Massawe ampe namba 12, "Mweeh, yaani unataka kunipa hivyo vitoto wakati hiyo mikulubambe bei moja, mwéeeh, lete hizo kubwa wewe, mi siyo mjinga mjomba, huko ninakotoka wananiita mi gangwe!"
 
Aaah!!Mkude nimemkubali kweli gangwe,aligoma kula maandazi badala yake akaagiza vitumbua ili apate mafuta ya kupakaa.....msikie hapa anamuagiza dada yake"Agwe Mwenda,seke ugule maandazi,kagule vitumbua chivije na mafuta tubakale"
 
Mkude ni zaidi ya gangwe,kaenda hotelini,kaagiza msosi wa bei mbaya,alipoletewa akaulipia kisha akaumwaga dustbin ili kuwakomoa wahudumu halafu akafungua hotpot lake lenye mihogo tele kutoka matombo na kuanza kuila taratibu.
 
Back
Top Bottom