Mkude ndiye kiungo bora wa chini kuwahi kutokea nchini?

craq

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
859
Reaction score
1,866
Kuna watu najua wanaabudu vya zamani vitu vikongwe hio ni kawaida kwa watu wengi wapo hivyo watakuja kupinga ila huu ndio ukweli

Jonas Mkude ndio kiungo wa chini bora kuwahi kumuona Tanzania na huenda akawa bora kuliko wote.

Mkude ni modern midfielder anacheza kiungo wa chini lakini ni mbunifu ,viungo wengi wa chini haswa wa zamani ni wakabaji wazuri lakini footwork yao mbovu lakini kwa Mkude ni tofauti ni mzuri wa kupiga pasi na pass accuracy yake ni nzuri sana ,


Pili ni deep lying playmaker ni kiungo mbunifu anayecheza chini anapokea mipira kutoka kwa beki na kuanza kucheza timu kwa kupiga pass na kupokea na kutembeza pasi na kufanya timu imiliki mpira muda mrefu


Tatu ana akili na mtulivu anapokea pasi anatoa pasi anafungua chumba kingine na kupokea pasi na kutoa ,ukimtizama unaona muda wote ana hamu ya mpira anaomba

Tokea Mkude aanze kucheza Simba sijaona timu pinzani ikaishinda simba kwa umiliki wa mpira

Mawakala wamfanyie mpango Mkude ,Mkude ana kila sifa ya kucheza nje ya nchi
 
Inategemea lini ulianza kufuatilia soka letu. Mimi nimeanza tangu miaka ya 1980 ambapo viungo bora kwa Yanga na Taifa Stars alikuwa Charles Boniface Mkwasa, pia alikuwepo Hussein Ngulungu wa Tumbaku ya Morogoro, na Mohammed Adolph Rishard wa Pan Africa na Taifa Stars, hao ndio walikuwa viungo wakabaji bora, hasa Charles Boniface.

Kwa Simba kulikuwa na Nico Njohole (Mapafu ya Mmbwa ) alikuwa hachoki na akihaha uwanja mzima. Baadae alikuja Ramadhani Lenny Maufi (Abega), huyo alikuwa vizuri sana, akichezea Simba na Taifa Stars na alienda kucheza Arabuni kabla ya kurejea Simba. Mkude anajitahidi na kwa kuwa bado ana muda mrefu wa kucheza iwapo atajitunza, anaweza kuweka historia.

Kwangu viungo wakabaji bora tangu miaka ya 1980 hadi leo ni hao.

Vv
 
mtoa mada hayo ni mawazo yako mazuri tu na tuwe na haki ya kutofautiana,ila kwangu mimi wakati nchi inacheza mpira sio chakacha ya sasa,viungo wafuatao walikuwa moto,Aluu Ally,Mohamed Richard(Adolf),Nicodemas Njohole,Masha(Pamba FC),Ramadhani Lenny,hawa walikuwa ni attacking and box to box viungo wa kati,ninakumbuka wakati nchi ina adabu kila kitu kilikuwa na adabu.
 
Mkude ana mapungufu mengi kuliko faida, kwenye transition yupo slow, anacheza back pass nyingi sana.Mzito Ku turn ana piga pass ulekeo mmoja tu, uelekeo ule anao tizama. Mzito/simzuri kwenye mipira yajuu,Ana bebwa na mfumo kwakua anazungukwa na viungo wengine wanne ,Angalia alipo achiwa acheze six bila viungo wasaidizi uone Kilimanjaro stars ilivyo teswa kwenye Challenge. Mzito kuitoa timu nyuma ili isogee kwenye goli la mpinzani.
Yeye mwenyewe yuko slow sana kimaamuzi. Ana achwa mbalisana na James Kotei kwa ubora katika eneo la namba sita.
Anacheza mamba mmoja tu. Kwaujumla hauziki nje ya nchi kwa namba anayo cheza kwa maana halisi ya mamba sita, labda afanye mabadiliko makubwa kwenye Soka lake.
Sifa ninayo iona kwake ni uwezo wa kuficha Mpira akiwa nao, anafaa kucheza timu ikiwa imeshinda ili a hold Mpira na si wakati timu inatafuta Ushindi.
Anapenda kufanya vitu visivyo na sababu yaani kucheza na jukwaa, Anatakiwa Ku focus kwenye mambo ya msingi ambayo ni kusaidia Mpira utoke kwenye eneo lake la goli kwa haraka na uhakika.
 
Uliwahi kumuona ATHUMANI CHINA? na HAMISI GAGA? hawa watu ni hatari sana,, hyo mkude anajaribu tu.... Sio FUNDI wa muda wote
Huko umeenda braza.hawez kukuelewa mtoto wa dotcom huyo...huyo mkude hajafikia kiwango cha marehemu Godfrey bony..au athuman iddi chuji wakati wake..achilia mbali kina china..gaga..method mogela (rip)..
 
Mkude yuko overrated na wavuta bangi wenzake....pass 10 mbili anapiga mbele..hana mbio.hayuko aggressive...kwangu namba sita bora Waziri Mahadhi kamuulize Matola alikuwa anasubiri Taifa stars
 
Nadhani hukuwahi kuwaona wakina Athumani idd chuji,marehem Godfrey bony ndanje, Waziri Mahadhi.
 
Nafuu umfunulie dogo yaliyopo katika soka haswaa.
 
Mkude bado uwezo wa soka mdogo sana kwa magwiji waliomtangulia kwenye soka
 
Mkude huyu ambaye hata Timu ya Taifa hafurukuti? Ulizia wanawajua akina Ali Maumba(Coastal Union). Hussein Masha(Pamba & Simba). Isa Athumani( Yanga). Au Michael Paul "Nylon" ( Simba)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…