Mkude Vs Pappy Tshimbi nazi zaidi

Shishimbi ni ni box to box ni kama Kamusoko, ukimchezesha sita anacheza vizuri, 8 anacheza vizuri ata 10 japo hajawai chezesha lakini Nina uhakika ataimudu. Anajiamini na ana maamuzi ya haraka na sahihi ndio maana ata zikicheza simba na yanga, Simba huwa inakua na viungo watano lakini shishimbi mwisho wa mchezo anaonekana bora.
 
Anatakiwa aisaidie timu yake katika michezo yote, sio dhidi ya Simba tu. Lengo liwe kushinda, sio kutoa sare
 
Naomba nitofautiane kidogo na wewe mkuu. Unaweza kishindanisha mchezaji wa nafasi yoyote dhidi ya nafasi nyengine tofauti, ilimradi umeweka vigezo. Kwa sababu kimsingi wachezaji wote wanahitajika kuwa na sifa zinazofanana kiujumla ( mf. Control, endurance, stamina, speed, strength, mobility, n.k.).Hata hizo sifa tunazohisi ni za wachezaji wa nafasi fulani tu (mf. ufungaji, kutengeneza pasi za mwisho, kukaba) zinatakiwa kila mchezaji awe nazo. Zipi kati ya sifa hizo mchezaji anazo zaidi ndio huamua acheze nafasi ipi. Kadri anavyokuwa nazo nyingi ndivyo mchezaji anavyomudu kucheza nafasi nyingi. (Mf. Mrhm Said Mwamba). Lakini ni nadra kumkuta mchezaji mwenye sifa zote hizo, ndio maana ni taabu kimkuta golikipa akicheza ndani (ukiondoa akina Rene Higuita). Kwa ufupi, ni sahihi kushindanisha wachezaji wa nafasi tofauti (ndicho kinachofanyika kwenye Ballon d’or na tozo nyingine kubwa kubwa) lakini vigezo ni lazima viwepo. Na kwamba mchezaji anayemudu nafasi nyingi zaidi uwanjani ni bora zaidi kuliko anayemudu chache.
 
Hujajibu swali zaid ya kuzunguuuuuuuuuuuka hata sijui ulikuwa unataka kusema nini?
 
Nimekupa like kwa analysid nzuri. Umekosea kushabikia rangi za Yanga
 
Wewe una akili za nzi, mkude anacheza nafasi gani.
Kufunga magoli ni uwezo na kipaji! Uwezo wa Mkude kufunga ni mdogo bila kujali nafas anayocheza! Mbona Asante Kwasi ni beki lakin uwezo wake wa kufunga ni mkubwa sana! Kubali tu kwamba Shishimbi amemzidi Jonas!
 
Siri moja kubwa sana ya Simba kupata ushindi mnono kwenye ligi ni baada ya Omog kuondoka maana alikhwa anamuweka Mkude bench.
Alipokuja Djuma akagundua Mkude ni bonge la midfielder, na sasa ndio tegemeo pale kati.
Simba hawakumchezesha kwenye mechi yao na Mwadui na katikati pakafa kabisa wakabaki Mwadui wametawala kati, matokeo yake ni draw.
Nasubiri mechi ya Yanga na Simba maana sasa Mkude na Ndemla watakuwa kati ili nimuone Tshishimbi kama atacheza mpira.
 
Nimekupa like kwa analysid nzuri. Umekosea kushabikia rangi za Yanga

Tena naomba unitake radhi upesi kama siyo haraka Mkuu kwani naamini kwa kila anayemjua GENTAMYCINE humu JamiiForums anajua kuwa Mimi ni Mnyama Mnyamani ' lia lia ' au ' kindakindaki ' nikimaanisha ni Mshabiki na Mwanachama wa Simba Sports Club. Umenitibua sana kuniambia Mimi nashabikia Yanga SC Mkuu.
 
Kufunga magoli ni uwezo na kipaji! Uwezo wa Mkude kufunga ni mdogo bila kujali nafas anayocheza! Mbona Asante Kwasi ni beki lakin uwezo wake wa kufunga ni mkubwa sana! Kubali tu kwamba Shishimbi amemzidi Jonas!
Sio kipaji ama uwezo tu, usiozingatia nafasi gani unacheza, Basi Yondani angekua na magori mengi tu, Ukimshanga Kwasi, utamshangaa na Kapombe na Kesi.
 
Kwenye umri ni uongo!!

Mkude ni sawa na Papii.

Chezea Okwi ana 25 hadi leo
 
Akhsante ila masahahisho kidogo Mimi siyo Mkurya kama labda unavyojua au kuhisi bali Kiumeni ni Mzanaki kutoka Mara ( Tanzania ) na Mtutsi kutoka Gisenyi ( Rwanda ) na Kikeni ni Mmakuwa na Mmwera kutoka Mikoani Mtwara na Lindi.

Kila la kheri.
Wewe Ni mmakuwa au mmwera kwani huko mtoto anarithi kwa mama
 
Ballon d'or haishindanishi wachezaji wawili kama thread hii ilivyokuja. Inashindanisha wachezaji wote wa soka duniani
 
Ballon d'or haishindanishi wachezaji wawili kama thread hii ilivyokuja. Inashindanisha wachezaji wote wa soka duniani

Sawa. Lakini je hao wachezaji wote wa soka duniani wanachezea nafasi ya aina moja kama alivyohoji niliyeomba kutofautiana maye, au ni kwa nafasi tofauti kama ninavyodai mimi?
 
Sawa. Lakini je hao wachezaji wote wa soka duniani wanachezea nafasi ya aina moja kama alivyohoji niliyeomba kutofautiana maye, au ni kwa nafasi tofauti kama ninavyodai mimi?
Ndio maana nimekwambia, Balon d'or ni halali kulinganisha wacheza soka wa nafasi zote kwa sababu inatafuta mchezaji bora miongoni mwa wacheza soka wote duniani, tofauti na uzi huu ambao unalinganisha wachezaji wawili tu duniani
 
Ndio maana nimekwambia, Balon d'or ni halali kulinganisha wacheza soka wa nafasi zote kwa sababu inatafuta mchezaji bora miongoni mwa wacheza soka wote duniani, tofauti na uzi huu ambao unalinganisha wachezaji wawili tu duniani
Unajua hoja yangu ya msingi lakini, au unataka kubishana kwa ajili ya kubishana? Narudia tena kukukumbusha na sidhani iwapo utaendelea kukariri ubishi huohuo nitaendelea kujibizana nawe. Nilichosema, na ndicho unavyosema wewe bila ya kujijua, ni kwamba ni sahihi kushindanisha wachezaji wawili wa nafasi tofauti uwanjani, kwa sababu vigezo vya msingi vya uchezaji ni kwa wachezaji wote, bila ya kujali nafasi wanazochezea. Na ushahidi wa hilo ni hiyo Ballon d’or inayoshindanisha wachezaji bila ya kujali nafasi wanazocheza. Kwa hivyo si makosa kushindanisha ni nani bora kati ya Tshishimbi na Mkude. Wassalaam!
 
Umelinganisha vizuri sana shemeji ( tumeoa mkurya).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…