Unajua hoja yangu ya msingi lakini, au unataka kubishana kwa ajili ya kubishana? Narudia tena kukukumbusha na sidhani iwapo utaendelea kukariri ubishi huohuo nitaendelea kujibizana nawe. Nilichosema, na ndicho unavyosema wewe bila ya kujijua, ni kwamba ni sahihi kushindanisha wachezaji wawili wa nafasi tofauti uwanjani, kwa sababu vigezo vya msingi vya uchezaji ni kwa wachezaji wote, bila ya kujali nafasi wanazochezea. Na ushahidi wa hilo ni hiyo Ballon d’or inayoshindanisha wachezaji bila ya kujali nafasi wanazocheza. Kwa hivyo si makosa kushindanisha ni nani bora kati ya Tshishimbi na Mkude. Wassalaam!