Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)

Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)

SEHEMU YA 113




Watu wote walikuwa kimiya wakitaka kusikia kauli ya shahidi huyo mpya, hasa pale alipotoa ombi,kwa mwenyekiti, la kuomba jambo ambalo hakuliweka wazi, na mwenyekiti akiwa na mashaka na huyo shahidi akamuuliza ni ombi gani hilo,

Tuendelee na kisa chetu..........


‘Kitu gani unachotuomba, ..?’ akauliza mwenyekiti

Badala ya shahidi kuongea, …yeye akatoka pale alipokuwa amekaa, akimpita mumewe, na kutembea kwa haraka hadi pale alipokaa mwenyekiti na kuanza kumnongoneza jambo…

Mwenyekiti, ilimshika kwa shutukizo, hata hivyo akawa makini kusikiliza kile anachonong’onezwa, huku mke wa mwenyekiti akiwa anatizama tukuio hilo kwa macho yenye shauku au mshangao fulani.

Kwa jinsi ilivyoonekana, mwenyekiti alionekana kama kutokukubaliana na hicho anachoongea huyo shahidi, akaonekana kama kupinga, kwa kutikisa kichwa mara kwa mara kama kukataa, lakini huyo shahidi hakuonekana kukata tamaa,...

Baadaye mwenyekiti akasema , kwa sauti ambayo tulimsikia ;

‘Nitampigia yeye mwenyewe, atajua ni nini la kufanya lakini mimi sitaki kabisa utaratibu huo...’akasema.

Shahidi akaonyesha ishara kuwa hataki hayo wanayoongea yasikiwe na hapo mwenyekiti akashusha sauti..na wakaendelea kuongea kwa namna hiyo na shahidi akazidi kusisitiza jambo, na alipoona mwenyekiti hakubaliani naye, akainuka maana pale alikwua kamuinamia mwenyekiti.

Ilionekana sasa kakata tamaa, kwanza hakugeuka moja kwa moja kule alipotoka, alichofanya ni kusogea kinyume nyume akiwa kama katahayari, hatua moja mbili kinyume nyuma halafu kawa haraka akageuka na kurudi sehemu yake.

Alipofika pale alipotakiwa kukaa,…maana yeye alikuwa akiongea akiwa pale pale sehemu aliyokuwepo, kinyume na wengine ambao walikuja mbele sehemu maalumu ya muongeaji,..alipofika pale karibu na mumewe, mumewe akamuuliza

‘Ulikuwa unamuambia nini mwenyekiti..?’ akauliza docta, lakini mdada hakumjibu mumewe, moja kwa moja akaanza kuongea;

‘Nafahamu kabisa wote humu ndani ni watu wenye hekima, akili na utashi wa kufikiri, haya nitakayowaelezea hapa ni mambo ambayo sikustahili kuwaelezea, ni mambo ambayo nilitakiwa niwaelezee polisi,..kwa utaratibu ulivyo, na hata mwenyekiti anafahamu hilo..’akatulia

‘Hata hivyo, mimi kwa uoni wangu, nahisi haki inaweza isitendeke, kama hali ilivyo itaendelea kuwa hivi..mimi ndiye niliyehusika moja kwa moja na tukio lilitokea ndani kwenye muhusika mkuu, hapa nikiwa na maana marehemu..na ndio maana polisi wananihitajia au sio…’akatulia akimuangalia mwenyekiti.

Lakini kuna mambo yalifanyika hata polisi hawafahamu, na sikutaka kuwaambia wao kwanza, kwasababu nafahamu kabisa watakumbilia kunishikilia, na wakifanya hivyo kuna mambo meng ya ushahidi yatapotea…

Sasa kwa ajili ya kuliweka hili jambo sawa, nimeamua kumuomba mwenyekiti aniruhusu niweze kuliezea hilo tukio kiundani zaidi, ili nyie muwe mashahidi wangu, na sitaongea uwongo, nataka niuseme ukweli wote ulivyokuwa,…leo nipo hapa, kesho naweza kuwa jela, na jela ni jela..huko nina maadui wengi, je nisipotoka hai,..je kesi hii ikichezewa faulo,..najuo hilo ndilo linataka kufanyika…’akasema

‘Na zaidi sitaki watu wakitoka hapa wawe na maneno yenye utata, nataka nyie mkitoka hapa muwe na ukweli,..ambao utaweza kuwasaidia wenye haki zao, kwasababu hili halitaishia hapa, hivi ni vita virefu vyenye hatua zake, leo hii nitakamatwa mimi, kesho itajengwa haoja nzito, ..nina wasiwasi sana na hili…’akatulia

Mwenyekiti sasa alikuwa akiongea na mkewe, wakawa nao hawakubaliani, inaonekana hilo swala sasa linakuwa nyeti, na mwenyekiti anakuwa kwenye wakati mgumu.

‘Najua nitakamatwa, na…mume wa familia …lakini je nikikamatwa mtakuja kuamini hayo watakayosema polisi, …kuhusu muuaji, …hebu kwanza niwarejeshe nyuma kidogo, nilipowahi kuongea na marehemu kabla ya kifo chake, aliniambia maneno ambayo nayakumbuka sana, na leo hii naona kama yanaweza kuleta mantiki japokwua tunaweza kusema aliyaongea kuhalalisha dhamira yake...

Mwenyekiti aliposikia hivyo, akainua simu yake na kumpigia mtu, na kumfanya shahidi atulie kwanza, na mwenyekiti akawa anaongea na simu huku akiwa kainama na alikuwa akiongea kwa sauti ndogo, kama vile hataki watu waliopo humo ndani kusikia anachoongea, na alipomaliza akasema;

‘Samahani kidogo, nilikuwa naweka mambo sawa, ...haya shahidi unaweza kuendelea na maelezo yako, lakini bado, sijarizika na hoja yako, endelea kutokana na ulivyoamriwa, unasikia, sehemu za kipolisi hapana, sija…endelea....’akasema mwenyekiti akionyesha kukerwa na kitu, na shahidi akatulia kwanza akimuangalia mwenyekiti na baadaye akasema;

‘Ni hivi...Makabrasha hayupo peke yake, japokuwa wenzake, wameamua kujifanya hawahusiki, na hata mimi sikuwahi kuwa na hawo wenzake kwa karibu,ila niliwahi kusikia wakiongea na Makabrasha wakipanga mipango yao..’akatulia akimuangalia mwenyekiti kwa uso wa kusubiria jambo.

Makabrasha alikuwa akitumika, …kuna watu wakubwa walikuwa juu yake na wao hawakutaka kufahamika,..na kwa nafasi yangu siwezi kusema lolote kuwahusu hao watu, lakini ni mambo ya kisiasa na upinzani wa Nyanja hizo,…

Kuna mtu mmoja ambaye alikuwa akifika mara kwa mara kuonana na Makabrasha, …nitakuja kumuelezea mwishoni kama mambo yakienda sawa huyo alikuwa kama mtu kati, na mambo yake sio rahisi ni mjanja ..mwenyekiti, niendelee au ....’akaelezea huyu shahidi akimuuliza mwenyekiti, na mwenyekiti akawa kimia tu, yaonekana alikuwa hataki hicho anachotaka kukielezea huyo shahidi.

‘Kwahiyo hili jambo sio swala dogo kama mnavyolifikiria nyie, ...mimi nitajitahidi kuelezea upande wa mtu wetu tu, ambaye anatuhusu sana,...huko kwingine hakuwahusu, kwahiyo ni bora nifuate sheria, lakini nitaelezea yale yenye kulata tija...kwa manufaa yenu, na kwa manufaa yangu pia,...’akainama kama anasoma jambo.

‘Nimesema nitawarejesha nyuma kidogo, ili muweze kunielewa, kwa wenye kuelewa wataelewa, na hata mkisikia leo nimekamatwa, au ku-uwawa, mjue jinsi gani ya kulieleza hili kwa jamii...’akasema sasa kwa sauti ndogo yenye kukatisha tamaa.

‘Mwenyekiti nafahamu toka awali umekuwa makini na swala hili, nafahamu ni kwanini, na nafahamu kuwa wewe na polisi mnaaminiana sana, lakini nakupa angalizo, kuwa kumbukumbu nyingine walizokupa wewe, ni za uwongo, kuna mambo wameyaficha..’hapo akasema kwa sauti na mwenyekiti akataka kumkatiza shahidi.

‘Mwenyekiti hili inabidi nikuambie …maana naona utafanya nishindwe kabisa kuelezea kile ninachotaka kukuelezea,…hao polisi, siwalaumu maana wao wanafanya kazi kutokana na ushahidi…lakini ushahidi waliokuja kuupata ni wa uwongo, ukweli halisi ulishaharibiwa,,,kwa makusudi, huenda ni katika mbinu zao kwa ajili ya kufanikisha kazi zao, au ni kwa ajili tu ya kuficha ukweli...mimi huko sitaongelea sana kuthibitisha hilo, lakini huo ndio ukweli, ..nakusihi mwenyekiti usiegemee kwenye ushahid wao wa moja kwa moja, kama ningepata nafsi ya kuliezelea hil kiundani ungelinielewa....’akasema

Mwenyekiti sasa akaniangalia mimi, na mimi pale nilipo nilitaka kumuambia mwenyekiti amruhusu tu mzungumzaji ili tuusikie huo ukweli, akam ni ukweli ili mambo yaishe, lakini kwa nafasi ya mwenyekiti ilikuwa ni ngumu sana, nililielewa hilo, siwezi kumlaumu mwenyekiti..lolote atakalofanya sasa linaweza kutafsiriwa vibaya,na inaweza kumweka mahali pabaya..

‘Nafahamu kabisa kuwa mwenyekiti hunifahamu undani wangu, zaidi ya historia ya wazazi wangu, ila kwa hapa Dar, hukuwahi kunifahamu nilichokuwa nikikifanya zaidi ungeliweza kunifahamu kwa kupitia kwa bosi wangu..zaidi ni kunielewa kuwa mimi ni mke wa docta, na wewe ulikuwa mstari wa mbele kuipinga ndoa yangu…’akatulia

‘Kiukweli mimi siwezi kukulaumu sana kwa hilo, ...kwa vile unafahamu sana asili ya huko nilipotoka, na kwa hekima zenu, haya yanayotokea kama tungeliwasikiliza nyie huenda haya yasingelitokea. Au sio ..?’ akawa kama anauliza

‘Lakini mimi nasema tu vyovyote iwavyo, yote ni maisha, haijalishi wewe unatokea nafasi gani katika maisha, uwe masikini au tajiri maisha yanawezekana, au sio, lakin kama mzazi ulijaribu kutimiza wajibu wako, na kwa hilo siwezi kukulaumu, ila sasa, dunia itabadilika vipi kama tukijitenga, ina maana wenye nacho watabakia kuwa nacho na wasio kuwa nacho wazidi kudidimia, hapo ndio namkumbuka marehemu....’akasema shahidi.

Marehemu aliniambia,…vyovyote iwavyo, tajiri hawezi kumuamini masikini, akishajua kuwa wewe ni masikini, na unatokea daraja hilo, itampa shida sana kumuamini mtu kama huyo..na vyovyote iwavyo, tajiri hatapenda kushirikiana kwenye utajiri wake na masikini, kwanini, ..ni kwa dhana ile ile ya kutokumuamini..

Marehemu alitokea kwenye maisha duni, japokuwa alisoma, …ni maisha kama haya ya kwetu, …mimi nilikuja kuliamini hilo, kama alivyokuwa akiongea marehemu, ndio maana nikawa najichanganya, nikawa nahangaika , licha ya ndoa, wengi wananifahamu kama mama shughuli, leo nipo hapa kesho nipo kule, hata mshirika wangu hajui zaidi ya kunitumia kwa manufaa yake

‘Huyu mume wa familia hadi hii leo, hajaniamini kuwa mimi …nilivyo sasa sio kam yule aliyekuwa kipindi kile,, na zaidi kanitambua tu kama mama shughuli..’akasema akimgeukia mume wa familia, ambaye naye kama wengine alikwua akimuangalai huyu mdada, kama mgeni fulani, sio kama yule mdada aliyekua akimfahamu.

‘Anayenifahamu vyema kwenye uhalisia wa sasa, ni rafiki wa mke wa familia, kwani yeye ndiye aliyekuwa bosi wangu, yeye ndiye aliyenibadilisha kutoka binti wa kijijini hadi kuwa mdada anayejitambua, mdada jasiri..lakini ujasiri nilio nao una kikomo chake, maisha ya binadamu yana mahali unafika uanshindwa, ndio maana hata docta aliponishauri mambo mambo ya kujibadili, alivyotaka yeye, alishindwa, kwanini….maji yalishanifika shingoni..

‘Inabidi niwaambie haya ili mje kuyaunganisha na tukio nzima, naomba msinichoke, nataka niliongee hili ili kila mtu alielewe ili kesho na kesho kutwa msije kuongopewa,
Sawa mwenyekiti amekuwa akiniuliza hili swali mara kwa mara, je ni wewe ulimuua, je ni nani kamuua marehemu..

Sio rahisi kulitamka jibu lake hivyo..naweza nikatamka, ndio ni mimi, au ndio sio mimi..huoni hapo kuna ‘ndio’…yawezekana nimetamka hivyo kumlinda mtu au kujilinda mimi mwenyewe, ndio maana nataka ukweli, na hali halisi isikikwe kwanza, kabala ya hitimisho ..’akatulia

‘Ndugu zangu…nawaambia haya, ili siku ya kesi, mjazane mahakamani ili ikiwezekana muwe mashahidi wa kuitafuta haki,…namuomba mungu kama mambo haya yatakwisha kwa amani, basi sitaki tena kazi hizi za hatari..sitaki tena …’akaonyesha mikono kama kunawa.

‘Lakini nataka maisha niliyopitia yawe ni funzo kwa wengine.., kiukweli mimi nimeshajipanga kivyangu, maisha ni popote, hata kijijini inawezekana....hilo nimeamini na ndivyo nataka maisha yangu yawe huko. Kama sitakiwa jela,…

Mzungumzaji akamuangalia mwenyekiti, ni kama anasubiria kitu kwa mwenyekiti, lakini mwenyekiti alikuwa katulia tu.

‘Mimi ninachotaka kuwaelezea ni jinsi gani ilivyotokea, siku Makabrasha alipouwawa, hili mwenyekiti hataki, kwa vile linagusa taratibu za kipolisi, lakini utalikwepaje wakati limefungamana na hii kadhia nzima,..’akasema

‘Ni kweli mimi nilikuwepo kwenye hilo jengo, lakini huwezi kufikia hatua hii ya .......na kwanini ilifanyika hivyo, kuna mambo muhimu lazima yafahamike kwetu , kwenu ..nina maana hiyo…..’akatulia kidogo akimwangalia mwenyekiti, kama anachelea kuongea jambo, lakini mwenyekiti akamuashiria asendelee kuongea hilo analotaka kuongea;

***********
‘Makabrasha alikuwa na maadui wengi, na wengi wao, walifikia hata kumlaani,na inapofikia hatua wanadamu wenzako wanakulaani, wanatamani hata ufe, ujue wewe huna thamani tena katika hii dunia, hata kama ni tajiri, lakini ndani ya mioyo ya watu, wewe ni mfu, ...’akatulia.

Kwa jinsi ilivyo mzungumzaji alikuwa anasubiria kibali cha mwenyekiti, na mwenyekiti alionekana naye akisubiria kibali kutoka kwa watu wa usalama, kwahiyo mzungumzaji akawa anaongea kwa kutegea akivuta muda, muda ukawa unakwenda.

Mwenyekiti alikuwa katulia kama anawaza jambo, lakini baadaye akachukua simu yake na kumpigia mtu akawa anasikiliza na kuwafanya watu watulie wakisubiria hata shahidi huyo alionekana mwingi wa wasiwasi , hadi mwenyekiti alipomaliza kuongea na simu, halafu akaonyeshea kidole gumba, kuashiria mambo yapo shwari..

‘Endelea shahidi uwanja ni wako, nimeshafikisha ujumbe wako, ila kama ujuavyo, baada ya maelezo yako, hakuna jinsi, vyovyote iwavyo, utanisamehe kwa hilo.....’akasema mwenyekiti na shahidi bado akiwa na wasiwasi akasema;.

‘Katika maisha yetu haya, watu wana matatizo yao, wengine hawajui wataishi vipi, wanahangaika usiku na mchana, ili wapate angalau riziki zao...lakini maisha ni magumu, usiombe..., watu hawa wenye maisha magumu, kamwe hawana utulivu wa moyo…’akaguka huku na kule kama anawasiwasi fulani.

‘Nazungumzia maisha yangu nilipotokea au sio, nazungumzia maisha ya watu kama Makabrasga walipotokea, nazungumzia maisha kama ya mume wa familia alipotokea,…watu wa chini, watu ambao hawana amani ndani ya nafsi zao, japokuwa kiwili wili utamuona yupo,...ndivyo maisha ya walio wengi yalivyo, watu kama hawa wanatafuta upenyo litokee jambo watoe hasira zao, litokee jambo watumie kama sababu...’akasema na kugeuka kumwangalia mume wa familia.

‘Watu wana matatizo yao makazini mwao, wananyonywa, wanachokifanya hakiliangani kabisa na kile wanachokipata, nguvu kazi yao inatumika vibaya, kazi wanayoifanya na malipo yake ni viti viwili tofauti, anayefaidika ni tajiri, na hata akipata ziaida ya kupindukia ni nadra sana kukumbuka,...hakuna anayewajali, wanahangaika, kupata, agalau huduma muhimu, angalau mahitajio muhimu, lakini kipato chao hakikidhi hata hizo huduma muhimu. Watu hawa wakipata njia, wanaweza kufanya jambo baya sana.

Watu wahali ya chini, wanachokipata ni kama vile wenzetu wanavyosema tonge mdomoni, hata mdomoni kwenyewe ni kama onja –onja, unategemea huyu mtu atakuwa na amani kweli...huyu akipata nafasi ya kufanya unyama ataufanya unyama kweli, ..hata kuua kwake itakuwa ni sehemu ya kama kulipiza kisasi..

Watu wana matatizo sana huko kijijini , usione watu wapo kimiya, mtu analima mvua hakuna, pembejeo hakuna, anatumia jembe la mkono, mtu huyu kila siku anakatwa kodi, kila anachonunua, ni kodi, akigeuka huku kodi, mtoto wake wanadaiwa ada, yeye anaumwa magonjwa yasiyohesabika, akienda hospitalini, hakuna dawa, akipatacho nini…anayefaidika san asana ni huyu mnunuzi anayekuja kununua kwa mkulima na kwenda kuwauzia wengine,..sio mkulima..huyu mtu akipata nafasi unafikiri atafanya nini..

Sio kwamba naongea haya kuwatetea watu, kama Marehemu, kama mume wa familia au kama mimi, naonega kiuhalisia, maana kwa bahati nzuri nimetokea huko na uzuri nimeweza kuishi na matajiri, nimeyaona hayo hata kwenye kazi zangu, hivyo…ndivyo ilivyo, asikudanganye mtu…ndio maana hata mwenyekiti hataki kuniamini..unafikiri ni kwanini..ni hulka,..za matajiri dhidi ya masikini..

Mwenyekiti pale akakuna kichwa, kama kusikitika, lakini…hakusema neno

‘Siku tulipoongea na mwenzangu tuliyajadili haya maisha yalivyo, na siku nilipoongea na Makabrasha kabla ya kifo chake yeye aliniambia hayo..ni muhimu sana myasikie...

Yeye alipenda kusema ‘system,’ akiwa na maana wale wenye mamlaka, wale waliopewa dhamana, …na zaidi wenye uwezo, hasa wawekezaji,…yeye marehemu aliwahi kuniambia hivi

‘Huko kwenye system(utawala, na wenye mamlaka, matajiri na wawekezaji, akiwa na maana hiyo),...ndio haki za wanyonge zinapopotelea, wahujumu, walaghai, wadhulumaji,mafisadi, wamejificha huko…, na huko ndipo kwenye watu wanaojifanya ni watetezi wa wanyonge, wakija kwenye majukwaa wanakuja kwa lugha nzuri tu, na wanajua jinsi gani ya kuwadanganya wanachi..

‘Mimi kama mimi, najau wengi wananichukia sana, ila mimi nimepata kuutumia ujuzi wahuu na taaluma yangu hii kuchukua kile walichoiba kwa wananchi na kukirejesha kwa wananchi…’akasema na mimi sikumuamini kwa kauli hizo..hadi nilipofuatilia kwenye ofisi yake na kuyaona hayo kwa vitendo.

Hili hamuwezi kuliamini, ndivyo marehemu alikuwa hivyo, kwanini hamuoni hilo, ukweli wa upande wake wa pili umefichwa, ila yeye alikuwa na vitega uchumi vichache tu, mali yake nyingi, aliyokuwa akipata, yeye alikuwa akiwapeleka masikini, wazee wasiojiweza kule kijijini kwao, ndio maana hadi leo ukienda kule mtu huyo anaheshimika sana

Watu walikuwa wakijiuliza ni kwanini mtu mkorofi kama huyu hafungwi, hakamatwi..huyu mtu aliheshimika, kwa wasiojiweza, alipata Baraka zao, kwa upande huo alikuwa na watetezi, huku akitumia kila mwanya wa sheria kujilinda…’akatulia

‘Hili wengi wataliona ni la ajabu, maana mazuri ya mtu huyu yakichanganyikana na mabaya yake..na mazuri yake ilivyo, hupotea tu..,..na hasa ukiwa kwenye usawa wa mtu wa daraja la chini kama sisi, ni nani atakuamini hata utende wema vipi..mimi mwenyewe kipindi nilichofanya kazi kwake nilikuwa nikishiriki kwenye kazi za kuwahudumia wale wasiojiweza kutoka kwenye mfuko wake maalumu aliouweka kwa kazi hiyo…

Makabrasha alikuwa akiwalipia,wasiojiweza shule, alikuwa akiwasaidia mayatima, alikuwa akiwasaidia wagonjwa kwenda kutibiwa nje.., angalia kumbukumbu zake, mtaziona hizo, lakini kumbukumbu hizi zilikuja kupotea, mimi niliziona na shule alizojenga, nazifahamu, lakini hakutaka watu wafahamu hilo, ni kwanini…mimi sijui.

‘ Zaidi ni kuwa huyu mtu alikuwa akitumiwa na huyo mpinzani wako mzee, mpinzani wako alikuwa mjanja, alikuwa akiuma na kupilizia, akienda kijijini, anawekeza kwa watu kama hao, na …ndio hivyo, mambo ya kisiasa yalivyo au sio…

Labda sera hizi huyo mpinzani wako… alizipata kutoka kwa marehemu, kuchukua kwa matajiri kurejesha kwa wayonge, japokuwa yeye alitumia njia hizo mbaya kuzipata hizo pesa au mali, na yeye aliona njia hizo ndio rahis kwake,, ..huyo ndiye Makabrasha.

Simtetezi jamani..ila nazungumza hali halisi, na sisemi haya kwa nia ya kutaka kujitetea hata mimi, ila kwenye ukweli tusema,..haya yatakusaidia hata wewe mwenyekiti, kuwa katika maisha, msijiangalie nyie wenyewe kama matajiri, kuwa masikini hafai kuoa au kulewa na tajiri, ili mfanikiwe jichanganyeni na masikini, wasaidieni masikini, ili na wao wawaone nyie kwa jicho la rehema.

Swali kama huyo mtu alikuwa hivyo, ni kwanini akauwawa,…..na ni nani hao waliofanya hivyo,…ndicho wengi wanakisubiria hapa au sio…lakini ukweli kwanza uili mje muone mazingira yaliyokuja hadi huyu mtu akauwawa..na sio rahisi kama watu wanvyoona..sio rahisi mtu mwenye akili zake kubonyeza trigger…
Na hilo halikufanyika …kirahisi hivyo,…kumbuka mazingira ya marehemuilikuwa ulinzi hadi akitembea ana vitu vya kumsaidia kumlinda, ikitokea hatari akibonyeza kitufe fulani, walinzi wake wameshafika…na kila anachoongea kilirekodiwa, mwisho wa siku anafuta kile alisichokitaka..huyu ndiye marehemu..

Swali alikujaje kuuwawa…kuna kitu mjifunze ukitaka kuficha kiatu, sehemu nzuri ni sehemu kunapowekwa viatu au sio..na mbaya wa mtu ni mtuwe au sio…adui wa mtu ni rafiki yake mkubwa,…sio rahis kwa mtu huyu aliyejilinda hivyo kuuwawa kirahis hivyo tena ndani ya sehemu yenye kila zana zake za kujilinda,…

Hamfahamu ofisi yake ilivyo..humu aliwekeza kila kitu chenye kumsaidia kujilinda, nahisi alitumia pesa nyingi sana, na yeye alikuwa akisema, akiwa ofisini kwake, anajihisi yupo salama kuliko sehemu yoyote…lakini humo humo ndio alipouwawa,..jiulize ni kwanini, …

Polisi hadi leo, hawajawa na uhakika …japokuwa wanadai kuwa wameshaupata ushahid lakini je ushahidi huo ni kamilifu,…kumbuka ukweli wote ulishaharibiwa, kilichobakia ni yale yale aliyokuwa akiyafanya marehemu..yamemrudia,…sasa je ni kweli kuwa hao washukiwa ndio kweli walifanya hivyo, na kama walifanya hivyo walitumia mbinu gani…

Kumbuka ulinzi, kumbuka zana zilizopo hapo,..je masikini anaweza kuvuka hivyo vihunzi…hahaha…ni movie yenye ujasiri…

Mwenyekiti, sasa naingia sehemu nyeti,…naomba univumilie, na naomba haya mazungumzo …wakili, haya ni mazungumzo nyeti, weka vitega masikio vyema, weka vitega sauti vyema, ili mkipae kile chenye uhakika,…najua baada ya hili,..nitakuwa nikibebwa kama muuaji, lakini ..ni bora niongee huu ukweli, ili mwisho wa siku, kama nitaonekana mimi ndiye muuji, basi niwe shujaa…’akasema na kuinamisha kichwa chini.

‘Shujaa wa mauaji, hapana…’aliyesema hili ni mama

‘Nianze mwenyekiti…?’ akauliza mzungumzaji, akimuangalia huyo mama, …na mwenyekiti, akawa anaangalia saa yake, na hakusema kitu pale pale akaangalia dirishani, akanyosha kidole kuwa muongeaji asubiri kidogo…

WAZO LA LEO: Kifo hakina hodi, kifo kila mtu kitamkuta kwa wakati wake, hata kama upo ndani ya handaki, hata kama wewe ni tajiri kupindukia ukawa unalindwa hata ukiwa chooni, hata kama umejizungushia gilasi zisizopitisha risasi, siku ikifika imefika,..hata kama wewe ni masikini, siku ikifika imefika,…
 
SEHEMU YA 114



Sasa kama hivyo, kumbe kuna mwenye mamlaka na uhai wetu, ambaye hawezekani, asiye na mfano wake, alipangalo kuwa liwe litakuwa,basi ni kwanini hatumuogopi yeye, tukamtii yeye, kwanini tunafikia mahali tunatakabari, tunakiuka maadili mema, tunaghilibika kwa tamaa za mali, utajiri, utawala, kama vile tutaishi milele, tuikumbuke siku hiyo ambayo, mtu ataicha mali yake, watoto wake, mpenzi wake,…utawala wake, imebakia kauli,..’yote ni mapenzi ya mungu…’


Ewe mola wetu tujalie tuwe na mwisho mwema…Aamin.



Shahidi akaendelea...

Namkumbuka sana Marehemu kwenye kauli zake, aliwahi kuniambia hivi;

‘Katika hii dunia, kila mtu na hamsini zake, kama una uwezo wa kufanya hivi, na ukapata, basi fanya, kama kuna sehemu unaweza kuitumia kama ngazi ili na wewe ulipate tunda fanya hivyo..mimi maadui zangu wakubwa ni wakubwa, matajiri, hawa tutapambana nao hadi kifo..

Najiuliza tu , kwanini sasa polisi wanahangaika na watu wa chini, wakati, kwa mujibu wa kauli ya huyu mtu yeye maadui zake wakubwa ni watu wakubwa, matajiri, watu wenye nyazifa eeh, hao ndio wanaoweza kumuua, au sio,….

Yeye alifikia kutuambia, sisi tumekubali kuolewa na matajiri, sasa tuamue moja, kuwa na yeye kupambana na mafisadi wadhumulaji, kama alivyowaita yeye, au kuwa upande huo wa hao watu, anasema anapambana nao…kama hatutashirikiana naye basi tupo upande huo…kama tupo huko, basi tutakuja kupata shida, na tutakuwa miongoni mwa wasaliti wake.

Unajua huyu mtu, yeye pamoja ya yakuwa kasoma sana sheria, aliamua kuigeuka sheria, au kuitumia sheria atalavyo yeye, au sio, kwa maneno yake ni ili kwuasaidia wanyonge, ... akachanganya na ujanja-ujanja wake eeh, hasa aliousoma vitabuni, …akakaa na kubunu njia zinazojulikana kama blackmail.Sijui tafsiri yake ni nini kwa Kiswahili, ....’akasema na kumwangalia mwenyekiti.

Watu kama hawa wapo wengi, wanaishi kiujanja ujanja, wanakuja kwako, wanakupima udhaifu wako, wanakuona una njaa kali, wanaanza kupenyeza sera zao, na nyie bila kujua…maana keshawasoma, mnakuja kukubaliana naye.

Ndio maana dunia ya leo imejaa vita unahisi ni kwanini..ni watu walishaumia, walikuwa wanasubira kisingizio tu, ili waweze kuzitoa hasira zao..hili watu hawalioni..hivi ni visasi kutoka ndani ya mioyo ya watu waliokuwa wakilalamika, wakisononeka, na mtu wetu akaamua kuwasaidia kwa kuchukua kutoka kwa matajiri kuleta kwao,

Swali hapa iweje sasa, hao wanaotaka kusaidiwa ndio wawe wauwaji,…maana polisi hadi sasa kwa ushahidi wao, wanaoshukiwa ni watu wa aina yetu, sio haooo een maadui za marehemu,…

Nimepata muda wa kuishi na marehemu na amekuwa kila siku akinihubiria ili nibadilika ili niwe kama yeye,..huyu mtu ni mjanja kwenye ushawishi..

Siwezi kulikataa hilo, … ilifika mahali na mimi nikajenga chuki nikiona ukweli ulivyo,kuwa hayo anayoongea yana namna ya ukweli fulani…

Hata hivyo kiukweli wangu, sikufikia hatua ya kutaka kuua, naogopa sana kumwaga damu ya mtu asiye na hatia, na ikizingatia kuwa mimi nimejifunza uaskari, na moja ya nidhamu ya uaskari, ni utii wa sheria bila shuruti, kuwalinda raia wema…sasa kwanini leo mimi niwe mshukiwa, sawa yawezekana, lakini kuna sababu au sio, ....

‘Nafahamu wengi watanishangaa, nikisema nimejifunza uaskari, naomba mlielewe hivyo, na mlichukulie hivyo hivyo…’

Ndio maana nikatoa ombi kwenu, kuwa haya nitakayo yaongea hapa, yaishie hapa hapa,, tukitoka hapa, kila mtu na hamsini zake, hayo mengine waachieni wahusika, wanajua ni nini wanachokifanya, lakini kama mtu atajitia kidomo domo, ....sawa nitakamatwa, kama mshukiwa, wa mauaji, lakini je ni kweli nilifanya hivyo...?’ akageuka kuwaangalia watu.

Nafahamu mpaka hapo nimewachanganya watu…mmh…, maana mlitaka msikie mnachokitaka nyie,..jibu la moja kwa moja ni nani muuaji, au sio.. lakini huko siwezi kufika hara hivyo, ninachotaka kwanza, muone tukio zima, ili nyie wenyewe mje kumpata muuaji halisi…..’hapo atakatulia kidogo akiwaangalia wajumbe.

**********

‘Sasa naomba nianze maelezo yangu kwa jinsi ilivyokuwa ....’akamuangalia mwenyekiti

‘Natumai kwa hivi sasa hakuna pingamizi…’

Alimuangalia mwenyekiti, mwenyekiti alikuwa katulia, kwa haraka akamwangalia mume wa familia ambaye naye alikuwa sasa kageuza kichwa nyuma kumwangalia huyo mdada anayeongea kwa hamasa, maana muongeaji alikuwa kiti cha nyuma cha mume wa familia, kiukweli hapo alipo, alikuwa kama haamini macho yake kwa kile anachokiona, kweli huyo mdada ni yule yule anayemfahamu yeye, au ni mwingine.

‘Ni hivi , kiuhalisia,..Mume wa familia alikuwa ameshapona muda mrefu tu,…’akasema hivyo, wajumbe wakawa kimia

‘Sio kupona kwa vile,… hapana, bado likuwa na majereha, unajua ile ajali ilikuwa ni kubwa sana,..lakini sio kivile alivyokuwa akijionyeshea, mtu mpaka kubebwa, ..na vitu kama hivyo,… kuna muda alitakiwa aigize, ili kukamilisha mambo fulani fulani, hiyo ikiwa mipango ya Makabrasha…’akasema

‘Mume wa familia aliambiwa hilo ni kwa manufaa yake yeye mwenyewe ili mambo yakamilike kwanza kwani akiwa amepona, basi atakuja kukumbuna na mkataba wao, ambao ungemuhukumu kama mkosaji, mvunjaji wa sheria, kama walivyokubaliana kwenye mkatana wao, si mshapata picha ya mkataba wao ulivyokuwa…’akasema muonegaji kama anauliza wajumbe.

‘Ukiangalia ni sawa, maana yeye alishaharibu, alishavunja mkataba au sio, kwa mujibu wa mkataba wao…na ili mkewe aendelea kuwa upande wake ni yeye aendelee kuwa mgonjwa, umeona hapo walivyocheza…kwa hali hiyo mume wa familia hakuwa na jinsi, ilibidi akubaliane na mtalaamu,, la sivyo ndoto yake ya muda mrefu ingelifutika..

Kiukweli mimi nilikuwa naumia sana, maana hayo yanavyoendelea nayaona, nayasikia, japokuwa nilijitahidi nisiyaingilie kiundani wake, …unajua tena, na mimi nilikuwa na yangu kwa upande wangu, kama nilivyosema huyu mtu alitunasa, na akawa anamvuruga kila mtu kwa upande wake..

Sasa tuende kwa huyu marehemu,…

Mimi nikawa nimepewa kazi ndani ya ofisi ya Makabrasha, nikiwa kama muhudumu wake maalumu, lakini nia na lengo lake ni lile lile, sisi, au mimi niwe karibu naye, nisije nikaharibu mipangilio yake, kwahiyo nikawa napangiwa kazi hata za usiku, hizi kazi za usiku, eeh zilikuwa na mambo yake…ujue awali nilikuwa nafanya kazi huku na kule, yaani kwa bosi wangu na kwa huyu mtu. Bosi wangu alikuwa halifahamu hilo…

Sasa siku zilivyokwenda ndio nikawa sasa nafanya kazi kiukweli ukweli chini ya Makabrasha…, sio ile kama kibarua tena wa kazi maalumu za siku moja moja… utaniuliza nilikuwa nafanyaje kazi kama hizo hata za usiku huku nipo ndani ya ndoa yangu. Mume wangu hafahamu…

Kumbuka kuwa , kwa muda fulani, mimi niliaga kwenda kijijini, kabla ya kuwawa kwa Makabrsha, ilikuwa nfanya hivyo kila mara kukiwa na kazi maalumu za muda naaga kuwa nakwenda kijijini kwetu,…nikawa naenda na kurudi, najua mwenyewe jinsi gani nilikuwa nafanya,..hata marehemu alikuwa nimeaga kwa mume wangu kuja kwake, kipindi hicho za kazi za siku moja moja,…ila kipindi sasa nipo kwake, nilimuelezea hali halisi, akaelewa.

Na hata bosi wangu hakuwa anafahamu hiyo kazi yangu ya muda kwa makabrasha, na hata ikafika muda, kwa mujibu wa Makabrsha niache kazi nyingine zozote nilizokuwa nafanya niwe namfanyia yeye kazi tu..ndio nikaomba kuacha kazi kwa bosi wangu, na nilipoacha kweli nilikwenda kijijini nikaweka mambo yangu sawa, sasa nikarudi jijin nikiwa mtu mwingine..

Na kwa muda huo sikuwa nawasiliana sana na mume, kiukweli nilimtesa sana, hakuwa na raha akiniona jinsi nilivyo..kwahiyo hata nilipomuambia kuwa nakwenda kuishi kijijini, hakukataa, mume wangu alitaka niwe na raha, niwe na uhuru, niweze kubadilika, niweze kuondokana na ile hali anayoniona nayo, mawazo…sina amani.

Hadi hapo utaona kuwa kazi ndani ya himaya ya Makabrsha ilishaanza siku nyingi hata kabla sijamuandikia rafiki yangu barua ya kuacha kazi kwake.

Kuacha akzi nyingine, shughuli nyingine, ilikuwa moja ya mikakati ya Makabrasha ili aweze kuwa karibu nami, ili awez kunitumia, hakujali kama nitavunja ndoa yangu au la. Na nataka muelewe hili, kuwa Makabrasha hakujua undani wangu na rafiki yangu kuwa nafanya kazi gani kwake, alijua kuwa nafanya kazi za kutangaza biashara zake tu, kiukweli kinje ndivyo nilivyokuwa najulikana hivyo.

Kwahiyo sasa rasmi nikaingia ndani ya jengo ambalo hata mimi sikulifahamu hivyo lilivyo kwa huko ndani, kuwa hilo jengo kwanza llikuwa likimilikiwa na marehemu, na humo ndani kuna mambo mengi ambayo hayajulikani kwa watu wa nje, na hata humo kuna wapangaji wa ofisi hawajui kinachoendelea huko chini, kuna ofisi za chini kwa chini, chini ya ardhi….

Wakati naingia humo, mipango mikubwa ya Makabrsha ilikuwa tayari imeshakamilishwa, mikataba imeshabadilishwa, na mikataba mipya imeshatayarishwa, na kuwekwa inapostahili, sasa Makabrasha akaanza kutoa makucha yake, akatayarisha mikataba mingine mipya ya kumuhalalisha yeye kama mumiliki mkuu wa baadhi ya makampuni likiwemo hilo la mume wa familia, lengo limashafikia penyewe, sasa Makabrsha sio yule wa zamani tena, mnanielewa hapo….

Hadi hapo, mume wa familia, alikuwa hana nguvu tena, kwani alishawekwa kwenye mikono ya Makabrasha. Kashfa nzito ilishajengwa hata kwa kizazi cha mke wa familia, japokuwa familia ya mke ilikuwa bado gizani, haifahamu kinachoendelea, na ndilo lengo…na kiukweli hiyo kashfa ilivyotengenezwa kama ingevuja,.. basi,.. hata kizazi cha mke wafamilia , kwa mzee hapo, ingeliharibu jina , na mambo ya kisiasa yangeliharibika kabisa..

Marehemu hakutaka kuifikisha hiyo kashafa haraka kwa adui wa mzee, yeye alitaka kuitumia hiyo kashfa kwanza kwa masilahi yake, baadae ikibidi ndio angeuvijisha, na hapo siju….

Ndio maana mume wa familia akawa anauma hilo kwa magego, sio kwa ajili yake tu bali pia kwa ajili ya familia nzima ya mkewe, japokuwa chanzo cha hiyo kashifa ilitokea kwa mume wa familia….mnaona ilivyo…sio kitu kidogo….

Kabla sijafika huko kwenye mpango rasmi…

Nikisema mpango rasmi, ina maana mpango ambao ndani yake ilipatikana kifo cha Makabrsaha, huo mpango sikutakiwa kuu-ongelea hapa, au kuongea lolote kuhusuiana na huo mpango,….huo mpango natafutwa nao, na kama nafahamu lolote nipo hatarini..

Walitaka kuniua…hahaha, lakini mungu ni mkubwa,…polis wakavumishiwa kuwa ni watu wanaotaka kulipiza kisasi cha marehemu,..sio kweli jamani, ni kwa vile mimi ndiye ninayefahamu kila kitu…

Sasa huo mpango umetumika kama ushahidi,… lakini katika namna ya upotoshaji, kwa namna maalumu..ndio maana mimi nataka niongee hapa kila kitu jinsi ilivyotokea, ili kama ni haki, basi haki kweli ije kutendeka..

Sasa kama mimi ndiye muuaji, au sio…nataka niwajibike kiukweli, na nyie mkiwa mashahidi, na kama yupo mwingine aliyeshirikiana nami, basi atanifuatia, au sio…nataka hili niliondoe kwanye nafsi yangu ili niwe huru…

Sasa.., ngoja niwarejeshe kwenye mazungumzo yangu ya mwisho na mume wa familia; nawarejsha huko maana hayo mazungumzo ndio ushahidi mkubwa wa polisi, huo ndio ushahidi unaowafanya mpaka sasa watuone sisi kuwa ndio wauwaji, labda, ni kweli, labda sio kweli, mimi sitaki nijihukumu, nataka nyie na baadae mahakama ije inihukumu kihalali, au sio…

Sasa tuwe tayari, na huu ushahidi…mimi nitauongea, ila ..kila kitu kipo kwenye video, utayasikia haya nitakayoyaongea, video hiyo imechakachuliwa kuna mengine hayapo……

**********a

‘Ina maana wewe hadi hapo umeshakubali kuwa wewe utakuwa mtumwa wa Makabrasha wa kudumu…?’ nikamuuliza mume wa familia

‘Nitafanya nini kwa sasa, huyu jamaa ana siri zangu nyingi, ana mambo yangu mengi, ambayo akimuonyesha mke wangu au wakwe zangu, nitafukuzwa kama mwizi, kwahiyo inabidi nimkubalie kila kitu...’akaniambia na mimi nikawa sina njia ya kumsaidia. Mimi nikamwambia

‘Kwa usalama wako ni bora ufanye hivyo maana humjui huyo mtu alivyo, huyo mtu kwa namna nyingine ni mbaya, anaweza kuyafanya hayo, na akahakikisha unazalilika mpaka utatamani kujiua,..lakini usichoke mimi nipo nyuma yako maana pamoja na hayo namfahamu vingine alivyo..’nikamwambia hivyo.

Mimi nilishaamua kuwa nilimalize hilo, kwani kama nisipofanya jambo, hali hiyo itaendelea kututesa katika maisha yetu yote, tutakuwa watumwa wa mtu mmoja, na hata kama tutaendelea kuishi kwenye ndoa zetu, itakuwa ni ndoa ya jina tu,..

Kwa mfano mimi nilitakiwa kumtii huyu mtu kama mtumwa wake, kila anachokitaka nimfanyie, hata kuzalilika, sasa kulikuwa na manufaa gani hapo,..na nitazalilika hivyo mpaka lini,..hata hivyo,..basi tena,.. nikaona nijitolee tu muhanga, nifanye kazi yangu, nitimize wajibu wangu, ili kulimaliza hili tatizo kabisa, lakini kwa vipi kwa mtu kama Makabrasha, wanasema mtu mwenye tabia hii kamwe haiachi labda auwawe…’akasema na kutabasamu.

‘Usijali, mshirika, mimi nitajitolea kwa ajili yako....kama utanikumbuka sawa, nafanya haya kwa vile nakupenda, japokuwa penzi kwako kwangu kwa hivi sasa halipo tena, siwezi kukulaumu, japokuwa, inauma sana,....nimeshakuona kuwa wewe unanitumia ili upate unachokitaka, huna tofauti na Makabrasha...’nikamwambia siku hiyo.

‘Kwanini unasema hivyo, mimi mbona nakupenda sana, umeshasahau tulivyoahidiana kule kijijini...kwa hali niliyo nayo, nashindwa kutimiza ahadi zetu zote, unafahamu ni kwa nini…wakati mwingine haya yanayotokea ni kwasababu nashindwa kuvumilia,..hata mimi nateseka kwa hilo nawaza sana, ..wewe hujui tu, ndio maana naamua kunywa kupoteza mawazo…sasa yametokea haya ya kutokea, sikupenda..ila nasema mimi ninakupenda, lakini kwa hali kama hii tutafanyaje,....’akasema

‘Najua..’nikasema

‘Wewe huoni sasa naumwa, na pia natakiwa niumwe ugonjwa wa kuigiza,…lakini hata bila kuigiza kuumwa..kuumwa bado kupo, hali niliyo nayo sio rahisi kuelezea, wakati mwingine nashindwa hata kuelewa mimi ninaumwa nini hasa..’akasema

‘Si umeumia, kwani hilo halijulikani..’nikasema

‘Aheri ya kuumia viungi kuliko kuumia moyoni, wewe hujui tu, aheri ya kuumwa magonjwa yanayojulikana, kuliko kuumwa magonjwa yasiyojulikana, nateseka tu wewe hujui..kichwa akili wakati mwingine inakuwa sio ya kwangu..mimi hata sijui nimekuwaje…’akasema

‘Kiukweli kwa vile nampenda huyu mtu, iliniuma sana alipoongea hivyo, siku ile nakumbuka nilitaka niongee na docta nijue huyu mtu ana tatizo gani, sikuweza..kutokana na muda, lakini akilini nilihisi huyu mtu kuna kitu kafanyiwa tofauti na matibabu yake..

‘Mimi nakuambia ukweli, hapa nilipo, siwezi kujijua naumwa nini..lakini naahidi mimi nikipona tu na yeye akifanikiwa alivyopanga iwe, nitatafuta njia ya kumkomoa, tutarudisha mali yetu yote...hata kama nikwa kumua, mimi nitamua kwa mkono wangu.., sitaogopa hilo, maana yeye mwenyewe hatujali, wewe huoni hilo…’akaniambia hivyo.

‘Chunga huo ulimi wako, …kauli yako hiyo ikisikiwa na wenyewe, itakuwa ushahidi, hata akitokea huyo mtu akauliwa na mtu mwingine, wanaweza kutumia kauli yako hiyo kama ushahidi …usipende kuropoka ropoka kauli kama hizo ovyo…’nikamkanya hivyo.

‘Sawa mpenzi..nimekuelewa…’alisema hivyo huyo mume wa familia

Nayazungumza haya maneno alivyoyatamka bila kuficha kitu…maana haya mazungumzo yapo kwenye ushahidi walio nao polisi! Ina maana hadi hapo polisi wamesharizika kuwa wameshampata muuaji tayari, sasa jiulize kwanini wamechukua muda kumkamata huyo muhusika, na kila kitu wanacho,…wanashindwa kufanya hivyo kwasababu bado kuna utata au sio, hiyo pekee haiwezi kuhalalisha kuwa yeye ni muuaji, ..lakini sio hivyo tu, tuendelee na haya mazungumzo kama ushahidi wa polisi…

Kuna kitu wanakiitai …’motive’ au motisha wa kuyafanya hayo mauji…ni nini ..huyu mshukiwa ana kitu gani, cha kuweza kuyafany haya, maana aliyemuua Makabrsha lazima ana jambo, je huyu mtu ana jambo gani dhidi yake…hicho ndicho walikuwa wakikitafuta, je walikipata,..sasa wakati wanatafuta wakajikuta wanapata taarifa nyingine za utata!

Mwenyekiti nisamehe hapo kidogo, nitaendelea kutoa maelezo kutokana na ushahidi wao kwa manufaa yetu na hata kwako pia..…

Alipozungumza hivyo, awali mwenyekiti alitaka kumzuia lakini baadae akaonekana kutulia akamuangalia tu huyo muongeaji…kiukweli mwenyekiti alionekana kuwa na wakati mgumu, nafikiri ni kutokana na huo mkanganyiko wa ushahidi…

Wakati nipo naongea na mwenzangu, tunamuongelea Makabrasha niliwahi kumwambia hivi

‘Kwa hivi sasa hatumuwezi tena Makabrasha, huyu jamaa keshajizatiti, na kiukweli kama akiendelea kuwepo duniani, sisi tutaendelea kuwa watumwa wake, na hata ndoa zetu hizi sizani kama tutaweza kuishi kwa amani na furaha..’niliongea hivyo

‘Ni kweli, sasa ..oh, … mimi naona..tumuue huyu mtu,..hakuna jinsi..’yeye akasema hivyo.

‘Nimeshakuambia, achana na hiyo lugha yako,…’nikasema

‘Sasa hebu niambie, utawezaje kuishi kwa amani kama huyu jamaa kila siku anatutushia amani..na ukumbuke hadi sasa huyu jamaa yetu ameshafanikisha mambo yake…’akasema

‘Bado wewe hujakamilisha na wewe ukikamilisha tu, kila kitu kimeshawekwa mikononi mwake, na wewe itabidi utii amri kutoka kwake, kwahiyo nafsi iliyobakia ni kupitia kwako, utafanyaje sasa…’nikamwambia.

‘Sawa nimekuelewa..hata hivyo sitaweza kumkatalia, maana nikimkatalia itakuwaje, labda hapo hapo nifanye jambo,…iwe mwisho wa haya yote,..au nitumie hiyo silaha, kum-maliza..japokuwa naogopa mimi…kwani nim-maliza watu watajua, eeh, mimi naumwa nipo hospitalini…au nimtafute mtu, anifanyie hiyo kazi, unasemaje..au sasa hebu nishauri, tutafanyaje kwa hali kama hii..?’ akaniuliza

‘Sasa hivi unaniuliza eeh, tutafanyaje…, kamuulize Makabrasha,…’nikasema hivyo.

‘Kwanini unasema hivyo, wewe ulitaka nifanye nini mimi…huoni hali tuliyo nayo,…mimi nikijulikana tu, kuwa wewe na mimi kitu kimoja, unafikiri itakuwaje, lakini Makabrasha anafahamu kila kitu ana ushahid wa kutosha, huoni kuwa keshatuwahi, tufanyeje sasa…’akasema

‘Nakuambia haya kwa vile tokea awali nikikushauri, eeh… utulie, tuwe makini, ukawa hunisikilizi, sasa hivi yamekufika shingoni unaniuliza tufanye nini, mimi sijui la kufanya hadi sasa, kiukweli ndio hivyo, mipango ipo mingi, lakini …siwezi ..nina wakati mgumu sana…’ nikasema nikionekana kuwaza.

‘Tusikate tamaa au sio..’akasema

‘Kiukweli ninachoweza kusema niliyo nayo mimi mwenyewe ni mazito zaidi ya haya unayoniuliza wewe tufanye nini… kwahiyo kwa hivi sasa niache kwanza na yangu, wewe endelea na Makabrasha wako, yeye si ndio wakili wako, na yeye ndio bwana wako, nikiwa na maana wewe ni mtumwa wake..si ndio hivyo, k.’nikamwambia.

‘Hivi wewe unajiamini nini , wewe unafahamu vyema huyu mtu alivyo, bila ya mimi na wewe kushirikiana, hatutafika popote, njama zake ni kututengenisha, kutokosanisha…sasa mimi nakuonya kama una jambo dhidi yake, unataka ulifanye kivyako, utakuwa unajitakia matatizo,achana na huyo mtu....’akasema.

‘Mimi ni askari, ninafahamu ni kitu gani ninachokitaka kukifanya, ninachohitajia kwa hivi sasa ni silaha tu,...sina silaha,na sitaki kuazima silaha kwa aliyekuwa bosi wangu, nimeshaacha kazi kwake, na nataka iwe hivyo, mhh...’nikamwambia.

‘Wewe ni askari!!!?...’akasema hivyo kwa mshtuko..

‘Ina maana zile ndoto zako umezifanyia kazi, hahaha siamini,..sio kweli, bado wewe unaota ndoto zako..usidanganyike , kazi hizo hazikufai, wewe ni mwanamke, ukijiingiza huko, utajiharibia maisha yako, na hivi, huo uaskari umejifunzia wapi, hahaha…unafikiri uaskari ni mchezo eeh….’akasema kucheka sana..ukumbuke haya yote yalikuwa yakirekodiwa na marehemu.

Nazungumza hapa nikiwa naangalia huo mkanda uliorekodiwa na marehemu ambao sasa upo mikononi mwa polisi…

‘Kusema mimi ni askari sina maana ya kuwa mimi ni polisi, huoni mitaani kuna migambo, usalama shirikishi, hayo yawezekana au sio, na mafunzo ya hapa na pale yamenifanya mimi nijiamini hivyo, kuwa mimi ni askari ..’nikasema

‘Sawa vyovyote iwavyo, usije kujilinganisha wewe na Makabrasha, kuwa utaweza kupambana na yeye, yeye kijizatiti kwa kila hali, unamfahamu alivyo, sio...’akasema

‘Hahaha, mimi ndio nikukanye wewe , maana mimi namfahamu zaidi ya unavyomfahamu wewe, nikuambie ukweli…’nikasema

‘Hahaha wewe mwanamke, haha, yule ni rafiki yangu, tumakulia pamoja japokuwa ni mkubwa wangu, na mara nyingi nikikwama nakuwa naye, hadi sasa, useme mimi simfahamu,….wewe ndio humfahamu unaigiza ndoto zako tu, haya niambia lini umejifunza kutumia silaha?’ akaniuliza.

‘Mimi nafaham kutumia silaha kama unvyofahamu wewe kutumia kijiko wakati wa kula,...’nikasema kwa mbwembwe , na yeye akaniangalia kwa macho ya mshangao, nikaendelea kumwambia;

‘Nipe hiyo silaha uone nitakavyoitumia, hilo kwangu ni dogo sana, na cha muhimu kwa sasa ni mimi kuipata hiyo silaha, sio jinsi gani ya kuitumia au kutaka kujua nilijifunza wapi kutumia silaha, huu sio wakati wa kuulizana hayo, ...cha muhimu kwa sasa ni muda, tunakimbizana na muda, sitaki huyu mtu aendelee kuwatesa watu...’nikamwambia.

Hapo akatulia kwa makini, baadae akasema;

‘Mhh, haya,... ndio maana kila mara upo na rafiki wa mke wangu, najua ni yeye kakufundisha ujinga huo.., lakini uwe makini na silaha, mimi sipendi sana kushika shika silaha, sina ujanja huo...’akasema.

Haya wajumbe kwa polisi hadi hapo wanaweza kumshuku tena huyu mtu, eeh, keshatoka hapo, kwa maneno hayo, sasa endeleeni kuyashika hayo mazungumzo, ambao ndio ushahidi wa polisi,.. awali muhusika alionekana ni mume wa familia, sasa uhusika wa mauaji unamtoka, ni nani mwingine

Kwa kauli zangu niliwahi kusema , …najua kutumia silaha,..mumeona hapo, pili natamani huy mtu afe akiendelea kuishi ni shida, au sio…nataka nielezee kila kitu kama ushahidi wa polis ulivyo, ili nikitoka hapa na kufikishwa kizimbani mje kuwa mashahidi wangu…kwa vile nastahiki au sio..niendee au nisiendee…’akasema akimuangalia mwenyekiti.

Mwenyekiti alibakia kimia, hakusema neno, ila wajumbe kwa pamoja wakasema.

‘Andelea, endelea..’wajumbe wakasema.

**********
Hapa bado nipo na mwenzangu tunaongea,…kama ushahidi wa polisi ulivyo….

‘Mimi ninahitaji sana silaha kipindi kama hiki, lakini sitaki mtu afahamu kuwa nina silaha,..hasa rafiki wa mke wako, na nimekuambia haya tu, iwe siri yako, mimi nitamuwinda huyu mtu hadi kieleweke,…’nikasema

‘Mhh..haya bwana…’akasema mume wa familia

‘Kwa hivi sasa nahitaji sana silaha, na tatizo ni muda, ningeenda kuazima kwa watu wangu ninaowafahamu, japokuwa sipendi iwe hivyo, lakini muda,…na mimi sitaki ushahidi zaidi kwa watu wengine, nikiazima kwao, utakuwa ni ushahidi , na kwa hili sitakie liwe hivyo…hapo nje wapo watu walionileta wananisubiria.’nikamwambia.

‘Oh, nimekumbuka jambo, ..unajua sisi tunayo silaha, silaha ya mke wangu,…’akasema

‘Mhh..kweli,..lakini utaipataje..?’ nikamuuliza

‘Mimi ninaweza kukupatia hiyo silaha sio kazi kubwa kwangu, nina ufunguo za makabato yote hadi hivi sasa…lakini mimi najiuliza tu, …nina wasiwasi na hilo, wewe unahitajia silaha ya nini, unataka kumuua nani, usiniambie umefikia hatua ya kutaka kumuua Makabrasha?’ akaniuliza kwa mashaka.

‘Hahaha, mimi sio muuaji bwana, ..na wala ….mimi sitaki kumuua mtu yoyote, na sina mpango huo, ila ikibidi..sitasita kufanya hivyo kwa kujilinda,..au ikibidi sana, kama ni lazima nitafanya hivyo kwa masilahi ya wengi, ni bora nifungwe lakini wengi wawe huru au sio….’nikasema nikiwaza jinsi gani ya kumfamisha mtu kama huyo.

‘Hapana hadi hapo unanipa mashaka..’akasema

‘Silaha ni muhimu sana kwangu kwa hivi sasa, kuliko wakati mwingine wowote…’nikamwambia hivyo

‘Nakuomba tafadhali usije ukafanya makosa kama hayo, nakuhitajia sana katika maisha yangu, na ukumbuke mimi ndio wewe na pendo letu ni la asili haliwezi kufutika abadani…sisi ni kama mapacha kwenye pendo,…’akasema akiniangalia kwa macho yaliyojaa huruma.

‘Mimi siwezi kufaya kosa kama hilo, niamini, mimi siwezi kuua, nitafanya hivyo, ikiwa ni lazima, najua sheria, najua ….na kwanini niue, kama ningelitaka kufanya hivyo ningelishafanya hilo jambo mapema sana, ...’nikatulia na yeye akainamisha kichwa chini…hayo mtayaona vyema kwenye ushahidi, ..naongea kama ilivyo

‘Sawa…naombea iwe hivyo…’akasema

‘Mimi nahitajia hiyo silaha kwa ajili ya kujilinda mimi mwenyewe, na zaidi ni katika kujihami..na sio kwa muda wote, ni kwa muda maalumu tu,..kwahiyo muda wake ukifika, nikiwa na hiyo silaha nitakuwa na amani sana, ninakuwa kama nina wasaidizi watano nyuma yangu, ..’nikamwambia na nikweli nikiwa an silaha, hunibabaishi, wanaonifahamu wanalijua hilo.

‘Unasema hiyo silaha ni kwa ajili ya kujihami, lakini hapo mimi nahisi kuna kitu kikubwa unataka kukifanya, wewe unanificha, …sikiliza sitapenda nije kusikia jambo kubwa limekutokea, nitajutia sana, na huenda na mimi, nikajiua…’akasema

‘Kuna jambo nataka kulifanya usiku wa leo, na asubuhi yake, ni muhimu sana niwe na wasaidizi wangu, na wasaidizi wangu ndio hiyo silaha..kama sitapata silaha, sitawezi kulifanya hilo ninalotaka kulifanya..huyu jamaa yetu kajizatiti kweli kweli, ana walinzi, ana mitandao ya ulinzi, ana mitambo ya ulinzi,.. kwahiyo hata nikiwa na silaha,…najiuliza nitafanya nini nayo, unaona hapo, kwahiyo kama ni kwa ajili ya kumdhuru huyo mtu, hilo mimi siliwezi....’nikamwambia.

‘Naona wewe unalako jambo, na kwa huyo mtu, wewe utajitakia matatizo makubwa, nahisi wewe hujamfahamu Makabrasha vyema....na nikuulize hivi yule mtoto wake mkorofi si bado anafika fika hapo kwa baba yake, je huyo mtu utawezaje kumdhibiti….maana yule ni kichaa, eti kasomea sheria, mbona haviendani! ...’akasema

‘Umeona eeh..huyo huyo… mtoto kama baba,..’nikasema

‘Kwahiyo kumbe unataka kumuua huyo mtu…’akasema

‘Hapana, nani kasema nataka kumuua mtu,…nielewe mimi hapo, sina haja ya kumuua mtu, sio kazi yangu kufanya hivyo,..kwani mpaka sasa nimeshajitolea kiasi gani, kama ningelitaka kufanya hivyo, nisingejizalilisha hivyo, unasikia, mimi naweza kufanya lolote, lakin kwanini nifanye hivyo, hapana....’nikasema

‘Sasa haya bwana,….maana ni kweli hadi sasa tulishaamua kuwapa kila kitu, ili tu..wasije kutuchafulia majina yetu, na sipendi kwakweli, lakini hakuna jinsi, wa kulaumiwa ni sisi, najua kabisa,wakwe zangu watakuwa wanasubiria hili kwa hamu, nifukuzwe kama mbwa, maana, ushahidi upo..ndio maana nasema ni heri kujitolea hivyo kwasasa, huku tukitafuta njia muafaka, au sio…’akasema

‘Umeonaeeh, nashukuru sasa unaanza kunielewa, kuwa tatizo ni wewe, wewe ndio mkosaji ,…’nikamwambia.

‘Sote ndio sababu ya haya yote…huo ndio ukweli..’akasema na mimi hapo nikabakia kimia, akaendelea kuongea.

‘Sawa waweza kusema mimi ndiye nimewakose watu hao zaidi…najihisi kuwa mbaya kuliko…, sijui kwanini,..hivi kweli ni kwanini..kwanini mimi nakuwa na tamaa kupita kiasi, nilikosa nini,..mmh, haya yote yasingelitokea,…’akawa anaongea kwa kujijutia, lakini baadae nikasikia akisema

‘Hata hivyo…kiuhalisia mikataba ile inanipa nafsi nyingine ya kufanya jambo, huenda nikashinda, unajua huo mkataba, unanipa mimi mamlaka ya kufanya kila jambo, kama mume wa familia....’akaniambia.

‘Upi huo..huo wa kugushi au,…hahaha, unafikiri mimi sifahamu janja yenu..’nikasema

‘Mimi sijui kama ni wa kugushi..’akasema

‘Haya sawa, vyovyote iwavyo, lakini wewe hujaliangalia hilo kwa mapana yake, hapo ulipo kwa lolote utakalolifanya kwa sasa, bado upo kwenye matatizo, hasa ya ndoa yako..’nikasema

‘Sawa lakini kwanini tusjaribu kwanza…’akasema

‘Tusi-au usi…mimi sihusiki na hayo mambo yenu,…kumbuka kuwa huo mikataba wa kugushi eeh, ni danganya toto, si chochoteni swala la muda tu..na hata hivyo hata ukiutumia je ni kweli utakuwa na amani na mke wako, atakubaliana na hilo..kiukweli nakuambia hili unisikie, hutaweza kuwa na amani, mke wako hataweza kutulia kwa hilo, na hataweza kukupatia hicho unachokitaka,..yeye sio mjinga, ni lazima atahangaika mpaka aupate ukweli, je huoni kuwa akiupata huo ukweli ndio itakuwa njia ya kuyabaini haya yote..na huku kwa upande wa pili unakuwa mtumwa wa Makabrasha, hatujui mwisho wake utakuwaje unaona ilivyo...'akasema.

'Ni sawa, ..sasa tufanyeje,…?’ akauliza na mimi nikakaa kimia, akaendelea kuongea.

‘Ndio maana mimi ikifikia hapo, nasema bora tu iwe hivyo…nitakuwa mtumwa wa Makabrsha sawa, lakini nitakuwa na mali, au sio..na nina uhakika itafika muda, maana usinione nipo hivyo, natafuta njia, nahangaika lazima kuna namna na yeye eeh…nitamnasa tu, najua ipo siku ataingia kwenye anga zangu, ipo siku, ni lazima nifanye jambo, ngoja nione cha kufanya…’akasema

‘Hahaha, kwa Makabrasha..unajisumbua,…, hapo ulipo kila unachokipanga keshakifahamu, kama mwanga vile… wakati mwingine huyu mtu simuamini kama ni mtu wa kawaida, kila ukipanga jambo analifahamu kabla..wewe hujaligundua hilo ...?' nikamuuliza.

‘Najua, yeye atakuwa kawekeza namna ya kupata mazungumzo…alishawahi kuniambia hilo, ana vifaa vya kunasia sauti, na matukio…lakini hataniweza ..hata mimi ni mjanja pia, wewe utaona tu ..’akasema kwa kujiamini.

'Haya bwana, ..hivi nikuulize kitu, hivi wewe unaifahamu vyema familia ya mke wako..walivyo , wakwe zako,…achilia mbali utajiri wao, unawafahamu kuwa wanakuchunguza kila mara, unafahamu kuwa wana namna zao za kugundua mambo, na huenda walishakufahamu ulichokifanya?’ nikamuuliza

‘Nawafahamu sana, uzuri wao, hawahangaiki sana na mambo ambayo sio muhimu kwao,…wanajifanya kufuata sheria,..zaidi ya hayo, kama ujuavyo wananichukia sana..walifikia sehemu wakasalimu amri..na kuniheshimu kama mkwe wao…ndio maana kwa hili nitajitolea kwa ajili yao, wananidai kwakweli, nijaitolea kuhakikisha kuwa hii kashafa imefutika…’akasema

‘Mhh….sasa nakuona umebadilika, sawa..lakini umeshachelewa, familia ya mke wako, sio ya kuchezea, mimi nimeshaichunguza vyema tu, ni heri ya huyu Makabrasha anayetumia njia za mkato, lakini familia ya mkeo wako ni watu wa sheria…kumbuka hilo, umeshakiuka sheria, na sheria ndio itakuhukumu..kwahiyo hadi sasa jihesabu kuwa sio mkwe wao tena,…’nikasema.

‘Haahaha…ndio hapo nakubali niwe tu mtumwa wa Makabrsha, alichofanya namvulia kofia…sasa nikuulize hadi hapa ulitaka mimi nifanye nini…?’ akaniuliza

‘Hdi hapa umeshachelewa, kama ungelinisikia toka mwanzo, haya yote yasingelifika hapa, tamaa zako za kimwili, na akili fupi ya kufikiri ndio imekufikisha hapo ulipo, na hata sijui itakuwaje huko baadae, lakini acha iwe hivyo upate fundisho, mtoto mwingine bila kumchapa hawezi kukua, na wewe bila kuonja jela, sizani kam utaweza kubadilika…’nikasema

‘Usinizalilishe kihivyo…’akasema kwa hasira.

‘Huo ndio ukweli sio tusi, ,...sijui kama kweli haya yataisha kwa amani, na hata yakiisha kwa amani, sijui kama ndoa yako itakuwepo tena, na baya zaidi unaweza ukaishia jela, wakikuhurumia sana, watakutupa kijijini ukawe omba omba...’nikamwambia.

‘Thubutu, hilo halitatokea..ndio maana nakuambia hadi hapa namshukuru sana Makabrasha, kafanya nisichoweza kukifikiria,…ok, likitokea la kutokea, basi utafanya nini,..lakini muhimu jitahada…mimi nina imani tufanikiwa,...’akasema

‘Hahaha, unajipa moyo sio, utafanya nini wewe kufanikiwa hizo ndoto zenu za mchana…....?’ nikamuuliza

‘Tuyaache hayo, kwanza hebu niambie hiyo silaha unahitajia ni kwa makusudio gani hasa, ..kiukweli ukiniambia ukweli mimi nitakusaidia, kuipata hiyo silaha, ila nina mashaka na wewe hivi kweli wewe unaweza kuitumia..?’ akaniuliza.

‘Ni kuhusu huyo mtoto wake, yeye ndiye namuogopa sana, anataka kunifanya mimi kama anavyonifanya baba yake, siwezi kuzalilika kiasi hicho, silaha itanifanya nimdhibiti...nataka silaha ya kujilinda..’nikamwambia bila kumfafanulia mambo mengine ambayo niliyapanga kichwani mwangu,sikuwa namuamini sana kwenye mambo hayo ya kivita..

‘Kama kweli unahitaji hiyo silaha kwa jaili ya kujilinda sawa… mimi nitafanya kila mbinu hadi niipate hiyo silaha,..hilo niachie mimi , nitachukua silaha ya mke wangu…’akasema

‘Kwa vipi…?’ nikamuuliza

‘Kwa vile ni vigumu kutoka humu,…mimi nitamtumia mdogo wangu..ila tukubaliane kitu…maana ujua hiyo silaha sio yangu, kwahiyo hiyo silaha itakuwa inaletwa kwako usiku kama ukiwa na kazi za usiku, asubuhi tunairudisha mahali pake..unasemaje kuhus mpango huo…?’ akaniuliza.

‘Kama unaweza kuipata hiyo silaha, itasaidia sana, nahitaji kuwa nayo sanasana usiku wa leo, na asubuhi utakapokwenda kukutana na Makabrasha, baada ya hapo inaweza isiwe na kazi tena, sitaihitajia kila siku ...’nikamwambia na yeye akaniangalia kwa mshangao, hakuamini kuwa mimi ninaweza kutumia silaha.

‘Sawa hilo litafanyika, usijali..’akasema

‘Sikiliza kwa makini, kesho ukifika kuonana na Makabrasha,..’nikasema

‘Wewe umejuaje hilo..!!!?’

‘Hayo sio muhimu wewe kufahamu fanya ninavyokuagiza, unasikia..’akasema

‘Ok sawa, wataka mimi nifanye nini…?’ akauliza

‘Mimi nataka wewe uwe unamchelewesha ili nipate muda wa kusimamisha mitandao yake ya ulinzi, na ...kwa vile mtoto wake, atakuwa hayupo, ...kama alivyodai, japokuwa simuamini, ...nitaweza kufanya mengine bila kujulikana, yote inategemeana na muda, muda ni kitu muhimu kwenye mapambano kama hayo...’nikamwambia.

‘Kwani unataka kufanya nini, mbona unanificha, maana mengi yameshafanyika, mikataba karibu yote nimeshaisaini kukubali, umebakia huo mmoja tu,.....na wewe mwenyewe umeshasaini mkataba wako, kilichobakia ni mume wako tu, na yeye nasikia alishakubali kuweka saini yake ..’akasema mume wa familia.

‘Mhh..hayo ya mume wangu achana nayo…’akasema

‘Kwanini, au.kwanza niambie mume wako ulishaongea naye...?’ akaniuliza.

‘Kuhusu nini..?’ nikamuuliza

‘Kuhusu nini! Si kuhusu haya, ili…usije kuharibu kote kote, sitaki uje kupata shida, maana hili ni letu sote, ni muhimu tutimize lengp letu kwanza mengine yatafuata baadae au sio..?’ akasema

‘Siwezi kufanya ujinga kama huo, unafikiri mimi ni mjinga kama wewe...kanisainisha huo mkataba, nimekubali kufanya hivyo, lakini siwezi kuongea na mume wangu, kuhusu haya mambo, ..nafahamu kabisa mume wangu hawezi kukubaliana na hilo.., sana sana, hiyo itakuwa, ni kunitafutia njia ya kupewa talaka haraka..ndio maana nahitaji hiyo silaha...’nikamwambia.

‘Kumbe...ni kwa ajili yako tu…ili wewe usipewe talaka haraka, je mim, itanisaidia nini hapo,..ujue mimi ndiye nabeba dhamana ya hiyo kitu, kukitokea tatizo ni mini nitawajibika, au sio...’akasema kwa shingo upande.

‘Tatizo gani, mimi ni kwa ajili ya kujilinda, …hakuna…’kabla hajamaliza

Kwenye simu yangu ukaingia ujumbe ukiniarifu kuwa muda wangu wa kuongea na huyo mtu umekwisha ninasubiriwa nje tuondoke.

‘Kuna nini…?’ akauliza

‘Natakiwa kuondoka, muda umekwisha..’nikasema

‘Ndio hayo…tutaendelea hivi mpaka lini..’akalalamika.

Kwenye huo ujumbe , pamoja na hili la kuwa muda umekwisha wa kuongea na mgonjwa, pia kulikuwa nanyongeza ‘nisisahau kuwa usiku wa leo kuna kazi…’

‘Kuna kazi..sawa..’nikajikuta nimesema hivyo, mimi nilifahamu hilo, lakini kuna kitu kilinitia mashaka mume wangu, alinitumia ujumbe kuwa anataka kuja huko kujijini, kunifuata , yeye anajua nipo huko kijijini… itakuwaje…je akifika huko kijijini akinikosa itakuwaje…kiukweli hapo akili ilishaanza kutatika.

‘Je hiyo silaha inaweza kupatikana kwa usiku wa leo, ...?’nikamuuliza nikiwa sasa najua hilo jambo lifanyika na mimi nitoweke, niende kwetu kijijini, huko nitatulia kwa muda, nikisubiria matokeo.

‘Nitajitahidi..lakini….’akasema

Nikianza kuondoka, na wakati huo, mume wa familia alikuwa akitaka kuongea jambo, mimi sikuweza kumpa nafasi tena.

Nilipofika mlangoni nikageuka kumuangalia mume wa familia, maana alikatiza kuongea, sikuwa na uhakika na kauli yake, nikasema

‘Mimi naondoka, …ni muhimu..’nikasema

‘Hilo niachie mimi, ...silaha itapatikana, na natumai hutaifanyia jambo la kijinga...’akasema na mimi nikasimama, ghafla nikageuka na kurudi pale kitandani, nikamwambia, kwa sauti ya chini chini;

‘Usiku wa leo kuna tafrija kwenye lile jengo, itakuwa ni nafasi nzuri ya mimi kuweza kuipenyeza hiyo silaha bila kujulikana,..je una uhakika leo itapatikana,…?, kama kweli itapatikana usiku wa leo muda wa saa tano hivi, itakuwa vyema, je mke wako hawezi kuhisi kuwa silaha yake haipo, hilo ni muhimu kufahamu?’ nikamuuliza.

‘Mara nyingi haitumii hiyo silaha.., ipo kwenye kabati lake siku zote, sijawahi kumuona akiichukua kwa muda mrefu sasa.., hata kama kuna tukio la hatari, kama ilivyokuwa zamani, sijui kwanini, ipo tu..sizani kama atakuwa na wasiwasi nayo...’akaniambia.

‘Basi wewe jitahidi, mtume mdogo wako,akaichukue ...mimi nitawasiliana na yeye, nione jinsi gani nitakavyoichukua hiyo silaha, lakini asifike sehemu ya mapokezi, anyway mimi nitaongea naye baada yaw ewe kuwa na uhakika wa kuipata sawa, au sio..’akasema

‘Hilo kwa ajili ya kuipta haina shaka…mengine nyie wawili mtajua, jinsi gani na wapi pa kukutana naye, kazi yangu ni kuhakikisha hiyo silaha umeipata au sio…’akasema

‘Ni muhimu yeye asije kuonekana yupo na mimi, au kuonekana karibu na hilo jengo, najua hata akionekana na mimi, nitakuwa sio mimi, hayo nayafahamu mimi mwenyewe, ..ok, tumemalizana, au kuna jingine...’nikamwambia.



Na mpaka hapo tukawa tumekubaliana hivyo...na tulikuwa tukiongea nje kwenye eneo analochukulia mazoezi ya viungo kwasababu ya matatizo yake ya ajali.

‘Na kweli usiku ule nikaipata hiyo silaha, silaha iliyokuja kumuua Makabrasha,...swali ni je niilipata pata vipi hiyo silaha, na ilitumikaje, nitawaelezea yote hayo..kama mwenyekiti ataniruhusu….’akasema na kutulia kidogo, akamwangalia mwenyekiti.

Mwenyekiti alikuwa akiangalia saa, na mara shahidi huyu akaenda pale alipokaa mwenyekiti wakawa wananong’ona, sikujua wanaongea kitu gani, lakini walipomaliza kuongea, mwenyekiti alichukua simu na kumpigia mtu, huku akiwa kamuangalia huyo shahidi kama vile anaogopa jambo kutoka kwa huyo shahidi.
. ...
NB: Je silaha hiyo ilifikaje kwa shahidi, na je ilitumikaje kumuua Makabrasha na je kwanini shahidi huyu anaongea sana na mwenyekiti, tukutane sehemu ya tatu ya hitimisho la kisa hiki.

WAZO LA LEO: Kila hila mbaya, ina walakini wake, na mwisho wa hila mbaya, ni kuumbuka tu, hakuna hila mbaye yenye kudumu.
 
SEHEMU YA 115


Niliwasiliana na mdogo wa mume wa familia;

‘Vipi umepewa ujumbe wowote na kaka yako..?’ nikamuuliza, nikasikia kama mngurumo wa gari kuonyesha kuwa yupo kwenye gari

‘Kaka ameshanipa ufunguo tayari, na hapa ndio nipo njiani, kwenda kuuchukua huo mzigo, … lakini kwanini mnafanya hivyo, hamuoni kuwa ni hatari, je shemeji akigundua…mimi naogopa sana haya mambo yenu…’akasema akionyesha kuwa na wasiwasi.

‘Usijali, ni mambo ya kawaida, hayo ni kwa ajili ya kaka yako, sasa hivi hali ilivyo ni lazima tufane jambo, vinginevyo, ..sasa, unasikia, fanya hivyo, ukiwa tayari niambie, unasikia, sikiliza kwanza….’nikamuelekeza jinsi ya kufanya.

‘Sawa nimekuelewa…’akasema

Kilichokuwa kimefanyika ni namna ya kuhakikisha kuwa mke wa familia hayupo nyumbani, na acheleweshwe kinamna ili kila jambo likamilike kwa wakati, kwani mke wa familia hakuwa anafahamu ni nini kinachoendelea. Kazi hiyo ilibakia mikononi mwa mume wake,…

Je ilifanyikaje…nahisi nyote mtapenda kusikia sehemu hiyo,…ukumbuke haya yanafanyika muda ambao mke wa familia anatarajia kurudi nyumbani.

*********

Mume wa familia aliigiza kuzidiwa…si nilishaambia huyu mtu kuna hali ilitakiwa aigize kuumwa zaidi ya anavyoumwa, hapa sasa uone ushahidi.

‘Docta najisikia vibaya sana..sizani kama nitapona…’mgonjwa huyo

‘Utapona tu usiwe na wasiwasi ni dawa hizo…unasikia, wewe lala na tulia..’docta akasema.

‘Hapana docta, oh… kwa hii hali naomba umuite tu mke wangu, nataka kuongea naye, nahisi kukata roho…aaah.’akasema huku akigugumia maumivu.

Kutokana na matatizo yake hayo, mara nyingi kila anachohitajia inabidi apewe ili asiwe na msongo wa mawazo, kwahiyo docta kwa haraka akachukua simu. Kiukweli hapa docta hakufanya kutokana na maagizo, hapa alifanya kazi yake.

‘Halloh, mimi ni docta hapa, tafadhali nakuomba ufike hospitalini haraka iwezekanavyo,…’docta akasema

‘Kuna nini, mgonjwa kazidiwa…?’ akauliza

‘Hali kidogo imebadilika, …anataka kuongea na wewe, ni muhimu uje, maana imekuwa ni kero,..’akasema docta

‘Kero kwa vipi docta..?’ akauliza

‘Anataka kuongea na wewe, unajua kutokana na hiyo hali na dawa anazotumia,anakuwa kama mtu anayeweweseka-weweseka ,..ni kawaida, hata hivyo, kila anachohitajia kwa hivi sasa, inabidi tu tumpatie, ili asiwe na msongo wa mawazo…..’akasema docta.

‘Lakini yupo vipi…?’ akauliza mke wa huyo mgonjwa.

‘Anahis maumivu…na ni kawaida, lakini ni muhim uje…’akasema docta.

‘Sawa nakuja docta, …nipo njiani, nilikuwa naelekea nyumbani, nakuja sasa hivi…’akasema mke wa familia.

Wakati hayo yanaendelea huku nyumbani mdogo wa mume wa familia alikuwa anafanya kazi aliyoagizwa, ….

Zoezi likakamilika!

Kitu kingine muelewe, huyu docta naye alishawekwa sawa na Makabrasha, kwahiyo naye kila anachoambiwa anakubali, ila kwa siki huyo docta alijua kabisa mgonjwa kazidiwa....Makabrsha alikuwa sio mchezo.

Silaha ikaletwa sasa kazi jinsi gani ya kuingiza humo kwenye jengo...ukumbuek jengo hilo linalindwa na mitambo ambayo ikihisi kitu kama silaha itapiga ukelele..kuashiria jambo..

Nilishamuelekeza mdogo mtu ni nini cha kufanya, anachotakiwa ni kuifunga ile silaha kwenye kamba ambayo niliining’iniza kutoka rosheni ya pili,…na taa za upande ule nilizima.

Kwahiyo mimi nilishajiandaa kwa hili, nilikuwa na kamba ndefu, inayofika chini, ujue lile jengo lina rosheni,lakini kwa ajili ya kuiingiza hiyo silaha ndani, nilitumia rosheni ya pili,…

Baada ya ile silaha kufungwa kwenye hiyo kamba, nikaivua hadi juu,…sasa jinsi ya kuifikisha kwenye chumba changu, nilitumia njia zangu nyingine, sio muhimu kuelezea hapa, cha muhimu ilikuwa kuhakikisha kuwa mitambo ya kutizama matukio na kengele ya hatari ilikuwa imezimwa, umeona hapo.

Nilifanya hilo, na kitu kingine muhimu, kuna huyu mtoto wa marehemu, mtoto wa kufikia, huyu ni Makabrasha wa pili, yeye pamoja na kazi yake ya uwakili, lakini pia alikuwa mtaalamu wa mitambo hiyo,…ndio yeye alikuwa akiisimamia, yeye anafahamu kila kitu cha baba yake.

Siku hiyo nlifanya uchunguzi wangu nikagundua kuwa mtoto huyo wa Makabrasha hayupo kwenye jengo maana mara nyingi yeye hufika usiku. Na alikuwa na kikao chake sehemu nyingine…lakini atafika hapo, sijui muda gani. Huyu ndiye niliyekuwa namuogopa hata kuliko baba yake!

Nikaichukua ile silaha na kuificha chumbani kwangu, kwani haikutakiwa kuwa mbali na mimi ili nikiihitaji nisipate taabu, nilihakikisha kuwa hayo yote niliyafanya kwa ujanja wa hali ya juu, mitambo imezimwa, na hakuna mtu aliyeniona nikiyafany hayo yote..…si unajua tena mimi ni nani.

Baada ya kukamilisha hayo, nikarudi kwenye hicho chumba, hicho chumba kinafungwa muda wote, hakuna anayeruhusiwa kuingia zaidi ya Makabrsha mwenyewe au mtoto wake,..au kama kuna tatizo ni fundi wao maalumu.

Nilipoona kila kitu kimezimwa, nikarudi haraka ofisini kwangu, nikijifanya sasa kuhangaika kwanin mitambo na umeme umezima,…pamoja na hayo sikujua jinsi gani ya kufuta matukio kwenye mtandao, maana ni lazima pale ilipoishia itanionyesha mimi nikiingia kwenye hicho chumba.

Sasa nikiwa kwenye ofisi yangu, najifanya kuhangaika na simu kumpigia fundi, ili aje awashe umeme, nikijifanya sijui wapi umeme ulipozimwa,..basi akiwasha niende kule kwenye mitambo niwashe, haya yalitakwia yafanyike kabla mtoto wa Makabrsha hajafika…

Nipo nampigia fundi,….mara mlango wangu ukagongwa, nikajua ni Makabrasha mwenyewe, huyu ningejua jinsi gani ya kumdanganya,…nikasogea kufungua,..mbele yangu nikakutana na yule mtu ambaye, sikutaka kukutana naye siku hiyo….

Mungu wangu huyu kaja saa ngapi!...

************

‘Mbona sipati ishara ya mawasiliano kutoka hapa, ni nani kazima mitambo ya usalama wa jengo, na kwanini umeme umezimika, kuna tatizo gani.. ?’ akaniuliza akionyesha wasiwasi

‘Mitambo ya usalama wa jengo, ipo wapi hiyo...aah, mimi sijui mambo yenu na wala sijui kama imezimwa, na kwanini izimwe!?...’ nikamuuliza kwa mshangao.

‘Na..na.umeme ndio umezimika nahis kulikuwa na shoti…mimi sijui ndio maana nampigia fundi…’

Na yeye hapo akaniangalia kwa mashaka, halafu akageuka..

‘Huyu mtu anakwenda huko kwenye mitambo..hapo nikajua nitaumbuka.

Basi kwa haraka na mimi nikaelekea huko, kwenye chumba cha mitambo hiyo…nilimfikia lakini hakugeuka na hakujua mimi nipo nyuma yake, namfuatilia kwa nyuma kiujanja….Naona, mawazo yake yalikuwa kwenye hilo jambo analilifuatilia.

Akafika na kufungua mlango, akaingia ndani, na mimi kwa haraka nikaingia, chumba kilikuwa giza, ila kwa mngurumo wa hiyo mitambo, …sijui kwanini iliendelea kunguruma wakati mimi nilishazima..na umeme umezima…na kulikuwa baridi sana....hakugeuka nyuma, akawasha sehemu ambayo mimi nilizima.

‘Unaona kuna mtu alizima hii mitambo,..atakuwa ni nani huyu…nani mwingine anayeweza kuingia humu…kama sio huyu mwanamke, na kwanini aizime..huyu mtu nina mashaka naye…’akawa anaongea peke yake.

Halafu akaenda kwenye meza yenye komputa na sehemu ya kuangalia kinachoendelea kwenye jengo,,…akakaa, ni baada ya kuwasha, sasa akatoa laptop, hiyo ipo ndani ya meza, inafungiwa, akaiwasha na kuanza kukagua kitu, akawa anaangalia ni nani aliyekaribia hicho chumba, ni wazi kuwa ningelionekana mimi, sikuwa nafahamu jinsi gani ya kufuta matukio ya nyuma yake.

‘Ssshiit….’akasema hivyo tu.

Kiukweli jinsi alivyowasha ile lapotop, niliona, japokuwa kwa shida, niligundua herufu alizobonyeza kuwasha ile komputa, ikanasa kichwani….alipohakikisha alichokitaka akatoka kwenye kiti chake sasa…akageuka nyuma, kama kutaka kutoka nje…

Ukumbuke nipo hapo ndani na sio mbali sana na hapo alipokaa,..na kwa hali kama ile nisingeliweza kurudi nyuma na kukimbia, angelinigundua na hapo ingelileta picha mbaya, na tendo hilo lingelionekana kwenye mitambo, nikatulia tu

Alipogeuka, akaniona,,,…nilitakiwa niondoke kwa haraka, lakini ikawa sio rahisi,…alipogeuka tu, akaniona. Akashituka na kuniangalia akiwa kakunja uso, kuashiria hasira na mshangao!.

‘Oh, wewe mtu, unakuwa kama mzimu, yaani ulikuwa ukinifuatilia nyuma, huku nilishawaambia hatakiwi watu kuingia huku, niambie umefuata nini, na inaonyesha wewe ndiye uliyefika huku, ...?’akasema kwa hasira.

‘Baba yako alinituma kufanya usafi sehemu zote...kwani kuna wageni muhimu alitarajia kuwa watakuja kumtembelea...’nikasema lakini nilifahamu kabisa kuwa kama ni usafi, huwa eneo hilo sijawahi kufika kufanya usafi na, yeye akasema;

‘Hata kama ni usafi, toka lini ukaja kufanya usafi eneo hili, wakati mimi sipo, haiwezekani, na hata kama ulifanya usafi kwanini ukazima mtambo mkubwa, ?’ akaniuliza kwa mashaka.

‘Mtambo mkubwa!!! Ndio mtambo gani huo…?’ nikauliza na yeye akawa ananiangalia kwa mashaka. Hapo hakusema neno kwanza, mimi nikasema;

‘ Mimi niliona kuwa eneo hili ni chafu, ndio nikaja kulifanyia usafi, ...na sijui kama nilizima, ndio kuna wakati nadeki, nikaona nisije nikarushwa maji, nikaharibu vitu vyenu,…sijui lakini nilipozima nikaona kila kitu kimezima, tatizo nilisahau kuwasha tena, kwani kuna kitu kimeharibika..?’ nikauliza

‘Wewe mtu sikuamini..nilishamuambia mzee, lakin..haya…’akasema

‘Tatizo ...mimi mambo yenu hayo siyajui…naogopa sana umeme..’nikasema

‘Ni nani alikupa ufungua wa chumba hiki?’ akaniuliza

‘Unauliza jibu, ninapotaka kufanya usafi, nilishawahi kuja kwako kukuuliza ufunguo upo wapi, eeh…, mimi ninafahamu wapi funguo zote zilipo, kwanini unaniuliza maswali mengi, mbona siku nyingine hujawahi kuniuliza, maswali kama hayo kuna nini kwani, mbona mnanitisha…’nikasema sasa kwa hasira.

‘Wewe mwanamke mimi sio mjinga…’akasema sasa akinionyeshea kidole, hakunifahamu kuwa mimi siogopi vitisho….nilitulia nione anataka kufanya nini.

Akasimama, aliponikaribia, akataka kugeuka, na mimi nikasema

‘Nani kakuambia wewe ni mjinga, kama hayo niliyofanya ni ujinga, basi unamtusi baba yako aliyeniamrisha mimi nifanye usafi..na ni mara ngapi nafanya usafi, na kwanini huendi kumuuliza baba yako, kama una wasiwasi na mimi, mbona unaniwekea vikwazo visivyo na msingi..mzee wako ananiamini ndio maana kaniajiri niwe karibu naye.’nikamwambia.

‘Mzee hajakufahamu kuwa wewe ni nani, mimi nimeshakufahamu…wewe sio mtu mnzuri kabisa…’akasema
‘Sawa nitamuambia baba yako, amtafute mtu mwingine, ..si ndio hivyo unataka au sio…ngoja akija,..leo itakuwa mwisho wa kuniona humu ndani..’nikasema

‘Leo iwe ni mwisho wako kuingia kwenye hiki chumba, tatizo ni kuwa umezima mtambo mkubwa wa mawasiliano, na kwahiyo umetufanya tushindwe kuwasiliana na humu ndani, ni hatari..na najua hili utakuwa umelifanya kwa makusudi....’akaniambia.

‘Kwa makusidi !!! Mbona sikuelewi…ili iweje,…’nikasema

Niliona hiyo hali ikiendelea itazidi kuchelewesha mambo mengine, nikajaribu kuifanya kazi yangu nyingine, plan B, taratibu nikatabasamu, na kusema

‘Samahani mrembo, unajua wewe ukikasirika, ndio unapendeza zaidi..’Nikasema na kujirembua, nilishafahamu udhaifu wao, mtoto kama baba, akategeka, na kunisogelea, huku akisema;

‘Tatizo lako wewe kwasababu ya tabia yako unahisi kila mtu ni kama wewe....’nikasema huku nikijerembua.

‘Mhh..hahaha eti mimi mrembo, toka lini mwanaume akawa mrembo…’akasema na mim nikawa nimeshafika karibu naye, na haraka akanyosha mikono kutaka kunikumbatia…sikuwa na muda huo…

Unajua wakati mwingine ukiwa katika kazi kama yangu inabidi utumie kila mbinu, lakini akili kichwani mwako. Na alipoliona lile jicho, mtoto kama baba, akasawajika, nikamuona mate yakimtoka, akasahahu alichokuwa akiniuliza mara akasema;

‘Kwanza nikulize lile ombi langu vipi,..?’ akanisogelea baada ya kuzima kitu kwenye mitambi, sikujua ni kwanini, na akanisogelea kujaribu kunishika na mimi nikasogea pembeni na kusema;

‘Ombi lako lipi, eeh, hivi wewe vipi..!!!’nikasema sasa nikibadilika ghafla

‘Aaah, vipi tena…’akasema

‘Wewe mwanaume,..unajifanya upo sawa na baba yako au sio, nilishakuambia upuuzi kama huo, siutaki, msinione nipo humu ndani mkafikiria mimi ni Malaya, kwanza kuhusu huo upuuzi wako nitamuuliza baba yako...kama yupo tayari kuchangia na mtoto wake...haya,’nikasema na yeye akageuka kuondoka karibu yangu, huku akisema;

‘Hivi wewe baba unamuona mtu wa maana kwako, ombi langu kwako ni siri yangu mimi na wewe, eti ukamuulize baba, unataka nilaaniwe nini....wewe jivunge tu, ipo siku utaingia kwenye anga zangu, ..’akasema na mimi hapo nikacheka. Nikaona sasa nimeshabadili muelekeo…

‘Kumbe unajua hilo, hehehe..mtoto kama baba…yatawashinda…’nikasema

‘Wewe cheka tu, unafikiri mzee yule atakuwa na wewe milele, akikuchoka anakutupa chini, wangapi walikuwa naye sasa hawatakiwi tena,.. hata kumsogelea hawawezi, yeye anamtaka mtu akiwa na shida naye shida zikiisha basi, huyu mtu ni takataka.., ...wewe jidanganye kwake, ukifikiria umefika....’akasema.

‘Kama alivyomfanyia mama yako au sio,…?’ nikauliza hivyo, na hapo ikawa kama nimemshika sehemu mbaya, akasimama, akageuka, sura ilikuwa imebadilika, ..…

‘Tafadhali, usimtaje mama yangu hapa, unasikia tuongee mambo mengine lakini usimtaje mama yangu, tafadhali nakuomba…’akasema

‘Ukiendelea kunifuata fuata sitasita kumtaja mama yako, unasikia,…’nikasema na hapo akageuka hakuniangalia sasa,…nikaona bado, nikasema..

‘Unafikiri mimi sijui… hata hivyo mimi sijawahi kukuambia kuwa nina haja na baba yako, ...baba yako ndiye kanilazimsiha kuja kwa ajili ya mambo yake, mimi nina mume wangu, nina maisha yangu mazuri tu, na mume wangu nampenda, kama isingelikuwa haya mambo yenu unafikiri ningelikuwa hapa, na ipo siku mtajuta kwa hayo mnayoyafanya....’nikamwambia.

‘Hayo unayafanyiwa ni yenu na baba, mimi siyajui, ...na vitisho vyako, kwangu havina nafasi, nafahamu ni nini ninachokifanya kwa nafasi gani, usinitishe kabisa, mimi ninafahamu sheria, na sijawahi kukulazimisha kwa lolote lile, na hata hivyo ombi langu lipo pale pale, usiponitimizia najua jinsi gani ya kukupata...’akaniambia

‘Hahaha utafanya nini...?’ nikamuuliza

‘Siri zako zote anazozitumia baba kwa ajili ya kukupata wewe ninazo mimi, zipo kwenye mtandao, yeye akizihitajia mpaka aingie kwenye mtandao, na mimi ndiye nimezihifadhi, sasa utanidanganay nini, nikiamua kuzitumia dhidi yako, siutaumbuka wewe...sasa uamue moja kuwa na mimi au na baba..’akasema.

‘Nakuambia hivi ni bora umenifahamisha hayo, nitamuambia baba yako kila kitu, na hizo mbinu zenu..kumbe ndio mlivyo eeeh,..na ni bora aniambie ukweli nipo hapa kuchangia mtu na mwanae..kanifanya mimi Malaya sio..keshaniita mimi ni mtumwa wake, sasa wewe wataka kunifanya mimi ni Malaya, mtaniambia....’nikamwambia.

‘Hivi wewe una akili kweli,...kila kitu utamwambia baba,..utamuambia baba, huyu baba ndio nani, eeh….ok, …tuyaache hayo, naomba yaishe, au sio, samahani basi, namba tafadhali usije kumuambia baba....’akasema

‘Sasa tuelewane, ili nisimwambia baba yako, unifundishe jinsi gani ya kutumia huo mtandao, jinsi ya kutengeneza picha na kuziweka kwenye huo mtandao..’nikamwambia.

‘Unataka nikifundishe ili uje uzifute, ..hilo umenoa..’akasema

‘Kwahiyo unataka nikamuambia baba yako au sio..’nikasema

‘Sikiliza kama unataka nikufundishe, kwanza na mimi unikubalia ombo langu, mimi nitakufundisha kila kitu unachotaka…tena tuanze leo, unasemaje…’akasema

‘Sawa…’nikasema

‘Lakini tumekubaliana, nitakufundisha lakini malipo yake ni ...maombi yangu..’akasema sasa akitabasamu, uso umeshasawajika.

‘Kwanza unifundishe, malipo si baada ya kazi…’nikasema

‘Hahaha wewe mjanja sana, sikiliza kama kweli unataka hilo, tukubaliane, mimi nipo tayari,...na safari hii sikubali, kama ulivyonidanganya siku ile… la sivyo, na mimi nitaweza kukufanyia kitu ambacho hutaweza kunisahau....’akasema

‘Kitu gani, hujui haya yote baba yako anayasikia..’nikasema

‘Hahaha, wewe hunijui eeh, mimi sio mjinga kihivyo,…nikuambie kitu,..ujue na mimi ni wakili kama baba…kila ninachokifanya najua jinsi gani ya kujilinda,…’akasema na mimi sikumjibu

Nikageuka kama kutaka kuondoka,..yeye akageuka, nahisi alitaka kukiwasha kile kitu alichokuwa kakizima….

**********

Alipogeuka akazima kile kitu na kutembea hadi mezani kwake hakugeuka, alishajua kuwa nimeondoka…akawasha ile laptop, akawa anatizama matukio, akawa sasa anafuta baadhi ya mtukio, nahisi ni hapo tulipokuwa tunaongea naye, alipomaliza, akazima ile laptop, akairejesha sehemu yake...

Mimi nilikuwa pale karibu na mlango, sijaondoka… na alipomaliza shughuli zake, sasa akawa anatoka, kutaka kutoka kabisa humo ndani, akaniona nipo nimesimama, nimeshikilia ufagio,..hapo hakushituka, akaniuliza..

‘Mimi nilijua umeshaondoka, sasa unasubiri nini, kama huna kazi ya kufanya, nenda nyumba ukalale..’akasema.

‘Nishakuambia kwa maagizo ya baba yako, natakiwa kuhakikisha kila kitu kipo sawa, ninafahamu ulipoingia kuna vitu umevuruga, kazi yangu ni kuhakikisha kila kitu kipo katika mpangilio wake, ili wageni wakija kusiwe na jambo la aibu...’nikasema

‘Ishia kule, nenda kaendelee na kazi zako huko,hapa sio sehemu ya watu, hii ni sehemu ya mitambo, huku hakuna mgeni anaweza kuingia ...’akasema na kutaka kuondoka.

‘Polisi je..?’ nikauliza hivyo, akashtuka, na kugeuka kuniangalia.

‘Polisi!!’ akasema kwa mshangao.

‘Hahaha, kumbe unawaogopa eeh, sasa ujue kuwa hao watu watakuja, kama sio leo, ni kesho….’nikasema

‘Kwanini, kuna nini kibaya…?’ akauliza

‘Naondoka, kaam hutaki nifanye usafi humu, nitamuambia baba yako umenizuia…’nikasema

Mimi nina akili za ajabu sana, ukinionyesha kitu, au nikaona unavyofanya, akili yangu hunasa haraka sana, nilishaona jisni anavyoweka neno lake la siri, nikalinasa bila ya hata ya yeye kujua.

Kwa muda ule nilijifanya mjinga kabisa nisiyefahamu kitu, hata baba yake anafahamu kuwa mambo ya mitambo, mitandao, komputa sijui kitu….kumbe !

Aliondoka hadi ofisini kwake, na huko nikamfuata nikitaka anifundishe…, nia ni kuhakikisha akili zao, zinajua mimi ni zezeta wa mitandao, na komputa, hakuogopa kunifundisha akijua kuwa mitambo ipo wazi, anaonekana kwa kila anachokifanya.

Alinifundisha kidogo jinsi ya kuwasha komputa, na kuzima, jinsi ya kufungua vitu kwenye komputa, ni vitu vya kawaida, baadae akasema niondoke kwani ana kazi zake anataka kufanya, kabla hajaondoka,…hata hivyo kwa jinsi ninavyomfahamu alionekana kama hayupo sawa.

Baadae akaondoka

Usiku wake, nilitaka niingie kwenye hiyo mitambo, kwani ndio siku peke yake ningeliweza kufanya jambo, nilichofanya ni kuchelewesha kununua mafuta ya genetaror, nilijua mara kwa mra umeme unakatika, na mimi ndiye niliyekuwa nahifadhi fedha za matumizi madogo madogo ya ofisi, na nilitakiwa kuhakikisha mafuta ya genetor yapo,

Nilijua ikifika saa tatu, mafuta yatakuwa yamekwisha, na siku hiyo umeme ulikuwa hakuna, huku nikiomba huyo mtoto wa huyo jamaa akaondoke na asirudi, au anachelewa, nilishangaa kweli siku hiyo kwani mpaka saa tatu alikuwa hajafika,....mara genetaror likazima, kukawa kizaa, zaa, giza, nilijua kwa jinsi ili mitambo ilivyo ikifika nusu saa itakuwa imezima, hapo nikajichelewesha kufuatilia, hadi nusu saa ikapita, ndio nikajitokeza

‘Mbona generator limezima, hujanunua mafuta..’akaniuliza Makabrasha

‘Naona nimepitiwa mambo yamekuwa mengi, ...nimemtuma mlinzi akanunue...’nikasema

‘Huo ni uzembe, unafahamu umuhimu wa umeme kwenye hili jengo, huoni watu wabaya wanaweza kutumia mwanya huu kufanya lolote...na kwanini hata ile mitambo ya akiba inayohifadhi umeme, umezima pia..ile inaweza kuhifadhi umeme wa masaa 24..’akasema.

‘Mimi nilishakuambia mambo ya mitambo, komputa, mimi sijui…kama hamukunielekeza jinsi ya kuwasha na kuzima nitajuaje..’nikasema

Hapo akachukua simu, akaongea na mtu wake ..

Mimi hapo nikaachana naye na kukimbilia kwenye hicho chumba. Kama nilivyojua, sehemu ile ya kuangalia matukio ya jengo ilikuwa imeshazima, kwa haraka nikakimbilia kwenye ile sehemu ilipowekwa laptop, ufungua wake nilikuwa nao tayari,…nikaichukua na kuifungua, nikawasaha, nilijaribu mara moja ile namba ya siri, ikakubali…

Nikatafuta sehemu hiyo inapohifadhia matukio..ile laptop ndio yenye kila kitu, ndio Server, …kwahiyo kwa kutumia yenyewe niliweza kuongoza mitambo yote humo ndani,…muhimu kwangu ni kufuta historia ya matukio ya nyume, yale ambayo nahis sio muhimu kubakia nayo.

Ilichukua muda kidogo kupata kumbukumbu ninazozitaka, ....nilikuta kumbukumbu nyingi za watu mbali mbali, ambazo kama zingeliwekwa hewani, nafikiri watu wengi wangeliumbuka, sikutaka kuangalia zaidi, kwani mambo niliyoyaona humo yanatisha,mimi nikazifutilia mbali, na kuhakikisha hazipo kwenye sehemu ya mabaki ya vitu vilivyofutwa, nikaangalia sehemu inayoangalia matukio ya jengo hadi umeme ulipozimika, nikazifuta.

Hapo nikapumua, sehemu ya kwanza ya mpango wangu ikakamilika.

Tuendelee…

WAZO LA LEO: Binadamu sio mtu au jiwe, ukasema utalichunga lisifanye kile usichotaka, kama kiumbe huyu aliyeumbwa na mola wake, hamtii yule aliyemuumba sembuse mamlaka…!!!
 
ITAENDELEA BAADAE

TUMEBAKIZA SEHEMU 10 KISA CHETU KIISHE, 🔥 🔥 🔥
 
SEHEMU YA 116


Kiukweli..ni kawaida ya wanadamu kukengeuka,…sheria ziliweka kwa ajili yake kwa masilahi yake, labda na mali zake,lakini wavunjaji sheria ni hao hao wanadamu..Na kiukweli wapo wanatajirika kwa hali hiyo ya kuvunja sheria, na wengine wanakuwa masikini kwa sababu hiyo hiyo ya uvunjwaji wa sheria… KIONGOZI ndiye anayebeba dhamana ya hili. Kumbe basi, kiongozi ni mtu muhimu kwetu, basi tusifanye makosa kumchagua kiongozi asiyefaa,…!!!



Kazi imeanza….

Nikaenda sehemu wanapohifadhia picha za video ambazo zilikuwa zinaonyesha mtu aliyefika kwenye hicho chumba karibu, nikajiona ni mimi peke yangu nikaifuta hiyo kumbukumbu, halafu nikatafuta sehemu ya kuzuia kamera za humo ndani zisichukue matukio hadi itakapokubaliwa tena ,nikaiweka OFF.

Ina maana kuanzia hapo hadi hapo mtu mwingine atakapokuja kuikubali kuonyesha matukio, kutakuwa hakuna kitu kitakachoonyeshwa, nilipoamaliza nikatoka kwa haraka, na wakati natoka tu, genetaror likaanza kunguruma na umeme ukarudi.

‘Oh huyo mtu kaniwahi, lakini bado…’nikasema kimoyo moyo

Nikatoka mle ndani kwa haraka nikawa natembea kuelekea ofisini kwangu, mara bosi huyu hapa…

‘Ulikuwa wapi wewe nakutafuta sehemu zote,..naona mitambo ya usalama humu ndani imezima, sio kawaida, hata umeme ukizimika inaweza kuhimili hata saa nzima, ..kuna tatizo,....’akasema Makabrasha huku akielekea kwenye chumba cha usalama, lakini baadaye akatoka huku akiongea peke yake.

‘Naona kuna tatizo kwenye mitambo ya usalama, ..siwezi kuingia kwenye komputa ya usalama, sijui huyu mtoto kafanya kitu gani,..kabadilisha neno la siri...kwanini anafanya hivyo bila kunipatia mimi taarifa, sasa tutafanye hapa..’akawa anaongea huku akinipita na mimi nikamwambia.

‘Mimi sijui, lakini tunaweza kujaribu pamoja huenda tukagundua jinsi gani ya kuingia, tukiwa wawili…’nikasema.

‘Hapana huko wewe huhusiki kabisa, ni mimi na yeye tu…’akasema

‘Kama yeye hayupo na hali kama hii imetokea itakuwaje…?’ nikamuuliza

‘Subiri wewe,…haya hayakuhus, ngoja nimpigie simu huyu mwanangu, japokuwa leo tumekorofishana, lakini hili ni muhimu, ni lazima afike, kwa hraka…’akasema sasa akishika simu kumpigia mwanae nikaona nimpoteze mawazo kwanza…

‘Mbona alishafika hapa…’nikasema
Ina maana kumbe alikuja kuzima na kubadili …kwanini lakini huyu mtu ni muhuni sana, ana nini leo..’akasema kwa hasira.

‘Nahisi kuna kitu, alitaka kufanya, labda anataka kurekebisha, nilisikia akisema kuna matatizo kwenye mitandao..ooh, unajua mimi sijui mambo zenu…’nikasema

‘Alitakiwa aniambia mimi, yeye ni mwanangu tu, haya mambo humu ni yangu sio yake, naona anataka kunipanda kichwa, …ni lazima niongee naye, au ni kweli labda kuna kaliona, ikabidi afanye hivyo, alitakiwa aniambie au sio…’akasema kama ananiuliza

‘Kapatiwa,…subiria si atakuja….’nikasema

‘Unajua leo sijisikii vyema, sipo hivi kabla, mwili wangu una afya tele, lakini leo, ooh, nahisi natakiwa baadae nioane na dakitari…halafu nahisi ....kama kuna tatizo kama kuna kitu kibaya kinata kutokea,.tokea jana hali haipo sawa..’akasema

‘Unaumwa, inabidi umuone dakitari, wewe si unaweza kumuita mmojawapo akaja kuutibia hapa nyumbani….’nikasema

‘Hapana mimi siumwi,…unajua jana nilikorofishana sana na huyu kijana wangu, namuona kabadilika ghafla,..mama yake anamfunza vibaya, sio yule mwanangu wa zamani ambaye alikuwa akinitii kila kitu…’akasema

‘Kwani mama yake karudi..?’ nikauliza

‘Ndio,…huyu kila mara akiwepo inakwua hivi..nilishamuambia kijana wangu asimsikilize mama yake…kwani mama yake hana nafasi kwangu, ilitokea bahato mbaya tu nikazaa naye, sina ….mahusiano naye kabisa…’akasema

‘Lakini si umezaa naye, huo ni uhusiano pia….wewe ulipozaa naye ulitegemea nini..?’ nikamuuliza

‘Wewe hujui tu…na…unajua akili yangu haipo sawa, nahisi kuna kitu ambacho sio cha kawaida humu ndani, huwa mimi ninakuwa na hisia kabla ya tukio…na hili limeanza pale tu nilipokorofishana na huyu kijana..maana aliondoka kwa hasira, ndio maana hajafika mpaka muda huu..’akasema

‘Mbona alifika halafu akaondoka, kwani mlikorofishana nini tena na mtoto wako kipenzi?’ nikamuuliza

‘Unafahamu hawa vijana wana tamaa sana, wao wakiona kitu kipo, hawajiulizi kimefika fikaje hadi hatua hiyo, hawafahamu kuwa sisi wazazi wao tumetumia miaka mingapi hadi kulifanikisha hilo, hawajui jinsi gani tulivyojijenga..unaona …’akasema.

‘Mimi hapo sikuelewi, nijuavyo mimi, wewe na huyo kijana wako mumekuwa naye bega kwa bega kwenye maendeleo yako, na kama yeye anataka jambo, basi ana haki, na nimegundua kuwa yeye ni mshauri wako muhimu sana..’nikamwambia.

‘Pamoja na hayo, kuna mambo mengi kayakuta, na sio kwamba tumeshirikiana naye, hilo ndio anakosea, yeye, mengi kayakuta, …na kwa vile nilimuona ni mtu anayefanana na mimi, ndio nikawa na mshirikisha, lakini sio kwamba, yeye ni sawa na mbia wangu, hapana…’akasema

‘Kwani tatizo lipo wapi…?’ nikauliza

‘Unajue yeye anataka mengi kwa muda mrefu, ana tamaa zaidi yangu..’akasema akiwa kasimama karibu yangu.

‘Kwani yeye anataka nini?’ nikamuuliza na akataka kuondoka, lakini akageuka na kuniangalia machine akasema;

‘Huyu kijana analalamika, ni kwanini nimeamua kubadili mirathi, kwanini sasa hiv nimeamua kumweka mwanangu huyu mkubwa kuwa mrithi wangu wa kwanza, nay eye sasa nimemfanya kama mtu wa pili..anadai yeye ndio ana haki ya kuwa mrithi wangu kama nilivyofanya awali..

‘Mimi sielewi, …’nikasema.

‘Unajua yeye hafahamu mawazo ya kikubwa, mimi nimtu mzima natizama mbele zaidi yake,nimefanya hayo baada ya kufikiria sana, hali imebailika, maisha yamebadilika sasa hivi mimi sio yule mtu wa jana…’akasema

‘Umetajirika au sio…?’ nikauliza

‘Ni kweli hilo siwezi kukuficha, ndio maana nimeona huyo mtoto wangu mkubwa ndiye anayeweza kuja kuendeleza kila kitu nikiwa sipo..na sio kwa vile naandika hayo ndio najitabiria kifo…mbona hayo yalikwepo toka awali, kama wakili hayo ni muhimu yawepo kwenye familia yangu…’akasema

‘Unahisi ni kwanini anaona yeye ndiye anastahiki kuwa mrithiw ako zaidi ya huyo mtoto wako mwingine aliyemkubwa…?’ nikamuuliza
Ni tamaa tu,..na mwanagu huyu hakuwa hivyo, nahis kuna kitu mama yake kambadili,..hajui kwanini mimi nimefanya hivyo…haya kaona, sasa anakuja juu, ni kwanin nimefanya hivyo, yeye hana haki ya kuingilia maisha yangu..’akasema

‘Leo hii unasema hivyo, mimi nakumbuka ulikuwa ukitamba kuwa huyo mtoto wako ni kila kitu au sio…?’ nikauliza.

‘Nimeona mbali,..unajua japo huyo kijana yupo mbali, lakini mimi nafuatilia maendeleo yake kwa karibu, ….anajitahidi sana, kielimu, na…anafaa kuwa kiongozi wa hii wa familia..na ukumbuke huyo ndiye mtoto wangu wa ndani ya ndoa, unaona eeh, ...’akasema

‘Lakini kihalali, …hata ingelikuwa mimi ningedai hivyo hivyo, kwasababu huyo kaka yao yupo nje, hajui chochote kinachoendelea hapa, na nakumbuka uliwahi kuniambia huyo mtoto wako wa huko Ulaya hampatani kabisa, hakujali…, na aliondoka na kukuambia hana haja na mali yako ..sasa kwanini unajipendekeza kwake....?’ nikamuuliza

‘Wewe hujui mambo ya wazazi na watoto, hata kama mtoto hampatani kwasababu kadhaa, lakini yeye atabakia kuwa mtoto wangu wa kwanza, na yeye nilimzaa na mke wangu wa ndoa, ana haki zote itakuwa sio halali kumfanyia hivyo, niliandika awali ile mirathi kwa hasira tu. …’akasema

‘Na huyu je…mbona ndiye anakutumikia kwa kila hali…?’ nikamuuliza

‘Huyu niliye naye hapa nimemzaa kwenye nyumba ndogo,..nilimsomesha na kumuandikisha kama watoto wangu wengine, na nimeona anastahili kuwa karibu na mimi, na ndio maana nimemuweka nafasi ya pili, atakuwa chini ya huyo kaka yao anayeishi huko Ulaya, kuna tatizo gani hapo....’akasema.

‘Kwahiyo wewe na mtoto wako mkaishia wapi?’nikamuuliza

‘Yeye alikuja na mipango yake, uone jinsi mtoto huyu alivyo balaa, kakaa sijui na mama yake, wakapanga mambo mengi tu, jinsi ya kugawanya mali eti keshaandaa na mikataba ya kifamilia, kama vile mimi ninakufa karibuni, kwenye mikatba hiyo, ambayo ni kama urithi, , ...na yeye awe ni mrithi wangu , yaani kiongozi wa familia,..’akasema kwa hasira

‘Wanataka mimi nife au sio..si ndio maana yake hawa watu hawana akili kabisa…, nimemwambia huo uchuro siutaki, kama ni mikataba ya urithi, mimi nimeshaupanga na ninafahamu ni nani awe kiongozi wa familia, kama mimi nikifa..lakini sijafa, na sitaraji kufa leo...siumwi,, sina tatizo la kiafya..kwanini anakuja na mipango hiyo, wana matatizo sana hawa watu....’akasema akijiangalia.

‘Lakini kufa sio lazima uumwe, wewe kama ulivyo, kutokana na mambo yako unayoyafanya,una maadui kila kona, wakija kuku-ua watu, hata hivyo kuandika mirathi, sio lazima mtu afe, ni katika kuwekana sawa kimajukumu au sio..vyovyote iwavyo ni muhimu kila mwanafamilia afahamu nafasi yake au sio....’nikasema

‘Kweli hilo ni la kuangalia sana,..nahisi maadui wananitafuta… ndio maana umeme ulipozimika, nimeshituka sana, sitaki uzembe huu utokee tena, ...unanisikia, ....sasa nisikilize kwa makini, kesho huyu mpenzi wako anakuja, nilishakumbia hilo, au umesahau au uliona naongea tu, tafadhali kwenye kazi iwe ni kazi tu ...’akasema

‘Mpenzi wangu gani, mimi ni mke wa mtu.?’ Nikamuuliza

‘Hebu acha utoto, nikisema mpenzi unanielewa ni nani, ..nimeshamweka sawa anakuja kuweka sahihi yake kwenye hiyo mikataba ambayo itanifanya mimi, niwe na haki ya kumiliki kila kitu…’akasema

‘Mhh..’nikaguna tu.

‘Nilishawaelezea hilo..sio nafanya hivyo kwa kupenda,..amelipa mdeni yangu kupitia kwenye hisa zake..ni halali kabisa,…kwahiyo wewe na wenzako mlitambue hilo, ...na tatizo ni huyu mtoto wangu anakuja na sera zake za ajabu ajabu, anataka na yeye awe na hisa,...anataka kunikorofisha, haya mambo hayajakaa sawa, keshaanza kugombea mali, ni uchuro huu…I don’t like this...’akasema kwa hasira

‘Mimi ninawashangaa kweli kweli, yaani mumeshaanza kugombea mali za watu, hata kabla hamjazipata, mumeshaanza kumiliki hata kabla humajamilikishwa, kweli akili zenu wote ni za kishetani wewe na mtoto wako, na mimi nahisi hamtafanikiwa kwa hilo, na mkifanikiwa mtakuja kupigana baba na mtoto wake, hiyo ni hatari....’nikasema

‘Kama mimi nipo hai, hakuna cha mtoto wala mama yao atakayeweza kunitawala, mimi, unasikia…mimi ndiye mwenye amri ya mwisho.., wote wanalifahamu hilo, najua kabisa huyo mtoto anaendeshwa na mama yake, na mama yake nilishamwambia simtambui tena, tulishamalizana mimi na yeye…’akasema

‘Kazi unayo, mali ya dhuluma kamwe haiwi na amani, nakuambia ukweli..’nikasema

‘Sikiliza,..usitake kunifanya mimi ni mdhalimu, nimemdhulumu nani hapa, umeona mwenyewe sera zangu, na nimejaribu kukuelimisha dhamira yangu, umeona jinsi gani ninavyoitumikia jamii…na hili la mpenzi wako, ni lazima lifanyike, ili na mimi niweze kuendelea kuwa juu…wakubwa huko wananisakama…’akasema

‘Wakubwa gani..?’ nikauliza

‘Sitaki niyaongee haya mara kwa mara, wewe unafahamu ni nani nawaongelea, sasa …huyo mtoto natakiwa nimuweke sawa, aacha upuzi wa kumsikiliza mama yake, mama yake hana nafasi kwangu, na zaidi mimi na mama yake...hatukuwahi kufunga ndoa naye…yeye alikuwa mpenzi wangu wa kupita tu, nikampa mimba ndio akapatikana huyo kichaa.’akasema kwa hasira.

‘Aaah, kumbe, una wangi sana, kazi yako ni kuzalisha tu, huyo alikuwa mpenzi wako wa zamani, nahisi wapo wengi wa namna hiyo, huyo wakati huo ulimuona mpenzi, sasa hafai, au ni kwa vile kazeeka,au?’nikamuuliza

‘Namfahamu sana huyo mwanamke, ana tamaa sana, hatuivani kabisa, na mtoto wake kachukua tabia zake zote, na kama ataendelea na hiyo tabia sizani kama tutaivana, na...namuona atakuwa kikwazo katika mipangilio yangu ya kimaisha kinyume na nilivyotarajia, kabadilika kabisa, hajui mipangilio yangu mingine..ni lazima niwe makini sana...’ akatikisa kichwa kusikitika halafu akaendelea kusema;

‘Sawa mimi nakushauri hivi, kwa hali ilivyo ni bora make muongee mkubaliane au sio, yeye ndio kama mlinzi wako au sio…yupo nawe wakati wote,..’nikasema

‘Ni kweli unayoyaongea,..mimi najiuliza tu ni kwanini siku hizi hanisikilizi mimi, na anakuwa akimsikiliza sana mama yake, ujue huyu mtoto mimi ndiye nimefundisha ujanja wa kimaisha , alipomaliza kisomo chake akataka kufanya kama alivyosoma, nikamwambia dunia hii, ina utaratibu, lakini ndani ya hizo taratibu kuna njia za mikato,..unaona eeh..’akasema

‘Kumbe ni wewe ulimuharibu…’nikasema

‘Sio kumuharibu,..hivi niambie kiukweli kwenye hali za maisha yetu kuna mtu anaweza kuinuka akawa tajir bila kufanya magendo,…sasa ni lazima nimfundish, ujanja wa dunia hii…ukijifanya unasubiria mshahara tu, utakufa masikini..ndio hivyo nikamuelekeza jinsi gani ya kuishi, kaiva sasa ananigeuka…’akasema

‘Ndio maana nawaambia dhuluma itawaandama hadi kaburini…’nikasema

‘Mhh..na wewe bwana, mbona hunielewi,…kwa namna nyingine upo sahihi, kuwa kuna kitu kama hicho, lakini tufanyeje sasa, wakati wakubwa wameamua kujitajirisha wao wenyewe, angalia hizi foleni za magari, makodi mengi yasiyomjali mtu wa chini, ..utafanaje kazi namna hii, angalia tatizo la umeme, kweli unaweza kuwekeza hivi, wao wakitaka kupita njia zinasafishwa, kwao umeme haukatiki…utafanyeje…’akasema

‘Ni hayo tu…?’ nikauliza

‘Natolea mfano kidogo kuwa ili ufanikiwe katika nchi yetu, huna budi kupita njia za mkato, ukitaka njia sahihi utaumia, kuna watu wanakuwa ni vikwanzo..hebu anza kufuatilia hati za kiwanja uone…au ..mifano ipo mingi… utasubirishwa wee..kumbe ni namna tu inatakiwa, bado sana….kwahiyo ilibid nimfundishe kijana aelimike…’akasema

Na sio hilo kazi..siku hizi watu binafsi, ukifanya kwao, eeh,…ujue utanyonywa kupitiliza, usipo kuwa mjanja utaishia kuwa masikini…umeonaeeh,…haki nyingi za mfanyakazi wanazikwepa, chunguza sana hili utaliona, sasa mimi kama Makabrsha nataka hawa watu niwakomoe kihivyo, nyie hamjui tu…’akasema

‘Hutafanikiwa, …maana unatumia njia hiyo kujitajirisha huku ukitafuta visingizio, hujui kiasi gani unawaumiza watu,….maana unatutumia sisi watu wa chini kwa ajili ya visasi vyako kwa watu wa juu…’nikasema

‘Naona wewe hutanielewa, ni kwanini lakini…nilitaka wewe unielewe ili umsaidia huyu kijana, umuelemishe ili tufanye kazi pamoja, wewe uwe mtu wangu wa karibu pia..’akasema.

‘Tatizo wote wawili hamuaminiki, mtoto kama baba yake...au kama wanavyosema mtoto wa nyoka ni nyoka..’nikasema kwa dharau huku nikijifanya kutabasamu .

‘Huyo haniwezi kabisa na hataweza kunifikia mimi, yeye anachukulia mambo kwa pupa, mimi natumia ujanja, hekima na akili, ndio maana unaona nimefanikiwa kwa kiasi hiki kikubwa, unaona jumba hili, ni nani anaweza kujua nimelijenga mimi kwa vipi,..ni akili, ..usione watu wana majumba, utajiri, ukfikiria ni kirahisi hivyo…’akasema sasa akiangalia juu.

‘Dhuluma tu hiyo..’nikasema

‘Sio dhuluma jamani, nielewe…, ni kutumia akili, na ujanja, lakini dhumuni kubwa ni kuwasaidia wanyonge, humu nimewekeza, angalia ajira kiasi gani nimezifufua hapa, unakula, na huku unasaidia, siwezi kusahau dhumuni langu, hapa nina mpango wa kuwajengea wazee sehemu yao,…ambapo wataweza kuwekeza, kila mtu na ujuzi wake, ngoja haya mambo yawe safi, wewe utaona tu..’akasema.

‘Kwahiyo yote hayo umemfundisha mtoto wako?’ nikamuuliza

‘Tatizo yeye hataki kutuliza kichwa, yeye anataka mambo kwa pupa, ana tamaa za haraka, hata sijui kwanini ameweza kufaulu masomo yake ya uanasheria, kazi hii hataiweza kama atakuwa na tabia ya namna hiyo, ya pupa, na ninavyomuona hatafika mbali..’akasema

‘Mhh..haya bwana..’nikasema

‘Sio nataka wewe unielewe, ili mkikaa kuongea umuelimishe…, hebu angalia, anataka kunirithi nikiwa hai...sijui kwa hali kama hiyo, tunaweza kukaa pamoja,....lakini mimi kama baba, nitamdhibiti tu, nimeshamfahamu vyema anakotaka kwenda, sasa ataona vipi baba livyo mjanja, haniwezi kabisa...’akasema.

Na mara simu yake ikalia, akaipokea bila kuiangalia, na mara akakunja sura ya uso wake na kuonekana kukasirika, akasema kwa sauti ya juu ya hasira;

‘Kwanini unasema hutafika leo, wakati unafahamu umuhimu wa wewe kuwepo leo, nataka uje hapa haraka,...kwanza kuna matatizo kwenye mitambo ya usalama, na pia ni wajibu wako kuwepo hapa, ili tukamilishe kazi , achana na tamaa zako hizo, nasema mimi kama baba yako uje hapa haraka,.....’akasema

‘Unasema nini, unanijibu mimi hivyo, kuwa hutafika,mpaka nikubaliane na matakwa yako, ina maana unanilazimisha kufanya unavyotaka wewe, hivi unaelewa unaongea na nani...unasema nini, ina maana umeshaota mapembe sasa eeh,...’akawa anaongea huku mwenzako naye anaongea, maana sauti ya huko nilikuwa naisikia, wakazozana hapo mwishowe akasema;

‘Sikiliza wewe mtoto, kama nimekuzaa mimi, utakuja hapa, kama una baba yako mwingine usije , usijione kuwa umekuwa sasa,...na kujiona hunihitaji tena, hujui ninaweza kukufanya lolote ukasahaulika katika hii dunia..’akasema na kusikiliza simu kwa muda halafu akaibamiza simu chini , na simu hiyo ikapasuka vipande vipande, na kusema;

‘Mwanaharamu mkubwa wewe...tutaona,....’akageuka na kuelekea ofisini kwake, ukumbuke hapo tulikuwa tunaongea kwenye varanda, nilipokutana naye wakati natoka huko kufanya mambo yangu,..hapo mimi nikachekelea kimoyo moyo, nikisema ‘mipango inakwenda sawia…’ ukitaka kumshinda adui , wagawanye, wasiwe na masikilizano..utwashinda kirahis sana..mimi huyoi nikurudi chumbani kwangu, sikutaka kumfuata huko ofisini kwake, kwani nilijua kwa hali aliyonayo hatutaweza kusikilizana.

Mimi kwa hali kama hiyo , ilikuwa kama vita vya kunguru, faraja kwangu, nilitaka watu hawa wawili wawe hivyo, ili mipango yangu iweze kufanikiwa,..na kimoyomoyo nikijua sasa sehemu muhimu imekamilika…

Mpaka hapo nilijipa moyo hivyo, hata hivyo, sikuwa nimeamini kabisa kuwa huyo mtoto wa marehemu hatafika, namfahamu sana, yeye na baba yake hawaeleweki, wao ni waarabu wa pemba, wanajua sana, utaona wamegombana hivyo baadae kidogo wapo pamoja wanajadili mambo yao,…kwahiyo nikachukua tahadhari,..

Nilikwenda kuongea na mlinzi mmoja ninayemuamini , nikamwambia , kama huyo mtoto wa bosi akija , anipigie simu kwa haraka,...kwani sehemu kubwa ya mitambo ya kunasa matukio ilikuwa haichukui picha, kwahiyo ningeliweza kufanya lolote bila kujulikana, kwa kiasi fulani nilikuwa na amani kidogo, nikasuburia muda muafaka, wa kumalizia kazi ambayo nilishaianza.

Nilikuwa najiamini maana sasa nina silaha, na nikiwa tayari , au nikisikia kuwa huyo jamaa kafika nitakwenda kuichukua, sikuwa na haraka nayo sana, nikatembea kuelekea ofisi ya siri ya Makabrasha, nikafungua, na kulitafuta kabati maalumu anapoweka nyaraka zake, nikachukua kile ninachokihitajia, na kurudi chumbani kwangu.

Kabla sijafika huko nikakumbuka kazi nyingine ya kufanya, kwani siku hiyo niliipanga iwe siku ya mwisho ya kukaa kwenye hilo jengo, nikaelekea sehemu ninapoweka vitu vyangu muhimu ambavyo nimevihifadhi mbali na chumba changu, sikutaka waje wavikute chumbani kwangu, kama ikitokea kuvitafuta, nikaviweka sawa, halafu nikarudi chumbani kwangu,sasa nikijiandaa kwenda kuichukua silaha yangu, sikutaka iwe mbali na mimi na wakati nafika chumbani kwangu, simu yangu ikaita, alikuwa mtoto wa Makabrasha,

‘Unasemaje?’ nikamuuliza kwa sauti isiyotaka kuongea,

‘Samahani sitaweza kufika kwenye shule niliyokuahidi, lakini ombi langu lipo palepale,na kwanini mitambo hapo haifanyi kazi, ...umeingia tena humo ndani?’akasema na kuniuliza

‘Umesema hutakuja, ina maana mkataba huo umekufa, labda useme kuna jingine..na kuhusu swala la mitambo hayo unayafahamu wewe, wewe ndio mtaalamu, huenda ulifanya hivyo makusdi kumuonyesha baba yako kuwa wewe ni zaidi au sio..?’nikasema kama namuuliza

‘Wewe nimeshakufahamu, wewe unajifanya ni mjanja, lakini ujue kuna wajanja zaidi yako, kuna kazi naifanya ikimalizika nitaangalia, kama nitakuja au la, ..lakini kwa vile hatujaafikiana na mzee ninaweza nisifike, na kama nikifika, nitahitaji maelezo ya kina kwanini umezima mitambo, na kwasasa siwezi kuona chochote kinachoendelea hapo, utakuwa ni wewe tu...na hilo litakufanya utimize ombi langu, la sivyo, mimi nitakuumbua kwa mzee ...’akasema

‘Una uhakika gani na hilo..na je nikimuambia mzee wewe unanitongoza,..nia ushahid hujui kila nikiongea na wewe nakureodi kwenye simu…hahaha, mimi ni mjanja kama wewe…au nimuambie?’ nikamuuliza

‘Utaona....mimi huwa sichezewi, mimi ni mtaalamu, nafahamu sana hiyo mitambo, na kawaida yangu, nikitaka jambo ni lazima nilipate, muulize baba atakuambia, ndio maana nipo naye karibu, ananifahamu sana,…’akasema

‘Mbona sasa kampa urithi kaka yako, ina maana wewe hufai, huna akili iliyotulia, sema wewe una tamaa, utawazaje mambo ya urithi wakati baba yako yupop hai, mna mipango gani wewe na mama yako…’nikasema

‘Nini..nimekuambia nini wewe…’akasema kwa hasira

Nakuulize wewe, maana baba yako kakasirika, sijawahi kumuona akiwa na hasira kiasi hiki, nisikilize mimi, pamoja na yote mzazi ni mzazi kumbuka ulipotoka..’nikasema kama kuuma na kupuliza.

‘Wewe hutujui…na kwa hili ni lazima nipiganie haki zangu, mfano tu, je mzee kama hayupo, unafikiri huyo kaka yangu atanijali,..yeye na mimi hatuivani kabisa,… je huyo kaka yangu anafahamu wapi tulipotokea, ni kwanini tumefika hapa tulipo, sema ukweli wako,..’akasema na kukatiza nahisi alikuwa akiongea namtumwingine.

‘Sasa…eeh ukiangalia hiyo mikataba aliyotayarisha baba, yeye kanisahau mimi nimejaribu kumtayarishia mikataba mizuri tu, nikimkumbushia wapi tulipotoka, yeye anakimbilia kumuingiza mama kwenye mazungumzo yetu.., eti mama ndiye ananiharibu…’akatulia kuna sauti ilikuwa kama inamsumbua.

‘Unajua nikuambie kitu , mama yangu masikini ana nini na yeye, alimpachika mimba yangu eeh, akamtelekeza, mama kaishi maisha magumu hadi anajifungua mimi…siwezi kusikia vizuri mtu akimuongelea vibaya, huyu ni mama yangu na mama yangu ni kila kitu kwangu,…sitajali ni nani, kama mtu anataka kuwa asui yangu amuongelee mama yangu vibaya,..sipendi…najua yeye ni baba yangu namuheshimu kwa hilo, lakini pia awe akinisikiliza na mimi,..’akasema lakini akawa kama anakatiza.

‘Ni nani huyo mpo naye, ni Malaya zako nini…?’ nikauliza

‘Hahaha…acha hayo, sio kweli…’akasema, na nikasikia akiongea na mtu, baadae akasema;

‘Sory, nipo na mtu karibu, ….sio kama unavyofikiria wewe…’akasema

‘Hahaha..mtoto kama baba, umalaya, na sasa mnagombea mali ya dhuluma eeh, nina uhakika kuwa dhuluma hiyo itawapeleka pabaya...na mwisho wake umeshafika, ..wewe njoo nakusubiri kwa hamu..’nikasema

‘Nini…!!1,…ina maana kweli unanitaka eeh, unasikia sikutaka kuja huko, lakini kama kweli utanitimizia ombi langu, mimi naweza kuja kwa ajili yako tu, sio kwa…na sikiliza kama unataka nije kwa ajili ya kupambana na wewe..hilo mimi hunitishi, sikiliza nina uhakika ni wewe umezima hiyo mitambo, sasa..ngoja tuone,….’akasema tamaa zake za mwili akazitanguliza mbele, na alipogundua kuwa mimi nina maana gani ndio akasema hivyo.

‘Ni hivi baba yako ameshakushitukia, kuwa wewe unanitaka na mimi, pili wewe una tamaa, na tatu, hufai kwenye uongozi wa familia, kwahiyo kuanzia sasa ujue wewe huna chako ....’nikasema

‘Nini,..haa, unasema nini, tutaona…’ akasema sasa kwa hasira, nikasikia sauti ya kike ikisema;

‘Kuwa makini…’

‘Ndio hivyo…sasa uje usije, huna maana kwake kwa sasa…’nikasema na mara nikasikia akikata simu kwa hasira huku akisonya.

NB: Je huyo jamaa alifika? na kama alifika kulitokea nini na je ombi lake lilitimizwa,ni nini kitatokea kwa Makarasha, tuonane kwenye sehemu ijayo ya shahdii huyu muhimu aliyekuwa karibu na Makabrsha..ambaye ni marehemu!


WAZO LA LEO:Tuwe makini na malezi ya watoto wetu, kama tunafanya shughuli zisizo na manufaa kwa watoto wetu kwa maisha yao ya badaye, ni bora tusiwahusishe. Tuwajengee watoto wetu misingi mema ya maisha yao ya baadaye, tukikwepa makosa tuliyoyafanya, ili wao waweze kuishi maisha bora, na kujenga kizazi bora cha baadaye.
 
SEHEMU YA 117



Binadamu tulivyo, hata ujitahidi vipi, hata uwe mjanja wa kuvumilia usingizi, kuna muda utafika, hasa usiku, ni lazima usingizi utakutinga,..inafika sehemu unashindwa kabisa kuvumilia na ndivyo ilivyotokea kwangu, lakini ni zaidi ya hapo, hadi leo sijaweza kutambua ni kwanini nilishikwa na usingizi mnzito kiasi kile...’ Shahidi akaendelea kuongea.

‘Japokuwa nilitaka usiku huo nikeshe, ili kuhakikisha mambo yangu yote yamekamilika, kama nilivyopanga...si nimeshazima mitambi ya kuonyesha matukio,..sasa kwanini nishindwe,...kikwazo ilikuwa ufunguo wa chumba cha Makabrasha...

Sasa cha ajabu,...usingizi mnzito ukanipitia,

Unajua ilikuwaje, inabidi niwaambia kila kitu kwenye sehemu , maana ni muhimu sana..

Baada ya kumaliza shughuli za usafi, kupanga mambo kama alivyonielekeza Makabrasha,..na kuweka vitu vyote kama alivyotaka yeye, maana alitakiwa kukutana na wageni wengi, na miongoni mwao ni mume wa familia, na kila mtu alikuwa na muda wake maalumu...kiukweli nilifanya kazi nyingi usiku huo, bila kupumzika, na sikuwa na msaidizi, hakutaka msaidizi...nikajikuta nimechoka sana.

Niliongea kidogo na Makabrasha kuhakikisha kuwa kila kitu chake kipo sawa, na akaniambia hatanihitajia tena kwa usiku huo, na yeye akatoka kwenda chini kwenye sehemu ya hoteli kujiburudisha na watu wake.

Mimi sio mtu wa kujiruisha , kunywa kunywa, hapana, mimi naijali kazi yangu, na hata hivyo, siku hiyo kwangu ilikuwa muhimu sana, nilikuwa na mpango kabambe, lazima ukamilike.

Baada ya hapo ndio nikaingia chumbani kwangu kubadili nguo...sasa kabla ya kufanya hivyo, nikaamua nijilaze kidogo kitandani kupumzisha mwili...na hapo akili yangu inawaza mpango huo wa usiku..., nikiwa kwenye hayo hayo mawazo, nikiwa nimejiegemeza tu,... kidogo kwenye mto, nikiwa nimeweka mikono yangu nyumba na kichwa changu kulalia viganja vya mikono, hapo hapo usingizi ukanipitia.


Kiukweli, sio kawaida yangu kulala hivyo nikiwa vitani..maana kutokana na mpango wangu huo, hiyo ilikuwa ni vita kufa kupona...…hata sielewi ilikuwaje, ila ninachoweza kusema ni kuwa nilishikwa na usingizi mnzito, ulionifanya nisifanye kazi yangu….

Nilishituka ni asubuhi, na kilichoniamusha ni simu yangu , iliyokuwa ikilia, nilikuwa nimeweka mlio wa kutikisika tu, ...bila kuangalia mpigaji , nikaipokea hiyo simu kwa haraka,

Nikasikia sauti ya mdogo wa mume wa familia..hapo hapo nikakurupuka na kukaa vyema kitandani...kwa haraka nikamuuliza kuna nini, na hapo nikasikia mlilio ya ndege nje, purukushani za nje, kelele za magari, kuna nini tena hapo, ni asubuhi

'Mbona asubuhi hivi kuna nini...?' nikajikuta nime muuliza hivyo,

Ndio akaniambia yupo karibu na eneo la hilo jengo alimleta kaka yake.

‘Oh, kumbe kumekucha...kwahiyo, mpo na kaka yako? ’nikamuuliza huku nikipiga miayo.

‘Hapana, yeye keshaingia huko, mimi nipo mbali kidogo na hapo, ina maana wewe bado umelala…?’ akauliza kwa mshangao, sasa kwa haraka, na aibu ndio nikasimama,kiukweli huu ni uzembe kama ningekuwa vitani, sijui ingekuwaje.

'Hapana mbona nipo macho,...nimechoka tu...'nikamwambia hivyo

‘Sawa mimi nimemlata mara moja na sitakiwi kuonekana eneo hili, vipi mambo yaliendaje..?’ akauliza

‘Mambo gani...eeh, sawa, hamna shida, yalikuwa safi, ngoja tuone itakuwaje…’nikasema

‘Kwahiyo nije kuichukua saa ngapi…?’ akauliza

‘Nitakuambia..usijali…’nikasema, sikuwa na mashaka hata angeliongea sana kwani kule kwenye mitambo nilikuwa nimeweka OFF, na kwa vile kumepambazuka natakiwa kwenda kuweka ON...

Kwa haraka nikainua godoro, pale nilipoficha silaha yangu, nikaiona ipo, nikarudishia godoro kwa haraka, kwani nilihisi kuna mtu anakuja kwa nje, nilisikia mlio wa nyayo za mtu, nikajiweka sawa, nilijua nitakuwa nahitajika kuweka mambo sawa, kwa ajili ya wageni, ...

Hata hivyo hakutokea mtu, nikafungua mlango kuchungulia kwenye korido, sikumuona mtu, lakini nina uhakika kulikuwa na mtu anakuja muelekeo wa chumba changu. Ni nani huyo kaingia kwenye chumba gani cha karibu, …nikapotezea tu, ila moyo wangu ukawa na mashaka.

Nikarudishia mlango na kutulia kidogo, nikamigia mdogo wa wa mume wa familia, nikamuuliza kama kaka yake ameshaingia ndani, nikaona haina haja ya kukaa na hiyo silaha tena , maana kazi yake ilikuwa ni usiku, kwahiyo nikaona nimrejeshee, yeye akasema;

‘Kwa hali ilivyo hapa nje, huwezi kunipa hiyo silaha, je usiku wa leo hutaihitajia…?’ akaniuliza?’ akaniuliza.

‘Kazi muhimu nimeshaimaliza, ila kuna kitu nataka kukufanya, kama itawezekana, lakini sio muhimu kwa sasa nilishaongea na kaka yako, kama akiwa mjinga na kusaini huo mkataba atakuwa kaharibu kila kitu, yote inategemea yeye, vinginevyo, kwa vile ni mchana siweze kufanya lolote na hiyo silaha, kwahiyo sio muhimu kwa mchana wa leo, lakini kama unaona hakuna usalama huko nje, basi ngoja ikae kae huku, huenda nikaihitajia...’nikamwambia.

‘Sawa hamna shida, kama alisema atafanya kama mlivyokubaliana, sijui mume kubaliana nini na kaka, ila yeye aliniambia kila asubuhi nije kuichukua, sasa ni bora muwasiliane naye,...’akasema na mimi nikamwambia.

‘Tutaongea baadaye, je unamuonaje kaka yako, yupo safi, anaweza kufanya niliyomuagiza afanye au bado kalewa na madawa ..mimi sijui hizo dawa kwanini wanampatia, anakuwa kama zezeta...?’ nikamuuliza, akasema;

‘Yupo safi, sikuona tatizo lolote kwake...nahisi hawakumpatia hizo dawa, kwasababu wanampa pale anapokuwa kachanganyikiwa, ili kumfanya alale, au sio, na sasa hivi huwezi kufahamu kuwa ndio yeye, nahis ni kutokana na mambo yenu, ..mimi sijui…’akasema na mimi nikakata simu…nikaenda zangu kuoga na kujiweka sawa, kiofisi zaidi, nilimpigia simu mume wangu, kumtakia hali…ili niwe nauhakika kama bado ana msiamo wake wa kuja huko kijijini;

‘Mume wangu haujambo, samahani sikuweza kukupigia simu usiku nilichoka sana, na simu inakuwa haina chaji, ila naendelea vyema, usiwe na wasiwasi..’nikasema kazi...’nikamwambia.

‘Una uhakika,…ina maana huwezi hata kuazima kwa mtu ukanitakia hali, mimi nataka kuja huko kukuchukua, ili ukakutane na docta mmoja mwenzangu....’akasema.

‘Kwanini, nilishakuambia sina tatizo la docta, ni matatizo yangu, ..na nina imani hivi sasa nitayamaliza, nitakwua, sawa..hata simu naona imeisha chaji ...’nikamwambia.

‘Sawa, uonavyo,..ila ni lazima nije huko...’akasema na tukamalizana hivyo

Kiukweli mume wangu alinijali sana, alinionyesha mapenzi yote tena ya dhati lakini sijui niwaelezeje, akili na mwili wangu wote ulikuwa kwa…ndio hivyo, asiyekuthamini hawezi kukuelewa...’akasema na kumwangalia mume wa familia ambaye alikuwa kainamisha kichwa chini kwa hivi sasa, lakini kaka kwenye kiti upande akimgeukia muongeaji.

‘Hata hivyo, kama isingelikuwa Makabrasha, na huyo mpenzi wangu wa asili kuja kuniharibia mipango yangu, mimi ilishafikia hatua, nikaamua kuwa huyu ndiye mume wangu nitajitahidi kumpenda hadi siku ya mwisho, lakini ghafla ndio akaja mume wa familia na matatizo yake, ikabidi niwe mtu wa kumliwaza, kumuhangaikia, kuwahangaikia yeye na familia yake, hawajui tu….

Swali wengi watauliza iliwezekanaje mimi kuishi na mume na huku huyu mume wa familia anakuja kwangu…iliwezekana sana,…lakini sio kila siku,…na tulijitahid sana kuhakikisha hakuna anayelifahamu hilo, aliyeweza kulifahamu hilo ni huyu Makabrasha baada ya kuwekeza vitu vyake.

Kuna kipindi mume wangu alinishuku…unajua tena binadami…yeye aliona kuna mabadiliko niliyokuwa nayo, lakini kwa vile mimi naifahamu kazi yangu vyema niliweza kumficha kabisa kuweza kunifahamu undani wangu…, japokuwa moyoni nilikuwa naumia sana, na sikuweza kumwambia mume wa familia kuwa mimi naumia sana kuendelea kumdanganya mume wangu...

Wakati nawaza hayo, nikasikia tena mtu akitembea kwenye korido, na mimi nikafungua chumba haraka na kutizama nje, nikaona mtu akingia kwenye moja ya chumba kilichokuwepo mbele yetu, sikuweza kumuona vyema, alikuwa ni mwanaume,ilikuwa ni kitendo cha haraka,...

Yeye...aliingia kwenye chumba kilichokuwa bado kwenye matengenezo, kilikuwa hakijamalizwa, nikahisi huenda ni mmoja wa mafundi, kaamua kuwahi, lakini kwa uhakika, nikaona niende nihakikishe. Lakini sikuwa nimevaa vizuri kutoka nje, …

Nikarudi ndani kidogo na kuvaa nguo za kikazo, nilifanya haraka haraka, nikatoka na kwenda hadi kwenye kile chumba, sikuona mtu, nahisi huyo mtu alishatoka, lakini atakuwa kafanya haraka sana, na atakuwa ni mwepesi sana, ila kulikuwa na dalili zote kuwa huyo mtu aliingia hapo, na kutoka. Nikatoka kwenye kile chumba na kuangalia sehemu zote hakukuwa na mtu maeneo ya karibu, nikajaribu kuangalia kila pande, lakini sikumuona huyo mtu.

Ili kuwa na uhakika zaidi nikawapigia walinzi kuwauliza kama kuna wafanyakazi wa ujenzi wameshawahi asubuhi, wakasema hawajafika. Hapo nikaingiwa na wasiwasi, na afadhali kama mitambo ingelikuwa ON, ningeliweza kujua ni nani, kwa kwenda kuangalia huko.

Mimi nikaondoa wasiwasi, nikajiandaa na kuelekea ofisini kwangu. Kabla sijafika huko, nikapitia chumba cha mitambo ya usalama, nikaingia na kuweka ile mitambo ON, halafu kwa haraka nikarudi ofisini kwangu....

Nilikuwa na ofisi yangu na humo nilikuwa kama mhasibu, mtunza masijala, na pia ni katibu muhutasi wa Makabrasha, kwahiyo utaona jinsi nilivyokuwa na kazi nyingi. Na hapo ndipo mara nyingi nakaa kama hakuna kazi nyingine. ni ofisi iliyokamilika kila kitu, komputa simu, mafile..nk.

Ofisi yangu hiyo ipo mbali kidogo na ofisi ya Makabrasha, ile ni kwenye korido moja. hiyo ni ofisi wakati nafanya kazi za kuweka kumbukumbu, ila nikiwa nafanya kazi za ukatibu muhutasi, huwa ninakuwa kwenye ofisi kubwa karibu na Makabrasha. Katika maswala ya usafi yupo mtu anafika kufanya hiyo kazi lakini kipindi hicho alikuwa likizo, kwahiyo nilikuwa na kazi kubwa ya usafi,na kazi nyingine....

Hata hivyo kazi kubwa nilishaifaya usiku, nikapitia pitia sehemu muhimu na kuhakikisha kuwa zipo safi, baadaye nikataka kwenda chumba cha Makabrasha, nilifahamu wakati kama huo yeye na rafiki yake yaani mume wa familia watakuwepo kwenye chumba cha maongezi, wakipata vinywaji, kabla hawajaingia ofisini .

Kumbuka mume wa familia anatambulikana kama ni mgonjwa, na jinsi gani aliingizwa humo bila watu kufahamu ni kitendawili, au sio..lakini kwa Makabrasha hiyo iliwezekana, maana hata mdogo wa familia alipomleta kaka yake hapo, anasema alimleta lakini akiwa kama sio yeye…

Muda wangu muhim ni huo, wakati wanazungumza mambo yao ya mikataba, nawafahamu sana taratibu zao kila wanapokuja kuonana, na wakikutana hivyo ndipo nafasi ya mume wa familia ya kupata kinywaji, kwani akitoka hapo anatakiwa kuigiza kuumwa...na ukumbuke kufika hapo sio mara ya kwanza..kuna ..haina haja kuwaelezea hilo,…muhimu muelewe kuwa hiyo sio safari ya kwanza kwa mume wa familia kufika hapo, tena akiwa mgonjwa.

Nilifika ofisi ya Makabrasha nikaona kafunga na ufunguo, kama nilivyotarajia,...huwa hataki kufanya makosa, chumba chake kama hayupo huwa kimefungwa, na hakuna mtu anaruhisiwi kuingia kama mwenye hayupo, hamuamini mtu, hata mtoto wake mwenyewe haruhusiwi kuingia hapo kwenye ofisi yake kama hayupo.

Hata mimi sina ufunguo wa chumba hicho wa akiba. Sikuwa na kazi kubwa kwenye chumba hicho, kwani usiku nilishakifanyia usafi, haikuwa na haja ya mimi kufanya usafi mwingine. Na hata yeye alishaniambia hanihitajii ofisini kwake mpaka aniite,kwahiyo haikuwa na haja ya kuingia tena humo, nikarudi ofisini kwangu

Nikiwa pale, nikapigiwa simu, na mtu ambaye hakunitajia jina lake, akaniambia;

‘Acha hayo unayokusudia kuyafanya, kwani tumeshakujua njama zako, kama utaendelea na mambo yako hayo,utakuja kujuta..ondoka kwenye hilo jengo haraka, ...’halafu simu ikakatika.

Mhh..hapo sikuelewa kitu, kwanza huyo mtu ni nani, na namba aliyopigia ni ngeni kabisa hata nilipojaribu kuigundua kama imesajiliwa kwa jina gani, ilionekana haijasajiliwa, ni nani, ni sauti ngeni kabisa, na..hata sauti ilionekana kama ya kuigiza, maana ilikuwa ya kukwaruza kwaruza, nahisi kaweka kitu mdomoni kuzuia sauti halisi, ...sikusema neno.

Kiukweli kutokana na kazi zetu vitisho kama hivyo tumeshavipata sana, na mara nyingi nina hulka yangu kuwa mtu mwoga hutanguliza vitisho, na mtu kama huyo hana lolote, mtu jasiri ni yule, anayetanguliza vitendo.

Na wakati nimetulia nikiwaza cha kufanya, mara simu nyingine ikalia, hii ilikuwa ya aliyekuwa bosi wangu, akaniambia yeye anaondoka,..kurudi ulaya masomoni

‘Sawa. Samahani nimeshindwa kuonana na wewe, lakini natumai mambo yanakwenda vyema, na mtoto wako umeshampata...’nikamuuliza.

‘Mtoto sijampata, licha ya kuwa nimewatimizia mambo yao yote, wameniambia nitakutana naye huko uwanja wa ndege, kwahiyo hapa nilipo sina amani kabisa, ila hawanijui tu, huyu mtu Makabrsha, nitamfanyia kitu hataweza kunisahau, kabla sijaondoka...’akasema.

‘Mimi nina uhakika mtoto utampata na yupo salama, huyo anayekaa naye, ni dada mwema sana anafahamu jinsi ya kulea watoto, nilimtafuta mwenyewe, niliambiwa nimtafute, kwahiyo kwa usalama wa mtoto wako acha iwe hivyo, unasikia, watakueletea huko uwanja wa ndege, usiwe na shaka na hilo...’nikasema.

‘Kwahiyo wewe upo wapi?’ akaniuliza.

‘Usijali, nakutakia safari njema, ukirudi natumai mambo yatakuwa yamebadilika,...’nikasema na kukata simu.

Baadaye nili-itwa na Makabrasha, nikaenda ofisini kwake, alikuwa peke yake, sikumuona huyo mgeni mwingine, ...sikuuliza, kwa makusudi…, yeye akasema;

‘Jamaa yako ameshafika, yupo wash-room,…. nimekuita mara moja, kuna kumbukumbu zangu sizioni kwenye mtandao wetu, na kwenye laptop ambay ndiyo ina namna ya kunasa vitu na kumbukumbu muhimu…neno lake la siri limebadilishwa, hatuwezi kuingia kwenye laptop,…hujui kama umeharibi kila kitu, ..niambie sasa ni wewe, je umefanya nini huko, unajua ile ndio kila kitu, mtoto wangu anasema anakushuku ni wewe…’akasema

‘Nimefanya nini..mimi…hapana, …unasema ni mtoto wako kasema hivyo, kuwa ni mimi nimefanya hivyo, na wewe ukamuamini….oh…ina maana wewe unanishuku mimi, kwa vipi…nimekuwa na wewe hapa kwa muda gani, kwanini nifanye hivyo,…sikiliza kama wewe unamuamini sana mtoto wako, kuliko mimi, ni sawa, lakini je wamfahamu huyo mtoto wako alivyo, mangapi anayokufanyia nyuma ya mgongo wako mimi nayafahamu, lakini naamua kumtunzia siri zake ili…’nikasema

Hapo akanikatisha na kusema….

‘Sikiliza mimi nakuambia alichoniambia yeye, unasikia, ..yeye kasema huenda ni wewe umeweza kuingia kwenye komputa ya kuhifadhi kumbukumbu na kuziharibu, maana ni nani angeliweza kuingia huko,…..hebu niambie ukweli,mimi ninakuamini sana wewe na haya nayafanya pia kwa jili yenu, mbona hamnielewi…’akasema

‘Mimi nakuelewa sana, wewe na mtoto wako…zaidi ya unavyofikiria wewe…’nikasema

‘Unanielewa kivipi eeh!..sikiliza mimi, sitaki tuje kukosana, unanielewe, tumetoka mbali jamani..huu ni wakati muhimu sana wa kuwa kitu kimoja, kwanini mnataka kunivuriga eeh, mtoto…sasa wewe….sikiliza mimi sitaki nije kuwaumiza nyie watu, nyie ni watu wangu muhimu sana katika kulikamilisha hili, hivi mnafahamu wenzetu wamejipangaje..hamjui ...’akasema na mara simu yake ikalia, akaniangalia na kusema;

‘Ondoka tutakuja kuongea badaye, na kama ni wewe unahusika na hayo, kama anavyodai mtoto wangu,…kasema ana ushaidi,…sasa kama akinileta huo ushahidi, mimisizani kama nitaweza kuvumilia, unanifahamu nilivyo…., hutaamini nitakachokufanyia, nitakufanyia jambo ambalo hutaweza kulisahau maishani mwako, na utajua, kuzaliwa…sitajali urafiki wetu..’akasema

‘Sawa, …ukweli upo wazi, muulize vyema huyo mtoto wako, huyo anataka kukuonyesha kuwa yeye ni nani, anataka kukurithi ukiwa hai, hata wanawake wako, ..kwanini huelewi…nisingelipenda kuwagombanisha, unasikia….’nikasema, na niliposema hivi nikaona kama uso unakunjama kwa hasira, halafu akasema

‘Huyo nitashughulika naye, ..huyo niachie mimi…nimeshamuelewa …, ila nilitaka kujua ukweli kutoka kwako, haya ondoka….ila sikia, kama ni wewe kweli, maana nitajua tu, usije kunilaumu…’akasema.

‘Mimi sijui unachokiongea, nitawezaje kuingia kwenye komputa na kuharibu hizo kumbukumbu, mimi sina ujuzi huo, na hapo huoni ...anayeweza kufanya hivyo, ni mtoto wako, kwanini umuamini mtoto wako, wakati kaonyesha dhahiri dalili za kukusaliti…hivi wataka nini tena kuligundua hilo,...’nikamweleza,

Mara nikasikia kitu kama mtu anataka kuja kutokea kule chumba cha chooni, na Makabrasha hakutaka huyo mgeni wake anione hapo, akawa ananiashiria nitoke na mimi nikasema huku natembea kuelekea mlangoni;

‘Mimi nahisi aliyefanya hivyo ni mtoto wako huenda kazificha hizo kumbukumbu kukukomoa, kwa vile hutaki kukubaliana naye, sasa ananitupia lawama mimi, ili kutukosanisha..nia yake ni hiyo hiyo unaifahamu wewe., hebu fikiria hilo kwa makini...’nikasema na yeye akakunja uso kama anawaza, na kuniashiria nitoke humo ndani haraka, akiashiria kwa mkono

Mimi nikatoka, na wakati natoka, hadi sehemu ya mapokezi ya ofisi hiyo, huwa mimi nakaa hapo kama kuna wateja maalumu, ila kwa leo sikutakiwa kukaa hapo, na mara mlango wa chooni ukafunguliwa akatokea mtu, ..

‘Mbona sio mume wa familia huyu…ni nani huyu…’ nikajikuta nikijisema moyoni,

Kilichonifanya niwe na mashaka zaidi ni jinsi ya utembeaji wake, kwa jinsi nilivyomzoea mume wa familia ningelimgundua kwenye utembeaji, lakini haikuwa hivyo, ila…kutembea kama kuchechemea, kuonyesha ana tatizo mahali,..

Kama ni mume wa familia basi wamefanya utundu wa hali ya juu, mpaka mimi nimeshindwa kumgundua, huyo mtu hakuniona, kwani alitoka kwa haraka na kuelekea kwenye mlango wa ofisi ya Makabrasha na kuingia huko.

Utembeaji wa kuchechemea, lakini mwendo ni wa kasi…huyu mtu keshapona hivyo…nikacheka kimoyo moyo..

Mimi nikatoka humo haraka, na kuelekea ofisini kwangu, ...sikuhitaji silaha kipindi kama hicho, ingenisaidia kama mume wa familia angesema hataweza kuifanya hiyo kazi niliyomuagiza, nilitaka akatae na kucheleweza kuweka saini kwenye hiyo mikataba, ili niweze kusafisha kila kitu kwenye kumbukumbu zao, nilijua humo ndani kwa Makabrasha huenda bado kuna kumbukumbu humo, nikawa nimepumzika nikifanya kazi zangu zingine.

Sikuonana na hawo watu, nikawa na kazi zangu zingine za kiofisi hadi mchana, na muda ukafika wa mimi kuondoka kurudi sehemu ninapolala, nikawasiliana na Makabrasha kwenye simu kuwa mimi natoka, na yeye akajibu kwa mkatao kwa kusema;

‘Sawa...’ na kabla hajakata simu akasema;

‘Natakuhitajia baadae...usije kuondoka…’akasema kwa sauti iliyonitia wasiwasi, nikafahamu labda, kama kweli mume wa familia kafanya hivyo, basi kuna kutokuelewana, nikahisi huenda zoezi limakamilika.

***********

Nikaelekea chumbani kwangu ninachojipumzisha, nilipumzika hapo nikiwa na mawazo ya kutaka kufahamu kilichoendelea huko, na baadaye nikarudi ofisini kwangu, baadaye nikampigia simu mume wa familia, simu ikawa haipatikani.

Kiukweli hapo nilikuwa na mashaka sana….baadae nikaona ni kwani ni nisiongee na Makabrasha mwenyewe,..

Nikafika ofisi kwake, …

‘Bosi vipi mambo yalikwendaje…?’ nikamuuliza

‘Bado….’akasema hivyo tu

‘Bado kwa vipi…?’ nikamuuliza akawa katulia tu,..baadae alipoona nasubiria jibu lake akasema

‘Kikao kimeahirishwa hadi baadae kidogo, tu wako alihitajika kurejeshwa hospitalini kwa haraka. …mambo yameharibika…’hapo akasema kwa hasira

‘Mhh..sasa?’ nikauliza

‘Bwanaeeh…hebu ondoka, …’akasema hivyo, hapo nikajua kumbe mambo hayakufanikiwa, na ndio nilikitaka, na wakati natoka, yeye akasema;

‘Ni lazima zoezi hili likamilike leo, kwa vyovyote iwavyo vile....sijui kwanini alichelewesha kuweka sahih hadi anaitwa huko hospitalini, mjinga sana huyo mtu wako..’akawa anaongea kwa ukali

‘Pole…labda haitawezekana kwa sasa…au..?’ nikasema.

‘Leo ndip mwisho,…hakuna baadae…na hili litafanyika, hanijui mimi, labda sio mimi..hawajui mimi nasubiriwa, hawajui, nilivyo kwenye wakati mgumu…zoezi hili ni muhimu sana hadi kwa wakubwa zangu…sitakubali lisifanikiwe, kabisa…jamaa yako ataniona mbaya, asipofanya hivyo, kwanini yeye..na hajui umuhimu wa hili…’akasema.

‘Haya utaniambia kinachoendelea mimi naondoka..’nikasema

‘Ondoka, msinichanganye, ila….bado sijamalizana na wewe, unasikia..ondoka, sitaki ni…basi ondoka…’akasema hivyo, niliondoka.

*********

Baadae nilitingwa na shughuli nyingine ikabidi nitoke kabisa kwenye hilo jengo, ..nikitoka humo nakuwa mtu mwingine kabisa,..nilitoka kwenda kununua vitu vya ofisi…, baadae nikarejea kwenye hilo jengo, nilihisi mwili ukinisisimuka, sikuelewa ni kwanini, nikawauliza walinzi kama mtoto wa Makabrasha alifika, wakasema hajafika siku nzima ya leo.

Kiukweli huyu mtu akiwepo, sina amani,… nikashukuru mungu, na nilipofika kwa Makabrasha akawa hayupo sawa vile vile…, nahisi ni kwa vile mume wa familia alimkatalia kusaini huo mkataba, na hakutaka kuongea na mimi kama alivyotaka asubuhi. Mimi sikujali, nikaingia kwenye chumba changu, nikahakikisha ile silaha bado ipo.

Silaha ilikuwepo pale pale, sikuigusa, maana nilikuwa mikono mitupu, nilikuwa mwangalifu sana kuigusa ile silaha, nilihakikisha kuwa siigusi mpaka niwe nimevaa kinga kwenye mikono yangu.

Nahisi hapo ndipo nilipofanya makosa..ya kiutendaji…, kwani ukumbuke, kuwa nilishaweka ile mitambo ya kuangalia matukio ya humo ndani, ON, kuruhusu kuonekana kwa matukio yote kwenye hilo jengo, na wakati naangalia hiyo silaha, sikukumbuka kuchukua tahadhari hiyo…, kwahiyo ni lazima itaonekana.

Ilipofika jioni mambo yakaanza, nikawa napilika pilika za hapa na pale, na nilitaka nihakikishe kuwa mkataba huo hausainiwi, hata kama mume wa familia atakuja tena ...ndilo lengo langu kubwa kwani yale yaliyokuwa yakitushinikiza kufanya hivyo, nilishayaharibu, atatushinikiza kwa jambo gani sasa.

Yawezekana huenda wana kumbukumbu hizo sehemu nyingine. Na ndio nilitaka nipate nafasi niweze kuingia chumba cha Makabrasha wakati hayupo...na ili hilo lifanyika ni vyema mtoto wa huyu mzee asiwepo.

Baadae…nikajaribu kumpigia mtoto wa Makabrasha ili kuhakikisha kama kweli hatakuja, na simu yake ikawa haipatikani,...nilijaribu simu yake nyingine ya siri, hata hiyo ikawa haipo hewani.

Baadae nilipata taarifa kuwa mume wa familia keshafika tena

Hapo mapigo ya moyo yakawa yanakwenda mbio, nifanye ili kulizuia hilo, nikafuatilia nikajua sasa wapo kwenye maongezi ya kushawishiana, ..hapo ilikuwa jioni ya kuingia usiku.

Siku waliongea muda mrefu..kubishana na ..nilijua itatokea hivyo, kwani nilishamshawishi mume wa familia asikubali,…na hapo ndio nikajiwa na maamuzi, maana hili jambo lisiposimamishwa, basi haitawezekana tena, ni lazima jambo lifanyike.

Hatua ya kwanza niliyoifikiria ni mimi kwenda kuichukua silaha, sasa silaha nitaichukuaje wakati mitambo ya kuonyesha matukio ipo ON,

Kwahiyo hatua muhimu ni kwenda kuzima mitambo, na nikichelewa najua mume wa familia ataweka sahihi, hataweza kuhimili mikiki mikiki ya Makabrasha, haraka nikaelekea chumba hicho cha mitambo…. Ili nikazime..

Bado nilikuwa na ufunguo wa kile chumba, nilikuwa bado sijaurudesha huo ufunguo kwa Makabrasha, huo ufungu huo ulikuwa nakala ya Makabrasha..japokuwa ana nyingine ya akiba, anaiweka anapojua yeye…ufunguo huo nilikuwa nimemuomba mapema sana, kuwa nataka kufanya usafi huko kwa kipindi kile hakuwa na wasiwasi na mimi, si anajua mimi sifahamu chochote kuhusu hiyo mitambo, au komputa.

Nilipofika kwenye hicho chumba, nikaingia na kuweka OFF kuzuia mitambo isione matukio, nikaingia kwenye komputa na kufuta matukio ya nyuma tangu pale nilipoweka ON, ,..ni lazima nifanye hivyo la sivyo mtu akija kutafiti, atagundua mtu aliyeingia mwishoni ni mimi…
Sikuwa na muda wa kuwachungulia maana ukiwemo humo unaweza kuona vyumba vyote, sikutaka kuingia huko kutokana na muda…

Haraka nikarudi ofisini kwangu ili niweke mambo yangu sawa kabla sijawaingilia Makabrasha na mume wa familia, nilitaka nikiwaingilia hapo nipo nimejiandaa silaha ipo mwilini,..kama ni kutumia nguvu basi itafanyika hivyo…lakini ni lazima hilo zoezi lizuilike leo, mikataba hiyo isisainiwe, na ikibidi niwapigie simu polisi aje, waone uozo wa huyu mtu.

Unajua..nayafanya haya nikijiamini kuwa zile kumbukumbu za picha zake za kashfa nimeshazifuta kwa watu wote…sikuwa na uhakika kama kuna nyingine lakini, vyovyote iwavyo, hilo zoezi liwe mwishi, kwani nilishakuwa na ushahidi wa kutosha wa kuonyesha uhalifu wa huyu mtu…

Pia ukumbuke niliwahi kumuambia mume wa familia, akiwa anaongea na Makabrasha ahakikishe simu yake inachukua maelezo yote, na nilitaka wakati nawavamia niwahi kuchukua ile simu yake na ya Makabrasha anayohifadhi maongezi yake na watu, ili iwe ni ushahidi.

Yote hayo yataweza kufanyika kiurahisi kama mtoto wa Makabrasha hatakuja, lakini akifika, itakuwa kazi nzito kidogo, hata hivyo, nilishajipanga nipambane nao.

Sikujali tena kwa ni hadi hapo, nimeshafanya mengi ambayo yatanifanya mimi na Makabrasha tusielewane tena, hasa akija huyo mtoto wake, na kumuonyesha kuwa ni mimi ndiye niliyefuta mambo yake kwenye kumputa ya kuhifadhi uchafu wake, kama atakuwa na ushahidi wa kufanya hivyo, sikuwa najali tena....

Leo ni leo…

NB, …Ngoja nimalizie…

WAZO LA LEO: Kila jambo utakalolifanya au ukiwa na nia ya kufanya jambo, usisahau kuwa kuna mwenye mamlaka ya kukupa pumzi,nguvu, na uwezo na uhai wa kulifanya hilo jambo liwe la jema au la ubaya. Wengi twajiona tuna mamlaka hayo, hadi kufikia kusema ‘unajua mimi ni nani..’ au ni lazima nitafanya, au lazima itakuwa, jeo ni nani anayefahamu kesho ya mtu….
 
SEHEMU YA 118


Kumbuka kusema nitafanya hiki au kile mola wangu akinijalia…



Leo ni leo….nikaingia kwenye mapambano…nikiwa peke yangu!

Nikiwa nimetulia ofisini kwangu nikimalizia kazi mbali mbali, na mara nyingi unapoanza kazi za mahesabu,kuweka kumbukumbu za mahesabu kwenye komputa, na kutayarisha taarifa mbali mbali, masaa yanakwenda haraka bila hata yaw ewe mwenyewe kujitambua, nikawa nimesahau kabisa wajibu wangu mwingine.

Nilipoangalia saa, ndio nikagundua hilo….nilikuwa nimetumia muda mwingi sana,...hapo hapo nikaacha kila kitu, na kujiandaa kutoka mle ndani, niende chumbani kwangu ikibidi nikachukue silaha, ili nikaweza kuwavamia Makabrasha na mume wa familia.

Kwanza nilitaka kuhakikisha kuwa hawo jamaa bado wanaongea, au mume wa familia keshaondoka maana muda mwingine ulishakwenda, nikachukua simu kutaka kupiga, lakini kitu kikanizuia, sikupiga simu.. nikawa sasa nataka kutoka mule ndani,…hapo ndio nikasikia king’ora cha polisi kwa mbali,

Muda huo moyo wangu unadunda sana,…na ikitokea hivi kama nipo kwenye mapambani ni ishara ya hatari…na niliposikia hicho king’ora cha polisi ndio ikawa ni zaidi,…hata hivyo mwanzoni nilijua ni polisi wanapita tu.., lakini kilipofika maeneo ya kwenye jengo kikasimama hapo, na mimi nikashituka, nikajua kuna kitu ..kuna jambo, na sio jambo dogo.

Nilichofanya kwa haraka nikumpigia simu mlinzi kumuuliza kuna nini, na mlinzi akasema hana uhakika

‘Huna uhakika, hilo sio gari la polis limesimama huko, limafuata nini…?’ nikauliza

‘Ndio na mimi nafuatilia madam…’akasema.

Hapo sasa sikujali nikampigia boso yaani Makabrasha..simu ikawa inaita bila kupokelewa,…moyoni nikajua kuna tatizo limetokea ofisini kwa makabrasha, nilitaka kumpigia mtoto wake kwani ndiye mlinzi wa baba yake, lakini sikupenda afike kwanza, nilijua akifika kila kitu kitaharibika.

Nikawa bado nipo mle ndani, moyo haunitumi kutoka nje…., nikapiga simu kwa walinzi kama mtoto wa Makabrasha keshafika, huyo mlinzi akasema hana uhakika, kwani yeye alitoka, na kumuachia mwenzake ulinzi, na huyo mwenzake ameshaondoka.

Baada ya dakika chache, nikapiga simu tena kwa walinzi kuulizia kuna nini, wakaniambia kuna tatizo kubwa limetokea ndani ya ofisi ya Makabrasha, na polisi wameshafika,..

‘Polisi!, tatizo gani la kuwahusisha polisi?, wamekuja kufanya nini?’ nikauliza maswali mengi kwa haraka bila kujua nauliza nini.

‘Makabrasha kapigwa risasi na hali yake ni mbaya sana, sijui kama atapona...’akasema huyo mlinzi na aliposema hivyo

‘Kapigwa risasi na nani…!’ nikauliza

‘Hatujui madam…’wakasema

‘Hamjui , huyu mtu aliingiaje ndani na silaha, bila kujulikana…’nikasema nikiwa nimesahau kila kitu kuwa kama ni wa kulaumiwa ni mimi, niliyezima mitambo ya kugundua vitu kama hivyo.

Pale mawazo yangu yalinipeleka kuwa liyefanya hivyo ni mume wa familia, japokuwa Makabrasha siku hiyo nzima alikuwa akikutana na watu mbali mbali, na wa mwishi ndio alikuwa mume wa familia kutokana na ratibba yake

‘Kama ni yeye amepatia wapi silaha, na aliingia nayo kw vipi, yawezekana..mungu wangu…’nikajikuta nikisema hivyo…

Nikampigia tena mlinzi mwingine kumuulizia,..sasa nikiwa na sauti ya kutaka kulia, nikasema;

‘Na nani kafanya hivyo, maana muda mfupi uliopita nilikuwa nikiongea naye, kwenye simu,haiwezekani..ngoja nikahakikishe....’nikasema na kukata simu.

Nilitoka mle ndani, nia nikuelekea huko, ili kama mume wa familia yupo hapo niweza kutoa msaada,lakini nilikuwa nimechelewa, kwani nilipotoa kichwa kuangalia kwenye korido, nikawaona maaskari. Wanakuja kuelekea chumba cha Makabrasha.

Kumbe maaskari walishafika, nikarudi ofisini kwangu kwa haraka kabla hawajaniona,na kujifungia, sikutoka kabisa, na sikutaka kufanya lolote maana sikujua nikikutana na hao polisi nitasema nini.

Nikawa namuomba munu wangu hayo yanipitilie mbali maana nikihojiwa, nikasema ni mimi nilizima mitambo ya kuonyesha matukio, nitakuwa hatarini, kwanini nilifanya hivyo, nk…

Maombo yangu yakajibiwa,…ajabu kabisa siku hiyo hakuna polisi aliyekuja kunihoji. Walikagua ofisi zote lakini ya kwangu wakaisahay,…baadae ndio nikasikia kuwa, wameshampata muaaji,...

‘Ni nani huyo..?’ nikauliza, wakanitajia sifa za huyo mtu aliyekamatwa, na jina lake,..oh...

‘Huyu mdada alifikaje hapa…., alikuja muda gani?’ nikauliza, na walinzi wakasema alifika hapo muda kabla polisi hawajafika, na inaonekana ndiye aliyemuua Makabrasha, na polisi wameshamshika, yupo chini ya ulinzi.

‘Aliingiaje na silaha..?’ nikauliza

‘Hata sisi hatuji Madam, maana mlinzi wa mlango wa kuingilia anakiri kuwa alimkagua na hakumkuta na silaha yoyote, na mitambo ya hatari haikuwahi kulia…’akasema na alipotaja mitambo, moyo wangu ukakumbuka jambo, hapo hapo nikauliza

‘Je yule mgeni wa Makabrasha, mwanaume aliondoka muda gani?’ nikauliza.

‘Alipoondoka tu ndio huyu mdada akaja…baadaye ndio hapo ikagundulikana kuwa Makabrasha amepigwa risasi...’akasema.

‘Ni nani sasa aligundua hilo?’ nikauliza.

‘Hatujui, hata sisi tuliona ajabu, maana hakuna mlio wowote wa hatari uliosikika, ina maana mitambo huko juu haifanyi kazi..na akti yetu hakuna aliyewahi kupanda huko juu, mpaka sasa polisi hawajasema ni nani aliwapigia simu…!’ akasema.

‘Sawa…tutajua tu..’nikasema

Wazo la haraka ni kwenda kuwasha mitambo ya kunasia matukio, …amoja na uamkini wangu, siku hiyo nilichanganyikiwa, maana…mawazo yangu yalikuwa kwa mume wa familia je yupo salama…

‘Je polis wakigundua hilo, kuwa ni mimi nilizima hiyo mitambo itakuwaje..’hilo nalo lilinisumbua sana…hapo sina ujanja, moja kwa moja nitashikwa kwa kuhusika na hayo mauaji, hapo nikawa na wakati mgumu.

Nikatafuta upenyo, hadi nikaupata nikatoka pale haraka na kwenda chumba cha mitambo ili niweze kuweka ile mitambo ON, niliingia kile chumba kwa haraka, nikaendelea ule mtambo...nilipotaka kugusa pale, nikagundua ipo ON tayari.

Unajua nilishituka,..ni kama vile mtu kaona kitu cha kutisha,.. ina maana kuna mtu alikuja akabadili, ...ni nani huyu, hakukuwa na muda wa kufikiri, ni kitendo cha haraka, kama ipo ON, ina maana matukio yote yatakuwa yapo bayana..

Hapo nikavutika nione kilichotokea kwenye ofisi ya Makabrasha, kwa haraka nikavuta droo ya ile komputa, laptop...ila nataka kuivuta mara....nikasikia kitu au mtu, hapo nikageuka kwa haraka kuangalia huku na kule, nilihisi ni mtoto wa Makabrasha kaja,..lakini hakukuwepo na mtu, hata nilipojaribu kuangalia kila sehemu sikuona mtu..ila nina uhakika huyo atakuwa ni mtu tu...

Nikaacha, kile nilichotaka kukifanya, sasa nikawa na wasiwasi kuwa hata polisi wanaweza kunikuta hapo, na ninaweza kuonekana kuwa nilikuwa natafuta njia za kuficha ukweli,...na wakatu nawaza hilo, mara nikasikia watu kama wanakuja mueleko huo nikajua ni polisi…nikatokeza kichwa.

Ni kweli walikuwa ni polis wanazunguka, hapo, nikaona hakuna usalama tena…nilipoona kuna upenyo nikatoka kwa haraka na kurudi ofisini kwangu, na kutulia kuwasubiri polisi wakija kunihoji, nilijua ni lazima watafika kunihoji...lakini hilo halikutokea kabisa siku hiyo.

Muda ule nipo hapo ofisi peke yangu, nikawa namuwazia Makabrasha, sikuamini kuwa huyu mtu anaweza kufa,..ina maana uhai wa mtu ndio hivyo, muda mpo naye ghafla keshapotea, ndio basi tena...nikamuwazia sana, zile tambo zake..kuwa yeye hawezi kufa hivi karibuni maana ana afya..., hata hivyo, kuna muda nilijikuta nikimuwazia kuwa huenda atapona hajafa...lakini kama alipigwa risasi, sijui sehemu gani, na huyo muuaji alidhamiria kumuua, sijui kama atapona!.

Unafahamu mtu hata awe mbaya vipi, linapomfika jambo kama hilo, la ugonjwa au umauti, hata kama ni ugonjwa tu, huwezi tena kumtakia mabaya, huruma itakuja tu, labda wewe uwe na nfasi mbaya, hapo mimi nikawa naombea apone tu, asife...sio dhamira yangu mtu huyo afe, mimi nilitaka akamatwe afungwe tu, ili haki itendeke, lakini sio kufa...

Kiukweli pamoja na mengine, kuwa alikuwa ni adui yangu na ilifikia muda natamani hata kumuua, lakini mtu huyo alikuwa na mazuri yake, ukiwa naye, ..na hata kwa jamii,..na kiukweli pamoja na hayo, alishakuwa mtu wangu wa karibu, sasa nikifikiria kuwa sitamuona tena, hapo kiukweli sikuweza kujizuia, nililia sana..kumbuka hapo nipo peke yangu…

Sikumbuki nilikaa muda gani nikilia hivyo,…kuangalia saa muda ukawa umepita sana, kupo kimia, na ile hali iliyozoeleka muda huo huwa nje kumechangamka, lakini siku hiyo ilikua kinyume chake, watu waliondoka, waliobakia ni wachache tu..

Hapo nikapiga simu kwa askari ili nijua kinachoendelea, askari huyo ndiye akaniambia kinachoendelea huko njem...kuwa Makabrasha kakimbizwa hospitalini...

'Ana hali mbaya sana..?' nikauliza

'Sijui Madam, hakuna aliyeweza kumuona, polisi hawaruhusu...'akasema

'Oh, basi, huenda atapona..'nikasema

'Sijui...'akasema huyo askari, na kukata simu

Nikawa hata sijui nifanye nini...kila ninachoshika hakishikiki, ule ujasiri wangu wote ukaondoka, ..nikachukua simu kumpigia mume wa familia, simu haipatikani, nikampigia docta wake ninayemfahamu simu haipatikani, nikampigia simu mume wangu halikadhalika....ikawa n ajabu kwangu, kwanini watu hao muhimu hawapatikani.

Sasa nimetulia, mara simu ya huyo askari niliyekuwa nampigia simu ikaita, nikapokea kwa haraka

'Nipe habari..?' nikauliza

'Makabrasha hatunaye tena duniani..'akasema

'Nini, una uhakika...?' nikauliza

'Ndio ukweli wenyewe, kafariki kwa jeraha la risasi,..uchunguzi bado unaendelea,…’ akasema huyo askari.

Shahidi huyu alipofika hapo akatulia kidogo kama kukumbuka kifo cha mtu huyo. Hata mume wa familia alionekana kuwa mbali zaidi maana sasa alikuwa kashika kichwa kwa mikono kichwa kimeegemea mikono.

Nilipopata taarifa hiyo, sasa akili ndio ikaanza kufanya kazi, sasa nikaona nitoke hapo haraka nirudi huko chumbani kwangu, niliangaza nje, nilipoona hakuna dalili ya askari haraka nikatembea hadi sehemu ya kushuka chini kulekea chumbani kwangu, karibu nionekane na askari, lakini hakuniona.

Wazo langu kwa muda huo ikiwezekana, nitokea kabisa kwenye hilo jengo nipotee kabisa, usiku kama huo angaliona nani,..na asubuhi na mapema nisafiri hadi huko kwetu kijijini, maana hata hapo watu humo jengo wananifahamu kwa sura ya bandia, sio ile sura yangu ya asili, kwangu ingelikuwa ni rahisi kutoka na ingelichukua muda watu kunigundua kuwa ni mimi nilikuwa nafanya kazi humo.

Nilishajipanga hivyo, lakini nisingeliweza kuondoka haraka hivyo,...bado kuna mambo ya kufanya, kwanza...hapo ndiop nikakumbuka ile silaha...nikawa sasa nipo chumbani, kwa haraka nikainua lile godoro....nilishikwa na butwaa...

Bastola haipo...!

‘Nani kaingia humu na kuichukua bastola…’ nikajikuta nikijiuliza mwenyewe, hapo nikainua godoro kabisa na kuliweka pembeni, hakuna kitu…

Mawazo ya haraka yakaniambia, bastola hiyo ndio imechukuliwa kufanyiwa mauaji…miguu yote ikalegea, nikajikuta nakaa sakafuni,..sina la kufanya, nikaiona jela ilee…

Maana hapo utajitetea nini..ni mimi niliyezima mitambo, bastla iliyoua nilikuwa nayo mimi, ni kwanini nilikuwa na bastola…nitasema nini kwa polisi…’hapo akatulia kwa muda, na aliyemzindua ni mwenyekiti,…

‘Bastola haipo imekwenda wapi…hapo tuambie ukweli, nahisi kuna kitu unatuficha?’ aliyeuliza swali hilo ni mwenyekiti…

‘Mimi sijui mwenyekiti sikujua imekwenda wapi….’akasema msimuliaji

‘Hapo kwakweli sisi hatukuelewi, Ina maana unataka kutuambia kuwa sio wewe uliyemuua Makabrasha…?’ akauliza mwenyekiti.

‘Mwenyekiti huo ndio ukweli anu, haya niliyosimulia ndivyo ilivyokuwa,…’akasema

‘Kiukweli inavyoonyesha hadi hapo, ni kuwa wewe na mpenzi wako ndio mlioshirikiana kumuua, makabrasha,…hadi hapo tu, huna cha kujitetea,…’akasema mwenyekiti

‘Mwenyekiti ndio maana nikaamua kuwaelezea ilivyotokea, nafahamu hilo, kuwa haya maelezo yangu ambayo ndio ya ukweli, yanaweza kunifunga, na mimi nitaonekana kuwa ndiye niliyeua,…lakini huo ndio ukweli, mkweli hana lawama..’akasema shahidi

‘Hebu nikuulize, hapo ulipokuwa kwenye ofisi na ofisi ya Makabrasha kuna umbali gani…?’ akauliza
‘Ni ofisi zilishikiana, yaani ni sema ni vyumba viwili vya karibu, sema ofisi ya Makabrasha ni kubwa, sio kama ilivyokuwa yangu…’akasema

‘Kwahiyo chochote kinachofanyika ofisi kwa Makabrsha hukuweza kukusikia..?’ akaulizwa

‘Huwezi kusikia kabisa,..alivyoitengeneza ofisi yake ni ‘sound proof..’ akasema

‘Lakini ungeliweza kutoka kwenye chumba chako kwa haraka na kufanya mauaji na kurejea ofisi kwako,…au sio…?’ akauliza mwenyekiti.

‘Ungeliweza…siwezi kusema huwezi maana …..ila nasema hivi, mim sijafanya hivyo,…’akasema

‘Polisi wanasema, wewe ndiye uliyezima mitambo ya kuonyesha matukio, wewe ulikuwa na bastola, bastola hiyo alikuelekea mdogo wa mume wako kwa siri..mdogo wa mume wako kalithibitisha, hilo…kwanini ulihitajia silaha mdogo wa mume wako kasema hajui…’akasema mwenyekiti.

‘Hawezi kujua hilo, maana hakuna aliyemuambia…alichosema ni sahihi..’akasema shahidi

‘Hadi hapo, sisi kama wanafamilia, unafikiri tunaweza kukuamini..?’ akauliza mwenyekiti

‘Nakumbuka, tangu mwanzo, kabla sijaongea mimi, wewe ulikuwa ukiamini kuwa aliyefanya hivyo ni mume wa familia na mdogo wake, au sio , sasa iweje kwa haraka uamini kwua ni mimi nimeyafanya hayo mauaji,…?’ akauliza shahidi.

‘Ni kutokana na maelezo yako…’akasema mwenyekiti.

‘Kwahiyo ukweli wangu ndio unaokufanya nionekane mimi ni muhalifu, au sio..kwahiyo mimi nimefanya kosa kuwaelezea huo ukweli, jinsi ilivyokuwa…?’ akauliza shahidi

‘Kutokana na maelezo yako toka mwanzo, inaonyesha ni wewe, kwasababu silaha iliyotumika kumuua Makabrasha ulikuwa nayo wewe hadi hatua ya mwisho, na wewe ndiye uliyafahamu wapi silaha hiyo ipo, na wewe ndiye ulizima mitambo ya kuonyesha matukio, kweli si kweli..?’ akauliza

‘Ndio…’akasema
na wewe umekiri kuwa ulishafikia sehemu upo tayari hata kumuua, kutokana na hali aliyowatendea, na..zaidi ulikuwa tayari kufanya lolote kumlinda mpenzi wako, na zaidi wewe unafahamu kutumia silaha vizuri, kuliko mpenzi wako
..huoni huo ukweli, hapo huwezi kukwepa hilo,..sema ukweli wako, ili tulimalize hili...’akasema mwenyekiti.

‘Ndugu mwenyekiti,..hayo niliyowasimulia hadi hapo, ndivyo ilivyokuwa, huo ndio ukweli, wa siku hiyo,...kama mliambiwa vinginevyo ni uwongo, maana mimi nilikuwepo humo ndani, tatizo, ni kuwa, ni kweli ni mimi nilizima kitufe cha kuonyesha matukio…’akatulia]

‘Subiri kidogo..ulisema ulipokwenda kuwasha uliona kipo ON…?’ akauliza mwenyekiti

‘Ndio..ndio maana nataka muwe na subira, kwasababu bado nina maelezo zaidi ya hayo, mkifanya haraka mtauharibu ukweli na nyie ndio ndugu zangu, mnahitajika muufahamu ukweli kabla sijaingia mikononi mwa polisi..’akasema

‘Sawa sisi tutakusikiliza tu, lakini hadi hapo, hata sisi tuna wasiwasi na wewe…’akasema mwenyekiti..

‘Wasiwasi wako hadi hapo, unakujaje, kuwa mimi ndiye niliweka hicho kitufe OFF, kwanini usiwe na wasiwasi kuwa NINANI, aliyekuja kuweka ON, na kwanini..na aliweka muda gani…?’ akauliza shahidi..

‘Hapo sijui, labda utuambie wewe…’akasema mwenyekiti.

‘Ndio nawakata msiwe na pupa,…maana kumbe baada ya hapo, huenda, huyo mtu alikuja kuweka ON, baada ya kumaliz hiyo kazi, au sio, kwanini matukio hayo yasionekana, hadi leo,..je polisi wanayo taarifa ya matukio yaliyotokea siku hiyo…?’ akauliza

‘Mimi sijui…’akasema mwenyekiti

‘Hawana, ukweli ni kwamba kuna mtu alikuja akaiba video, ya amtuki ya siku hiyo, ina maana kama ingelikuwepo, ingelionyesha yote yaliyotokea baada ya kuwekwa ON, nina imani,..kuna kitu hapo…’akatulia

‘Kwanini unasema hivyo…?’ akauliza mwenyekiti.

‘Sikiliza,..mimi niliweka OFF,..akaja mtu mwingine, huyu mtu mwingine hajui kuwa mimi nimeweka off…ukiwaja kwa haraka, usipoangalia kwa makini unaweza kuweka ON, ukijua mwenzako kaweka OFF, au ukaweka OFF, ukijua mwenzako kaweka ON, na ndivyo ilivyotokea…’akasema

‘Una maana gani..?’ akauliza mwenyekiti.

‘Ndugu mwenyekiti…baada ya kufikiri sana na kupata taabu ya kuliwazia hilo tukio lilivyokuwa, nikaona ni bora niseme huo ukweli ulivyokuwa, lakini nikijua kabisa, nikielezea huo ukweli kwa polis kwanza nitakwua mshukiwa namba moja , achilia mbali polisi,yoyote nitakayemuelezea huu ukweli, jinsi ilivyokuwa hataamini kuwa sio mimi niliyemuua Makabrasha,

‘Hata mimi…’akasema mwenyekiti

‘Ni sawa, sio kosa lako mwenyekiti,sio kosa la yoyote aliyepo humu ndani, lakini mimi ninaamini ukweli ndio silaha ya mtu yoyote yule…’akatulia

‘Sawa tuelezee ukweli wote, ndio tunataka sisi..kama wanafamilia..’akasema mwenyekiti

‘Ukweli wangu ndio huo, nyie ndio kwa mara ya kwanza nimweza kuwalezea kila kitu kilivyokuwa, bila kukwepesha jambo, maana hapo ningeliweza kukepesha, hebu jiulize kwanini hadi leo polisi hawajaweza kunikamata…?’ akauliza

‘Walitaka kukukamata mimi ndio nimewazuia…’akasema

‘Sasa ndugu mwenyekitu huo ndio ukweli, ni wajibu wenu, kuukubali kama ulivyo, au kuungana na polisi, siwezi kuwazuia kwa hilo, lakini ukweli halisi ndio huo, na sikuwaficha kitu hata kimoja,…ndio maana nilitaka nielezee hatu kwa hatua…,kama nimewaficha kitu mungu pekee ndiye anayejua zaidi….siwezi kukumbuka kila kitu au sio…’akasema

Aliposema hivyo mwenyekiti akakuna kichwa kidogo ile yakufikiri halafu akasema;

‘Mhh,… mimi sijui, lakini nionavyo mimi polisi wakisikia hayo maelezo yako , moja kwa moja wewe utakuwa mshukiwa namba moja, je hujatuficha kitu, mimi naomba uwe mkweli ili wakili wetu aweze kukutetea, nipo tayari kumtoa wakili wangu kwa ajili hiyo…?’ akaniuliza mwenyekiti.

‘Mwenyekiti, pamoja na hayo mimi nimeshaongea na polisi, lakini nilijua jinsi gani ya kuwaambia..niliwaambia yale niliyoyafanya kama mfanyakazi wa Marehemu lakini sikuwaambia kuhusu bastola au kuzima mitambo, ili nipate muda wa kukamilisha upelelezi wangu, ni muhimu sana ili haki iweze kutendeka...’akasema.

Mwenyekiti akaangalia saa yake, na alionekana na maswali mengi ya kumuuliza huyo shahidi, lakini kabla hajamuuliza huyo shahidi, huyo shahidi akasema;

‘Mimi imenichukua muda kuliwaza hilo, lakini moyo unanisuta, na kila nikiwaza sana naona sijatenda uadilifu, na watu wengine wanakamatwa ovyo, wakishukiwa kwa hayo mauaji,…wakati sio kweli,… na imekwenda, inafikia hali kama inafifia hivi, kwanini..ina maana kuna mtu anafichwa, ukweli sasa unaanza kubatilishwa, na kuna watu wengine, wanatarajiwa kukamatwa..na ni baada ya propaganda potofu..’akatulia

Na wasiwasi wangu ni huo kuwa atakayefuata kwa hivi sasa ni mume wa familia na mdogo wake, ambaye keshausema ukweli ..na huo ukweli kama kausema ulivyo, mume wa familia yupo matatani, mimi ndio naanza kuingizwa sasa....ndio maana nikaona sasa inapokwenda ni kubaya, ni bora nijitokeze mimi mwenyewe, wasiwasi wangu ni kuwa bado sijamaliza kazi yangu,....'akasema.

'Kwahiyo umeamua kujitokeza kwa vile sasa inaelekea kumgusa mpenzi wako wa asili..kwahiyo kwa hivi sasa upo tayari kufungwa kwa ajili yake…?' akauliza mwenye huku akitabsamu kwa utani.

'Hapana, ....mimi kama mpelelezi, hilo nilikuwa nalifanyia kazi, nilikuwa kwenye uchunguzi binafsi, kumjua ni nani hasa aliye-yafanya hayo mauaji, maana nashindwa kujua, ni nani mwingine angeliweza kufika hapo na kuchukua silaha hiyo, ..’akatulia

‘Kwanza kabisa kwenye shuku zangu nilimuwazia mtoto wa Makabrasha, lakini ukumbuke hadi walinzi walithibitisha kuwa mtu huyu hakuwahi kufika eneo la jengo hilo…wapo walinzi ninaowaamini sana,… na yeye pamoja na kukosana na baba yake asingeliweza kumuua baba yake, anampenda sana baba yake, sasa ni nani mwingine angeliweza kulifanya hilo...'akatulia kidogo, halafu akasema;

'Kiufupi, sikutaka kusema huo ukweli, kabla sijamaliza uchunguzi wangu, ila ninachotaka kuwaambia hapa ni hivi, ...mimi sijamuua Makabrasha huo ndio ukweli...na sikuwa na mipango huo, mimi nilikuwa na mipango yangu mingine kabisa ya kumnasa huyo mtu na kumfikisha kwenye vyombo vya dola, nikiwa na ushahidi ambao ulikuwa unafichwa na Makabrsha..ili iwe ni mwisho kwa mtu huyu, na kundi lake haramu, maana yeye anatumiwa tu....’akasema

‘Ushahidi huo unao sasa…?’ akauliza mwenyekiti.

‘Siwezi kukujibu hilo swali kwa hivi sasa…’akasema shahidi

‘Kwanini…?’ akauliza mwenyekiti.

‘Nina maana yangu kama mpelelezi, niamini kwa hilo…’akasema hivyo

‘Sasa kama sio wewe uliyemuua Makabrasha ni nani basi,…maana kwa muda huo, mweye silaha, na aliyekuwa humo ndani ni wewe?’ akauliza mwenyekiti.

‘Kama mtaniruhusu ninaweza kuongea nionavyo mimi,kutokana na uchunguzi wangu kiogo nilioufanya, ningelipata muda zaidi eeh, nikaweza kumalizia uchunguzi wangu, ningelimaliza kazi..lakini naona haraka haraka za polisi zitafanya nisifanikiwe, na nafahamu ni kwanini..’akasema

Mwenyekiti alisita kumuuliza ni kwanini, akawa anaangalia nje, halafu shahidi akasema

‘Japo sio sahihi, hata mimi sipendi, je ndugu mwenyekitu upo tayari niutoe ushahdi mwingine wa ni nani kamuua Makabrasha, kitu ambacho hata polis hawajaweza kukigundua,..?’ akauliza

‘Hayo ..kwanini usiwaambie polis wenyewe, maana wanasubiria huko nje…?’ akasema mwenyekiti na watu wakageuka kuangalia huko nje, na kweli askari walionekana wakiranda randa nje, kuhakikisha hakuna mtu anayetoka.

Shahidi akainamisha kichwa chini, kama anamuomba mungu wake, halafu akasema

‘Mwenyekiti wewe ndiye unayweza kulisawazisha hili, na ukweli ukapatikana, wewe ndiye waliyekuamini, au sio…mimi nasema hivi, fanya kile unachoona ni sahihi, lakini kwangu mimi, …bado nilikuwa na mengi ya kufanya,..unaonaje… yao…’akasema nakusita, alipoona mwenyekiti akisoma ujumbe wa simu yake

Ilionekana Mwenyekiti yupo kwenye wakati mgumu. Baadaye mwenyekiti akachukua simu yake akitaka sasa akitaka kupiga , huku akimwangalia huyo shahidi, na shahidi akageuka pembeni kumuangalia mume wake, alijua hadi hapo hakuna jinsi, ni lazima mwenyekiti atimize aajibu wake, hata hivyo nafsi mwake alijua bado hajakamilisha kazi yake. Shahidi huyo sasa akaniangalia mimi, nahisi alihitajia msaada wangu…

NB: Ni nini kitaendelea.



WAZO LA LEO: Dhana mbaya haitakiwi, hii ni pamoja na kusengenya, kuwateta watu wengine vibaya,..hivi vitu sasa hivi vinaonekana ni vya kawaida tu! Watu kutetana, kuandikana mambo ya aibu, kupiga picha mbaya na kuziweka mitandaoni, kuzusha uwongo, au propaganda,..au jambo halijathibiti,a u kuruhusiwa kuongea wewe unakuwa wa kwanza kulitangaza... nia wakati wmingine ni kuharibiana majina. Hii ni dhambi kubwa, hebu fikiri kama ni wewe ungelifanyiwa hivyo ungelifurahi, ukijua kuwa ni uwongo. Inaumiza sana..je utawezaje kulilipa hilo jeraha la mtu aliyeumia moyoni kutokana na dhana hizo potofu..Tujiepusheni na tabia hii jamani.
 
SEHEMU YA 119



Shahidi alipoona mwenyekiti kashikilia simu, akajua sasa kila kitu kimeharibika,

Akawa anamuangalia mwenyekiti kwa mashaka, akiangalia vidole vya mwenyekiti vikianza kugusa batan za simu, ili kuanza kupiga namba, kama vile anavyoangalia adui wakati anataka kufyatua risasi, mara nyingi unaangalia kidole kinachovuta kiwambo cha kuruhusu risasi itoke...hapo ndio unatakiwa uchukua maamuzi ya haraka.

Shahidi kwa haraka akasema;

‘Mwenyekiti hivi wewe huoni , kama usipoufahamu ukweli wote uliobakia inaweza ikaja kukuathiri wewe kisiasa maana ukweli umepotoshwa na nia ni kukuharibia wewe kisiasa na kiuchumi, hulioni hilo….’akasema shahidi na mwenyekiti akawa kama hajali

Vidole vya mwenyekiti vikabonyesha namba au sehemu tatu....huenda sasa ....

‘Najua mwenyekiti unatimiza wajibu wako kisiasa, lakini ninaomba unipe muda kidogo tu nimalizie kazi yangu, nina uhakika hata wewe mwenyewe utakuja kunishukuruu kwa hilo, …’akasema mzungumzaji na kunigeukia mimi, kama vile anaomba msaada kwangu. Mimi nilikuwa kimia tu…

Shahidi sasa akakata tamaa …mimi nikaona na mimi nijaribu bahati yangu, hapo nikafunua mdomo na kusema;

‘Baba naomba tumpatie muda, huyu shahid ili aweze kutimiza kile alichokianza, hatujui ukweli wa haya yote, nimependezewa na kazi yake,…mimi naona labda akimalizia kazi yake aliyoianza, tunaweza kumuamini, naomba tafadhali baba usiwaite polisi kwanza, jitahidi waendelee kusubiria…’nikasema

Hapo baba akawa kama anaiweka simu pembeni…

Ndipo huyo mzungumzaji ambaye ni shahidi akasema;

‘Mwenyekiti nashukuru sana kama mtanikubalia ombo langu hilo.., hapa nilipo nipo kazini, nawasiliana na watu wangu wanaonisaidia kwa hili, najua nikitoka nje sasa hivi kwa hali ilivyo ninaweza kukamatwa, lakini muda mchache tu nitapata taarifa muhimu ninayoitegemea,…’akasema.

‘Kwahiyo ina maana huo muda unaoutaka kuikamilisha hiyo kazi, sio lazima utoke hapa, hata ukiwa hapa unaweza kuifanya hiyo kazi yako..?’ akauliza mwenyekiti

‘Ndio mwenyekiti…ikibidi nitatoka, lakini, kwa hivi sasa…’akasema mzungumzaji na kukatiza akiwa anaoma ujumbe pepe kwenye simu yake.

‘Sawa..mimi sijui wao wamesema tukimaliza hiki kikao, watafika, kuna watu wanawahitajia, sasa kwanini, watakuja kutuambia…’akasema mwenyekiti

‘Kwahiyo hawajasema kwanini wanawahitajia hao watu..?’ akauliza wakili wa mume.

‘Wamesema kuna watu wanahitajika kuisaidia polis wapo humu kwenye hiki kikao chetu, wanataka kuja kuwachukua, …mimi siwezi kuwazuia kwani aliyeniambia hivyo sio mtu mdogo…ila yeye kwa kuniamini wamesema tuendee na kikao chetu tu, hadi hapo tutakapomaliza…ila asitoke mtu, au sisi tusiongelee swala la marehemu maana hilo lipo polisi....’sasa akasema mwenyekiti.

Mdada shahid akasema;

‘Najua wao mpaka sasa wanahisi kuwa mimi na mume wa familia tumeshirikiana kulifanya hilo jambo, …muhimu nipate muda wa kutafuta ushahidi wa kuliwakilisha hili jambo kwao…’akasema shahidi na kabla mwenyekiti hajaongea shahidi akaendelea kusema;

‘Mimi…ninajua baada ya kukamilisha hiyo kazi, haki itatendekea, sasa kama wao kweli wanaoushahidi kuwa sisi ndio tumehusika,..tutapambana kwenye mahakama…’akasema shahidi

Sasa mwenyekiti akawa anashughulika na simu, kuonyesha anawasilian na watu…baadae mwenyekiti akasema;.

‘Elewa nafasi yangu kwa sasa…, hayo uliyoyaelezea hapa yalitakiwa yawafikie wao, je ukisimamishwa kizambani ukasema uliwahi kunilezea haya mimi, je kisheria mimi nitakuwa kwenye nafasi gani, ukumbuke nilishapewa amri kuwa swala linalohusiana na marehemu tusiliongelee hapa, sisi tumekiuka..’akasema mwenyekiti.

‘Na haya nimeyasikia uliyoyaongea , mimi nitaulizwa je nilipoyasiki hayo kama kiongozi wa siasa nilichukua hatua gani…unaona ilivyo, mimi nitasema nini, nikisema bado nilihitajia ushahidi zaidi , nitaambiwa je wewe ni polisi…’akasema

‘Ni kweli mwenyekiti, mimi naona…basi tuendelee na mambo mengine huku nikifanya kazi yangu, au na hilo siruhusiwi..’akasema shahidi.

‘Tutaendelea lakini ilitaka hili swala limalizike ili tuweze kuwa huru kuendelea na vipengele vingine….’akasema mwenyekiti.

‘Ndugu mwenyekiti mimi ninakuahidi nikishakamilisha hii kazi,mimi mwenyewe kwa wakati wangu nitakwenda kuonana nao, bado kuna mambo machache nahitajia ushahid wake, nipo hapa lakini nayafuatilia mambo fulani fulani…’akasema

‘Sawa hilo …unasikia baada ya kikao, wewe ndio utaongea nao, sisi baada ya kikao tutakuwa hatuna mamlaka ya kumzuia mtu yoyote asiwajibike kwenye vyombo vya usama…’akasema mwenyekiti.

‘Hamna shida ndugu mwenyekiti…’akasema shahidi kwa kujiamini.

‘Najua mwenyekiti unatimiza wajibu wako, lakini kwa jinsi ilivyo, ukitoa kauli yako waje kunikamata, ambacho ndicho hao watu wanakihitajia, itakuwa na nguvu sana kwao, na utaona magazeti yao yatakavyoandika..kisiasa…’akasema

‘Kwahiyo unavyosema hivyo, ina maana leo polisi hawatakukamata au, wakati wameshajiandaa kuifanya hiyo kazi?’ akauliza

‘Hapo mimi sijui, kama wamejiandaa kufanya hivyo, lakini wanatakiwa wawe na jambo la kunnikamatia nalo, hapo ndio wanasita kufanya hivyo hata wao bado hawajawa na uhakika na kazi waliyoifanya,haijakamilika ..na na..’akasema akasita baadae akasema

‘Mimi kama raia mwema nina haki zangu, sawa watasema wananikamata ili mimi nikaisaidie polisi, haya kwanini niisaidie polisi…na hili tukio limtokea lini, ndio wanahaki hiyo ya kuniitakisheria niende kituo cha polisi au wao waje hapa kunikamata, lakini hata mimi nina haki zangu za kujitetea….’akasema

‘Nikuulize swali wewe unapofanya kazi zako , huwa wakati mwingine unashirikiana na polisi..?’ akauliza mwenyekiti

‘Ndugu mwenyekiti naomba mnielewe ..kazi zangu mimi sishirikiani na polisi ,kuna wakati inabid niombe kibali chao, ikibidi lakini ilivyo, mimi sikutakiwa kufahamika na mtu kuwa naifanya hiyo kazi,…’akasema

‘Je una kibali cha polis cha kuifanya hiyo kazi..?’ akauliza mwenyekiti

‘Ndugu mwenyekiti inapofika polisi kunihoji lolote kuhusu kibali changu cha kazi, anayeweza kuyajibu hayo maswali ni bosi wangu, ndio maana sitaki polisi waje kunikamata kwa hivi sasa…na kwa hili kama nilivyoeleza tokea awali, sijapata kibali kwa bosi wangu, au sikutumwa na bosi wangu, hii ni kazi yangu binafsi, nimeifanya hili kazi kwa manufaa yangu...’akasema.

‘Sasa kumbe hata kibali cha kufanya kazi kama hiyo huna huoni bado unanitia mashaka..?’ akauliza mwenyekiti

‘Kwa kauli yako hiyo mwenyekiti hata mimi unanitia mashaka, kwanini unachelea kusubiria, wakati hayo ninayotaka kuyafanya pia ni kwa masilahi yako…ninahis ni kwanini, lakini hisia zangu nazo zinaanza kuingiwa na mashaka..’akasema

‘Mimi natimiza wajibu wangu kwa mujibu wa sheria,…’akasema mwenyekiti.

‘Ni sawa, je ni kweli kila kazi unayoifanya inafuata mtiririko huo, tuseme ukweli ndugu mwenyekiti,..angalia mwenzako aanavyocheza rafu, na bado haonekani kuvunja sheria ni kwanini, ni kwavile kwenye uwanja wenu huo, kuna mambo mengina yanakubidi tu ufanye hivyo, kwa masilahi ya uma...’akasema

‘Kwahiyo wewe unataka na mimi nifanye hivyo…?’ akauliza mwenyekiti

‘Mimi sina mamlaka ya kukushauri ufanye hivyo ndugu mwenyekiti, ila nakuelezea hali halisi…’akasema

‘Kwa mimi nilivyoona, ninahisi umeifanya hiyo kazi hasa hasa kwa manufaa ya mpenzi wako wa zamani,..na hapo ndio inaigusa familia,..unielewe hapo,..vinginevyo ,eeh, hili jambo lisingelizungumziwa hapa,..kwahiyo hayo yakusema kuna mkono wa siasa, na unataka kulifanya hivyo ili hata mimi nifaidikie …hapana, siliungi mkono kinadharia,…’akasema

‘Lakini kivitendo, nafahamu sana hizo mbinu zipo, lakini sio kwangu,..sasa ngoja nione, kuna kitu kidogo nataka nikiweke sawa, ngoja niongee na wahusika, wanipe muda kidogo…’akasema na kuanza kupiga simu, aliongea kwa muda, kukawa kama vile hilo ombi linakataliwa, na baadae akamaliza na kusema;

‘Unajua nimegundua kitu..wewe kwa jinsi ulivyompenda mwenzako, ulikuwa tayari kufanya lolote kwa ajili yake, nimeyafuatilia maelezo yako yote, na hasa pale ulipofikia kuacha kazi kwa mtu wako wa kwanza kwa ajili ya kwenda kupambana na wale walioingilia maisha yenu na mipango yenu,na mpenzi wako au sio, wivu ukakutawala, ni kweli si kweli…?’ akauliza mwenyekiti

‘Mwenyekiti unaweza kuliweka hilo, kwa jinsi unavyoliona wewe, lakini kwanini hujiuliza kama nilifanya hivyo kwa ajili yake kwanini niseme kila kitu ambacho kinaweza kumuhatarisha yeye, au mimi ….kwanini sijaficha hu ukweli na nilikuwa na nafasi ya kufanya hivyo…, nimefanya hivyo kukwepesha athari zake ambazo zitakuja kutokea baadae…’akasema

‘Ni sawa nakuelewa sana, hapa nataka kufahamu jambo, kwanini ujitolee kufanya kazi hiyo ya hatari, wakati kisheria ina wenyewe,,…sawa labda ulijihimiza hivyo ili uweze kufuta kashfa alizokuwa nazo marehemu dhidi yako…, na ilionekana ulifanikiwa ..sasa kwanini bado ukaendelea kujiweka hatarini..na hapo ndipo inaonekana lengo lako sasa ilikuwa kumaliza hiyo kazi kabisa, na kuimaliza hiyo kazi ka-bi-sa, ni kuhakikisha huyo mtu hayupo au sio…?’ akaulizwa

‘Ndugu mwenyekiti..majibu ya swali lako, yangeliweza kujibiwa kwenye ukamilifu wa uchunguzi wangu, tafadhali nipeni muda, nina uhakika majibu hayo pia yatawasaidia hata hao polisi….’akasema

‘ Mimi nataka kusema hivi…unajua kila mtu ana ndoto zake, lakini tuwe makini katika kujitolea muhanga kwa nafsi nyingine..halafu unafanya hivyo hata bila kibali..unaona hatari ilivyo…’akasema

‘Ndugu mwenyekiti mengine siwezi kukuambia…kuwa nina kibali au sina…siwezi kuongea kila kitu hapa, kwa …anajua sana rafiki yangu hapa, kwanini sitaki kujielezea zaidi mimi kuhusu kazi yangu…’akasema na mwenyekiti akageuka kumuangalia rafiki wa mke wa familia, ambaye kwa muda huo alikuwa kama anawasiliana na watu wake kwa njia ya ujumbe wa maneno.

‘Sawa umenikatiza …nilitaka kusema hivi, ni sawa unawajibika, ..lakini kwanini usifanye hayo kisheria, na kama unawajibika kwa mtu, je kweli huyo unayewajibika kwake yupo na wewe….., huenda mwenzako anakutumia tu, kwa masilahi yake, hali kama hiyo ni hatari…umeona sasa kinachotokea…’akasema mwenyekiti na shahidi akatikisa kichwa kukubaliana na ushauri huo.

Mwenyekiti akaendelea kuongea….

‘Kwa uhakika zaidi, hebu mwangalie mwenzako, alivyokufanyia wewe naona humfahamu vyema huyo mpenzi wako, kama unavyodai unamfahamu kihivyo, yeye kwa tabia yake, imeonyesha dhahiri kuwa yeye ni mbinafsi, yupo tayari akutumie wewe kwa manufaa yake, na mwisho wa siku anaweza asiwe nawe tena....’akasema mwenyekiti.

‘Ni sawa…lakini…’akasema shahidi na kukatisha pale aliposikia mume wa familia akikohoa kama vile kusafisha koo. Akatulia akimuangalia, akitamani mtu huyo azungumze neno..

Mume wa familia, aliinua kichwa na kumwangalia mwenyekiti, akiwa kakunja uso,wa kutafakari, nahisi kuna kitu alitaka kukizungumza, lakini akawa anasita kukiongea, hakusema neno, alimwangalia mwenyekiti kwa muda, halafu akageuka kumwangalia huyo shahidi, .

Wawili hawa waliangaliana tu, na baadaye akatikisa kichwa kama kusikitika, halafu akainamisha kichwa chini na kutulia, hakusema neno, na mwenyekiti ambaye alikuwa akiwaangalia wawili hao,…akitarajia kauli kutoka kwa mume wangu, lakini alipomuona huyo mtu katulia tu, akaendelea kusema kwa kumchokoza huyo mtu;

‘Kama ni uwongo kuwa huyu mtu unayemuhangaikia, hana huruma nawe, kama nimemzulia uwongo, huyo hapo muulize, ...kama kweli yupo na wewe mia kwa mia, kama kweli, yupo na wewe au kama kweli yupo na mke wake aliyemu-oa, ambaye kamuoa kwa ajili ya mali, ili tu kujinufaisha, aseme tusikie, uwanja ni wake, ...’akasema mwenyekiti.

Walipoona mume wa familia kakaa kimiya, shahidi aliyepita, akasema;

‘Ndugu mwenyekiti, mimi nafahamu ni kitu gani ninachokifanya, na sikufanya hayo kwa ajili yake tu, nilifanya hayo kwa vile nawajibika kufanya hivyo, kwa ajili ya watu wengi, hata akiwemo yeye, na mungu wa ni shahidi, nimeyafanya hayo , bila kutarajia kitu kwa mtu yoyote…’akatulia

‘Ni kweli…kama ni kweli nilitarajia msaada wa kauli njema kutoka kwake, …naona kama anakusanifu tu…’akasema mwenyekiti akimchokoza mume wa familia.

‘Sasa kama yeye ataona kuwa mimi ni mjinga, sikuwa na maana njema kwake, hilo ni yeye na kichwa chake, na haliniumizi sana kichwa changu,ingeniumiza sana, kama ningelikaa kimiya baada ya kuona hayo yalitokea…’akatulia kidogo halafu akaendelea

‘Nimeyaona yote…lakini sasa, kwa jinsi yanavyokwenda, badala ya kutafuta ufumbuzi, inakuwa kinyume chake, jambo hilo sasa linatumiwa kisiasa, na sio kwa nia njema, bali ni kwa masilahi ya mtu…aheri sasa yangelifanyiak hivyo ili na haki itendeke, lakini sivyo hivyo…, ndio maana nikaamua kuusema huo ukweli kwenu, kwani nafahamu nyie ndio waathirika wakubwa wa kadhia hii yote...kweli si kweli ndugu mwenyekiti’akasema huyo shahidi.

Mwenyekiti, akiwa bado kamuangalia mume wa familia akasema

‘Kweli si kweli mume wa familia mimi sasa hivi nahitajia kauli yako, awali ulijifanya mjanja unaongea sana,…, nataka nikusikie sasa ukijitetea…’akasema mwenyekiti na mume wa familia alibakia kimia.

‘Ok, ndugu shahidi, ..sasa kama unakubali kusema ukweli na kufichua maovu kwanini usishirikiane na wale walipewa dhamana hiyo na serikali, ambao ni polisi, kwanini ufanye hayo kimiya kimiya, peke yako, huoni kuwa kwa kufanya hivyo ni makosa…au bado unahisi nyie wawili mna makosa?’ akauliza mwenyekiti alipoona mume wa familia kabakia kimia tu.

‘Muheshimiwa Mwenyekiti , nafahamu fika wewe unafahamu vyema hilo ninalolifanya, na sio geni kwako, kuwa kuna mambo mengine hutakiwi kukimbilia kuwaambia polisi kwanza…’akatulia

‘Wewe unasema…’akasema mwenyekiti na watu wakacheka kidogo

Aaah….naomba mwenyekiti nieleweke vyema, nafahamu kwanini huwezi kukubaliana na mimi, lakini kiuhalisia unalifahamu hilo..wakati mwingine, inabidi ujirizishe mwenyewe kwanza, kwani ukikimbilia huko, wao watakachokifanya ni kukushika, wakisema unakamatwa kwa ajili ya kuisaidia polisi, na hata kama hawatakukamata kwa bahati mbaya, wao watakuzuia usifanye uchunguzi wako, ili wao waufanye, kwani ndio kazi yao au sio...’akatulia kidogo, halafu akasema.

‘Ndio ni utaratibu wao, kwa nia njema lakini, wakakushika au kukuzuia, ila wao wafanye wajuavyo wao, kiutalaamu wao, huenda wakafanikiwa au wasifanikiwe kwa kile ulichokianza au kukigundua…’akatulia kama mwalimu anayetaka wanafunzi wake waelewe.

‘Lakini kwa vile wao wanaona ni kazi yao, hata kama itawashinda hawatatka kukubali,..lakini mimi kama raia mwema huenda ningelifanikisha hilo kwa njia zangu za usalama-raia, na kuwarahishia kazi, kwa vile mimi nina utaalamu huo kwa namna ya kijamii zaidi..’akasema

Mweyekiti akamkatiza kwa kusema;

‘Sasa kosa lipo wapi, wewe ukienda kushirikiana nao, ukawaonyesha kile ulichokigundua, kijamii-usalama …itawapa nafasi nzuri kukamlisha kazi yao..au sio…’akasema mwenyekiti.

‘Ni sawa usemavyo mwenyekiti, lakini ukumbuke ushahidi mkubwa walio nao umeshachakachuliwa, na wao, watakuwa wakiutumia ushahdi huo kuwakamata wasio husika na wakifanya hivyo, ndio itakuwa mwanya wa wahalifu kuzidi kujilinda, na ukweli unaweza kupotea kabisa…ni nani ataumia, kama sio upande wako mwenyekiti..’akasema.

‘Usipende kuyafanya hayo kama vile ni mimi nimekutuma, sijakutuma..unanielewa hapo..’akasema mwenyekiti

‘Unajua Ndugu mwenyekiti, nayafanya haya kwa vile nafahamu, sio mara yangu ya kwanza kukutana na vitu kama hivi, wao sasa hivi ukisema mtu wenu yupo hapa njooni mumukamate,..watanikamata, na nikiwaelezea haya, ooh, wewe ndiye tulikuwa tunakutafuta…naenda kusota jela…na hapo kila kitu kitaharibiwa, ukweli utageuzwa, maana bado sijafanikisha,…’akatulia.

‘Mimi kutokana na utendaji wangu wa hii kazi,nimejifunza mengi, kwahiyo sioni kama nafanya kosa, kutokuwaambia yale niliyoyaona, nafahamu wengi mtaona hivyo,...’akatulia

‘Ila mimi nafahamu nafasi yangu kama raia mwema, ni wakati gani niwakilishe hayo niliyoyaona kwao, na muda huo ukifika, utaona matunda yake, sio mara ya kwanza kuyafanya hayo..nakuhakikishia ndugu mwenyekiti, baada ya kukamlisha kazi yangu haki itatendeka, na mwenyewe utakuja kuja kunishukuru, labda hawo wahusika waniwahi na kuniua...’akasema.

‘Na wakiniua ni ajali kazini, ni kama askari kufa vitani, sioni ajabu...’akasema hivyo baada ya kutulia kidogo, na mwenyekiti akatabsamu na kusema;

‘Ndio hapo unapokosea, labda hao wakikuwahi na kukuua, huoni kwa kusema hivyo unahitajia ulinzi wa polisi,..maana wao ni kazi yao kulinda raia, na kuhakikisha haki inatendeka, na kwa jinsi unavyoongea ni kuwa una wasiwasi kuwa hao jamaa wanaweza kukudhuru, au sio… ni vyema ukajisalimisha kwa usalama, na wao watawajibika kwa hilo, kwani wao wana mamlaka na uwezo wa kukulinda...’akasema mwenyekiti.

‘Una uhakika na hilo ndugu mwenyekiti, kuwa wanaweza kunilinda, mbele ya hao upande wa pili,…hahaha...’akasema

‘Kwanini nisiwe na uhakika, hao watu hawapo juu ya sheria, au…ni nani hao,…hapana ni wakati raia mnatakiwa muwaamini watu wenu wa usalama, wao wamekula kiapo cha uaminifu au sio…’akasema mwenyekiti.

‘Mwenyekiti nazungumza haya maana mimi katika kazi hii nimekuwa nao japokuwa sipo kwa mujibu wa taratibu zao, nimekuwa nao kwa kupitia bosi wangu ambaye kasajiliwa kisheria, ni kweli wapo wengi watendaji wazuri lakini pia wapo wakosaji wachache wanaharibu kazi njema ya kazi zao,…’akasema

‘Una uhakika gani na hao wachache…’mwenyekiti akataka kuendelea, nahisi alikuwa akipoteza muda kwa makusudi maalumu, anayoyafahamu yeye mwenyewe

Hapo mzungumza akasema ..

‘Ni wangapi wangapi waliahidiwa hivyo kuwa tutakulinda, na sasa tumeshawasahau, kukulinda kwao ni kukuweka jela, wanasema kwa manufaa yako, au manufaa ya jamii, au sio..huko jela kweli ni sehemu nzuri ya kumlinda mtu, ndugu mwenyekiti, ulishawahi kukaa jela…?’ akauliza

‘Hebu muulize binti yako, akuambie ukweli,na ukumbuke yeye aliweka sehemu nzuri, je wote wanaweza kuwekwa sehemu hizo, na je hizo sehemu nzuri, ni nzuri kweli, muulize binti yako atakuambia,

‘Kwa kifupi,…, jela sio mahali pema pa kuishi, kuna hatari zake hasa za kiafya, achilia mbali kuathirika kisaikolojia, huko pia kuna watukutu wasiojali, wao huko wameona ndio miliki yao....sawa ikibidi nitaenda huko, lakini kuna jambo bado nalifuatilia, nisingelipenda kuliongelea hapa kwa hivi sasa na hasa kutokana na hali ninayoiona…, tafadhali mwenyekiti nakuomba unielewe hivyo...’akasema.

Mwenyekiti akamgeukia mume wa familia na kumwangalia, akageuka kuniangalia mimi, halafu akasema,;

‘Kama alivyosema shahidi, hayo ya nani muuaji wa Makabrasha ni mambo ya polisi, na hatutakiwi kimujibu wa sheria, kuyaongelea hapa, kilichotuweka hapa na mambo yetu ya kifamilia, tufanye yale yaliyopo kwenye mipaka yetu, tusipende kujifanya tunajua saana, na kuingilia kazi za watu wengine waliopewa dhamana hiyo na wanao-elewa,…

‘Aheri ya kwako wewe mwenzetu anajua jua mambo hayo, sasa sisi tukiulizwa kwanini, tutasema nini....hilo kwa hivi sasa tuliache…tuwaachie wanaohusika, sasa turejee kwenye msingi wa kikao chetu…au sio mawakili’akasema mwenyekiti na kuwaangalia mawakili.

Muda wote mawakili hao walikuwa kimia…, kuacha wakili wa mume wa familia

‘Ninashukuru tuna watu wetu wa sheria, na wameona juhudi zetu katika kuliweka hilo sawa, kama tunakosea wao watatusahihisha, ila cha muhimu ni kufuata ajenda zetu…

‘Sasa kabla hatujaingia kwenye kipengele kuhitimisha tatizo hili, ili baadae tuingie kwenye hukumu, au suluhu…’hapo akatulia kidogo

‘Unajua sisi kama wanafamilia, kwa kupitia vikao hivi, na sio mara ya kwanza hii, tuna jinsi yetu ya kuhukumu, au kusuluhisha migogoro ndani ta familia, na tumekuwa tukijitahidi tusiende kinyume na sheria za nchi, au sio…mnielewe hapo…’akatulia

‘Mfano mkosaji, kakosea, na hukumu yake ni kulipa alichoiba au kupoteza, tutamuhukumu hivyo, alipe…lakini kuna hukumu zitabakia kwenye mikono ya wanandoa, mfano kama hukumu ni talaka, je ni nani atamlazimisha mume kuacha mkewe wake…, hapo eeh,…sisi tutajaribu kushauri iwe hivyo kama ni lazima lakini mwishi wa siku kazi hiyo ni ya mume na mkewe, japokuwa kama kikao kitaona ni heri ya kutoa talaka au sio…na vitu kama hivyo, naomba mnielewe hapo.

‘Pia naongeza kidogo hapo samahani, kwa vile ukiangalia ilivyo, kinachotizamwa hapa ni mali, watu wamaingiwa na tamaa jinsi gani ya kumiliki mali, isivyo halali, kwahiyo tatizo hapa ni mali, sisi kama wanafamilia, tukiona kiongozi fulani hafai kwa ubinafsi wake, kama kikao kitasema mtu huyo hafai, tutampendekeza mtu mwingine au sio..ndio hukumu zetu zipo kwa mtindo huo.

‘Sasa kwa hili la familia wameturahishia, kumbe wao walikuwa na mkataba wao, ..mkataba ule halali eeh, sio huo wao wa kugushi,…’akasema akimuangalia wakili wa mume.

‘Sasa kama bado wahusika hawajaridhiana na hilo…ila sisi kama kikao tumerizika kuwa mkataba halali ni ule wa mwazo, huu wao wa kugishi hautambuliki, sasa kama wahusika wana pingamizi, sisi hatutakuwa na neno zaidi ya hapo, itabidi swala hilo lifikishwe mahakamani.

‘Sasa kama mkataba wa zamani umepitishwa…hapa hakuna hoja, sisi kama kikao, tutafuata mkataba wao, tutaona jinsi gani unavyosema mtu akikosea makosa kama hayo, ambayo yana ushahidi..au sio……’akatulia

‘Lakini kabla ya kufanya hivyo, kabla ya kufikia hapo, najua hadi hapo kuna tatizo..kuna mgogoro, kuna mtu anatakiwa kuwajibishwa kifamilia, au sio…’akatulia mwenyekiti alipoona wakili akiteta na mtu wake, wakawa kama hawaelewani, na mwenyekiti akaendelea kusema;

‘Hata hivyo kikao hiki ni cha familia, tupo wazee, wapo mawakili,..wapo watu walioenda shule…hakuna jambo litaharibika, tutahakikisha kila mtu kapata haki yake na hiyo familia itakuwa na amani, au sio, sisi wajibu wetu ni huo…’akatulia

‘Baada ya kuongea hayo, mimi kwa upendeleo kabisa, ningelipenda tumsimamishe mume wa familia aongee, ajitetee, kwa nafasi yake, na hili hatutaki wakili wake aliingilie kati, kwani kwa hivi sasa kila kitu kipo wazi, ...ukweli umedhihiri, na uwongo umejitenga...’akasema mwenyekiti, na kumwangalia mume wa familia.

‘Mume wa familia kwanza tnahitajia kauli yako je unakubali kuwa mkataba huo ndio halali mliotayarisha wewe na mke wako, kwa ajili ya masilahi yenu., pili je hayo aliyoyaongea mke wa docta ni kweli…?’

Mume wa familia kwanza alitulia kimia,…baadae akainua kichwa, akitaka kumuangalia mwenyekiti….akawa kama anawaza jambo, wakili wake alikuwa kainama tu akisoma kitu kwenye makabrasha yake..

Baadae sana mume wa familia…akainamisha kichwa, …halafu akainua tena..

NB: Naona niishie hapa


WAZO LA LEO: Ni kwanini watu hawataki kuubali ukweli hata kama wamekosea, watu huona ulimi, kuongea sana, kubishana, kujitetea , au kutetea madhambi yao ndio njia pakee ya kujisafisha, hata kama nafsi inamsuta, je kwa kufanya hivyo tunamdanganya nani…huenda tukashinda au tukapata kwa njia hiyo, je hatuoni tunakula mali ya dhuluma, tunaishi maisha ya dhuluma, tunatawala tukiwa watawala wa dhuluma, …ina maana kila chumo hapo litakuwa la dhuluma! Kiukweli mwisho wa mtu kama huyo hautakuwa ni mwema…
 
SEHEMU YA 120


Mume wa familia, akainamisha kichwa na alipoona watu wapo kimia, taratibu akainua kichwa na kumuangalia mwenyekiti,…alimuangalia kwa muda, halafu akatikisa kichwa kama kukataa, haikueleweka, kwanini anatikisa kichwa vile, anakataa kuongea ana anakataa nini, na zaidi akaendelea kubakia kimiya hakuongea, baadaye akainamisha kichwa chake kama ilivyokuwa awali, akatulia kimiya.

Mwenyekiti akabakia kaduwaa, akasema ….

‘Je mume wa familia hayo yaliyoongewa na mpenzi wako wa zamani ni kweli au na yeye kajitungia uzushi wake?’ akaulizwa mwenyekiti, sasa kwa sauti kubwa yenye mamlaka,

Mume wa familia aliendelea kubakia vile vile, kajiinamishia kichwa chake chini, kama vile hawezi kukuinua na kumwangalia mume wa familia, ambaye alikuwa bado katulia kimiya, na mwenyekiti akaongeza kuongea kwa kusema;

‘Huyo ni mtu wako, yupo kwenye moyo wako, kipenzi chako cha asili, ...asingeliweza kusema hayo aliyoyasema kama angelijua kuwa yatakuumiza, kajitosa kwa ajili yako, na kwa kuongea hivyo anatarajia mema kwako, japokuwa ni kwa kukuumiza au sio,…sasa je hayo aliyoyaongea yana ukweli, unayakubali, au ni kama yale yale ya rafiki wa mke wa familia,…?’ akauliza

Mume wa familia kimia…hata wakili wake ambaye alikuwa katulia akiangalia mbele sasa akawa anamuangalia yeye.

‘Na ujue..tunajitahidi sana kukupatia nafasi hizi, ili mwenzetu ujirudi, ujue makosa, yako utubu,…’akasema mwenyekiti.

‘Ilivyo ni kuwa kila kitu kimeshaongelewa, lakini una nafsi ya kuyathibitisha hayo au kuyakana, hasa hayo aliyoyangea mke wa docta…ya rafiki wa mke wa familia uliyapinga, sasa je na haya aliyoyaongea ex- wako, unayapinga pia, ni uzushi, hayana ukweli, toa kauli yako kama mwanaume...’akasema mwenyekiti, na hapo mume wa familia akainua uso kidogo, lakini hakusema neno.

‘Kukaa kwako kimiya inaonyesha nini, ama ni kutuzarau, au ama ni kiburi, au tusemeje, au ndio wakili wako kakushauri hivyo,…?’ akauliza mwenyekiti, na mume wa familia akaendelea kukaa kimiya, na wakili akataka kuongea, lakini akasita na kukaa kimia

Mimi nilipoona hivyo, nikaona niingilie kati, nikasema;

‘Ndugu mwenyekiti, mimi naona tusipoteze muda, kuna mengi yamesemwa na yote ni ukweli mtupu, kwa mwenye hekima, ataelewa, na kukiri kosa, lakini kwa mtu mwenye tabia yake, ataona ni yale yale,tu, na ndivyo inavyoonekana, labda kaona tunamuonea, au labda, kasingiziwa, hatujui, lakini kwanini tupoteze muda...’ nikasema.

‘Mimi nataka aongee yeye mwenyewe…’akasema mwenyekiti, na mume wa familia, akageuza geuza kichwa halafu akainamisha kichwa hakusema neno

‘Unaona….’nikasema

‘Ndugu mwenyekiti naomba niendelee kuongea,…’nikasema na mwenyekiti hakuniambia niendelee kuongea mimi nikaendelea kuongea tu.

‘Ndugu mwenyekit tuyaangalie hayo mambo kwa mapana yake kihekima zaidi…,kama unavyoona mtu anaulizwa anakaa kimia, hapa sisi sio watoto wadogo, pili anayeuliza swali hilo ni kiongozi wetu, ….baba mkwe, mtu anazarau nna kukaa kimia,…lakini hilo tuliache labda kama ulivyosema mwenyekiti wameshauriana afanye hivyo…’nikasema

‘Lakini mimi nimejiuliza sana…kukaa kwangu kimia muda mrefu nimegundua jambo, kuwa haya yote yalikuwa na maana gani, ni nani alilengwa, kwa haraka nimegundua kuwa mimi ndiye mlengwa,..sasa najiuliza ni kwanini ni mimi, ….kwasababu ya mali,? Au kuna jingine, jibu lipo wazi ndio sababu ya mali,

‘Mali zimechukuliwa kama kigezo, mengine ni kuzunguka tu, lakini tujiulize mali ni ya nani,…ukilendeleza hivyo utakwenda kuwakuta wazazi wangu, sasa kumbe mimi nilichaguliwa kama njia ya kufika kwa wazazi wangu, ili iwe ni kashfa na baadae wafanikiwe…’ nikatulia

‘Sisemi haya kwa kujitukuza, lakini ndio ukweli ulivyo,…, mali zilizotoka kwa wazazi wangu, zimewavuta watu kufanya waliyoyafanya, maana hawafanyi bure, hayo waliyoyafanya yana gharama, au sio..

‘Ni kweli wazazi wangu, walifanya juhudi hadi tukafikiwa sisi hapo tulipo…na sisi tulitakiwa tupokee kijiti au sio,..ndio maana mimi nilijaribu kumshirikisha mwenzangu, ili ajifunze, ili tuwe sambamba,…na niwaambie ukweli, hili halikuwa jambo rahisi, ..kama mnalivyoona hivi,.. ilikuwa ni kazi kubwa, kumjenga mtu wa namna hiyo nilificha kila adha nilizozipata,…sikusikiliza ushauri wa wazazi wangu...’nikasema.

‘Wakati mwingine, ilibidi mimi nigeuka kuwa kama mume wa familia, kufoka, na …na..kiukweli haikupendeza kabisa maana baada ya hapo nakaa nakujuta kwanii nimefanya hivyo, kwanini nimemfokea mume wangu…unaona eeh,,..lakini nilifanya hivyo, kwa vile mimi nafahamu,…ni kwanini nafanya hivyo,…sio kazi rahisi kama watu wanavyofikiria ..’akatulia

‘Mimi nimekulia katika familia ya hali hiyo,…familia ya kazi,…familia ambayo haina muda wa kupoteza, starehe ni kwa nadra sana, maana bado tunachuma bado twawekeza…

Niwaambie ukweli,…. japokuwa wazazi wangu walikuwa wana uwezo wao, lakini sikudekezwa kabisa..mimi nilitakiwa niishi kama wengine, nijua hali ngumu ipoje ili nikue nayo, nijifunze…, kuna muda niliweza hata kukataliwa kula, chakula kipo, lakini kwa uzembe wangu, napewa adhabu ya kukosa kula,, ilifikia hata nachapwa viboko, wakati huo nimeshakuwa mkubwa.

Wazazi wangu walianzia mbali,…nakumbuka nikiwa mdogo, niliwaona wazazi wangu wakiamuka usiku kukanda, chapati, kutengeneza maandazi kwa ajili ya kuuza kesho yake, usiku kwao ilikuwa ni kazi hiyo, asubuhi, kubeba vikapu vilivyojazwa hayo maandazi na chapo kwenye hoteli za watu, baadae ndio wakaanisha hoteli yao wenyewe, na ndio mwanzo wa kuanza kuchipukia,…..kazi kwetu ilikuwa kipimo cha utu,…starehe ilikuwa sehemu ya ziada tu, hakuwa na nafasi kwenye nyumba ya wazazi wangu…’akatulia

‘Kwa….kifupi, kazi kwetu ni jadi, hayo mnayoyaona, hizo mali, na utajiri kama mnavyouita, haukuja hivi hivi...nayasema haya ili watu waelewe wapi familia yetu ilipotokea....’nikamwangalia mume wa familia aliyekuwa bado kainama.

‘Nafahamu kabisa kusudio lao hawa wenzetu, ni kuwa kila tajiri, kila mwenye uwezo, kaupata utajiri huo kwa njia za kubumashi, kutepeli, kuiba, dhuluma… nk tukirejea zile kauli za marehemu....jamani sio kweli, ...wapo wengine, kama sisi, ..najivunia hilo, kwani mimi nimeishi na wazazi wangu, nimeona jinsi gani walivyokuwa wakijituma, mali na vitega uchumi hivyo vimetokana na jasho la wanafamilia.

‘Kiukweli inaniuma sana, nikukumbuka wapo wazazi wangu walipoanzia, halafu watu wengine wanakuja kusema sisi mali na vitega uchumi hivyo tumevipata kwa dhuluma….kiukweli inauma sana,…’ pale mke wa familia akawa anajizuia kulia.

‘Sisemi haya kwa vile…, ila nataka kuwaelezea wapi mali na vitega uchumi hivyo vilipotokea…, sio wote jamani…mnamkosea sana, mnaweka shuku zisizo na ukweli.., na kwanza sisi hatujafikia ngazi hiyo ya kuitwa matajiri, tunajitahidi tu, na mali hizo mnazoziona ni juhudu zetu, juhudi za wazazi wangu,…’akatulia kidogo

‘Kwahiyo kwa jinsi ilivyo, watu, eeh, kama mume wangu walitaka mimi nilale, nibweteke, niwe mtu wa matumzi tu,…mali si zipo, mali za baba na mama zipo, nitumie tu, je zikiisha…maana mtumie huku zinazalisha, lakini mnatumia uzalishaji duni, masoko hakuna, mnaandamwa na madeni, mtafika wapi hivyo…vizazi vyetu vitakuja kufaidika na nini…hilo hawajiulize, kwangu mimi nasema hilo haliwezekani...’nikatulia kidogo.

‘Ndio maana ilifika mahali, nikasahau kila kitu, nikasema sasa ni kazi, starehe baadaye, huenda kwa kufanya hivyo, nilimkwaza mwenzangu, akaona nadharau majukumu muhimu ya ndoa, eti mimi ni bakhili, aliwahi kuniambia hivyo, kuwa mimi ni bakhili..

Na…nimuulize tu kama nilisahau majukumu yangu ya ndoa…, hawo watoto wangelipatikana, awali nilimdekezea, si unajua kupenda, nikawa namuhenga henga, ili nimuone, mwisho wake…nikijua mwenzangu atakuja kuona umuhimu wake kama mume wa familia, nilikwenda naye hivyo,..biashara ikashuka tukaanza kuyumba,…’akatulia

‘Hali ikawa mbaya, ikanibidi niende kuongea na wazazi wangu, wakaja kutuinua tena, kwa mkopo, lakini huku wakituasa..

‘Jamani, tutainualiwa mpaka lini,..ndio maana..ikafika mahali nikaona kuna umuhimu wa kujitosa ili kulikoa jahazi…, ikawa hakuna kulala, hakuna starehe tena
Angalau tufike mahali tusema sasa tunazalisha kwa faida,ndilo lilikuwa lengo langu, hapo kiukweli sikueleweka kivitendo….!

‘Nimejifunza mengi kwa hili, na kwa kauli ya haraka haraka , ninaweza kusema, imekuwa kama mtoto akililia, wembe muache, ukimkata atajifunza, lakini pia imekuwa changamoto kwangu, kwani yote haya yaliyotokea muathirika mkubwa ni nani, ni mimi na watoto wangu...,

Ni wazazi wangu pia, ambao walikuwa wamelengwa kisiasa, na hata kiuchumi…

‘Hebu angalieni huo mlolongo mzima, kumbe haya yalikuwa yamepangwa kutoka huko kijijini hata kabla ya ndoa yangu, na ndoa yangu ikawa kama kisingizio, na udhaifu wangu wa kibinadamu ukatumiwa kama ngazi ya kutekeleza hayo yaliyokwisha pangwa…

‘Nawashukuruni sana kwa hayo,nawashukuruni sana, wote, mliokuja kwangu na nikawapa kila kitu changu, ikiwemo nafsi yangu katika moyo, nikawaona kama ndugu, kama marafiki wema, kama mume mpenzi,...lakini hii ndio faida yake, mtoto akililia wembe muache, ukimkata atajifunza. Na mimi nimejifunza, japokuwa nakejeliwa kuwa mkuki sasa umenipata ndio maana napiga ukelele, sawa…nimekubali mkuki ni kwa nguruwe….

‘Kwa hivi sasa nina machungu mengi moyoni, huenda nikitoa uamuzi wangu, naweza kuharibu, nahitajia muda wa kulitafakari hili kwa undani, ...yaliyotokea yamenifungua macho na masikio, nimejua ni nini nahitajika kukifanya…’akamuangalia mwenyekiti

‘Naomba sana,…kama yawezekana kikao hiki kiahirishwe , ili mimi niweze kukaa na kulitafakari hili jambo vizuri..na ili nikija kusema neno la moyoni, liwe sahihi.

Nina mengi ya kuja kuyasema, sasa kama ni kesho au ije kupangwa siku nyingine nitashukuru sana, ndugu mwenyekiti…

Lakini hata hivyo, leo, kabla hatujaweza kuondoka hapa, mimi mwenyewe ningelipenda kumuuliza mume wa familia, maswali machache, mbele yenu, na nataka ayajibu yeye mwenyewe kwa kinywa chake, ...bila kuficha, mwenyekiti kamuuliza kamzarau, sasa mimi kama mkewe na kama atakaa kimia hivyo basi, atakuwa kanizarau na mimi mkewe…na kwa maana hiyo, mimi nitaona sina mume, maana nini maana ya kikao hiki, ni kutatua mgogoro wa kifamilia ndani ya hii ndoa, au sio…sasa ewe mume wa familia, nataka unijibu hayo maswali....'nikasema na kumgeukia mume wa familia,

'Mimi ninayekuuliza haya ni mke wa familia nakuuliza wewe kama mume wa familia, nategemea wewe kama mume wa familia, utayajibu hayo bila kuniogopa, kama utaniogopa itakuwa ni ajabu, ...uanaume wako utatiliwa mashaka...’nikasema na watu wakacheka.

Na mume wangu hapo akaniangalia kwa macho yaliyojaa hasira, ni mimi sikujali macho yake, nikasema;

‘Swali langu la kwanza, ni swali la msingi na lenye hekima, umeshaulizwa ukazarau na mimi kama mkeo nakuuliza swali hilo tena,… je hayo yaliyosemwa na wote hasa shahidi wa mwisho aliyekuja kuthibitisha…yeye alithibitisha, na kufafanua zaidi yale yale ya shahid wa kwanza,…, je hayo aliyoyathibitisha ni ya kweli au kajitungia yeye mwenyewe?’...nataka unijibu hilo swali, kwani majibu yake, yataweza kunipa mimi mwanga,ili tukirudi tena, niwe na kauli ya hekima,…’nikatulia

Mume wa familia sasa akaonekana kama ana uhai, akataka kusema neno, na mimi nikamkatili na kusema;

‘Na kauli yangu, ya hekima…haitakuwa mbali nay ale tuliyokubaliana, lakini mimi ni binadamu, wengi tunakosea, hatuna muamala wa kusema mimi ni mtakatifu, mimi…nimeshajikomboa sitafanya dhambi, kusema hivyo tunajidanganya sisi wenyewe…

Lakini sisi wawili tulikaa pamoja tukaona kuna haja ya kuweka misingi yetu ya jinsi ya kuishi, misingi hiyo itaweza kutulinda, ili tusije kukengauka, tukajidhulumu nafasi zetu na kuja kuwadhulumu wengine ndio nikaandika huo mkataba,..sasa kwanini tuje kuuharibu tena,….

‘Tunauharibu kwa kutokujiheshimu, na kutokuamini maamuzi yetu kama watu wazima,…sasa haya kama watu wazime tumajivua nguo, kwanini tusikimbilie kujisitiri, na kujisitiri, ni kutubu, kurejea ndani na kuvaa nguo zetu, au sio

‘Wakati tunaandika hiyo mikataba tulikuwa na akili zetu timami, na tuliandika tukisema sisi,… yoyote atakayekiuka huo mkataba…, atawajibika, au sio, sio mimi, au yule akifanya atawajibika, haukuwepo huo ubinafsi,… sasa iweje mkuki huo uje kuniumiza mimi mwenyewe....’nikamwangalia mume wa familia na yeye akaniangalia kwa macho yale yale yaliyojaa hasira;

‘Sasa nikuulize wewe mume wa familia, najua sasa umeshajitambua, je unaweza kunijibu hilo swali langu la kwanza au niendelee na maswali mengine?’ nikauliza

Hapo mume wa familia, akajiweka vyema, usoni alionekana kukerwa, na ilionekana akianza kuongea hapo anaweza kuongea maneno makali sana..lakini haikuwa hivyo,

Alipoanza kuongea, akaanza kwa sauti ya taratibu, …, akasema;

‘Nilijua kuwa mwisho wa yote ni nini kinatafutwa, nilifahamu kuwa ni mtego wa panya, sawa…., nimekubali, na sina haja ya kung’ang’ania mali zenu,...’akasema na watu wakaguna, mwenyekiti akasema

‘Tulieni…mpeni nafasi huu ndio wakati wake, huenda anasingizwa, sasa atuambie ukweli wake wa mooni,…’akasema mwenyekiti

************

‘Mimi ninachoweza kusema kwa hivi sasa na huenda ndiyo wengi wanavyotaka mimi niseme…

‘Mke wangu nakuomba unisamehe sana…na sio mara yangu ya kwanza kulisema hili, nikijua kuwa nimekosa…’akatulia

‘Ni kweli yaliyosemwa na waliotangulia mengine ya ukweli, siwezi kuyakataa, au kuyapinga…nitasema nini tena..ukiaka kumuua mbwa, ni lazima kwanza umuita majina mabaya…

‘Mimi,..sijali tena, maana hatua iliyofikia, nimeshajua ni nini kitafuta…nimekubali kushindwa, nimekiri nimekosa,...lakini mke wangu, katika maisha kuna kukosa, kuna kupanda an kushuka,..hayo ni majaribu tu na kama binadamu unaweza kuyapitia, na mimi sio wa kwanza, nilijaribu kwa njia hiyo, nia ni kwa ajili ya familia yangu, hilo hamlioni kabisa....’akasema na sasa akabadili uso wa hasira na kuwa uso wa huzuni.

‘Mke wangu, nakupenda sana...nilijitahidi kufanya hivyo, kukupenda..lakini huenda namna ya kukuonyesha kwangu sivyo ulivyokuwa ukitaka wewe..

‘Hata hivyo, vyovyote iwavyo, nakuomba sana, uwakumbuke watoto wetu, watoto hao wanawahitajia baba na mama yao,…ndio maana nilifanya kila niliwezalo nionekane na mimi ni baba wa familia, niwe mkali, niwe na mamlaka…’akatulia

‘Je mimi ningeendelea kuwa hivyo, hadi lini, baba asiye na meno, jamani hili hamlioni…, lakini juhudi zangu za kuleta mabadiliko katika familia, zikaja kuvurugwa na watu wengine, ....’akatulia

‘Mimi sitaki kuwatupia hao watu wengine lawama, nafahamu haitaeleweka vyema kwa hivi sasa, nimeshavuliwa nguo, nimesha…..sina maana tena,..hata hivyo kauli yangu ni kuwa, mimi ndiye baba wa familia, na hayo niliyoyafanya, nilitaka nieleweke hivyo, kama nimekosea nakubali na mimi nimekiri kosa...’akasema nahapo akatulia…na ilionekana kama keshamaliza.

Mke wa familia, akaanza kama kucheka, akasema….

‘Hahahaha, huko ndio kukiri kosa jamani….’nikasema

‘Mhh…haya jamani, hatimaye mume wa familia anakiri kosa, japokuwa kwa shingo upande, lakini sio kutoka moyoni, kasema yeye anakubali kwa vile ametegwa kama panya, jamani, hebu angalieni huo mlolongo wote, kuna kutegwa hapa…?’ akauliza mwenyekiti akiwaangalia wajumbe

‘Ndugu mwenyekiti niache mimi niendelee naye …mume wa familia, tuambie ukweli,…na nia yeti ni wewe utujibu, sio lazima uongee kwa maneno mengi sana kihivyo, sawa upo hiari kujitetea utakavyo, lakini swali letu lilikuwa wazi, je hayo aliyoyasema shahidi aliyepita ni kweli au ni uwongo, je kazua kama yule shaidi wa kwanza…?’ nimamuuliza sasa akabakia kimia.

‘Maana wewe una watoto wangapi vile…kuonyesha kuwa wewe ni nani kijogoo, anayeweza kupanda mitetea popote pale, leo huyu kesho yule..hivi kweli ni ubinadamu huo, ni utu huo, je hayo umesingiziwa, maana hapa nakuotolea mifanio iliyo halali, hilo umesingiziwa hao sio watoto wako, je hujatembea na hao watu…’nikamuuliza.

‘Unataka nijibu nini tena hapo, umeshaongea uliyotaka kuyaongea, umeshajirizisha, sasa hapo unataka niongee nini, …nizid kujitukana au…?’akasema mume wa familia

‘Mimi au kikao, kinahitajia jibu la moja kwa moja, kutoka kwako wewe mwanaume, kwanini unaogopa,…kwa jinsi ulivyojibu ni kuwa unasingiziwa, umetegwa kama ulivyosema, huko kutegwa kuna maana gani, hebu toa kauli ya kujiamini,…’nikasema na mume wa familia kwanza alitaka kuongea baadae akaghairi, hapo mwenyekiti akasema;

‘Tunakusubiria mume wa familia,…’akasema mwenyekiti

‘Mimi nimeshajibu mwenyekiti, naona kama mnanizalilisha sasa, hizo kauli zeni sizipendi, nafahamu kuwa nimekosea, na nimeshatoa kauli yangu, lakina hizo kauli zenu ni za kunifanya mimi mtoto mdogo…na si chochote, nafikiri ni zarau, kutokana na asili yetu, kuwa labda sisi tumekulia, na kulelewa kitabia mbaya, hatupendi kazi, tuna tamaa,na kitu kama hicho…’akatulia

‘Lakini mkumbuke yoyote anaweza kupitiwa, na shetani, akaghibilka na ni ibilisi, na .....ni nimeshawaambia kuwa sikuwa na nia mbaya, kwa hayo niliyoyatenda, na hamtaki kukubali ukweli kuwa nilifanya hayo yoate kwa ajili ya kuilinda familia yangu, kwani kama nisingelifanya hivyo, hamjui ni kitu gani Makabrasha alinitishia nacho...’akasema

‘Haya sasa …mume wa familia anasema hayo aliyoyafanya sio kwa matakwa yake ni kutokana na vitisho kwa marehemu…’akasema mwenyekiti…

‘Tunataka tusikie hicho kitisho alichokutishia Makabrasha, maana kukutishia wewe ni kama alitishia familia yote hapa, je alikuambia nini, sisi tunavyojua ni kuwa Makabrasha alikutishia kuwa usipofanya anavyotaka yeye, atakuumbua kwa machafu yako uliyoyafanya, atakwenda kumwambia mke wako, na mkwe wako, au sio?’ akauliza mwenyekiti.

‘Pamoja na hayo, ...’akatulia na kutikisa kichwa kama kusikitika,

‘Hamkumjua Makabrasha nyie, hamkuwahi kuishi naye kwa karibu, yeye alisema, anaweza kuiumiza familia yangu, hasa watoto, atawateka nyara na kuwafanya wasionekane tena, ..hata wakionekana watakuwa mazezeta...hivi wewe kama mzazi ukisikia hivyo, utachukua hatua gani...’akasema

‘Hivi wewe kwa akili zako uliamini kuwa Makabrasha angeliweza kufanya hayo aliyokutishia, au alishakufahamu udhaifu wako kuwa wewe ni mwoga, ...au hebu tupe mifano hai, ambayo yeye aliwahi kuwafanyia watu wengine, ili tuamini kuwa vitisho vyake vilikuwa ni kweli...’akasema mwenyekiti.

‘Mimi nawapenda watoto wangu, nipenda familia yangu, siwezi kubahatisha kwenye familia yangu, iwe ni kweli au si kweli, iwe ni vitisho tu au ni kweli, mimi nilichotakiwa kufanya ni kile nilichoona ni sahihi, kwa ajili ya kuilinda familia yangu...’akasema.

‘Ina maana hata kutembea na wake za watu, mfanyakazi wako wa ndani inatokana na vitisho vya Makabrasha?’ akaulizwa na hapo akakaa kimiya.

‘Au labda tukuulize hili swali huenda nalo linaweza kuwa ni sababu ya Makabrasha, je ni kitu gani kilichokufanya uwe mnzizi na kuisaliti ndoa yako?’ akaulizwa

‘Ni hali iliyokuwa imenizunguka, nilikuwa nimechanganyikiwa na mambo mengi yalikuwa yakiniandama, ikiwemo hilo la mipango aliyoibuni Makabrasha, na hata hivyo, mke wangu alikuwa na kazi nyingi sana, na yeye alitakiwa awe karibu na mimi ili niweze kuyasahau yote hayo, lakini hata nilipojaribu kumvuta ili aniliwaze, niliona kama yeye ananisukumio huko...’akajitetea.

Mimi nikamwangalia kwa hasira na kusema; ‘Huo ndio utetezi wako, kuwa mimi sikuwa karibu nawewe, je uliwahi kuniambia hilo, kwa kinywa chako nikakukatalia au kukusukuma, ...?’ nikamuuliza

‘Kwa vitendo visivyo dhahiri, unaweza ukamkatalia mtu, kwa vitendo visivyo vya moja kwa moja, na mimi
kama mtu mzima nililiona hilo, kuwa hukuwa karibu na mimi na niliposema kusukuma sio kwa kusukuma kwa mikono, ni kwa vitendo, visivyo moja kwa moja...’akasema

‘Kwa matendo hayo ina maana nilionyesha hivyo kwa vile sikupendi,au ni kwa vile nilikuwa nawajibika kwa ajili ya kujiendeleza, kwa ajili ya maisha yetu ya baadaye na familia?’ nikamuuliza

‘Hapana sijasema hivyo, kuwa hunipendi, na hujawahi kunitamkia hivyo, kuwa hunipendi…., kiukweli ulikuwa unanipenda na ulikuwa ukifanya hivyo kwa ajili ya kuinua kipato chetu zaidi na zaidi, hili siwezi kulipinga, …lakini hukufanya yale yanayostahili kuonyesha upendo wa mke na mume…, ulijali sana kazi hata muda usio wake...’akasema.

‘Ina maana wakati mke wako anahangaika na kazi hadi kusahau majukumu yake ya ndoa wewe ulikuwa huna kazi , unafikiria mambo ya mke na mume….au sio, hebu fafanua hapo kidogo,… huenda kweli mke wako hakuwa na kazi kweli, alikuwa akijifanya ana kazi kwa mbinu za kukwepa majukumu yake ya ndoa, sema ukweli, jitetee?’ akaulizwa.

‘Hayo yapo wazi, kazi ni kazi, na majukumu ya ni majukumu ya ndoa, na mahali pale panajulikana, na muda wake muafaka unajulikana,...siwezi kusema alifanya hivyo kwa ajili ya kukwepa majukumu yake ya ndoa, hapana, ni kweli alikuwa akifanya kazi kiukweli, niliona kwa macho yangu, na siwezi kumlaumu sana kwa hilo…lakini kila siku, ..hata muda wa usiku, hapana….’akasema

‘Kama huwezi kumlaumu kwanini ukamsaliti, kwani ukafikia hadi kutembea na mfanyakazi wako wa ndani, kwanini ukafikia hadi kutembea na mke wa mtu,...kwahiyo huko ndio kujitetea kwako kuwa ulifikia mahali ukazidiwa, kwa vile hukutendewa haki kwenye majukumu ya kindoa au sio, ?’ akaulizwa tena na mwenyekiti.

‘Nimeshasema ndio hivyo, mimi ni mtu mzima siwezi kusema kila kitu kiuwazi zaidi, mnataka nisema nini zaidi ya hapo,…sawa na nimeshakiri kosa, mbona mnatka kuvua nguo zaidi ..’akasema hapo kwa ukali.

Mimi nikamwangalia na nikasema ;

‘Ndugu mwenyekiti, mimi nimesharizika na jibu la swali hilo, ngoja nimuulize swali la pili...’nikasema na mwenyekiti akatabasamu na akamwangalia mume wa familia, halafu akasema;

‘Haya muulize maana ni mume wako unamfahamu sana kuliko sisi, ...’akasema mwenyekiti

Swali langu la pili, ni hili, ni muhimu sana , tena sana unijibu kutoka moyoni mwako, ...maana ukinidanganya tutajua,...hili swali ni kwa ajili yangu na wake wenzangu.’nikasema na kumwangalia na yeye akaniangalia kwa mashaka, akisubiri hilo swali.

‘Je unampenda mpenzi wako wa asili?’ nikamuuliza

Ilikuwa kama kashikwa na butwaa kwa swali hilo, …kwanza akahema kwa nguvu, na akaniangalia mimi moja kwa moja kwanza, ..halafu akatabasamu…ni lile tabasamu kama nimemuuliza swali la mzaha tu, halafu kwa haraka akageuka kumwangalia huyo mpenzi wake wa asili na baadaye akamwangalia rafiki yake, yaani docta, halafu akasema;

‘Kwanini mnaniuliza swali kama hilo, ...sioni umuhimu wake kwa sasa, hapa naona mnaendelea kunitega tu, hilo swali nafahmu kabisa lina ajenda ya siri, na mimi kama binadamu, siwezi kudanganyika, niliyoyafanya niliyafanya nikijua mimi ni mume wa familia, nilikuwa na mimi nawajibika, kwa manufaa ya familia yangu, mlitaka nikae tu,...’akawa katoa macho ya hasira akimwangalia mke wake.

‘Jibu swali kama mwanaume…’akasema mwenyekiti

‘Mzee, samahani sana baba yangu kama nitakosea, ni hivi kweli kuna mtu anaweza kuja pale kwako baba akakupangia jinsi gani ya kuishi,wewe umeshaoa au sio, wewe una mke wako,halafu watu wengine waje na sera zao...au ni kwa vile mimi...’akasema

‘Una maana gani hapo…?’ akauliza mwenyekiti.

‘Nimekuuliza hivyo ili unielewe,…nimekuuliza hivi, baba ulipomuoa mama, familia ya mama waliwahi kuja kwako na kuwapangia jinsi gani bora ya kuishi na familia yako...mbona hayo hamyafikirii, kwanini nyie mnakuja kutupangia sisi jinsi gani ya kuishi, wajumbe hivi hamuoni hawa watu walivyo eeh...’akasema huku akigeuka kumwangalia mama yangu.Na mama akawa anamwangalia tu.

Alipoona wajumbe wapo kimia

‘Kiukweli haya sio maswali ya kuniuliza hapa mbele ya kadamnasi, ni kunizalilisha tu,ni kunitega tu ,sitaki maswali ya namna hiyo, nooh, now its too much...naona sasa mnataka kunikalia puani, mumeshanizalilisha vya kutosha, sasa nasema basi, amueni mnalolitaka....’akasema kwa hasira huku akisimama na huku anamwangalia mwenyekiti akiwa ametoa macho.

‘Huna haja ya kukasirika hivyo, na hoja uliyotoa, au kama ni swali uliloniuliza, halina msingi, ni kuonyesha jinsi gani usivyokuwa makini na ndoa yako,...kwanini tumefikia hapa, ni kwasababu umekiuka sheria za ndoa...hatukuja kuingilia ndoa yako, tumekuja kusikiliza mashitaka ....usitake kuturudisha nyuma....'akasema mwenyekiti.

Mume wa familia akatulia na mwenyekiti akasema;

'Na hilo swali kauliza mke wako, anataka majibu, na ana maana yake kukuuliza hilo swali,kwa wenye hekima wanaelewa ni kwanini kakuuliza hivyo, hatumtetei, bali mimi kama mwenyekiti nimeona hekina ya hilo swali…’akasema mwenyekiti


‘Kwahiyo unataka mimi nijibu hilo swali…?’ akauliza mume wa familia

‘Ndio, jibu swali …baba, usikwepe mada kwa jaziba, jaziba hapa hazitakusaidia kitu,hilo swali hata mimi naona lina umhimu wake, ili kubainisha ukweli wako ndani ya moyo wako....jibu kama ulivyoulizwa…je ni kweli unampenda mchumba wako wa asili, kwanini hujiamini…’akasema mwenyekiti, na mume wa familia akainama kidogo, na watu walifikiria hatajibu, lakini baadaye akainu akichwa na kusema;

‘Kwa hali iliyofikia naona kama mnanilazimisha niseme hata yale yasiyostahili, sawa mimi nitasema ili muweze kufanya mnayotaka, sitajali tena..nitajibu kama ifuatavyo....,’akatulia

‘Kiukweli hakuna asiye-elewa jibu la swali hilo, japokuwa nafsi itatamani kusema vinginevyo, nakubali nimeshakubali kosa, nakubali kuwa na sisi kutokana na umasikini wetu, tulikuwa katika harakati za kutafuta maisha bora, na njia tuliyoona ni sahihi ni hiyo, kwa vile tulikuwa na mwalimu wetu na yeye kwa kipindi hicho tulimuamini, ..hatukuwa na njia nyingine...’akageuka kumwangalia docta.

‘Docta ataweza kunisaidia hilo, kuwa moyo wa binadamu unakuwa na kitu kikishanasa kwenye moyo, inakuwa vigumu kukiondoa, kutegemeana na mazingira,...tunaweza kujidanganya, tunaweza kujitahidi, lakini kama kitu hicho kipo, kinaonekana kila siku, ..hutaweza kukisahau,…’akatulia

‘Na huenda hilo ndilo kosa lililotokea,...kama mwenzangu angeliolewa mbali kabisa, tukawa hatuonani, huenda tungalisahauliana, lakini ukumbuke kuwa nyuma yetu alikuwepo Makabrasha, anataka tutimize ahadi zake,..na alifanya vitisho vya kila namna hilo hamuwezi kuliona kwasasa… ‘akatulia

‘Jamani mitihani yake ilikuwa mingi , lugha za hadaa, ili tu tuweze kuhadaika,…mtu aje kwako kila siku anakuelezea lugha za kukutamanisha, eeh,..wewe ni mwanaume wewe…ndio mimi kama mtu mzima nilitakiwa niyapime kwanza hayo.lakini nitawaambia nini ili mnielewe...ni vitu ambavyo kama hujakutana navyo huwezi kuelewa...’akasema na kutulia na mwenyekiti alipoona katulia akasema

‘Swali bado lipo pale pale...hujalijibu kama linavyotakiwa kujibiwa, je unampenda mpenzi wako wa asili, au tuulize hivi bado unampenda mpenzi wako wa asili au ulikuwa ukimtumia tu, ili upate yale uliyokuwa ukiyataka,....?’ akaulizwa na mwenyekiti.

‘Umeshasema mpenzi au penzi la asili,...hilo kwa wengi, wanaolifahamu halifutikia,kuna watu walikuwa na wapenzi wao wa asili, lakini hawakuoana, wakaenda kuoa wengine, lakini moyoni bado ule upendo upo, ...siwezi kudanganya, nampenda, ...’akasema na kutulia kidogo.

‘Lakini nilishaoa…na mapenzi hayo yalikuwa ni ujana, ni mapenzi ya asili tu, kama unavyosema,…mimi sasa nina mke, kwahiyo nafasi ya upendo wake kama mpenzi wa asili inafichika, unabakia upendo kwa mke wangu..

Sasa mimi siwezi kulikana hilo,…upendo wangu na mwenzangu niwa asili, upon a utendelea kuwepo,…lakini kwa nafasi yake, iliyojificha, nafasi iliyo wazi ni upendo wangu na mke wangu, nampenda sana mke wangu ...ndio maana nikamuoa,...’akasema.

‘Hujaulizwa kuhusu mke wako, kuwa unampenda au la, vitendo vyako vimeshajielezea,swali uliloulizwa ambalo ni muhimu kwako kulijibu ni je bado unampenda mpenzi wako wa asili, ...au hayupo tena moyoni kwako, ikiwa na maana ulikuwa unamtumia tu kukamilisha mambo yako....?’ akaulizwa swali hilo tena.

‘Nampenda, sijasema kuwa simpendi, sio kweli kuwa nilikuwa namtumia tu,upendo wetu haujafutika, ila ni kwa upendo huo wa kiasili, kwa hivi sasa nina mke, kwahiyo mpenzi huyo wa zamani hana nafasi sawa kama ilivyokuwa ....ninaweza kusema hivyo, sina zaidi....’akasema na kuinama chini.

Mwenyekiti, mimi nimeshapata jibu la swali hilo, naomba nieleweka hivyo,...’nikamwambia mwenyekiti na kumgeukia mume wa familia, nikasema;

‘Nashukuru kwa jibu lako hilo, nimekuelewa, kama binadamu hayo yapo...siwezi kuyapinga, lakini mlolongo mzima unajieleza, dhamira yenu, ipo wazi, ....

Mimi nimekuuliza maswali hayo kama nyongeza tu, ili kusikia kauli yako kutoka kwenye kinywa chako mwenyewe, kwani wenzako walishatamka yao kutoka moyoni, wewe hukupenda kufanya hivyo kwa hiari yako mwenyewe, mpaka shinikizo la ushahidi, sawa, hiyo ndio hulka yako hatuwezi kuigeuza..., sio shida, nimeshakuelewa, ....’nikasema an kumgeukia mwenyekiti.

‘Ndugu mwenyekiti, mimi naona tufunge kikao, ili kila mtu aweza kuyafikiria haya yote yaliyoongelewa hapa, na wanasheria, wayafanye kazi zao kisheria,

Ila bado mimi nasisitiza, nyie kama watu wazima, wajumbe kama watu wazima walioenda shule, nawaomba hili jambo tukae nalo tulitafakarikwa kina, mtusaidie kwa hekima zenu…tusilichukulie kijaziba…’nikatulia

‘Nayasema haya kwa vile sote ni watu wazima,…tuna familia , tuna watoto, tunakuza, je haya yalitokea tufanyeje,..tusaidiane kwa hilo…kabla mimi sijaweza kuyasema ya kwangu,…tuziangalia familia zetu,…tuangalia maisha yetu, tuiangalia jamii, je haya yalitokea tufanye nini,..,...nafikiri tukikaa tukitafakari tutaweza kuja kwa majibu mazuri,…

Sasa kwa niabaya yangu nay a familia yangu, samahani sana kuwasumbua wazee wetu, majirani zetu, marafiki,… nafahamu mlihitajika kupumzika, lakini hili pia ni jukumu lenu, kama wazazi, naowaombeni tena mkae mtumie hekima zenu, ili muone tutalitatuaje hili tatizo…kwahiyo nawaombeni tukutane tena siku nyingine…’nikasema na mwenyekiti akawa sasa anaangalia saa yake..

‘Ila kiukweli, mimi napenda kusimamia kwenye haki na ukweli…na sijajua maamuzi yangu hadi hivi sasa, akili bado imeganda, sio jambo rahisi kama mnavyoliona nahitajika kutafakari kwa kina ….naombeni mnielewe hapo....’nikageuka kumwangalia mume wangu.

Yeye sasa alikuwa akiniangalia mimi nikiongea kwa macho yanye kutoa huruma, lakini kwa muda huo sikuweza kuiona huruma yake zaidi ya kuona jambo jingine akilini mwangu.

Nikageuka kuwaangalia wanasheria wetu,..walikuwa wakiandika andika mambo yao, na baadae nikageuka kuwaangalia wale walioitwa marafiki zangu…huwezi amini kila niliyemuangalia nilikuwa simuoni yeye, naona taswira nyingine kila mmoja kwa uhalisi wa fikira zangu, halafu nikageuka kumwangalia mwenyekiti, na kuendelea kusema;

‘ Basi ndugu mwenyekiti, kwa ruhusa yako,…sijui kama tutaweza kuendelea na ajenda nyingine mimi siwezi kukuingilia, ila kwa hili letu naomba tupatiwe muda kwanza..’nikasema

‘Mnahitajia muda gani…?’ akauliza mwenyekiti akituangalia sisi wawili

‘Hata kesho tunaweza kuitisha kikao, kwa …nafasi za wajumbe, labda muda gani ni wao wasema..kiukweli mimi hapa, akili yangu hapa haifanyi kazi tena,tatizo ni kuwa kuna wale wa kusafiri,..na kama ulivyosema kuna watu wa usalama wapo nyuma yetu, sasa sijui.... ‘nikasema

‘Hilo la watu wa kusafiri na watu wa usalama niachie mimi…’akasema mwenyekiti.

‘Basi kama ni hivyo, sisi tutakusikiliza wewe, au wajumbe mnasemaje..?’ nikauliza

Wajumbe wakajielezea kila mtu kwa kauli yake, lakini ikaonekana kuwa wajumbe wapo tayari kwa hilo, ila muda ukawa ni tatizo.

‘Sawa mke wa familia, lakini nakuonya, usiniingilie uenyekiti wangu,...’akasema na kuangalia saa yake, halafu akageuka kuwangalia watu, akasema;

‘Ni kweli, nikiaangalia saa muda umekwenda sana, na kuna watu wapo hapa, japokuwa wanahusika kwa namna moja au nyingine, lakini wanakazi zao, kuendelea kuwachosha hapa ni kuwatesa, yupo docta hapo, japokuwa kaniambia yupo mapumziko, lakini anahitajia kupumzika, wapo mawakili wetu, na kulikuwa na watu wa kusafiri kesho, tunaomba, ...kama ilivyoombwa, waahirishe safari zao...’akasema na kumwangalia mke wa docta, na mke wa docta akasema;

‘Kwangu haina shida, nitaangalia, na muelekeo ulivyo, kama nilivyokudokezea..’akasema na mwenyekiti
akamwangalia kwa mashaka, halafu akageuka kuangalia wajumbe huku akisema;

‘Kwa upande wa binti yetu wa kufikia..oooh, hilo nitaongea na mwenzangu, tutangalia kama inawezekana kuahirisha hiyo safari yake, maana alishajiandaa kuondoka, hata hivyo kwa vile ni muhimu sana na inagusa hatima yake na mtoto wake, tutaliangalia hilo, na nitawajulisha kesho asubuhi na mapema kama kikao kipo au tupange siku nyingine

‘Hata hivyo wasi wasi wangu ni kwa watu wa usalama, nahitajia kupata kibali chao, hili tatizo sio la ndani ya familia tu, tatizo letu limegusa na maswala ya kijinai, ni muhimu sana mkalielewa hilo, kwahiyo kila tunalolifanya kama familia, tunahitajika kuwajulisha wenzetu wa usalama, ili tuweze kusaidiana nao, ndio jukumu letu kama raia wema,...kwahiyo kwa hili lipo nje ya uwezo wetu maamuzi yao yanaweza kuathiri muda wa kikao…hatujui…

‘Kwa hivi sasa tunavyoongea hapa, wao , watu wa usalama wapo kazini, wanahangaika kumtafuta muuaji wa Makabrasha, msifikiri kifo chake kimefukiwa na mchanga, hapana, wanawajibika, usifikiri umesalamika kama unahusika, kifo cha mtu kinamuandama mtendaji hadi siku anaingia kaburini,

‘Na kwa taarifa tu, wao wamesema wao tayari kumnasa muuaji halisi. Anaweza akawa miongoni mwetu, hatujui, kwani kafanya hilo tendo kwa ujanja wa hali ya juu....’akakatiza mazungumzo, kwani simu yake ilikuwa inalia, akaangalia mpigaji, akawaangalia wajumbe, halafu akasema;

‘Samahani subirini kidogo niongee na watu wa usalama, naona ndio hao wananipigia huenda kuna amri nyingine,...subirini kidogo msiondoke....’akasema huku akipokea hiyo simu...

NB: Haya tunasubiri hukumu..


WAZO LE LEO:Jehivi kweli kuna kisingizio cha kuisaliti ndoa yako? Je unaposalitiwa au kusaliti ndoa yako kama mwanandoa unahitajika kufanya nini?. Ni maswali madogo lakini yenye mambo makubwa, wewe kama mwanandoa kama mwenzako kaislaiti ndoa yenu mtafanya nini..


Toa maoni yako hapa…


Kikao cha hitimisho hakikufanyika siku ya pili kama ilivyopangwa, kwani siku ile ya hicho kikao cha mwanzo tulipomaliza tu,polisi walifika kabla watu hawajatawanyika, na kuwakamata mume wa familia, mpenzi wake wa asili, na mdogo wa mume wangu ambaye walishamkamta mapema. Polisi walisema sababu za kukamatwa kwao ni kuisaidia poilisi kutokana na kifo cha Makabrasha.

Kesho yake, mimi na Docta, tulikwenda kituo cha polisi waliposhikiliwa watuhumiwa hao. Tulipofika hapo tukaambiwa mke wa docta hayupo kwenye kituo hicho, kapelekwa kituo kingine kwa sababu za kiusalam, kwahiyo docta akaondoka kuelekea huko alipo mkewe.

Hata hivyo docta alitaka kuongea na rafiki yake kabla hajaondoka. Polisi walikuwa wagumu kuturuhus kuongea na huyo mtu hata pale alipofika wakili, ambaye alitakiwa kushughulikia dhamana ya huyo mshukiwa.

‘Mume ambiwa hao watu wameshikiliwa kuisaidia polis,….’akasema polisi

‘Lakini mumemshikilia huyo mtu zaidi ya masaa 24, tuna haki ya kudai huyu mtu aachiliwe au mtuambie kashikiliwa kwa kosa gani ili tufanye taratibu za dhamana…’ikawa ni mabishano ya polis na wakili.

Kiukweli masaa mengi yalipita, tukiendelea kupigwa danadana, kila tuliyemuuliza alisema yeye hahusiki, mpaka ikabidi sasa kuomba kuonana na mkuu wa kituo hicho, ambaye alisema;

‘Hawa watu tumewakamata kwa ajili ya kuisaidia polisi, hatujawakamata kama wa halifu, tuna maana yetu kubwa kufanya hivyo, kwahiyo hamuhitajiki kuwawekea dhamana...tafadhali mtuelewe hivyo..’akasema huyo mkuu.

‘Lakini dhamana ni haki ya mtu yoyote...’nilijitetea, sikufika na wakili wetu kwa vile mume wangu alishamkataa, wakili tuliyekuwa naye ni yule aliyekubalika na mume wangu.

‘Sikiliza niwaambie, hawo watu wapo hatarini, kuna tetesi, na sio tetesi, ni kweli, kuwa kuna watu wanataka kuwauwa jamaa zenu hao, kwa vile wanafahamu mengi kuhusu kifo cha Makabrasha, ....hivyo ndivyo ninavyoweza kuwalezea, na kama mna akili ya kulifikiri hilo, na kama mnawajali wenzenu hao mtaondoka na kusubiria…’akasema huyo mkuu .

‘Kama ni hivyo, basi mnaweza kuweka ulinzi nyumbani kwa hawo watu, sio kuwaweka rumande hamuoni kuwa sehemu hiyo mliyowaweka sio nzuri, kiafya...’akasema docta.

‘Ni kwa muda tu,…pamoja na hayo tulikuwa na maswali machache tumewauliza, tatizo hawajataka kutoa ushirikiano, ni kwa usalama wao, na wakitujibu vyema, ili tuweze kuyabaini mengine, hata leo wataondoka…’akasema

‘Kwahiyo kumbe sio kwa usalama wao, si ndio umesema hivyo awali…’nikasema

‘Ni kwa usalama wao, na hayo maswali ni katika kutuwezesha kujua mambo mengine zaidi ya kuwezesha kuwabaini hao watu walio na nia mbaya ya kuhatarisha usalama wa raia…’akasema.

Baadae baada ya kusihi sana, ndio tukapata muda wa kuongea na mume wangu, na mdogo wake, wote walikuwa kwenye kituo hicho, hutaamini, mume wangu hakutaka kuongea na mimi kabisa, akidai kuwa mimi nimetumia mbinu ili tuachane naye, sikujali sana, kwahiyo akawa anaongea na docta tu, na hata nilipomsalimia hakuitikia. Walipomaliza kuongea na docta, nikamwambia;

‘Hamna shida, tutaonana ukitoka, nina imani tutayamaliza haya mambo kwa amani, ..’nikasema

Na yeye hakusema chochote zaidi ya kuniangalia kwa hasira.

Na tulipotoka hapo tukaelekea kumuona mke wa docta,na Mke wa docta hakuonekena na wasiwasi au kuonyesha kinyongo chochote, zaidi ya kujiona yeye ni mkosaji,mbele ya mume wake, na tuliongea kwa pamoja na tulipomaliza kuongea haya na yale, muda ulikwisha,na wakati tunataka kuondoka, mke wa docta akamshika mume mkonona kusema;

‘Samahani sana docta,...utanisamehe sana, ...'hakutumia neno ‘ mume wangu’, nikajiuliza kwanini, lakini sikutaka kuyaingilia kwa undani.

'Nafahamu sana, mpendwa, jinsi gani nilivyokuumiza, lakini natumai umenielewa, nataka uanze kuizoea hii hali, ya kuwa mbali na mimi,maana nikitoka hapa, nataka nikaanza maisha yangu mengine, sitaki kitu kinachoitwa mume..’akasema na kuniacha mimi njia panda, kumbe wao wameshafikia hapo...

‘Hayo sio muhimu, kwa sasa , cha muhimu ni wewe kumalizana na hili hapa, na mimi nipo pamoja na wewe, hadi mwisho wa hili, na tutaongea vyema haya yakiisha, ...’akasema docta.

‘Hili sio kubwa sana ,na hakuna cha kuongea na wewe, tumeshayamaliza, mimi kinachonikwaza ni haya yaliyotokea huko nyuma, na sitaki kuja kumuumiza mtu mwingine tena, nataka kuanza maisha yangu nikiwa huru...’akasema.

Hapo nikamwangalia mdada huyu kwa makini, nikimuona kama mmoja wa watu walioniharibia ndoa yangu, lakini sikuwa na kinyongo naye, kwani kwa upande mwingine nilimuona ni mdada jasiri,…

Na wakati tunatoka tutakutana na rafki yangu, kaja kumtembelea mke wa docta, akanisalimia, na mimi nikamuitikia kwa mkato, sikutaka kuongea naye sana.

‘Bosi hujanijibu barua yangu, sijui kama natakiwa kazini au mkataba wangu mimi na wewe umeshakwisha ....’akaniuliza.

‘Yote hayo tutayajua siku ya kikao cha familia, kwa hivi sasa siwezi kukujibu lolote, endelea na shughuli zako binafsi tu, …maana ajira kwangu ilikuwa ni kwa pale ni kikuhitajia, au sio, kwa hivi sasa sina kazi ya kukuhitajia wewe...’nikasema na sikutaka kuongea naye, nikamuacha akiwa kaduwaa.

Docta akaja, kwani nilimuacha akiongea na mke wake na alipokutana na rafiki yangu wakawa wanaongea na mimi nikatangulia kwenye gari, kwani tulikuja kwa kutumia gari lake, na alipokuja, akaniambia;

‘Rafiki yako anasema nimsaidie kumuombea msamaha, hasa kwa hayo aliyokutendea,...na mimi natimiza wajibu, nakuomba sana, umsamehe rafiki yako, kwani aliyoyafanya aliyafanya kwa vile ulimshauri afanye hivyo…’akasema

‘Una uhakika na kauli hiyo…?’ nikamuuliza

‘Ndivyo alivyoniambia…yeye kasema kama alivyosema kwenye kikao, yeye hakujua kuwa itakuja kuwa hivyo, anakuomba sana umsamehe mrejee urafiki wenu kama zamani, kwani wewe unakuona kama dada yake mlezi, na kukukosa wewe ni kama kumkosa mlezi wake katika maisha..’akasema

‘Hiyo kauli ndio itanifanya hata nisiongee naye, mimi nilimshauri akazini na mume wangu, ina maana mimi sina akili..achana naye, na sitaki kabisa kusikia neno rafiki yangu, sio rafiki yangu tena..’nikasema.

‘Ina maana hata mume wako hutamsamehe...?’ akaniuliza.

‘Nikuulize na wewe swali hilo, je na wewe utaweza kumsamehe mke wako kwa hayo aliyokufanyia maana sote tupo njia moja..nashangaa kauli zenu, ina maana mumeshaachana tayari?’ nikamuuliza.

‘Mke wangu kachukua maamuzi yake yeye mwenyewe, sikuwa nimeshafikia maamuzi ya kuachana naye, japokuwa kitendo alichonitendea, nisingeliweza kuishi naye kwa amani…’akatulia

‘Kumbe…’nikasema hivyo kabla sijaendelea kuongea, yeye akawa anaendelea kuongea kwa kusema

‘Hata hivyo nilishamsamehe, na yeye mwenyewe akasema hataweza kuishi na mimi tena, akaniomba na sio kuniomba , akasema tupeane talaka, haraka iwezekanavyo, na hataki hilo tuliongelee kwenye kikao, yeye mwenyewe ataliongea kama ikibidi,...’akasema.

‘Na wewe ukakubali kirahisi,…kwa kukubali kwako kirahidi hivyo, inaonyesha kuwa moyoni mwako ilikuwa hujamsamehe, hukutaka kuonyesha dhahiri kama mimi ninavyoonyesha,…au sio..?’ nikamuuliza.

‘Nilijaribu kumshawishi, na kumwambia kuwa mimi kama docta nafahamu udhaifu huo, nipo tayari kumsamehe, na tutajaribu kuona kama maisha yanaweza kuendelea, na hata kama ni kuachana tusifanye haraka hivyo,…..lakini kakataa kata kata, nikaona ni bora iwe hivyo, ….’akasema

‘Je na wewe una umauizi gani juu ya mume wako...?’akaniuliza.

‘Mimi maamuzi yangu yatasikiwa kwenye kikao, kwa hivi sasa sina la kusema, na leo natakiwa kukutana na wazazi wangu,...sijui wameniitia nini...nahisi ni kuniuliza swali kama hilo, na kwa hali ilivyo, nahitaji muda wa kufikiri sana, hasa nikiwaangalia watoto, watoto kwa ujumla....’nikasema nikikumbuka kuwa wazazi wangu walinitaka niwe na kikao nao, wakasisitiza kuwa ni muhimu sana.

‘Ni kweli katika maamuzi yako fikiria sana watoto, sio kwamba nataka ufanye hivyo, kwa ajili yule ni rafiki yangu, hapana, na siwezi kuchukua hiyo hali nikakushinikiza uachane na mume wako, ili turejeane…’akasema

‘Turejeane…!!’ nikasema kwa mshangao

‘Nasemea hivyo kihisia…unajua sisi sasa hivi ni watu wazima, maamuzi yetu yanatakiwa yawe kiyoo cha watoto wetu,….’akasema

‘Ni kweli ndio maana , nataka maamuzi yangu nitakayofikia, yasikiwe na kila mtu, sitaki kuyaongea pembeni, …’nikasema

‘Sawa ila kwa vyovyote iwavyo, ukumbuke mimi nipo na wewe… na kiukweli mimi nakiri moyoni kuwa hatujachelewa bado….mimi nakuomba sana, kama inawezekana turejeshe urafiki wetu wa zamani...’akasema na kunifanya nishituke na kumgeukia.

‘Urafiki upo, mimi sizani kama tulikuwa maadui…’nikasema

‘Mhh…sio wa kihivyo, nataka ule wa kuelekea kwema, hata ikibidi tumalizie pale tulipooshia….’akasema

‘Hahaha,...wewe una akili kweli, ina maana wewe bado kwenye akili yako unaniwazia mimi, acha mzaha huo, hayo yalikuwa zilipendwa na kama utaachana na mke wako nakushauri, tafuta mwanadada, ambaye anakustahili, mimi tena, ni mama watoto, sikufai…nahitajia kukaa na watoto wngu tu…’nikamwambia.

‘Kwangu mimi wewe ni mwandada, mrembo, ....hata kama itakuwaje, ...naweza kusema mimi na wewe tuna pendo la asili, kama alilolisema mume wangu na mke wako, kumbe hata sisi ni hivyo hivyo...’akasema.

‘Hapana, ..nakuomba sana, usije ukafanya makosa hayo, tafuta msichana mrembo umuoe, hilo kwangu halipo nafsini kabisa, na wala usipoteze muda wako, tafadhali unielewe, tutaendelea kuwa marafiki hivi hivi na huyo utakayemuoa, atakuwa wifi yangu...’nikamwambia.

‘Kwanini nimtafute msichana wakati mimi sio kijana mdogo,...mimi ni mtu mzima, ni vyema nioe mwanamke anayeendana na mimi, na wewe ndiye chaguo langu...’aliposema hivyo

Nikageuka kuangalia pembeni, sikutaka mazungumzo kama hayo, nilikuwa na mambo mengi kichwani ya kufikiri, nikamwambia;

‘Tuyaache hayo mazungumzo kabisa, na nakuomba tukikutana tuongee mambo mengine sio hayo,hapa nilipo ninamawazo ya familia yangu,nina mawazo ya maamuzi ya busara kwa hili lililotokea na sitaki nichukue maamuzi kwa kishawishi kingine, nataka nichukue maamuzi kwa utashi wangu, na kwa manufaa ya familia...’nikasema.

‘Hamna shida, uamuzi wowote utakaochukua nipo pamoja na wewe, mimi ni rafiki yako wa ukweli...’akasema na tukawa tumefika nyumbani, mimi nikaingia kwangu na kujiandaa kukutana na wazazi wangu.

***********

‘Hebu tuambie binti yetu umefikia maamuzi gani, ..?’ lilikuwa swali la kwanza kutoka kwa baba

‘Baba siwezi kuwajibu hilo swali kwa sasa, ingelikuwa ni uwezo wangu , na maamuzi yangu mwenyewe, ningekuwa na jibu la moja kwa moja, lakini kuna mambo mengi natakiwa kuyafikiri, hasa watoto....’nikasema.

‘Swala la watoto, tulishakuambia, sisi tupo nao, na hata wakija hapa hawakumbuki kabisa maswala ya baba, ndio maana tumewazoesha kila wakitoka shule waje huku, wewe hufahamu ni kwanini tulianzisha utaratibu huo...’akasema mama.

‘Mama, ni rahisi kusema hivyo, ....lakini, mkumbuke yule alikuwa mwanandoa mwenzangu, na nisije nikachukua maamuzi ya haraka, hata nyie mkaja kunilaumu, naombeni muda, na maamuzi yangu nitakuja kuwapa kwenye kikao,...’nikasema.

‘Hicho kikao si mpaka huyo mumeo atoke huko jela, je ikionekana kuwa kweli ndiye aliyemuua, ...kwahiyo mpaka amalize kifungo ndio utaweza kutoa hayo maamuzi yako...?’ akauliza mama, nilimuona mama akishabikia sana nitoe maamuzi yangu, ambayo sikutaka nichukulie haraka, nikasema;

‘Wazazi wangu nawaombeni sana, mvute subira, mimi nipo tayari kumsubiria hata afungwe miaka kumi, huo ndio msimamo wangu....’nikasema na baba akasema;

‘Unajua hata mimi nimelifikiria sana hilo, nimeliangalia katika upande mwingine, nikawaza je ingelikuwa mimi nipo kwenye nafasi hiyo ningelifanya nini…’akasema baba

‘Ungelifanya nini…?’ akauliza mkewe

‘Sio sahihi wawili hawa kuachana kwa kwasasa…’akasema, na mkewe akabakia mdomo wazi,..

‘Leo hii unasema hivyo, unanigeuka tena…’akasema mkewe

‘Kiukweli, sio sahihi kumshawishi binti yatu afanye hivyo, hasa baada ya kumuona mume wake pale kwenye kikao akifanya juhudi kuitetea familia yake, hii ni konyesha kuwa kabadilika, na keshajifunza, na kwa hayo aliyokutana nayo keshabadilika na sasa atakuwa mume mwema....’akasema baba na kunifanya nimuangalia mara mbili, sikutegemea yeye kutoa ushauri kama huo.

‘Eti nini, hivi kweli, baba nanihii, unamshauri mtoto wako hivyo, amrudie huyo mtu baada ya yote hayo yaliyotokea, kwanza ulimsikia mwenyewe, huyo mume wake akitamka mbele ya watu kuwa bado anampenda mpenzi wake wa asili,…’akasema mama

‘Ndio nilimsikia sana , lakini ile kauli haina nguvu mbele ya mke…’akasema babaa

‘Mhh kwa hiyo hata kama watayasawazisha hayo yaliyotokea na binti yetu akafanya makosa ya kumsamehe mwenzake, ajue kuwa anaishi na gogo, ni sawa na gogo, maana mtu upo naye, lakini mawazo yake yapo kwa mwingine, huyo mume wake ataendelea kuiba nje tu, wataendelea kuwa na mapenzi yao ya siri na mpenzi wake wa asili , na ndoa yao itakuwa haina raha...’akasema mama.

‘Haitaweza kutokea tena hivyo, huyo mume atakuwa kama mtu aliyeumwa na nyoka, hataweza kuyarudia tena hayo makosa, hilo nawahakikishia, ila hayo nayasema kama mimi, kama nionavyo mimi,hata hivyo, binti yetu..’akasema baba

‘Hata hivyo sio kwamba nimesema hivyo kukushauri ufanye nitakavyo mimi, hapana, maamuzi ya hatima yako, yapo mikononi mwako, tunakuachia wewe mke wa familia,uamue mwenyewe, mimi nimeshakuona kuwa unaweza kufanya maamuzi yenye busara kwa manufaa yako na ya familia yako, unaweza, na sio busara sisi tukikuingilia ....’akasema baba.

Mimi nikawaangalia wazazi wangu kila mmoja kwa nafasi yake, nikaona kweli sasa wazazi wangu wamenielewa, na wapo tayari kunipa nafasi ya kufanya kile ambacho nimekuwa nikikiwaza, na hapo nikasema;

‘Wazazi wangu nimewaelewa, sana, ndio maana nahitaji muda wa kwa peke yangu kulitafakari sana hilo jambo, nisingelipenda kuchukua maamuzi ya haraka haraka, nafahamu kabisa mume wangu na mwenzake , huyo mpenzi wake wa asili wanapendana sana

‘Lakini pia huyo ni mume wa ngu wa ndoa,..japokuwa ukichunguza kwa makini ndoa ni kama haipo, sijaulizia upande wa dini, maana ndoa yetu imesimikwa kwenye imani ya dini, je imani ya dini inasemaje..

‘Hata hivyo pamoja na hayo, mimi sitaki kuja kuwanyima watu haki zao,…kwa hayo na mengine , nahitaji muda sana wa kutafakari kwaa mapana yake,..kama alivyosema baba, huyu mtu anaweza kujirudi na kuona makosa yake, na akawa mume mwema, lakini kuna maswala mengine, ya familia na maisha yao ya baadaye, nini watoto watajifunza kutoka kwake, na vitu kama hivyo ....mimi mwenyewe nahitaji kulihakiki hilo...’hapo nikatulia.

‘Pengine katika maamuzi yako unaweza ukawa na wasiwasi kuwa watoto hawatakua katika maisha ya raha, kisaikolojia wakimkosa baba yao wa kuwazaa, au una wasiwasi gani binti yetu, mimi nataka nikusaidie katika maamuzi yako?’ akauliza mama.

‘Mama hilo ni moja ya jambo linalonipa shida, lakini..mmmh, ngoja nawaulize wazazi wangu, kwa uzoefu wenu, tabia za wazazi kwa watoto wao, zinaweza kurithiwa?’ nikauliza.

‘Hilo ndilo tulilokuitia, kabla ya kulizungumzia hilo tulitaka tusikie kama una maamuzi yoyote, ...sasa ngoja tukupe shule kidogo ya mambo hayo, unafahamu, ni muhimu sana, kama wazazi, ni muhimu sana kwa wale wanaotaka kuoa, au kuolewa kuangalia maswala haya kizalia…akasema baba

‘Hatutaki kurejea nyuma kuwa tulikukanya nk…lakini kwa hili wengi hawalijali kwa sasa, wanaona watu wakioana litajipanga lenyewe kutokana na jinsi mtakavyoishi...kwani sasa hivi jamii zinaitwa zimestaarabika, watuy wanakutana wanabadilika kutokana na mazingira,…’akasema baba na kumwangalia mke wake, na mke wake, akasema;

‘Mueleweshe binti yako aelewe vyema hapo..., lakini sio kumshauri amrejee huyo muhuni, mlevi na muongo, hizo sio tabia nzuri, zinaweza kuwarejea watoto....watoto wenu wanaweza kuziiga hizo tabia mbaya, watarithi machafu ya wazazi wao, ni muhimu sana hilo...’akasema mama.

‘Ina maana watoto wangu watakuwa na tabia kama ya baba yao?’ nikauliza

‘Tutakujibu hilo kwa mfano hai, angalia watoto waMarehemu Makabrasha, chukua watoto wake hao wawili kutoka kwa mama wawili tofauti, wenye tabia mbili tofauti, huyo mmoja mkubwa, aliyetelekezwa na baba yake, ....mama akawa anaishi kijijini, angalia tabia zake zilivyokuwa, yeye kwa vile aliishi muda wote na mama yake, na familia ya mama yake, akawa kachukua tabia kutoka kwa mama yake, na wazazi wa mama yake ....’akasema baba.

‘Mimi nawafahamu sana wazazi wa mama yake huyo , familia ile sio mchezo, wanajua kulea watoto, angalia, mtoto wao alivyokuja kubadilika, na hakutaka kabisa kuwa karibu na baba yake alipojifunza, na kufahamu ubaya wa baba yake na hayo anayoyafanya, akajengeka na kuwa kijana mwema kabisa..

‘Sasa angalia huyo mtoto mwingine, wa mama mwingine, wanyewe mnaiita nyumba ndogo, mtoto yule pia alilelewa na mama yake kwa kiasi kikubwa, lakini hebu angalia tabia ya mama yake huyo na familia ya mama yake huyo, wengi tunaifahamu,...mama yake ni mama wa mjini, na ana tabia zisizo faa,ndio akawa anaishi na mtoto wake huyo, hataki mtoto wake aguswe,...kwa ujumla, mtoto wao huyo hakupata matunzo mema, na baba yake akamchukua, aishi naye akamsomesha, mtoto yule akawa kama baba yake ....’akasema baba.

‘Kwahiyo mnataka kuniambia nini hapo hicho ndio kizalia au ni malezi ya kutegemea na ulezi, na mazingira..?’ nikauliza nilioona maelezo yanazidi kuwa marefu.

‘Ni kuwa usione kuwa tulikuwa tunaingilia ndoa yenu,sisi kama wazazi, tunafahamu mengi , kwa yakini, hatukuangalii wewe tu kama wewe, tunaangalia na matunda yenu, mke mwema na mume mwema, huzaa matunda mema, ...matunda mema,ndio kizazi, ndio jamii, ambayo inaweza kuleta amani na upendo baadaye, au pia ndiyo inayoweza kuleta matatizo baadaye...’akasema baba.

‘Sisi tulifahamu kuwa haya yaliyotokea yatakuja kutokea, kwani tunamfahamu mume wako na chimbuko lake, ..tulikushauri sana hilo, lakini kwa vile nyie ni watoto wa taifa la leo, tukashindwa, lakini sasa umejionea mwenyewe, sasa ni wakati wa wewe kukaa chini na kutathimini matokeo ya juhudi zako, ya kile ulichoona ni bora kwako,...labda sisi wazazi tumepitwa na wakati, nyie mnaona ya kisasa zaidi...’akasema baba.

‘Nikuambie kitu, mimi na mama yako, hatukuwa tunapenda kuweka wafanyakazi wa ndani, uliona mwenyewe maisha tuliyoishi,sio kwamba hatukuwa na uwezo huo, hali zetu zilituruhusu, tulikuwa na wafanyakazi wa kawaida, lakini sio wa kulea watoto, watoto wetu, nyie…tuliwalea sisi wenyewe...wewe umelelewa na mama yako na sana sana, alikulea bibi na shangazi yako...kweli si kweli..?’akasema baba.

‘Unafikiri ni kwanini tulifanya hivyo, ..?’ akauliza baba, na mimi nikawa kimiya sikujua niwajibu nini.

‘Mtoto anaiga na kuwa na tabia kutoka kwa yule anayemlea,...kuna tabia za kurithi, na kuna tabia za kujijenga! Tabia za kurithi, ni zile za asili kutoka kwa wazazi, kama baba au mama walikuwa na tabia hizo..

Kuna tabia kama za ukali kupindukia, upole, kuongea, uvivu, uchapakazi au tabia za namna fulanifulani za kimaumbile, utaona na watoto wanakuwa hivyo hivyo, na tabia hizo zinaweza kufifia kutokana na tabia za kujijenga, au kujengwa, na yule mlezi, sio zote, lakini zile za matendo, nyingi zinafifia kipindi hicho....’akamwangalia mama

‘Wazee wetu waliliona hilo, ndio maana walijenga tabia ya kulea watoto wao wenyewe au kulelewa na ndugu zao wa karibu, siku hizi mnalelewa na wafanyakazi wa ndani, ...ndio maendelea kwasababu baba na mama wote ni wanafanya kazi, au sio

‘Lakini watu hawa wana ndugu zao kijijini, hawataki kuwachukua ndugu zao hawo toka kijijini, waje wawalelee watoto wao, kwasababu gani…hawaoni wanavunja udugu badala ya kuendeleza…umetuelewa hapo?’ akawa kama anauliza tena.

‘Kwasababu mke hataki ndugu wa mume wajazane nyumbani kwake...ubinafasi unaanzia hapo, kwa vile mke yule sio mke mwema, hajui kujenga nasaba,....’akaendelea kuongea baba.

‘Lakini pia ndugu wengine wa mume wana tabia mbaya...hilo nalo mume wangu uliangalie…usiangalie upande mmoja’akasema mama.

‘Sikatai hilo...nazungumzia wazazi wale waliojengwa na mke na mume mwema, wanaotoa kizazi bora, watoto wao wanakuja kulea watoto wa wenzao, na kizazi hicho kinakua, na maadili safi...hawa wanaifahamu vyema nasaba yao, na wanajua nini maana ya familia bora sizungumzii vizazi vyenye maadili mabaya...’akasema baba.

‘Angalia watoto hawa wanaolelewa sasa na wafanyakazi wa nyumbani, wanakua je, baba na mama wanakutana na watoto wao jioni, na watoto hawa wanakua hivyo hivyo, hadi wanafikia muda wa kwenda shule za awali, ...mtoto huyu anakwenda kukutana na mwalimu....ni sawa sikatai ni maendeleo, kwani kwa mwalimu sina shaka nako,...

‘Nasema kwa mwalimu sina shaka nako sana, kwani mwalimu kajifunza jinsi ya kulea mtoto,...lakini mwalimu huyu atamlea, na kumfunza kitaaluma, sio kiasili ya wazazi, kuna mambo muhimu hapo atayakosa, hatajua mila nzuri na desturi za wazazi hao, tabia ya asili ya baba na mama inakuwa imesahaulika kabisa, ....’akatulia kidogo.

‘Wakati mwingine ni vizuri,hasa kwa ajili ya kusafisha tabia mbaya za kurithi, lakini wakati mwingine ni vibaya,kwani kuna vitu kama lugha, na tamaduni muhimu kwa watoto hawa, hivyo vyote vinapotea, kwani hapa, walimu wanachojua ni taaluma, na sio asilia,na mara nyingi, watakachofundishwa hapo ni taamduni za nje, tunalioan hilo kila siku, hata shikamoo kwa mzazi inakuwa shida ...’akatulia.

‘Mimi nimekaa na watoto wako hapa, na kwanza kabisa ulisema tuwapeleke watoto shule za awali, mimi nikakukatalia, ukaona labda tunataka kuwapoteza watoto wako, lakini uliona tulivyokushauri, kuwa kwanza watoto hawa waende shule za maadili ya dini, unafikiri ni kwanini tulikushauri hivyo...?’ akawa kama anauliza.

‘Ni kwasababu maadili ya dini, humjenga mtoto awe na hulka ya imani ya kutenda mema na kukataa mabaya, imani inayomweka mtoto afahamu kuwa yeye ni kiumbe tu, na wazazi wake ni watu muhimu sana, na hatakiwi kufanya mabaya, kwahiyo anajengeka kimaadili mema…

‘ Mtoto huyu akikutana na mwalimu anayejua vyema kazi yake, ile hulka ya asili, ila tabia mbaya ya asili, inaondoka kabisa, na hataweza kufanya makosa kwani muda wote anafahamu kuwa mungu yupo pamoja naye.

‘Mtoto kama huyu anfahamu kuwa nikiiba, nikisema uwongo ni makosa, mungu ananiona wakati wote...leo hii hiyo ipo wapi, watoto wanakimbilia kujua masomo ya taaluma tu lakini maadili ya imani ya moyoni, yanakuwa hayapo.

‘Na wenzetu kwa malengo yao wakaanzisha kinachoitwa haki za watoto, ni sawa hatuzikatai, lakini haki zipi basi, haki za kumtukana mzazi ukae kimia, eeh..je hizo haki zinamjengaje huyo mtoto, je ni maadili mema,....wao wanasema mtoto hatakiwi kuchapwa, wala kukaripiwa, alelewe kama yai, aamue anavyotaka yeye, hivi kweli sisi tungefanyiwa hivyo dunia hii mngeikutaje....’hapo baba katikisa kichwa kwa masikitiko.

‘Mimi ningelikuwa kiongozi wa wizara ya elimu,ningesisitiza kuwa elimu za awali, ziwe za mfumo wa dini, walimu wa dini ndio wapew hizo kazi, ili ziambatane na maadili mema,, watoto wasomeshwe wajue jinsi gani ya kujiweka mbali na uchafu, madhambi, wiz ink….somo la dini liwe ni lazima, kwa shule za awali.Natambua kuwa Serikali haina dini, lakini dini ni muhimu kwa ajili ya kuleta amani na upendo, ...’

‘Nikuambie ukweli binti yangu, maadili mema hujengeka vyema, kwenye dini....hilo binti yangu nakushauri sana, uwe nalo akilini, usije ukatekwa na propaganda potofu, maana dini sasa zinaonekana kama ni sehemu ya kunyima watu uhuru wao, angalia dunia inapokwenda sasa, kwa ajili ya kuiga tamaduni za watu

Hebu angalia hili tatizo baya linalotaka kuenezwa duniani, watu wa jinsia moja wanaoana…hivi hawa ni watu ni wanyama, ..hivi kweli viongozi kama hawa wanataka dunia ije kuwa vipi, halafu wanajifanya ni wacha mungu, huo ni unafiki tu.....

‘Kwanini tunakuambia haya yote,...ni kwasababu tunataka ukitoa maamuzi yako, uwe na yakini, uwe na uwoni wa mbali, kuwa msije mkajibidisha tu kwenye kazi zenu, mkasahau mstakabali mzima wa malezi bora ya watoto wenu, mkawa mnategemea wafanyakazi wenu wa ndani na walimu wa chekechea kuwalelea watoto wenu, msikwepe majukumu, ..malezi mema ya watoto wenu hutoka kwa wazazi, sasa hivi ni kila mzazi achunge familia yake, dunia imeharibika....’akamwangalia binti yake halafu mama yake.

‘Ilivyo sasa, baba akitoka kazini anapitia kuweka moja moto moja baridi na marafiki zake, mama anapewa kazi za maalumu ofisini, ...wote wanachelewa kurudi, ...wakikutana nyumbani, baba kalewa, mama naye kachokeshwa, ni nani hapo ana habari na watoto, sana sana baba na mama hawa wengine huishia kugombana au kuzozana mbele ya watoto wao,watoto wanayaona hayo, wanajengeka hivyo, kisaikolojia wanaathirika, na mwisho wake, na wao wanaona hayo ndiyo maisha ya kawaida.

‘Jamii kimaadili inaanza kuharibika kutoka kwa wazazi wao, chanzo kikubwa kimeanzia ndani ya familia, kwa baba na mama ambao hawakutimiza wajibu wao,...mnawaachia watoto waangalia mapicha mabaya kwenye runinga na sasa kwenye simu, simu mlizonunua kwa pesa zenu, mtoto huyu anakua akijua kuwa ugomvi ni jadi, ulevi ni kawaida, bangi, vita ni mambo ya kawaida tu,..jamii ndivyo inavyoanza kuharibiwa hivyo...

‘Angalia siku hizi, hizo haki zinazopigiwa debe, nyingine ni nzuri sikatai, lakini pale mtoto aliyelelewa kama yai anapoadhibiwa na mwalimu na wewe mzazi ukaja juu, mwalimu akijaribu kutimiza wajibu wake, kwa kumuadhibu, wazazi wanakuja juu..hapa tunazidi kuiharibu jamii...,

Ndio wapo walimu wanakomoa, au wanaadhibu bila kipimo, anaumiza badala ya kujenga huyu ni mpuuzi tu, nazungumzia walimu kwa ujumla, wanaojua kazi yao,…ambao wanahakikisha mtoto anakulia kwenye maadili mema,

Kwahiyo kwa kifupi mtoto aliyekulia kwenye maadili mema, kuanzia kwa wazazi hadi shuleni, huyu akipata kazi ofisini atakuwa mtendani mnzuri, lakini kinyume chake ndio hapo tunapata viongozi mafisadi, wala rushwa, nk, kwani watoto hawa wamedekezwa wamezoea kufanya wapendavyo, hawatajua umuhimu wa kutii sheria, inafika mahali tunasema asiyefunzwa na wazazi wake, dunia itamfunza, sasa hilo ni kosa....tuweni makini wazazi, makosa tunayaaanza sisi wenyewe, tusije tukakimbilia kuilaumu serikali...’akasema baba.

‘Sisi tutaishi na watoto wako hapa, kwasababu tunahitajia kizazi chako kiwe na msingi mwema kama ule tuliokulelea wewe, kwahiyo usiwe na wasiwasi kabisa kuhusu mstakabali mzima wa watoto wako,....

Ila kaa chini,fikiria na sahau kidogo kuhusu watoto, fikiria maisha yako ya baadaye, ila kumbuka malezi ya watoto ya awali ni wajibu wa wazazi...na cha msingi usije ukatekwa na ushauri wa watu wengine usiowafahamu vyema, ...hayo ndio tuliyokuitia, kama una swali uliza...’akamaliza baba. Mimi nikainama chini na kuzama kwenye mawazo na mama ndiye alinishitua, akauliza;

‘Kwani huko polisi wamesema nini, kuhusu mume wako na wengineo,.....?’ akauliza mama.

‘Hawo hawataachiwa mapema, mpaka wakubali kumtaja muuaji, mpaka wasema yale wanayohitaji polisi..’akasema baba.

‘Kwani wao wanamfahamu muuaji ni nani?’ akauliza mama.

‘Kutokana na uchunguzi wa polisi wamegundua kuwa hawa watu wanafahamu mengi yatakayowasaidia polisi kumpata huyo muuaji, lakini watu wetu hawa hawataki kusema ukweli wote, kwasababu zao mbali mbali,...polisi sio malaika kuwa watajua ni nini kimetokea, kama sisi raia hatutaoa ushirikiani, ukificha ukweli unawapa shida polisi, ndio maana wakati mwingine wanaamua kutumia nguvu, ...

'Ina maana inawezekana muuaji anaweza kuwa miongoni mwa hao waliokamatwa....'akauliza mama kumkatisha mume wake.

'Kwa uchunguzi wao polisi, wanahisi hivyo, kuwa huenda miongoni mwao yupo huyu muuaji...ndio hapo polisi wakaja na wazo hilo, kuwakamata wote, na huko wanajua mbinu zao,...watawafinya kidogo, watasema yote..., kwahiyo wakitoka hapo ni mahakamani....’akasema baba.

‘Kwa namna hiyo, ina maana kikao hicho cha maamuzi na hukumu hakitaweza kufanyika karibuni au hakitafanyika kabisa, ni maamuzi tu...?’ akauliza mama.

‘Kikao kitafanyika , cha muhimu ni bintio yetu awe na maamuzi huru, afahamu kuwa maamuzi yake ndiyo msimamo wa ndoa yake ijayo au maisha yake yajayo… na ni muhimu, akae stulize kichwa, atoe maamuzi yenye muafaka, lakini hata hivyo, kwa vile bado hakuna mabadiliko mengine, yeye bado ni mke wa mtu, anahitajika kumsaidia mume wake...’akasema baba.

‘Mimi hapo ndio sikuelewi mume wangu, huoni kama unamchanganya mtoto, mwambie moja kwa moja, kuwa ajipange kuwa sasa kuwa hana mume,huyo mume wake hamfai tena, kwanini tumzungushe mtoto..’akasema mama na baba aktikisa kichwa kukataa.

‘Mbona hata wewe unanichanganya,….wewe ulianza vyema kuwa yeye, anahitajiwa kuwa na mume mwema, lakini huyo mume aliyempata sio mume mwema,anahitajika kuachana naye....sio ndio hivyo, sasa ukimchanganya mtoto atashindwa kukuelewa,..jamani kuna ugumu gani kusema hivyo?’ mama akasema akimwangalia mume wake.

‘Mke wangu sisi ni wazazi, jukumu na lengo letu ni kumshauri binti yetu..., na kama ushauri wetu haukuwa na maana toka awali, unafikiri sasa utakuwa na maana...’akawa kama anauliza akimgeukia mkewe, halafu akaongea kwa kusema;

‘Sisi kama wazazi sio jukumu letu kuwatenganisha wanandoa, awe binti yetu au mwanetu...., bali sisi kama wazazi jukumu letu, ni kuwasuluhisha, kuwashauri na kuwajenga, ili wajaribu kuwa na ndoa njema...’akasema baba huku mama akitikisa kama vile anapingana na maneno yake, lakini baba akendelea kuongea kwa kusema;

‘Mke wangu, ukumbuke kuwa hawa wameshaoana, hivi sasa bado wao ni mume na mke, tulijitahidi awali binti yetu ampate mume bora haikufanikiwa,yeye akasema keshampata mume anayemuona anamfaa, hivyo basi mume aliye naye ndiye chaguo lake, hana ujanja hapo, mpaka kuwe na maamuzi mengine, na hayo maamuzi mengine sisi hatuwezi kuyaingilia, ..anachohitajika kwa sasa ni kumsaidia mume wake,kipindi kama hiki, ...huo ndio ushauri wetu,...’akasema baba.

‘Mhhh, hapana mume wangu, bado binti yetu hajachelewa, na bado ana nafasi ya kumpata mume bora...’mama kabla hajaendelea mara simu ya baba ikaita, na ikabidi anyamaze na kukatiza kile alichokuwa akikielezea.

Na mara simu yake ikalia, akaishika mkononi kwa kuangalia mpigaji, na alipoona ni nani akasema;

‘Mhh, naona kuna jambo ...rafiki yangu huyu, mtu wa usalama, anayenipa habari za ndani, ...nahisi kuna jambo kubwa huwa hanipigii mpaka kuwa na jambo muhimu kwangu, ngoja niongee naye nisikia anasemaje..
Akasimama na kusogea pembeni, huku akiweka simu yake skioni, akawa anasikiliza kwa muda, halafu akauliza;

‘Kwahiyo humjamkamata japokuwa mumethibitisha kuwa anaweza kuwa ni yeye. ......ohoo, kuna ushahidi wa kutosha, sawa kabisa, hapo naona mumemaliza kazi, hongereni sana, ..tupo pamoja....’akasema na kukata simu, halafu akatugeukia na kusema;

‘Hatimaye muuaji yupo mbioni kupatikana.....

NB: Hatimaye muuaji yupo mbioni kupatikana, ni nani...na je ni maamuzi gani atakayoyachukua mke wa familia, tukutane mwisho wa kisa hiki.



WAZO LA LEO:Asili ya jamii, ni kutoka kwa wanandoa, ndio maana tunaona ni muhimu kwa yule anayetaka kuoa au kuolewa kumtafuta mwenza mwema. Wanandoa hawa ndio watakaopata watoto, na kama ni mume mwema na mke mwema, basi watajua umuhimu wa malezi kwa watoto, watoto ambao wanakuja kuwekeza kwenye jamii. Ni muhimu sana, kwa wazazi na serikali, kuwaangalia watoto kwa macho mawili, hawa ndio chanzo cha amani au vurugu.
 
SEHEMU YA 121


‘Ndugu wajumbe hiki ni kikao cha hitimisho cha kikao kilichopita, kama mnakumbuka vyema, kikao kilichopita tulikikatisha kutokana na muda, na pia wajumbe walishachoka, na pia tukaomba wale wajumbe waliotarajia kusafiri waahirishe safari zao, lakini kutokana na mambo yaliyokuwa juu ya uwezo wetu, mengi hayakufanyika kwa wakati, kama mlivyoona wenyewe,...sintofahamu iliyotokea na baadhi ya wajumbe wa kikao hiki wakakamatwa.....’Mwenyekiti akaanza kuongea.

‘Poleni sana kwa mkasa huo, kama wanafamilia sote lilitugusa, ndio maana tulikuwa bega kwa bega kuwaombea dhamana wale waliokamatwa, lakini tulikataliwa kutokana na pingamizi za wanausalama hao...’akaendelea mwenyekiti.

‘Wakati mwingine tunaweza kuwalaumu polisi kwa jitihada zao, tukaona kuwa wanatusumbua, wanatumia mabavu nk, lakini wakati mwingine inakuwa haina jinsi, kwani raia ambao walitakiwa kutoa ushirikiano, wanakuwa wagumu, wanaficha ukweli kwasababu zao binafsi, na hapo ndipo polisi wanapoamua kutumia nguvu...na wakati mwingine wanafanikiwa, au sio..'akasema mwenyekiti, na wajumbe wakikuwa kimia.

‘Siwezi kuwalaumu sana wale mliofanya hivyo, lakini kuna mambo ambayo nataka kuyaweka wazi kama wanafamilia, huenda wengine hawatanielewa, lakini ni vyema nikaeleza sera na taratibu za familia hii, mimi bado ni mwenyekiti wake, na kama bado mnanitambua hivyo, ni lazima nisimamie yale mamlaka ya kifamilia yetu hii kuu...’akatulia.

‘Katika familia hii, tumejitahidi sana kuwa mbali na kashifa,...na hili nimekuwa nikilirudia mara kwa mara katika kila kikao, na kile anayekuja kuoa kwetu, au tukimleta muolewaji hapa, ninajaribu kuwaasa kuhusu hili, lakini hali inazidi kubadilika, ...sijui kwanini, labda ndio karne hii ilivyo.

Kiukweli hili lililotokea limetutia doa kubwa, na sijui tutafanyaje ili tutaweza kujiisafisha, japokuwa tumesalimika kihivyo...mimi sitaacha kulisema hili...sikufurahia na kitendo hiki kabisa,, nawaonya tena, hili lisijirudie. Hatutaki kashfa kwenye hii familia, mnasikia…

'Ndioooh..'wajumbe wakasema

‘Hebu niwauliza ni nani anayependa kukaa jela, hivi jela ni kuzuri,....hivi ni nani anapenda kukaa na wasiwasi, akakosa raha na amani akawa anaishi kwa mashaka-mashaka, hakuna anayependa kuwa hivyo, sasa kama hatupendi kuwa hivyo, kwanini tujiingize kwenye yale mambo ambayo tunayaona yanaleta kashfa, yanatuweka katika hali ya kukosa amani na usingizi, kwanini....?’ akawa kama anauliza.

‘Ndio maana katika familia hii tunalipinga sana hilo..., na wale wanao-olewa au kuoa ndani ya familia hii, nimewaonya na nitendelea kuwaonya tena na tena, hatutaki kashifa, na kama una dalili na mienendoo hiyo mibovu,...tutakusakama, mpaka ubadilike, au uondoke wewe mwenyewe maana hutufai.

‘Sasa basi, tunaanza kikao chetu, na ajenda moja kubwa, ni hitimisho ya ajenda muhimu ya matatizo ya familia husika…tunaweza kuiita ni ajenda ya hukumu.

Lakini kabla ya hukumu, ningelipenda tuliweke wazi tukio zima lilivyokuwa, najua kila mmoja ana dukuduku la kufahamu ni nini kilitokea, ni nani hasa muuaji wa Makabrasha, huyu mmuaji kapatikana au bado.

Tunashukuru mungu kuwa wajumbe mpoo,..nani hayupo, maana kama kuna mtu hayupo ujue bado yupo na wenyewe polisi...

Sasa bila kupoteza muda,...nimeona hili ni muhimu, na niliongea na watu wa usalama, wakasema haina shida, tunaweza kuliongea tu,...kuwa mwenzetu mmoja hapa ambaye alishirikiana na polisi hadi kufanikisha juhudi za watu wa usalama, na tunavyoongea hapa, muuaji anaweza kuwa mbaroni, ...

Aliposema hivyo watu wakapiga makofi.

Sitaki mimi niongee hili mwenzenu ndiye ataongea hili, nasikia mahakama mahakama ilimpa onyo kwa kuingilia kazi za polis bila kibali, lakini kwa namna nyingine imemshukuru sana, na wamependekeza kama inafaa apate ajira huko huko, ni yeye mwenyewe tu.

Kwahiyo basi….tunakuomba, mke wa docta, uchukue nafasi hii utuliezee japokuwa kidogo, jinsi ilivyotokea hadi mkafanikiwa kumpata Muuaji, sasa hivi hakuna kikikwazo, kuelezea hilo au sio, au badoi haturuhusiwi maana mimi sijapewa taarifa na nilipoomba kibali cha kikao, niliambiwa niendelee tu hakuna shida...’akasema mwenyekiti,

Mke wa docta, akakohoa kidogo na kusema;

‘Mhh, naona hiyo mke wa docta, unaipenda sana mzee, hahaha, sawa sio shida, itaendelea kuwepo tu kama sifa..., japokuwa imeshafika mwisho…hata hivyo, sio mbaya, ila yupo atakayekuwa hivyo, mungu akipenda sio mimi tena....’akasema huyo msemaji, na mwenyekiti akadakia na kusema;

‘Samahani, unafahamu hilo halijawa wazi kwenye hiki kikao ndio maana tunaendelea kukuita hivyo mke wa docta, mimi kama mwenyekiti sijapata taarifa kamili, na hata kikao hiki ambacho ni wanafamilia, na wao wanahitajia kulisikia hilo....’akasema mwenyekiti

‘Kwakweli mazoea yana taabu, hata mimi mwenyewe huwa ninajisahau na kujiita mke wa docta, lakini ukweli ndio huo, na kuanzia leo ningelifurahia mkisema, aliyekuwa mke wa docta,...’akasema huku akiinamisha kichwa chini.

‘Hili msishangae, nimeamua hivyo kwa hiari yangu mwenyewe, baada ya kuona kuwa sitakuwa nimemtendea haki mwenzangu , kwa yale yaliyotokea mimi nimeona niwajibike, na kuwajibika kwa muungwana ni kuachia ngazi zu sio…na pia kutokana na kazi zangu mwenywe nimeona kuwa nahitaji kukaa mwenyewe ...maana huwezi kulazimisha jambo kama moyo hautaki.

‘Ni ukweli usiopingika kuwa tumeshamaliza taratibu zote za talaka, kisheria, na hivi mnavyoniona nipo mbioni kuelekea kijijini, huko nimeshajipanga, nina miradi yangu na maisha yangu, na nitakaa kwa muda hadi hapo nitakapoamua ni nini kingine cha kufanya, maana ukiingia kwenye hii fani, muda wote unahitajika, ..ila kiukweli kutokana na haya yaliyotokea nisingelipenda kufanya kazi za kutumwa-tumwa tena, inafikia sehemu unajizalilisha,...ndio kazi…, lakini jamii haiwezi kukuelewa, sasa hivi nataka kujituma, na kujiajiri....’akasema .

‘Kwanza kabisa nawaombeni sana radhi wajumbe wa kikao hiki na wanafamilia hii, kwa hayo yaliyotokea, mimi kama binadamu nimkosaji, na mkosaji anastahili kusamehewa, ...ni kweli nimekosa sana, hasa kwa mume wangu, yeye nimeshamuomba sana masamaha, na japokuwa kanikubalia, lakini bado nahisi sijasamehewa, moyoni nahisi hivyo…., maana kosa nililolifanya kwake ni kubwa sana,...’akasema huku akimgeukia docta.

Docta akatikisa kichwa kukubali tu...hakusema neno.

Naona nianze kutoa maelezo, japokuwa yameshapita, lakini kwa faida ya wanafamilia, nitaelezea ilivyokuwa;

‘Kwa ujumla aliyemua Makabrasha ni mtalaamu wa hali ya juu, alifanya hilo jambo kwa kuangalia nyakati, ..., na aliyapanga hayo mauaji kwa utaalamu wa aina yake...ilikuwa vigumu sana kumnasa, kwanza alienda na muda na pili akawa anatumia madhaifu ya watu, na kuyachanganya na matukio, kiasi kwamba polisi walifikia kuhisi huyu au yule, bila kupata ushaidi kamili.

Hata mimi mwenyewe sikuwa na uhakika na kile nilichokuwa nikikiwaza kwani hata yule niliyemuwaza kuwa ndiye, mwisho wa siku nilijikuta nakosa ushahidi kamili, na hata nilipotoa wazo kwa polisi, wao walishia kuniona mimi ndiye muuaji.

Wao walishakusanya ushaidi wao wa kutosha kwa muuaji, kuwa ni mimi , nikishirikiana na mume wa familia, kwani mimi ndiye niliyekuwepo kwenye hilo jengo, na silaha niliagiza mimi, na silaha iliyotumika nilikuwa nayo mimi, na sababu za kumuua marehemu nilikuwa nazo mimi, na nilishawahi kutamka kuwa nitafanya hivyo......

Mwishowe nikapewa mimi jukumu la kumpata huyo muuaji, kama sio mimi, kilichonisaidia ni kuwa humo ndani ya watu wao kuna watu wananifahamu japokuwa ni kwa siri kubwa, na wananiamini,..pia nafahamu sheria na jinsi ya kujitetea, na kwahiyo hawakuwa na jinsi bali ni kunitumia mimi.

Kwa pamoja tukafanya jambo lililoshindikana.

**********

Kwanza niliwaambia ili kumpata huyo muuaji, kwanza tumchambue huyo mtu, aliyefanya hayo mauji, anaweza kuwa na sifa gani,… kwani mimi nilikuwepo humo ndani, na mazingira ya humo ndani nilishayasoma karibu yote.

'Humo ndani hawezi kuingia mtu akafanya mauaji kama hayafahamu mazingira ya humo..'nikawaambia

'Maana kuna vifaa vya hali ya juu vya kuhisi silaha...kuna walinzi wa seehmu ya kuingilia na walinzi wa nje wasiojulikana wapi walipo, wanatumia mitandao tu, kwahiyo ni lazima mtu huyu alifahamu hilo, pili awe,analifahamu hilo jengo vyema kiramani.., maana mauaji hayo yalifanyika kwa muda mfupi, na kwa tahadhari ya hali ya juu, ...

Niliwaambia kuwa mtu huyo inaonekana kama alipita mlangoni ni mtu nayefahamika, na hata walinzi hawakuwa na shaka naye, 'kama alipitia mlangoni,..', na angelipitia wapi maana mlango ni mmoja na mlangoni hapo ndio utaruhusiwa kwenda juu au chini,..

Jengo hilo lina juu na chini, watu wengi hawafahamu hilo...na sehemu ya chini haitambulishwi kabisa, zaidi ya marehemu na watu wake maalumu.


Nikawaambia huyo muuaji, alipomaliza hiyo kazi atakuwa alikimbilia vyumba vya chini na kukaa huko hadi hali ilipotulia, ...na ina maana huyu muuaji ana chumba maalumu cha kujificha huko chini, sasa ni nani anayelifahamu hilo jengo vyema, zaidi ya Makabrasha na mjenzi wake....hapo ikawa kazi kumtafuta mtu anayejulikana kuwa analifahamu hilo jengo vyema, ..

‘Lakini pia mtu huyo awe anafahamu mtandao wa ulinzi wa lile jengo, awe anaweza kuusimamia huo mtandao, bila watu kujua, na awe anaweza kuona ni kitu gani kinafanyika ndani ya hilo jengo, ina maana basi kwasabbau hii huyo mtu hawezi kuwa ni mmoja, ni lazima walishirikiana watu wawili....

‘Kwa hoja hizo, hakuna zaidi ya Makabrasha mwenyewe,..’wakasema

'Mimi nina tetesi na watu watatu, ...'nikasema

'Kwa uchunguzi wangu niliwachuja mpaka nikabakiwa na watu watatu, mjenzi wa hilo jengo, mtu wa karibu wa Makabrasha na mtoto wake Marehemu, kati ya watu hao nahisi mmoja atakuwa anahusika, au wawili walikula njama ya pamoja.lakini huyo wa tatu hana nguvu, …huyu wa tatu namuondoa

'Mjenzi wa hilo jengo nilishamchunguza sana nikaona kuwa haweza kufanya kitu kama hicho, tunabakiwa na watu wawili ninaowafahamu mimi …’nikasema

‘Tuambie ni nani na nani

‘Mmoja ni mtu aliyaminika sana na Makabrasha, na huyo ni mtu mwanifu sana kwa Makabrsha, lakini huwezi kumuona akiwa karibu na Makabrasha, mtu huyu hajulikani sana machoni mwa watu, maana hajionyeshi, kuwa ana mahusiano na marehemu.. Anayemfahamu huyo mtu kuwa ana ukaribu na Marehemu ni mtoto wake, na mimi tu

‘Ni nani huyo mtu..?’ wakaniuliza.

‘Ni mlinzi wake wa karibu, ...lakini sio wa kukaa naye !..’ nikasema

'Kwa vipi...?' wakauliza

'Huyu anamlinda Makabrsha kwa mtandao,..na akiona shaka tu anawapigia walinzi wa karibu wa Makabrasha...yeye anavyoingia kwenye jengo, wengi hawafahamu, wakati mwingine wanamuita 'mzuka'...

'Ni nani huyo...?' wakauliza

'Basi nikawatajia huyo mtu ni nani na wapi anaishi, polisi hawakutaka zaidi kwanza, wakaanza kumfanyia uchunguzi bila hata ya yeye mwenyewe kufahamu, ikaja kugundulikana kuwa ni kweli siku hiyo ya mauaji huyo mlinzi kweli alikuwepo sehemu yake.

**************

Lakini muda mchache baadae mtu huyo alipigiwa simu, mkewe alikuwa mjamnzito, akawa anahitajika nyumbani kwake kwa haraka, kumbe mkewe alikuwa mbioni kujifungua, kwahiyo akaondoka sehemu yake hiyo baada ya kuwasiliana na Marehemu mwenyewe

Na ushahidi upo, muda mwingi, alikuwa hospitalini, na muda aliotoka hapo hospitalini kurudi nyumbani ulikuwa muda ambao mauaji yalishafanyika, kwahiyo akawa hahusiki kwa upelelezi wa polisi..kwahiyo akaambiwa huyo mtoe

‘Haya tuambie huyo wa pili ni nani,....?’ wakaniuliza

‘Ni mtoto wa Makabrasha,...’ nikawaambia na wao wakaguna na kuniambia, haya tuelezee toka lini mtoto akamuua baba yake...lakini ngoja tuone,

Wakachunguza nyendo za huyo mtu kwa siku hiyo, ikaonekana kweli siku hiyo hakuwahi kufika kwenye hilo jengo, hata mimi pamoja na kumweka kwenye orodha hiyo, sikuwa nimempa nafasi ya kuwa muuaji...maana haya mimi mwenyewe nafahamu kuwa siku ile muda wote hakuonekana kwenye jengo, na kama angelionekana walinzi wangeliniambia,…’nikasema

‘Una uhakika gani kuwa walinzi walikuambia ukweli wote..?’ wakaniuliza

‘Kuna watu wangu humo humo wasingeliweza kunificha mimi,…kwahiyo yeye haiwezekani kuwa aliingia humo, atakuwa alipitia wapi, na isitoshe yeye ni mtoto wa marehemu, kwahiyo mimi siwezi kumshuku sana yeye.

‘Ni nani mwingine ambaye ana sifa hizo zote..?’ nikaulizwa

Hapo sasa nikawa sina la kusema, ina maana aliyebakia ni mimi, ....’

‘Na wa tatu ni wewe au sio....’wakasema polisi na hapo ndio walipasubiria ili kuninasa mimi

‘Ni mimi…! Hapana…sijamuua Makabrasha…’nikajikuta nimesema hivyo, na wao wakacheka,

‘Sasa nani mwingine..tuliyajua haya yote, tulitaka ujilete wewe mwenyewe na hoja zako hizo sio kwamba tulikuwa hatujazifanyia kazi, tulishazifanyia kazi, lakini tulitaka tukuone labda mwenzetu una hoja za ziada, aliyebakia ni nani, kama sio wewe..’wakasema

‘Lakini mimi nisingeliweza kumuua Makabrasha, kama ningelitaka kufanya hivyo, ningelishamuua siku nyingi tu, na kwa namna nyingine kabisa, .....’nikajitetea.

‘Tuambie ukweli, maana wewe ulisema alikufanyia mambo mengi mabaya na ulikuwa na hasira naye na sifa zote za huyo muuaji unazo wewe kama ulivyozibainisha wewe mwenyewe.., kama sio wewe ni nani mwingine..?’ polisi wakaniuliza.

‘Mimi nataka tusaidiane kwa hili, nina uhakika muuaji yupo, na anatuchezea akili, ila sio mimi, ila yupo...ninachowaomba ni jambo moja, nipeni muda nitamtafuta huyo muuaji,wa halali…’nikasema

‘Jambo gani…?’ wakauliza

‘Kwanza…nataka ijulikane kuwa bado nipo humu rumande, muwe mnanipa nafasi ya kutoka kila ninapohitaji kutoka, ili niendelee na uchunguzi wangu, nina uhakika tutampata huyo muuaji, lakini kwa njia zangu nijuavyo mimi..nawaomba msiniingilia kabisa...’nikawaambia.

‘Hatuwezi kukuachia kwasababu sasa hivi wewe ni mshukiwa namba moja,na pili kuna tetesi kuwa kuna watu wanataka kukuua, ni tetesi, na tetesi hatuwezi kuzipuuzia,….sasa ni kwanini wanataka kukuua, ndio hapo tunamashaka...’wakaniambia.

‘Kwanini watake kuniua mimi…, kama sio kwamba wao ndio wauwaji, na sasa wameona kuwa nilikuwa mbioni kuwafichua ndio maana wanataka kuniua, kwanini hamjiulizi hilo, nipeni hiyo nafasi, nina uhakika tutampata huyo muuaji halisi kuliko kuning'ang'ania mimi, niamini mimi, mimi sijamuua Makabrasha,..’nikawaambia polisi.

‘Hebu tuambie huo mpango wako wa kumpata muuaji,...?’ akaniuliza mpelelezi wao, nikamuambia hii kazi nataka kushirikiana na mmoja wa wapelelezi wao ninaowaaamini mimi…

‘Akina nani…?’ wakaniuliza na mimi nikawatajia, maana nawafahamu nimeshawahi kufanya kazi na watu hao, ni wasiri wangu wa kubwa,...hata hivyo wakataka wafahamu mipangilio yangu ipoje.

‘Mimi nawaomba jambo moja, mimi nitaendelea kuwepo humu, ila muda fulani fulani nipeni ruhusa ya kutoka, na nyuma yangu wawepo hao wapelelezi, kwa kificho, wasijulikane kabisa,…’nikawaambia.

Na pili chombo cha kuvaa ambacho, nikikivaa mtaniona kila ninapokwenda...’ wakaitana na kukaa kikao chao, wakajadiliana na baadaye wakanikubalia, lakini ni baada ya mabishano yao marefu, kwani wao walitaka kila hatua niwe pamoja nao, nikawaambia kwa njia hiyo hatufanikiwa. ..

‘Siku ya kwanza sikufanikiwa, na ya pili,….ikawa sasa kuna kukata tamaa, yaonekana mimi najaribu kupoteza muda, …ujue hadi hapo bado na wao walikuwa hawana ushahidi wa uhakika kuwa mimi ndiye muuaji...ni kwanini kuna watu wanataka kuniua mimi...ni kwanini....., vinginevyo wasingelipatia hiyo nafasi.

Siku ya tatu, ndio mambo yakajileta, na siku zote hizo nilikuwa nikienda kwenye hoteli moja ambayo jamaa hawo ninaowashuku hupenda kwenda kustarehe hapo, na humo kuna seehmu maalumu marehemu aliweka vifaa vyake pia, ...vya kuangalia jengo lake kwa mbalia...humo kuna kila starehe, na nilijua udhaifu wao, ni pombe na umalaya...

‘Mimi nikajiweka kinamna, nilipewa gari, la kifahari, na pesa kidogo, nikajifanya kama binti wa geti kali, nilijibadili kabisa, na ungeniona usingelinitambua kuwa ni mimi, huwa nikiwa kazini nabadilika kabisa,....maumbile, mwendo, sauti...huwezi amini...

‘Wanaume kwa uroho wao, waliponiona ile siku ya kwanza, wakaanza kunimezea mate, maana nilitokelezea, hata ingelikuwa ni nani, angenitaka. Wakwanza nikamtolea nje, maana sikuwa na haja naye, akaja mwingine na mwingine, hadi siku ya tatu alipokuja mtu wangu ninayemtaka....

‘Mtu niliyemlenga sana na huyu mlinzi wa karibu wa Marehemu, mimi huyu nilimweka kwenye shuku zangu...

Kwa kipindi hiki, sasa anafanya kazi kwa mtoto wa Makabrasha, huyu nilikuwa bado sijakata tamaa naye, ..hisia zangu zilinituma kuwa huyu mtu atakuwa anahusika kwa namna mja au nyingine...na hasa nilipoona bado anaendelee kuwa karibu na mtoto wa Makabrasha, nikajua kuna kifo kingine kitakuja,...

Jingine hawa watu wawili, mtoto wa marehemu na huyu mlinzi walikuwa hawaivani kabisa, kipindi cha uhai wa marehemu,...walikuwa ni maadui, leo hii wanaelewana, hapa nikatilia shaka..ni kwanini....

‘Siku hiyo huyu jamaa akanijia,...nilikuwa nimekaa meza ya peke yanu nikionekana kumsubiria mtu...nashangaa mtu huyu.... na alionekana kuwa na pesa kweli, nikahisi wana jambo wamelifanya, nikajibaragua na baadaye tukaelewana, hakunitambua kabisa kuwa ni mimi, hata ingelikuwa nani, asingelitambua, ...

‘Tukaanza kuongea kidogo, moja likazaa jingine, tukawa marafiki wa muda mfupi, mimi naifahamu sana hiyo kazi, nina uzoefu nayo, jinsi ya kuwanasa hawa viumbe waitwao wanaume,..sijisifii, lakini sijawahi kufanya makosa, najua madhaifu yao yapo wapi.....jamaa bila kujijua akanasa kwenye anga zangu....sikumchelewesaha, wakati anakwenda kujisaidia mimi nikaweka kitu kwenye kinywaji chake.

‘Kuna aina ya madawa ukimwekea mtu, analewa haraka, anakuwa kama kapagawa hivi...lakini hapotezi fahamu, wanaitumia sana majasusi wanapotaka kupata taarifa kwa mtu,...niliiomba kwa watu wa usalama, wakanigaia, na hiyo ndiyo ilikuwa silaha yangu, sikutaka bastola hapo...

Aliporudii kutoka kujisaidia, nikaendelea kumelegezea, kwanza alijaribu kuwa muangalifu,…unajua tena watu waliopitia uaskari walivyo,..lakini hakunielewa, ikafika muda akajisahau na kuanza kunywa kile kinywaji,..nilimuona kama anasita lakini huyo akanywa,..mara kaanza kulegea, na akili ikaanza kumtoka, na mimi hapo hapo nikamwambia;

‘Mimi ni mchumba wa mtu, sitaki kuonekana onekana hadharani hivi, nilikuja hapa tu kupotza mawazo,…nataka kuondoka,…’nikasema

‘Oooh, hapana, usiwe na wasiwasi, kuna sehemu tunaweza kwenda hutaonekana kabisa, unasikia, unajua mimi nimevutiwa sana na wewe,…kiukweli wewe nai maalumu, unsikia, sikilizaa…twende sehemu pesa sio shida…’akasema

‘Usinihadae,…nawafahamu sana nyie waume, nikiharibu kwangu utakuja kunikimbia, na mimi sitakubali…’nikasema;

‘Kuna sehemu naifahamu, twende.....’ akasema, basi nikajifanya nimekubali kwa shingo upande.

Nikamwambia atangulie nje…nitakuja…

‘Sikiliza wewe acha gari lako hapa, huyu mlinzi wa hapa namafahmu, atakulindia kwa muda wowote unaoutaka, …au unasemaje, usijali kabisa..’akasema, na alionekana kweli kazimia kwangu

Basi tukatoka hapo kwa kupitia mlango wa nyuma, yeye akaniambia nibakie nyuma, ili yeye atangulia akaongee na mlinzi, basi akafanya hivyo, baadae nikajitokeza na tukakutana kwenye gari lake, kabla sijaingia kwenye gari lake ndio akaniuliza.

‘Huwa unafika hapa mara kwa mara..?’ akaniuliza

‘Ndio, lakini mara nyingi nafika na mchumba wangu, sema kasafiri, lakini kwa vile ni sehemu nimeizoea, ..siachi kufika, lakini ni mtu ambaye anaweza kuja ghafla,..si unajua tena…’nikasema

‘Ok..akija,…gari lipo, au sio, na sisi tukirudi nitahakikisha unaingia mlango wa nyuma,…unaonaeeh, atajua ulitoka kidogo au sio…’akasema

‘Hata hivyo sura yao sio ngeni sana kwangu…’ akasema hapoo nikashtuka ina maana keshanigundua nini..lakini nilikuwa na uhakika hawezi kunifahamu, maana kuna utaalamu wa kubadili nyusi, na rangi za macho, na nywele, sikuhitaji kuvaa ngozi bandia,...mimi katika kazi yangu hiii wanapenda kuniita kinyonga, ....naweza tukawa pamoja sasa hivi nikaingia chumbani nikitoka hunikumbuki tena....

Basi, yule jamaa akasema kwa vile naogopa, atanipelekea sehemu ambayo anaiona ni salama zaidi ambayo sio mbali na hapo.., tukaingia kwenye gari lake, na kuanza kuendesha, kama nilivyotarajia nikaona tunelekea uwanja wa ndege, nikajua ni kule kule, na mtego umefanikiwa,

Tukafika karibu na jengo la Marehemu, jamaa huyo hakulipeleka moja kwa moja kwenye maegesho ya mgari, akalipitisha kwa nyuma, hadi sehemu nyingine, kunapohifadhiwa magari ya jengo la pili yake, akachukua ufungua na kufungua geti, kulikuwa na geti dogo la jengo hilo la pili kwa nyuma....kulikuwa hakuna walinzi.

‘Huku ni wapi? Nikamuuliza

‘Huku ni kwa rafiki yangu, ila nataka tuingie kwenye hilo jengo hapo, ni la marehemu, kuna hoteli ya ndani kwa ndani, humo tutastarehe tupendavyo, huyo mchumba wako hatakuona kabisa..’akasema kwa sauti ya kuonyesha hayo dawa imemchukua na sikupenda hiyo dawa iishe nguvu kabla hatujaingia ndani.

Tulipoingia kwenye hilo geti dogo, nikaona akifungua mfuniko, kama ile mifuniko ya mashimo ya maji machafu, nikamuuliza;

‘Unafanya nini ...mbona unafungua mifuniko ya choo?’ nikamuuliza

‘Usijali hii ni njia muhimu ya kuingia ndani, hakuna anayeifahamu zaidi yangu mimi na marehemu na mtoto wa marehemu....’akasema.

‘Huyo marehemu unayemtaja ni nani?’ nikamuuliza

‘Mhh, alikuwa akiitwa Makabrasha ameshafariki....’akasema

‘Mhh, yaani kafariki na kuliacha jengo nzuri hivyo, na wewe ni mtoto wake?’ nikamuuliza

‘Hapana yupo mtoto wake, ndiye anayelimiki hilo jengo kwa sasa..’akasema

‘Na huyo mtoto wake ni nani anaonekana ni tajiri sana....?’ nikamuuliza

‘Achana naye, akikuona wewe najua ataninyang’anya anapenda sana kuninyanganya mawindo yangu...sio mtu mzuri, ...hana huruma, akikuambia utakuwa chakula cha mchwa utakuwa kweli...haogopi, ...’akasema.

‘Una maana gani..?’ nikauliza

‘Usiwe na wasiwasi upo na mimi, …najua yeye ku-ua mtu sio tatizo….sio mtu wa mchezo ila kwangu ananiheshimu, ukiwa nami hakuna shaka…hata hivyo mimi ndiye ninayefahamu siri zake…’akasema na moyoni nikasema sawa kabisa.

‘Kumbe kuna njia hii ...’ hapo nikasema kimoyo moyo…nikatulia kwanza, sikutaka kumuuliza sana, asije akanitilia mashaka, akafungua kile kifuniko na kuninyoshea mkono kuwa nisogee pale, hakufahamu kuwa mimi ni mkakamavu wa kijeshi.

‘Sasa tunaingia,…njia hii ni safi kabisa, kwa nje kunaonekana hivyo, lakini ukiaanza kuingia ndani utazikuta ngazi, unateremka nazo..hizo zinakwenda moja kwa moja hadi kwenye hilo jengo la marehemu, hii ni sehem yake maalumu ya usalama, ni njia za dharura...’akasema.

‘Oh, kwanini awe na njia za namna hii, mnauza madawa ya kulevya nini?’ nikamuuliza

‘Matajiri wengi wana mbinu zao za kuishi, wanajihami kwa kila njia...’akasema.

‘Sasa kama ni hivyo huyo marehemu alikufa kwa ugonjwa au aliuwawa?’ nikamuuliza

‘Walimua bwana,..alikuwa bosi wangu, nikiwa na shida, ananisaidia, sasa nimebakia na huyu mnyama, ananifanya kama mtumwa wake, inabidi nitumie mbinu za kumuibia, sina ujanja...kama jana nimemchomoa mamilioni ya pesa..bila hata kufahamu, akabakia kusema kaibiwa na watu wa benki...’akasema.

‘Oh kumbe walimuua, jamaa wa watu, kwanini walimuua....?’ nikamuuliza

‘Mambo ya mali hayo, unafikiri, ukiwa na watoto waroho, wanawake waroho, na una mali, ujue upo hatarini, na ikizingatiwa kuwa hata marehemu mwenyewe alizipata mali hizo kwa dhuluma..kwahiy ndio hivyo maisha ya dhuluma mwisho wake ndio huo.....’akasema na kutulia.

‘Na mara nyingi watu kama hao wanauliwa na watu wao wa karibu, ..hasa nyie mliokuwa mkifanya naye kazi karibu…’nikasema na kucheka, na yeye akasema

‘Hahaha…acha zako hizo,…keshaondoka basi …acha sisi tutumie, japokuwa kiukweli nilikuwa na mpenda sana…’akasema

'Kwahiyo ina maana waliomuua ni mtoto wake, au mke wake, au walishirikiana kumuua....au ni wewe ?' nikamuuliza, hapo akabakia kimia.

Akafungua mlango wa kuingia kwenye jengo, huku akiwa kimiya, halafu akaniangalia na kusema;

'Tumeshafika...karibu hoteli ya maraha ya Marehemu, hapa usiwe na wasiwasi kabisa....'akasema na mimi nikamuuliza

'Mhh, wasije kuniua na mimi, nimeshaanza kuogopa,…kama watu wanafikia kumuua tajiri kama huyo sembuse mimi....'nikasema

‘Hahaha usijali , mimi nitakulinda usijali kabisa, ..’akasema

‘Mbona hukuweza kumlinda bosi wako…?’ nikamuuliza na hapo kidogo akashtuka.

‘Mbona maswali yako yapo hivyo, usiwe na wasiwasi…’akasema

‘Hapana mimi sipendi maisha ya mashaka mashaka, …ndio maana nakuhoji, ili nijue nipo sehemu kweli salama…’nikasema

‘Usijali…’akasema

‘Au nimekosea kukuuliza…’nikasema

‘Hapana wewe uliza tu…’akawa anaongea kilevi kilevi.

‘Mimi ukinambia jambo napenda kujiuliza uliza sana…ni nani alimuua huyu mtu wa watu naogopa sana, mtu tajiri kama huyu anauliwa,…si alikuwa mtu mwema, anasaidia watu au sio..?’ nikamuuliza,

‘Alikuwa mwema, wakati mwingine, wakti mwingine ndio hivyo kutafuta, sasa kutafutwa na yeye akawahiwa, ndio maisha ajali kazini,…, unajua ukimuongelea nakumbuka mbali sana, nilimpenda sana, lakini kazi ni kazi, utafanyaje …’akasema

‘Kama ulimpenda kwanini hukusaidia polis wampate huyo muuaji wake, ..au muuaji unamfahamu au ni wewe?’ nikamuuliza na hapo akatabasamu, halafu akatikisa kichwa na kusema;

‘We acha…ndio maana nakuambia ni ajali kazini, alikuwa sio mtu rahisi kihivyo, mmh, sasa sikiliza tusiongee sana hayo, au…’akasema na kunywa, alionekana kama dawa inaisha nguvu nilitaka nipate mwanya wa kumuongezea nyingine,..na kweli ikapatikana kwenye gilasi yangu mwenyewe, ndio nikaweza, na kujivunga kama nakunywa, aliporudi nikawa nimebadili zile gilasi kia-aina, akanywa.

‘Mbona hujanijibu swali langu, mimi huwa nikiuliza swali mtu asiponijibu nakuwa na mashaka naye…’nikasema

‘Swali gani mpenzi, uliza chochote mimi nitakujibu,..unasikia chochote…’akasema

‘Ni nani alimuua huyu tajiri wa watu jamani…?’ nikamuuliza hapa, akatikisa kichwa kusikitika, inaonekana kweli inamchukua hiyo hali ya kumbukumbu, na anakuwa kama anawaza mbali, au kuogopa, vyote viwili,…nikasubiria jibu

NB: Tuishie hapa kwa leo..naombeni maoni yenu maana kisa kinafikia ukingoni, je kuna kitu tumekisahau....



WAZO LA LEO: Mali na watoto ni mtihani mkubwa kwa wazazi, ukiwa navyo ni ufahari,...lakini vyote hivi vina mitihani yake. Mali ikiwa ni ya halali, inaweza isiwe ni tatizo, muhimu ni jinsi gani y kuitendea haki yake. Ama kwa watoto ujue jinsi gani ya kuwalea..wawe na elimu na maadili mema. Elimu pekee haitoshi. Elimu bila maadili mema inaweza kugeuka kuwa tatizo pia, wasomi wangapi wazuri lakini wanafanya mambo ya hatari kwenye jamii, kwa kutumia elimu yao, ukichunguza sana ni kutokana na ukosefu wa maadili mema,...

Tumuombe mola atupe mali za halali zenye tija, na watoto wema, wenye elimu na maadili mema. Aamin
 
SEHEMU YA 122


‘Ni mali zake mwenyewe ndizo chanzo cha kifo chake....’akasema sasa akionekana kulewa anajiongelea tu…

‘Kwa vipi, mbona sikuelewi,....mbona unapenda kuongea kimafumbo-mafumbo...maana mimi nijuavyo mali ni utajiri unaokufanya upate kile unachokitaka, sasa ilikuwaje mali zake mwenyewe zimuue huyo marehemu...?’ nikamuuliza.

‘Kutokana na mali zake kulitokea kutokuelewana yeye na familia yake ya pembeni…unaonaeeh….ndio hivyo watu wengine bwana..’akasema na kubekuwa…akawa anakunywa tu.

‘Kumbe alikuwa na familia ya pembeni, mke au hawara tu..?’ nikauliza

‘Ufahamu huyu mtoto sio mtoto wa mke wake wa ndoa, japo anajifanya karithi mali yote ya baba yake…ni mwizi tu huyu, …, yeye alizaliwa nje ya ndoa, mama yake alikuwa hawara wa marehemu…kuna mtoto halali alitakiwa ndiye arithi, lakini huyo mtoto haki mali ya dhuluma, kaacha kaondoka zake..’akasema kama kumnyodoa bosi wake.

‘Nyie wanaume jamani…kwanini lakini’nikasema hivyo, na yeye akaendelea kuongea.

‘Sasa huyo aliyekuwa hawara yake eeh…, akawa anamfunda mtoto wake, kumfisidi baba yake, hebu fikiri mama anamfundisha mtoto wake kumuibia baba yake na si kumuibia tu…unajua nikuambie kitu eeh...mwanzoni mtoto huyo alikuwa hataki, maana namfahamu hata tukakosana kwa hilo…’akatulia

‘Nilimuambia achana na mawazo ya mama yako, weeh, ukitaka ukosane na huyo jamaa mtaje mama yake, akanijia juu kweli, tukawa hatupatani tena mimi nay eye, sikujali..lakini ukweli nilimpa…sasa wanaume nao bwana,…Marehemu alikuwa kichwa lakini wakati mwingine namlaumu…’akatulia

‘Unajua walikuka kukosana baba na mtoto wake kwenye mambo ya …kuandikisha mirathi, si ujinga huu jamani, utaandikishaje mirathi hujafa eeh,..hilo lilimponza huyo jamaa…mtoto akaona, kwanza….eeh nimekumbuka, kwanza baba kwa kupenda alimuandikisha mtoto..kuwa ndiye mrithi mkuu…’akatulia

‘Baadae baba kapata mawazo huku na kule akagundua kafanya makosa, sijui madawa aliyowekewa yalishakwisha, akabadili mirathi,..hapo sasa ndio mambo yakaharibika….mtoto akawa haivani na baba yake…mtoto akawa sasa anamfuata mama yake kile anchotaka kumfisidi baba yake….’akafunguka hivyo

‘Mungu wangu kwahiyo mama akamtuma mwanae afanya mabaya,…ina maana gani hapo…kuwa ndiye alimtuma akamuue baba yake au…?’ nikamuuliza

‘Wewewe…sijasema hivyo mimi…unajua uhuni ni mbaya sana, ukifanya haya mambo kwa siri….haya eeh, hayaaah…nasema taratibu, haya…, ipo siku siri hiyo itakuumbua, marehemu ana watoto wengine, lakini hawo wengine hawana matatizo, tatizo lipo kwa huyo mtoto wake aliyemuona ni kichwa chake...’akasema

‘Kwahiyo alimpenda sanaa mtoto wake huyo…kwanini hakumlinda baba yake asiuwawe..?’ nikauliza

‘Subiri nikuambie sasa…huyo mtoto na mama yake, wakawa sasa hiki….’ Akaonyeshea kwa kidole..

‘Umenielewa hapo…kitu kimoja, sasa wakawa na ajenda moja ya siri,...huku wakijipendekeza kwa marehemu kuwa wanamjali wanampenda, siunajua tena ile ya kujipendekeza.....mimi hilo nalifahamu sana….’akahema kidogo

‘Nahisi kama nimelewa haraka, sio kawaida yangu …lakini usijali…unajua eeh, mimi nilijaribu kumuonya mzee, lakini …watu wengine mimi namshauri kwa nia njema, anakuja kunigeuka kuwa mimi ndiye nawachonganisha,..mimi najali maisha yake na uhai wake, leo hii naonekana mbaya, lakini, sawa maana mimi si kibarua tu…hajui jinsi gani nilivyohangaika naye..’akasema akilegeza domo.

‘Kwahiyo unataka kusema nini, kuwa mtoto huyo huenda ndiye alimuua baba yake au sio, na wewe uliona kwa vile alishakuudhi ukaachia tu, au njama hizo na wewe ulihusika…?’ nikamuuliza lakini hakulijibu hilo swali moja kwa moja.

‘Mimi na mzee tulihangaika naye sana kuweza kufikia hapo alipo, nilijitokea nafsi yangu kumlinda, ndio maana mzee aliniweka karibu sana,…na nilijua mimi nitakwua kama mtoto wake,…ile mirathi ya kwanza alinipa mali, lakini alipobadili, sikuweza kuona jina langu,…watanificha nini wakati mimi naona kwa kiona mbali, hakuniweka, iliniuma sana..unajua kuumia, niliumia, nika-fikia kuapa, nitamkomesha, unajua tena…’akasema

‘Oh,…kwahiyo…ukapanga mbinu za kumuua huyo mzee, sasa nimeshaelewa, kumbe, lakini kwanini ulisahau fadhila, au..?’ nikauliza

‘Unajua haya mambo yasikie tu….kuna watu wanajua kucheza na vichwa vya watu, watu wanapanga mambo wakiangalia matukio…wakajua kuna mambo nikifanya hivi watu wataegemea huku..unaona, …sasa mmh, mimi nahisi kulewa, kwanini leo imekuwa hivi..’akashika kichwa.

‘Kumbe …wewe ni mtoto wa pombe…’ nikasema

‘Mimi…weeeh, hata nikikesha,…nipo imara kabia, na …tukienda kustarehe, utakimbia…’akasema

‘Kustarehe..kupi tena…’nikasema

‘Hahaha, usijali…leo tunywe tu, wewe si rafiki yangu eeh, nimeshakupenda, wewe utakuwa mke wangu..unasemaje…’akawa sasa anajiongelea nikaona hapa nikichelewa gari linaweza kuzimika kabisa.

‘Tunywe huku tunaongea, au…?’ nikauliza

‘Ni wewe tu…mimi ni wako au sio…’akasema

‘Sasa hebu nikuulize maana hii hadithi, inafurahisha sana…’nikasema

‘Hadithi gani…?’ akauliza

‘Si ya marehemu na mali yake iliyomuua…’nikasema

‘Hahaha…ndio hivyo, ndio maana nasema mali yake mwenyewe ndiyo ilimuua,…mali na watoto, unaona, na watoto wenyewe wa nje ambao, wanajali mali tu…’akasema

‘Haiwezekani ina maana mtoto ndiye aliyemuua mzazi wake, kwasababu ya mali, haiwezekani...ungelisema mke, hapo ningelikubaliana na wewe, maana sisi wanawake, tukiamua jambo, tunaweza…’nikasema

‘Mhh, unaonaeeh,…hata huyo mtoto alibadilika kutokana na mama yake, sio yeey..mwanzoni alikuwa mtu mnzuri tu… lakini, mama..maana mama alijua mzee akiondoka atapatia wapi mali, kwahiyo cha muhimu ni kuwahi…akamfunda mtoto, umeona hapo…’akasema

‘Kwahiyo..ikawaje..?’ nikauliza

‘Unajua… tuyaache hayo maana jamaa ana msikio, na tukiongea kwenye hili jengo jamaa atakuwa anatuona, na kutusikia, kwahiyo, ngoja ....’akasema na mimi nikamkatisha na kusema;

‘Kama anatuona na kutusikia, mimi siwezi kukaa hapa, wewe uliniambia hapa ni sehemu ya usalama, kumbe kuna watu wanatuona, hapana, wewe hunitakii mema,mimi naondoka zangu...’nikajifanya kutoka kuondoka.

‘Hahaha…sikia bwana, humu ndani kawezeka vitu vya kuona matukio, uliniona wakati naingia nilifanya nini…taaaa…nikazima ule mtambo, kwahiyo hapo alipo seehmu hii hawezi kuona kitu, kesho atagomba, lakini..ndio hivyo…’akasema

‘Hili jengo ni la ajabu sana…kuna vitu vingi eeh ina maana kuna mitambo ya matukio, kuna mitambo ya ulinzi, …kwanini sasa marehemu akauwawa kirahisi hivyo…?’ nikauliza

‘Ni kweli mambo ya ulinzi yalikuwa mikononi mwangu, mimi najua kila kitu kuhusu ulinzi wa humu ndani..unajua kuna kipindi marehemu alimchukua binti mmoja, yule binti alikuja kuharibu mitambo yote…imechukua muda kuijenga upya, lakini bado..na nafanya hivyo makusudi kumkomoa huyu bosi wangu mpya…’akasema

‘Juu kuna sehemu nyingine au sio…?’ nikauliza

‘Yah…ipo lakini imekodishiwa watu wengine sisi makao yetu ni huku,…huku anamiliki mwenyewe bosi na mambo yake,…juu ni mradi wake wa kuingiza mapesa,..huko juu hawajui kabisa kuhusu huku chini…’akasema

‘Ina maana ukiwa huko juu, huwezi kuteremka huku chini..?’ nikamuuliza

‘Kuna chumba kama store,…kimejengwa ovyo ovyo..ni mbinu tu, ukifungua humo huwezi kujua siri yake, sasa humo ndio kuna ngazi za kushuka chini, unafungua mlango…unateremka, watu hawajui, hizo ni mbinu nilimfundisha mzee, zinatoka izraili…nilijifunza huko, hahaha…’akacheka sana.

‘Kwahiyo huku chini mnatumia kwa kazi gani…maana sioni watu wengi, …?’ nikauliza

‘Starehe na biashara haramu…na umalaya tu , huyo mtoto ndio zake, akitaka kufanya shughuli zake za haramu, ni huku..akitaka kumtesa adui yake ni huku, akiteka watu watu ni huku …hakuingiliki ovyo…nimekuingiza wewe kwa vile tu..nakupe-ndaaa…’akataka kunishika
‘Ohh, sory….’akasema nilipomkwepa.

Ilibid nibadili muelekeo wa kumuhoji kwanza, kwasababu kwa maelezo yake hayo, huku kutakuwa na siri nyingi sana, ambazo zitasaidia kama ushahidi, sikutaka kwanza kushinikiza kufahamu muuaji wa Makabrasha, nilijua hilo litafikia muda wake.

‘Kwahiyo huku kuna siri nyingi sana za marehemu au sio…?’ nikauliza

‘Marehemu keshaondoka, sasa hivi ongelea siri za bosi mpya,…kuna vyumba vingi tu, kila chumba kina mambo yake, ..mimi kila kitu najua,..hanibabaishi mimi..’akasema

‘Sasa hebu niambie ni nani aliyemuua huyo jamaa wa watu, maana naanza kuingiwa na hamasa ya kumtambua huyo marehemu na familia yake, wakati mwingine unaweza kujifunza kutoka kwa familia za watu wengine au sio...?’ nikaanza kumchota tena kuhusu mauaji...

‘Hiyo familia achana nayo, ni familia ya laana, walichokitenda hawataweza kuishi kwa amani, nikuambie ukweli, pamoja na utajiri wao wote, bado wanaishi kwa majuto, na wakati mwingine nasikia huyo jamaa analia na hata kupiga makeleke usiku...’akasema

‘Ni nani analia, ....?’ nikamuuliza

‘Si huyo mtoto wa marehemu, wewe unacheza na damu za watu...’akasema

‘Ina maana yeye ukimkosea tu anaku-ua, ..mbona unanitisha…?’ nikauliza

‘Upo na mimi,…mimi nilikuwa mlinzi hodari wa mzee, sasa wa kijana wake, wananiamini, mimi sio mchezo, …’akasema akijipiga kifua

‘Kwanini anaweweseka usiku…kaua watu wengi au…?’ nikauliza

‘Laana ya watu waliowaua..na zaidi laana ya mzazi wake yeye mwenyewe…’akasema hapo nikaona hajasema ninalotaka kulisikia.

‘Lakini huyu mtoto alimpenda sana baba yake au sio, sasa iweje apate laana…?’ nikamuuliza

‘Hivi unafikiri mzazi ni mchezo…hata kama asipokutamkia,..kama wewe umaimwaga damu yake, si lazima utapata laana yake…’akasema
‘Ni kweli kama alimuua baba yake ni lazima atapata laana yake …’nikasema

‘Ndio maana halali…anaweweseka….’akasema

‘Una uhakika gani kuwa yeye ndiye aliyemuua baba yake?’ nikamuuliza huku akimimina kinywaji...

‘Uhakika sikuwa nao mwanzoni, lakini nilikuja kuangalia mkanda wa matukio, niliouchukua pale ofisini kwa Makabrasha, yeye mwenyewe aliniambi siku nikisikia kafa, nifungue sehemu moja ya siri, iliyokuwa chumbani kwake, nitoe hicho kifaa cha kuhifadhi matukio ya hilo jengo, nimpe mtoto wake mkubwa..’akaniambia.

‘Kwanini alikuambia hivyo, ina maana alishafahamu kuwa atakufa?’ nikamuuliza

‘Watu kana hawo, hujihami tu, ...na sijui kwanini, nahisi kama alishatabiri kifo chake kwani siku ile ya mwisho aliniambia, niondoke, ila nikisikia lolote limetokea, nisisahau kufanya kama alivyoniagiza, na mimi nikamuitikia, na niliposikia kuwa amekufa cha kwanza kukifanya ni hicho, nikafungua sehemu hiyo ya siri ma nikachukua hicho chombo, na alipofika huyo mtoto wao mkubwa nikamkabidhi...

‘Ina maana huyo mtoto wao mkubwa anafahamu ni nani aliyemuua baba yao?’ nikamuuliza.

‘Kile chombo kilikuwa kinachukua matukio ya mle ndani ya ofisi na mazungumzo yake na watu mbali mbali, na muuaji, alijitokea mara moja akiwa kavaa nguo za kuficha sura, kwahiyo sizani kama huyo mtoto wake anamfahamu huyo muuaji...,mimi niliwahi kuchukua kile ambacho hakikuwa wazi, ambacho mitambo yake ndio ipo huku chini,

‘Sasa wewe ulifahamu vipi kuwa muuaji ni nani?

‘Wewe unauliza sana maswali, kama polisi, tunywe, tustarehe, tusahau machungu ya dunia, unasemaje...’akasema huku akinisogelea akitaka kunibusu, nikawa natumia mbinu za kumweka mbali, ili niaweze kupata taarifa muhimu, nikasema;

‘Kuongea pia ni sehemu ya starehe, niambie kwanza,una wasiwasi gani, umeshasema huku hakuna mtu anayeweza kutuingilia, tuongee, ili tujuane vyema, mimi sipendi mpenzi mwenye papara au ndio zenu za hit-and run...’nikamwambia.

‘Aaa, bwana, wewe umesema una mcumba, hata nikikufahamu vyema itasaidia nini, leo ok, nimekuelewa, tutakuwa tukikutana hivi kwa siri au sio, ...’akasema.

‘Unajua mimi nina tatizo moja, ukiniambia jambo likanivutia, natamani kulifahamu vyema, na mimi nimekupendea kwa jinsi unavyoweza kuchunguza mambo na ujanja mwingi, …’nikasema

‘Hapa uemfika kila kitu najua…’akasema

‘Sasa wewe mwenyewe umenugusia maisha ya huyo marehemu yamenivutia sana, niambie wewe ulimgunduaje huyo muaji wa marehemu kwasababu mimi ulivyonieleza, naweza kukuhisi kuwa wewe huenda ndiye uliyemuaa huyo marehemu, ?’ nikamuuliza

‘Hapana mimi nisingemuua tajiri wangu, ili nipate nini, mimi siku ile niliondoka mapema niliposikia mke wangu kashikwa na uchungu, na nikapigiwa simu kuwa tajiri yangu kapigwa risasi, nikaja kwa haraka, na cha kwanza ni kufanya kama alivyoniagiza mimi nifanye nikatimiza…’akasema,

‘Kwahiyo kumbe hata wewe humfahamu vyema huyo muuaji wa marehemu , unafanya kukisia tu, na ujanja wote huo, ulishindwa kumfahamu muuaji wa bosi wake, au unaogopa kuniambia...?’ nikamuuliza

‘Kwakweli mwanzoni nilikuwa nachanganyikiwa hata mimi , kwa asilimia kubwa nilikuwa nawatuhumu watu wawili, ...kuna jamaa mmoja, alikuwa anafika fika sana na ni rafiki wa marehemu namfahamu sana, japokuwa alikuwa mgonjwa,..siri zao nazifahamu…’akatulia

‘Nilishangaa mtu mgonjwa, anawezaje kufika hapo…nikachunguza nikajua watu hawa wapo kitu kimoja..huyu mtu wakawa hawaelewani, unajua siku ile mitambo ilizima kama isingelizima ningeligundua kila kitu..,..., hata siku ile wakati naondoka, huyo jamaa alikuwa ameshafika....yeye nikamtuhumu sana, polisi hawakufaamu kuwa mtu huyo aliwahi kufika hapo mimi nilikuwa najua...’akasema.

‘Mtu gani huyo wewe ulimgunduaje?’ nikauliza

‘Mimi na marehemu siri yetu ni moja, ....aah, achana nye huyo, ila kulikuwa pia na dada mwingine, ni mtu wa karibu na huyo marehemu , nilimshuku sana, nakumbuka hata wakati naondoka, niliongea na mtoto wa marehemu, huyo mtoto wa marehemu akaniambia niwe makini sana na huyo dada, kwani kamshuku anaweza kufanya jambo baya kwa baba yake....’akasema.

‘Mhh, kwahiyo....?’ nikataka kumuuliza swali, lakini akanikatiza na kusema.

‘Hawo wawili niliwatilia mashaka sana, nikajua wao ndio walishirikiana kumuua Bosi wangu mpendwa....’akasema

‘Kwanini uwatilia mashaka hawo watu wawili…?’ nikamuuliza.

‘Kuna mabishano ya mara kwa mara ya watu hawo, na kulikuwa na mambo ya mikataba yao ya siri, walikuwa hawajaelewana, nikajua ni yale mambo ya marehemu ya kuwabana watu ili apate pesa kutoka kwao, japokuwa nilikuwa nawafahamu hao watu, lakini mambo mengine kama siri za mikataba yao alikuwa haniambii, .....’akasema.

‘Kwahiyo ikawaje tena usiwashuku watu hawo?’ nikamuuliza.

‘Siku moja, nilifika nyumbani kwa huyo bosi, wakati nafika mlangoni, nikawasikia,, ...mtoto alikuwa akiongea na mama yake,...hiyo sehemu nimeirekodi, siunajua tena mitambo ipo wazi wakati wote,hawakufahamu kuwa mimi nipo hapo mlangoni,, na wakawa wanaongea jinsi gani wataweza kuisafisha damu ya marehemu, kwani mtoto alikuwa akisema alikuwa akimuota baba yake akimjia mara kwa mara

‘Mimi nitakutafutia mtaalamu atakusaidia...lakini usije ukajiweka roho juu, kuwa marehemu anakujia, hizo ni ndoto tu, unasikia mwanangu....’mama akamwambia mtoto wake

‘Lakini naota ndoto za kutisha, najuta kwanini nilifuata ushauri wako, mama sizani kama nitaweza kulisahau hili, nilikuwa nampenda sana baba...’akasema huyo jamaa kumwambia mama yake

‘Kama usingelifanya hivyo, ungeliwezaje kumiliki hilo jengo na mali za marehemu nishukuru sana mimi kwa kukushauri hivyo, ...;akasema huyo mtoto.

‘Mama mimi sitaweza kulisahau hilo tukio,japokuwa tumelifanya kwa makini na hakuna anayeweza kutushuku sisi, labda huyu mlinzi wetu , nina wasiwasi kuwa atakuwa katuhisi, kwani nilipochelewa kumpa zile pesa zake, aliniambia anafahamu kuwa sisi huenda tunahusika na kifo cha baba,.....’akasema.

‘Atafahamu vipi, kwani siulisema uliharibu kumbukumbu zote kwenye ule mtambo wa kunasia matukio,..’mama akasema.

‘Kuna ule mtambo wa chumba cha baba, ….unajua ile ni siri ya baba, niligundua kuwa pale pia panachukua matukio, na siku nilipofika sikukuta kitu, ina maana kuna kitu kilichukuliwa, sasa nina wasiwasi na huyu mlinzi, ..kitu ambacho kinanitia wasiwasi...’akasema

‘Kama ni hivyo, kwanini asimfuate huyo marehemu ....kwasababu akibakia hai, hutakuwa na amani...’akasema mama.

‘Tukianza hivyo, tutaua wengi, kwasababu hata yule mwanadada aliyekuwa akifanya kazi na mzee, pia na yeye anadai ana ushahidi huo huo , na yule ni hatari zaidi ya huyu mlinzi wetu, huyu mlinzi wetu, ukimpa pesa atanyamaza lakini yule mwanamke, hawezi kufanya hivyo, na amekuwa akihangaika kumtafuta muaji, ...’akasema.

‘Kama ni hivyo unafikiri tutafanya nini, ....ni kuwamaliza mmoja baada ya mwingine kwa mbinu zetu…, sio lazima kwa kifo cha hapo hapo, tunaweza kutumia sumu,...na ajali za kawaida tu, hilo niachie mimi, wewe hakikisha huyo mlinzi, unamweka sawa...’akasema mama.

‘Basi niliposikia hivyo, sikuwa na amani....cha kwanza nilichofanya ni kwenda kuangalia kile kifaa nilichokichukua kwa marehemu, ....nilikuwa sijapata muda wa kukiangalia mwanzo hadi mwisho, ndipo nikagundua ukweli...kumbe...ndio yeye aliyefanya hivyo...’akasema an kutulia.

‘Nikagundua kuwa kumbe nina ushahidi mzuri sana, nikawa nawaza nifanye nini, niwaambie polisi, nikaona hapana muda bado wa kufanya hivyo...

‘Nikahakikisha ule ushidi nimeuweka sehemu ambayo hawataweza kuupata, kwanza nilitaka niutumie kutajirika, baada ya hapo, kama watanizid nguvu, nawakamatisha kwa polisi,..ndio sasa wameanza kunijali, nafahamu wanatafuta mbinu kuupata huo ushahidi nilio nao, halafu waniue, lakini nilimwambia huyo jamaa akiniua na yeye ajue anakamatwa...’akasema.

‘Kwa vipi sasa....akikuua, polisi hawajui kuwa unafahamu siri zako..’nikamwambia.

‘Nimeziweka mahali ambapo, hawataziona, na nimeshatayarisha taarifa yangu, nikaiweka mahali ambapo, nikifa tu, itasambaa...kuwepo kwangu hai ndio naweza kuidhibiti isivuje…mimi ni mtaalamu usinione hivi..’akasema.

‘Sasa kwanini uishi maisha ya hatari kihivyo, waambie polisi, utakuwa umejiokoa, kwasababu kwa hivi sasa unafanya makosa, polisi walifahamu kuwa unamfahamu muuaji na una ushahidi umeuficha, utashikwa kama na wewe ulihusika, waambie polisi, uoshe mikono yako....’nikamwambia.

‘Mpaka nihakikishe nimekipata ninachokitaka, wana mali nyingi sana,na pia wameharibu, urithi wa baba yao, kwenye huo urithi, mimi nilitakiwa kupewa sehemu ya mali, kwani mimi mzee yule alinithamini sana, sasa nimewaambia ili hayo yaishe, wanijengee jumba la maana, na liwe na miradi, ili niweza kukaa hapo na kusahau kila kitu...’akasema

‘Wameshalitimiza hilo?’ nikamuuliza

‘Wameanza, nimepata kiwanja, na tayari ujenzi umeanza, sina wasiwasi, ndio unaniona na mimi nastarehe, kama alivyokuwa akifanya yule mzee, yule, ..kwasababu mzee, alikuwa akinijali, wao wakajifanya wanaanza kunisahau...’akasema.

‘Kwenye huo mtambo, hakuna ushahidi unaoweza kuwakamata hawa watu kuachilia mbali huo ushahidi ulio nao wewe?’ nikamuuliza, nikamuona keshachoka na maswali, akasema ...

‘Wewe sasa unauliza maswali mengi, ...hebu njoo hapa nikuonyeshe..’akasema na tukatoka hapo akanipeleka kwenye hicho chumba chenye mitambo ya usalama, mimi sikuwahi kukisia kuwa chumba hicho nacho kina mitambo hiyo, kilikuwa chumba, kama stoo, lakini kwa ndani kuna chumba kingine, na humo kuna mitambo kama ile ile ninayoifahamu mimi, usingeliweza kuligudua hilo.

‘Unaona hapa, hapa kuna mitambo, ambayo haijawahi kuzimwa, ile ya juu, inazimwa mara kwa mara, lakini hii ipo wakati wote, na anayeusimamia huu mtambo, ni huyo mtoto wa marehemu, akifika, anahifadhi kumbukumbu zote za siku, na kusiweka, mahali pa usalama, kwahiyo hilo tukio analo yeye, na sizani kama atakuwa hajaharibu hiyo sehemu.

‘Sasa wewe uliwezaje kuipata hiyo sehemu?’ nikamuuliza.

‘Si nimeshakuambia kuwa ,Marehemu alikuwa anafahamu hayo yote, kwahiyo kule kwake, kuna mtambo mdogo, wenye mawasiliano na huku,..kila akifika, anaangalia, anawasiliana na huu mtambo mkubwa, anajua ni kitu gani kilitokea, hakuwa na haja ya kufika huku.

‘Kwahiyo wewe ulipofungua, kama alivyokuelekeza mzee, ukaona tukio zima..hukumwambia mtoto wake mkubwa?’ nikamuuliza.

‘Nilipokichukua, sikuwa na haraka ya kuangalia kila kitu, nilikuja kukiangalia baada ya kusikiliza hayo mazungumzo kati ya mtoto wa marehemu na mama yake,siku ile...ndipo baadaye nikaenda kukiangalia kwa makini, ndio nikaoana tukio lilivyokuwa...aliiingia kwa njia hiyo tuliyoingilia sisi pale pale…umeona eeh…, akajibadili, akavaa kama mafundi, akajifunika uso mzima, usingeliweza kumtambua...akaenda chumba cha yule mwanadada,akachukua bastola...

Hapo hapo….polisi mpoo….akilini nikawa nasema hivyo!

Tuendelee…

WAZO LA LEO: Hakuna siri hapa duniani…kila mtenda mema atakumbukwa kwa wema wake, na kila mtenda maovu atakumbukwa kwa uovu wake, usijifanye wewe ni mjanja sana wa maovu, ukafikiria siri zako hazitagundulikana….unajidanganya,… uovu, dhuluma,ukatili unanuka kama mzoga, japokuwa hatuhisi harufu yake…lililojema ni kutubu, kwa toba ya haki na kumrejea mola wako….
 
SEHEMU YA 123

Nilipoichukua sikuwa na haraka ya kuiangalia,…lakini niliposikia wakiongea nikataka kuhakiki, sikuamini nilichosikia hadi pale nilipoangalia hiyo video ya matukio ya siku ile,….sikuamini, hadi leo nashindwa kuamini…we acha tu…

‘Niambie ukweli maana wewe si umesema hapa kuna ulinzi, kuna mitambo, iliwezekanaje mtu kuchukua silaha na kwenda kumuua bosi…bila hata kujulikana, kwahiyo hiyo mitambo iliisha chaji au..…?’ nikamuuliza kuonyesha sijui kitu

‘Hahaha, sio chaji…. kuna mtu alizima hiyo mitambi, ina maana ni mtu anayeifahamu, na mtu huyo ni huyo huyo…unaonaeeh, …’akatulia kidogo

‘Mimi niliona kila kitu kwenye hiyo video, nashukuru niliipata kabla haijafika mikononi mwa hao watu wake, au polisi, maana inaonyesha kila kitu hakuna kilichobakia, …inaonyesha kila kitu, …

‘Kama nilivyosema japokuwa mtu kazima mtambo mkubwa lakini huo mdogo ndani ya chumba kwa Marehemu bado uliendelea kuchukua taarifa, wenyewe hauzimiki haraka, Marehem alilijua hilo kuwa kunaweza kutokea tatizo mitambo ikazima, kwahiyo akaweka server……’akasema

‘Ok, sasa hiyo silaha ilifikaje…?’ nikauliza

‘Mhh..hapo hata mimi sijui..ila kilichoonekana silaha hiyo ilikuwa chumbani kwa mdada…’akasema

‘Wewe si mlinzi wa mbali, unamlinda mzee, ilikuwaje silaha ifike humo ndani wewe usione ..hapo ndio nakuwa na mashaka na ulinzi wako, au na wewe ulihusika…’nikasema

‘Mimi namlinda mzee, ..sio jengo, sio kila kitu kwenye jengo, unasikia, ulinzi wa jengo wapo watu wengine, na mkuu wao ni mtoto wa mzee, unasikia, kwahiyo jinsi silaha ilivyoingia sijui…mimi isingelikuwa hilo tatizo,…la mke wangu mzee asingeliuwawa…’akasema

‘Kwahiyo silaha ilikuwa chumbani kwa mdada, huyu jamaa alijuaje kuwa ipo huko…?’ nikauliza

‘Unataka kutunga kitabu…?’ akauliza huku akicheka

‘Au usije ukawa ni shushushu…nitakuua….’akasema na kucheka

‘Hahahaha, hapana….ni hadithi au tukio la kuvutia….’nikasema

‘Sio hadithi, hilo ni tukio la kweli, upo ushahidi…silaha ilikuwepo kwa huyo mdada, swali ilifikaje, kama huyo mdada naye hakuwa na nia mbaya na bosi, ndio maana awali nilijua yeye ndiye kamuua…’akasema

‘Endelea,..very interesting story…’akasema

****************

Jamaa akaingia chumbani kwa mdada, akaichukua hiyo silaha, maana huyo mdada hakuwepo hapo chumbani kwake alikuwa kwenye ofisi yake…usingelimuona awali, usingelijua ni yeye, alivyojivika hayo manguo, kuonyesha kweli huyo jamaa ni jasusi..

Ili kuwa ni kitendo cha haraka sana…wakati huo marehemu alikuwa akiongea na yule jamaa yake, walikuwa hawaelewani,…walikuwa wanabishana sana, unajua kama isingelikuwa ni huo ushahid , pia ungelisema huyo jamaa yake ndiye alimuua, maana ilifikia mahali, huyo jamaa yake anasema kwa sauti.

‘Ipo siku nitakuua kwa hili….’

‘Nani alisema hivyo…?’ nikamuuliza

‘Huyo jamaa yake waliyekuwa wakiongea naye…’akasema

‘Unamfahamu huyo jamaa…?’ nikauliza

‘Unajua…awali, sikuweza kumfahamu maana alikuwa kajibadili…lakini nikaja kugundua kuwa ni jamaa gani,...ni jamaa mmoja bwege-bwege fulani, yeye hakujua tu, alikuwa kitumiwa kwa masilahi ya wengine……’akasema na kutulia

‘Ulikuja kumgunduaje kuwa ni yeye…?’ nikauliza

‘Mtandao..unaweka picha, …inakuambia huyo mtu ni mtu fulani, kajibadili…siku hizi mambo ya kisasa…haikuwa kazi kwangu kumgundua,…mimi ni mtaalamu usinione hivi..mzee alikuwa akinifahamu ndio maana akaniamini.

‘Ok, sawa endelea…’nikasema nikijifanya kuangalia saa.

Ikaonekana jamaa katoka na silaha…lakini wakati anatoka alikuwa kaifutika kwenye koti…, nilishangaa kwanini mlio wa hatari haukulia, kwani yeye alikuwa na silaha, nikagundua kuwa yeye kwa vile ni mtaalamu aliweza kuzima sehemu ya mlio wa hatari....

‘Alikuwa yeye peke yake…?’ nikauliza

‘Peke yake….ila alionekana kama anawasilana na watu…kwenye simu kabla na baada ya tukio…’akasema

‘Ok endelea…’nikasema

‘Basi akafika kwenye ile ofisi, ..akasimama, kama anasita kufanya anachotaka kukifanya, ghafla akasukuma mlango.

‘Ile video inazunguka, kwahiyo ilikuwa kama ..imekata, halafu ikaonekana sasa anamlenga baba yake, hiyo inaonyesha wazi, hakuna kuremba, bila chenga, risasi inatoka inakwenda kutua kifuani kwa mzee..…nahisi baba yake alimuona….ila huenda baba yake hakufahamu ni nani.

‘Akawa sasa anataka kummaliza huyo jamaa mwingine, ile bastola ikawa imeishiwa risasi, kwa ujinga wake, aliichukua ile bastola, bila kuhakikisha kuwa ina risasi za kutosha, kwa mshituko wa kile alichokifanya, akairusha kwa ndani...nahisi alifanya hivyo makusudi ili watu wengine, hasa huyo jamaa aliyekuwepo humo ndani ashukiwe kama muuaji,...

‘Kwahiyo una uhakika kuwa huyu mtu ndiye huyo mtoto wa mzee,…maana hapa ni muhimu…?’ nikauliza

‘Uhakika gani sasa..ukiangalia hiyo video ya matukio utaona kila kitu…..’akasema

‘Oh….inatisha, mtoto kumuua baba yake…haiwezekani…’nikasema

‘Ndio maana nakuambia hata mimi siamini….ukiangalia hiyo video, utafikiri ya kuigiza, lakini ndio tukio lenyewe,…sasa hebu niambia mtu kama huyo utaweza kuishi naye bila kuwa na mashaka…’akasema
‘Halafu ikawaje…?’ nikamuuliza sasa nikiwa sina hamu na mengine ni kupoteza muda sasa…

‘Baadaye sasa, akaonekana mwanadada mwingine akiingia, huyo ndiye waliyekuja kum-kamata kama mshukiwa,…’akasema

‘Huyu mwanadada ni nani…?’ nikauliza

‘Yaani huwezi amini, huyo mwanadada ni mke wa huyu jamaa aliyekuwa akiongea na marehemu…’akasema kwa sauti ya chini..

‘Oh…alikuja kufanya nini…?’ nikauliza

‘Nahisi alikuwa na yake,…na marehemu, ..si unajua marehemu ana wateja wengi, na mambo yake ni mengi tu…’ akasema

‘Kwahiyo wakazidi kuchelewa, kumpata muuaji halisi,…na ushahidi mwingi ukawa unapotea bure, ila halisi ya matukio, ikawa imechakachuliwa, lakini ya kwangu ilibakia kama ilivyo, kila kitu kipo...’akasema kwa haraka haraka, nilimpata kwa vile nilishajua mengine...

‘Sasa nikuulize kumbe wewe ulikuwa na ushahidi wote huo, kwanini hukuwafahamisha wanafamilia, yaani mtoto mkubwa wa marehemu?’ nikamuuliza

‘Sikufanya haraka hivyo, hata hivyo, wao yaani yeye na mama yake hawakutaka kuingilia yote hayo, japokuwa walihisi kuwa kuna mtu anahusika, wao walirizika na taarifa ya polisi kuwa huenda muuaji ni miongoni mwa maadui zake.

‘Mhh..wewe ulilionaje hilo…?’ nikauliza
‘Sikuona cha ajabu,…hawakuwa karibu sana na mzee, kabisa, walifanya tu kutumiza wajibu,, wewe huoni ajabu kuwa hawakutaka mali ya marehemu kabisa, urithi ulikuwepo kwa ajili yao, mtoto na mama yake, lakini hawakuutaka kabisa....’akatulia kidogo.

‘Sina uhakika na hilo, ila nakala halali ya nani arithi, ilipatikana,..ikionyesha kuwa kaka mkubwa ndiye msimamizi wa kila kitu, na msaidizi wake ndio huyo mtoto mwingine …aliyemuua baba yake…ile ya kwako waliyogushi ikachelewa kupatikana,kukawa na mkanganyiko hapo.

‘Maana hadi kufanya hayo mauaji ni ili …mirathi yao waliyotengeneza wao, iwe halali na hiyo ya mzee ipotezewe, ikawa kinyuma chake, mtoto na mama walihaha, kilichowafanya wasifanye jambo, ni pale walipoona wenzao hawana tamaa na mali, hawataki chochote kutoka kwa marehemu.

‘Sasa kibaya zaidi ni pale wenzao walipoanza kugawa mali,..hilo lilifanya kuzuke mgongano, lakini wenzao walikuwa wastaarabu, wakasema wao hawatagusa mali kubwa kubwa, wao, wanataka mali zile ambazo zinaondosheka, wauze, kulipia madeni, ..na kuwalipa wale waliodhulimuwa, japokuwa hazikutosha.

‘Mambo yakawa yanachelewa..huyu mtoto mkubwa, akaona bora aondoke na iliyobakia ikawa chini ya huyu msaidizi wake,..alipoondoka tu, huyo mdogo mtu akacheza, akahakikisha ile mirathi yake ndio inatambulikana, hadi sasa utaona hivyo…

‘Kwa vipi sasa, wakili wao si yupo…wakili aliyekabidhiwa hayo mambo na mzee…?’ akaulizwa

‘Wakili hahaha…tuyaache tu hayo…nikuambie kitu.., huyu sio sawa na Makabrasha, akikutisha anakutisha kweli…wakili akafyata mkia, akawa sasa anafuata anachotaka bosi mpya…’akaangalia saa nahisi alinihofia mimi nachelewa kuondoka, akili za kunijali bado zilikuwepo.

‘Unafikiri kwanini huyu mtoto mkubwa na mama yake hawakutaka kuchunguza kwa undani kifo cha Makabrasha, hapo bado mimi najiuliza, isije ikawa na wao wapo nyuma na jambo fulani….?’ nikamuuliza

‘Hapo hata mimi sijui,...sijui kwanini hawakutaka kufanya uchunguzi wao wa kina...ila mimi nilitaka kumwambia huyo mtoto wa mzee yale niliyokuwa nayafahamu kwa wakati huo, lakini huyo mtoto wake, aliniambia niachane kabisa na maisha ya baba yake, kwani yeye hataki kabisa kuyaingilia na wala hataki mali yake, alishajitoa kwake, yeye amefika kwasababu ni baba yake na niwajibu wake kumzika, mengine kama ninayo ni mwambie huyo mdogo wake….yeye keshamaliza kilichomleta na kama nina ushahid wa kutosha wa muuaji, niwaone polisi….

‘Aliponiambia hivyo nikaona basi haina haja...nitautumia huo ushahidi nilionao nionavyo mimi,..siunaona, imanisaidia na mimi, japokuwa nahisi nipo kwenye hatari, hata hivyo, hatari imekuwa ndio maisha yangu,...huwezi jua, kifo changu kinaweza kuwa kama cha marehemu..’akasema.

‘Mimi nakushauri kitu, ongea na polisi, jisalimishe, ili uwe na maisha ya usalama, maana hujui wenzako wamejipanga vipi, kwanza kama ulivyosema kwenye mirathi halali ya marehemu alikutaja kama mmoja wa warithi wake, huoni utafaidika kihalali ukifanya hivyo...?’nikamwambia.

‘Mhh, ni rahisi kusema hivyo,… lakini huwajui hawa watu, ...mimi siwaamini, na wala siamini kuwa polisi watawaweza kunisaidia kwa hili jambo, nahisi likifika mikononi mwao, hata kile kidogo nilichotarajia kukipata sitakipata tena,…’akasema

‘Unajua huyu …mtoto wa marehemu , kama alivyokuwa baba yake, hata yeye kuna wanamtumia wenye pesa, japokuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa wanahusika kwenye hayo mauaji,…ni wajanja sana…’akasema

‘Wewe unao ushahidi wa kuonyesha kuwa hao watu wanahusika…?’ nikamuuliza

‘Unajua nikuambie kitu…hawa watu walishafikia sehemu wamemchukia Makabrasha…kuna video inaonyesha hivyo…ninayo…, kwani Marehemu alipoona kafanikiwa mambo yake, akavunja mahusiano na hao wafadhili, …sio moja kwa moja y akukatisha mkataba nao, hapana, alikuwa kama hawajali-jali fulani hivi…, na kazi aliyopewa akawa anaifanya kwa masilahi yake…’akatulia

‘Ehe…’nikasema

‘Kwahiyo kwa hali hiyo, huenda..huyu mtoto wake pamoja na mawazo ya mama yake, pia yawezekana aliahidiwa donge nono, kumbuka kutokana na madeni yaliyobakia ya mzee, jengo lilitakiwa kupigwa mnada, yeye akaligomboa, akalipa madeni yote,…sasa huyu jamaa pesa alipatia wapi, walichunguza hilo watagundua mengi…’akasema

‘Mhh..hapo yawezekana, lakini hata hivyo hakuna ushahidi kuwa hao watu walihusika kwenye hayo mauaji, huo uhakika haupo, au sio..’nikasema

‘Mimi nilivyoona ni hivyo…, sikutaka kuingia huko sana, maana huko sio pa kuingilia, huko waachie wenyewe…’akasema

‘Mimi ninachojiuliza ni kwanini, toka marehemu afariki hadi leo, wewe unao ushahidi, kwanini hukuwaambia polisi, unajitia matatani bure…’nikasema

‘Wao wamefanya nini muda wote huo, kazi kuwakamata watu wasiohusika, kwanini wanawasikiliza wanasiasa, kwanini hawafanyi kazi yao ....mimi naona wengi wao, ni wale wale tu…mimi ndio maana nimeamua nifanye nionavyo mimi, kwa masilahi yangu kwanza, hapo nitakaposhindiwa basi nitajua la kufanya...’akasema.

‘Je na huyu mtoto wa marehemu akikugundua huoni utakuwa ndio mwisho wako?’ nikamuuliza.

‘Kunigundua kwa vipi sasa, wao wanafahamu kuwa nina siri hizo,…wao wanachojitahidi ni kutafuta wapi siri hizo zipo…lakini hawataweza kugundua ng’ooo…mimi sio mjinga…’akasema

‘Wao kila wanachokifanya ninakiona, kwanza mimi mwenyewe ni mtaalamu , na pia...mzee wao alinifundisha mambo mengi, ndio maana aliniamini, ...unaona nilivyo mjanja, pale nyumbani kwako, napaona kila siku, ...wakiongea , wakipanga, mimi napata taarifa, ni kwa usalama wao, lakini pia mimi nachunguza zaidi ya hayo...’akasema.

‘Kwahiyo wao kwa sasa, wapo wapi, wapo hapa nchini au wamewekeza huko nchi za nje… ?’ nikamuuliza, maana mama na mtoto wake, hawajaonekana hapa jijini kwa siku ya tatu sasa, nikaona niulize hilo swali ili watu wa usalama wasikie na wajue jinsi gani ya kufanya.

‘Hao wamekwenda hapo jirani tu,- Kenya, kuna miradi yao wanaifuatilia, ilikuwa miradi ya marehemu, ilikuwa haijakamlika wakati wa uhai wake kwahiyo wao wanataka kuhamisha umiliki kutoka kwa baba kwenda kwa huyo mtoto…’akasema

‘Mhh, ni mradi mkubwa sana…?’ nikauliza

‘Ndio, kama wakifanikiwa, basi wao sio wenzetu tena, na jiulize pesa za kuendeleza mradi huo wamezipatia wapi, ni zawadi kutoka kwa maadui wa marehemu au kuna nini nyuma ya pazia,…aah, mimi huko sipo, ila nitakula nao….’akasema

‘Huenda wakija watakupatia angalau hisa kidogo..?’ nikauliza

‘Hapo ndipo naumia kwanini wachukue kila kitu, kwanini mimi wasinipe haki yangu, ndio maana nimelifanya hili, …kuwakomoa kwanza,…kwa hivi sasa kila kitu wameniachia mimi mpaka wakirudi, wakirudi tu, nawabana, vitisho vyangu ni vile vile...’akasema

‘Kumbe sasa wewe ni bosi...’nikasema.

‘Hahaha, kwa hivi sasa eeh, nimeachiwa usukani,..ila wakirudi wanaweza kuja na ajenda ya siri, lakini mimi nitaigundua tu, ..hawaniwezi...’akasema.

‘Inakuwaje mtu afahamu siri za watu wengine, hicho chombo alichokuachia marehemu kipoje...naona dunia ina mambo mengi, mimi mambo mengi siyajui, naona kama miujiza tu...?’ nikamuuliza

‘Unafikiri ni chombo kikubwa sana wewe…’akasema akionyesha kuchoka.

‘Ni kitu kidogo tu…kama simu tu, unatembea nayo, ukitaka kuangalia mahali fulani ulipoweka vitu vyako, unabonyeza namba, unavuta ule mnara wake, basi unatafuta muelekeo wa namba, unawaona, ...

‘Sasa kama unataka kukihamisha hicho kidude kwenye komputa unakiweka, ...hapo unaweza kuangalia, kama unavyoangalia picha za kawaida, wanawasanifu watu kweli kweli, lakini mpaka upandikize chombo fulani hapo unapotaka kupata taarifa ....mimi ni mtaalamu bwana..’akasema kwa sauti ya kilevi.

‘Sasa wewe una uhakika gani kuwa mwenzako huyo naye hakufanyii kama unavyo mfanyia yeye,huenda huko alipo anakuona..huenda hata nyumbani kwako unapoishi kapandikiza kitu kama hicho?’ nikamuuliza.

‘Kuna kifaa kingine cha kugundua hivyo vitu vya kupandakiza, mimi kama mlinzi ninacho, kama kuna kitu kimepandikizwa kwako kinakuashiria, lakini sijawahi kumuonyesha huyo mtoto wa marehemu, aliwahi kukipandikiza kwangu, nikakigundua, kwahiyo mimi nipo mbele zaidi yake....’akasema.

‘Wao wanarudi lini?’ nikamuuliza

‘Kesho, ila kila siku nawasiliana nao, wanaweza wakaja hata leo, kwa usalama mara nyingi hawasemi lini wanafika, ndio maisha ya watu kama hawo, kama alivyokuwa marehemu, ila mimi nafahamu ni kesho.....’akasema.

Mara simu yake ikalia, akaiangalia, na kusema, ...
*****************

‘Bosi,...naona keshafika, huenda wapo hapo uwanja wa ndege,...sasa mimi kwa hali niliyo nayo,sijui kama nitaweza kuwafuata, inabidi nimwambia mtu akawachukue, ngoja niongee naye kwanza, maana nahisi nimelewa sitaweza kuongea nao katika hali hii, au unasemaje mpenzi,....’akasema.

‘Kweli...’mimi nikasema huku nikijua sasa kazi imekwisha, nikahakikisha namsogelea ili kusikia anachoongea, sikuweza kusikia huyo bosi wao anaongea nini, lakini alivyokuwa akijibiwa nilisikia, jamaa akawa anajiuma uma,..mimi kwa haraka nikawasiliana na watu wangu kwa ujumbe wa simu, na wao wakanijibu kuwa wananifuatilia kwa karibu,nisiwe na wasiwasi.

‘Haloo bosi, mnasemaje?’ akawa anaongea kwa kujitahidi kuficha kuwa kalewa, huku pia akijaribu kunikwepa ili nisiwe karibu naye, lakini sikumpa nafasi hiyo nikamsogelea, akawa sasa anaongea na simu, akasema;

‘Unasema mumeshafika, mpo nyumbani, mbona hamkuniambia nije kuwapokea hapo uwanja wa ndege, nipo hapa karibu kabisa...!’akasema kwa akionyesha mshangao.

‘Ohoo, ndio nilizima kidogo, maana nina mtoto, nastarehe kidogo, siunajua leo ni mapumziko bosi...sasa sikutaka mambo yangu yaonekane huko, nitawasha,...nikimaliza..nipe nusu saa,...sasa hivi, kwanini bosi, mbona unaniharibia starehe zangu, unasema kuna nini..hapana bosi, mimi nina uhakika hakuna kitu kama hicho...una uhakika,...’akasema na nilimuona akiwa na wasiwasi.

Baadaye alinigeukia, na kusema;

‘Mhh, naona mambo yameharibika, kitumbua kimeingia mchanga....’akasema akionyesha wasiwasi.

‘Kuna nini kimetokea....? nikamuuliza

‘Jamaa anasema kafika tu ,polisi wamemvamia, ananihisi eti mimi ndiye nimemuuza, polisi wameshafika kwa bosi, haapo kajiiba ,kusogea pembeni, kunipa tahadhari, nihakikishe hawafiki huku, sasa naona mambo yangu yameharibika, sijui nifanye nini, ..kwanini polisi wamefanya haraka kiasi hiki hata ujenzi haujakamilika...’akasema, na mimi nikamwambia.

‘Wewe usijali, ..cha muhimu ni kutoa ushirikiano na polisi, maana inavyoonekana polisi wameshafahamu ni nani muuaji, sasa ukijificha, na wewe utashikwa kama mshirika wao..mimi naona hapa hakuna usalama tena nataka kuondoka....’nikamwambia na yeye akawa kama anafikiria jambo.

‘Sasa bosi kasema niharibu kila kitu, ....’akasema

‘Wewe, usije ukafanya hilo kosa, unaharibu vidhibiti vya polisi, huoni kuwa wewe utaonekana mshirika wa hayo mauaji..’nikamwambia.

‘Ok, nimekuelewa, lakini kwanini huyu bosi anasema hata sasa hapa nilipo, nipo na watu wa usalama, mimi simuelewi kabisa... ngoja nikawashe hiyo mitambo niliyokuwa nimeizima, tuondoke zetu, wameniharibia starehe yangu,....nisubiri...’akasema na mimi nikamuuliza

‘Tutatokea wapi?’ nikamuuliza nikimchelewesha na yeye akaniangalia halafu akaingalia kule tulipoingilia, na kusema

‘Hukohuko tulipoingilia....’akasema, na kabla hajamaliza mara tukasikia mlango ukigongwa, akawa anangalia huku akionyesha wasiwasi, akaniashiria kwa mkono, nitoke, kwa kupitia ule mlango tulioingilia, huku yeye akianza kuelekea kwenye kile chumba cha ile mitambo, lakini kabla hajaufikia huo mlango, mara mlango ukafunguliwa.

Wa kwanza kuingia alikuwa askari, mwenye sare, na baadaye wakaingia wengine, wakiwa wamevalia kiraia, wote hawo nawafahamu,...

‘Sisi ni askari usalama, mpo chini ya ulinzi, hakuna kusogea au kugusa kitu chochote..’akasema huyo mwenyesare, lakini hakuwa na silaha yoyote zaidi ya rungu, ...nikajua kwanini, wasingeliweza kuingia na silaha kwa kupitia upande wa juu, mlio wa hatari ungelitushitua, na huyu jamaa angelikimbia, ...lakini na mara tukasikia sauti kutoka kule tulipoingilia wakaingia askari wengine, hawa walikuwa na silaha, na hapo hapo mlio wa hatari ukaanza kulia...

‘Kwanini mnanivamia nimefanya kosa gani?’ akauliza na wao wakamshika na kumfunga pingu, na kumweka chini ya ulinzi, mimi taratibu nikatoka,nikijua nimetimiza wajibu wangu ...kazi nyingine yote waliimalizia wao, kila kitu kikawa wazi, muuaji akajulikana, na ushahidi wote ukapatikana,mtoto na mama yake, ndio waliomuua Makabrasha,...’akasema huku akimwangalia mwenyekiti.

‘Inatosha, tunakushukuru sana, mengine yote, tunayafahamu kwa wale waliokuwa wakifuatilia hiyo kesi na kuhudhuria mahakamani, kuwa wahalifu hawo, wanatumikia jela zao, haki imtendwa, iliyobakia ni sisi kama familia, tutimize yale yanatuhusu, na kusuluhisha tatizo la familia hii, kama wazazi ni lazima tutimize na sisi wajibu wetu,..’akasema mwenyekiti.

‘Sasa ni ajenda yetu ya mwisho kama nilivyosema…, ajenda hii ni hukumu, au mstakabali wa ndoa ya mke na mume wa familia ....na hapa mimi sitaingilia sana, maana wanandoa waliosababisha hiki kikao wapo hapa, na walishapata muda wa kukaa pamoja na kulijadili hili, nasikia bado kuna mvutano, ...sasa mimi kama mwenyekiti, nahitajika kutumia rungu langu la uenyekiti...kulimaliza hili tatizo,...,

NB: Naona tuishie hapa kwanza.


WAZO LA LEO: Ubaya na matendo mabaya, sio sifa ya kujinadi mbele ya wenzako, kuwa mimi ni mjuzi wa ubaya fulani, watu hawaniwezi, nk....kwanini tusijisifu kwa matendo mema, tuangalie wenzetu waliobuni , na kugundua mambo ambayo mpaka leo yapo, yanatumika kwa manufaa ya jamii, ina maana watu hawo, ni kama vile bado wapo hai, ...hizo ndio sifa njema,...,
 
SEHEMU YA 124


‘Sasa ni ajenda ya mwisho, ajenda ya kusikia kauli na maamuzi ya wanandoa ambao ndio waliotuweka hapa…

Kwa namna nyingine tunaweza kuiita ajenda hii kuwa ni ajenda ya hukumu au hitimisho ya kile tuliyochokuwa tumeitiwa,.....na hapa mimi sitaingilia sana, maana wanandoa waliosababisha hiki kikao wapo hapa, na walishapata muda wa kukaa pamoja na kulijadili tatizo lao hili kwa mapana yake.....’akasema mwenyekiti.

‘Japokuwa kwa nilivyolisikia…’hapo akageuka kumuangalia mume wa familia, ambaye alikuwa kainamisha kichwa chini, halafu akageuka kuniangalia mimi.

‘Sitaki niongee mimi,..japokuwa naona …kama bado kuna sintofahamu kwa wanandoa hawa wawili..wengine kama docta na mwenzake wameshamalizana..

Sasa kwa vile tupo kwenye kikao cha wengi, na penye wengi hapaharibiki neno, natumai tutalimaliza hili swala kwa amani na upendo, ikishindikana mimi mwenyekiti nipo, itanibidi nitumie rungu langu la uenyekiti...’ hapo akatabasamu akimuangalia mke wake.

‘Sio shida…kulimaliza hili tatizo,sio shida kabisa.lakini kwanini tulazimishane, ..hapana, hili ni swala la wawili , waliopendana wenyewe, na kama ni kulimaliza tatizo lao walimalize kwa amani…au sio...

Tuendelee na sehemu ya kwanza ya hitimisho la kisa hiki...........

**********

‘Kama mnakumbuka kikao kilichopita ilibidi tuendeshe jambo hili la kifamilia kama kesi ili tuone haki inatendeka, kwa vile mlalamikiwa hakukubali wala kukiri kosa lake, kwahiyo tukaona ni vyema tukaliangalia hili jambo kwa undani zaidi…

Ilibidi tuliendesha kama kesi…kwa kutoa ushahidi, na maelezo yenye ushahid ndani yake,.. hadi pale ukweli mnzima ulipobainika,..ukweli huo ulikuja kufichua mambo mengine kabisa..lakini chanzo, ..ni familia husika,…sasa sijui ni kwa bahati mbaya, au ilikusudiwa, yote hayo tuliyaona wenyewe.

Hayo mambo yaliyotokea, ambayo kwa ushahid, yalipangwa, nisinelipenda kuyarajea hayo mambo, kila mtu kayasikia na kujionea..sasa leo kiko chetu kinaendelea,.

‘Sasa basi mimi kama mwenyekiti, inabidi nilisimamie hili kwa hekima zote ili mwisho wa siku tukimalize hiki kikao kwa kushikana mikono ..’ hapo akamuangalia mume wa familia ambaye bado alikuwa kainamisha kichwa chini.

‘Mimi bado natoa angalizo, kuwa hii ni familia yenye maadili yake, kama kuna mtu anaona kuwa hataweza kuishi nasi, kwa kufuata sheria zetu za kifamilia, basi awe huru kuondoka, hata kama ni mtoto wangu wa kumzaa,...ni vyema tukafynza kutii amri na sheria kuanzia kwenye familia, na hili liwe wazi kwa kila mtu,...

Hata hivyo, taratibu za familia ndogo, yaani za mke na mume zitaendelea kutumika,..hatuwezi kuziingilia, labda wao wenyewe wasema kuwa basi, hizo sheria kwa vile zimeleta mgongano, hatutazifuata tena, na kwa minajil hiyo kwa vile waliusajili huo mkataba, itabidi wafuate taratibu zao.

Haya yote tunawaachia wao,..leo ukumbi ni wao, wawili, sisi kama familia kuu hatustahili kuwaingilia,..hitimisho hili ni lao, kama kuna kusameheana, ni heri sana kwetu, kama kuna kuwajibishana, hewala....

Naombeni muda wenu kidogo, nataka kuteta na mawakili…kabla hatujaendelea…na mawakili wakasogea pale alipokuwa mwenyekiti wakawa wanaongea, ilitakiwa iwe maongezi kidogo, lakini ikachukua muda..naona wakili wa mume wa familia alikuwa akipinga jambo..

Lakini baadae wakakubaliana, na mwenyekiti akasema;

‘Unajua kama nilivyosema hapa kila kitu kimekamilika, pamoja na hayo yaliyoamuliwa huko mahakamani,lakini sis bado tuna maamuzi yetu, au sio, ndio maana pamoja na hukumu, bado sisi tuliambiwa turejee tukae kama familia kulimaliza hili tatizo letu…

‘Sasa basi wazee walisema, yaliyopita ni ndwele tugange yajayo, au sio jamani…’akasema mwenyekiti na wajumba wakasema

‘Sawa…’suti hafifu lakini.

‘Hayo yaliyotokea yawe ni fundisho kwetu, na tuape kuwa hatutarudia tena,tusameheane na kukiri kuwa tulikosea, na hatutareeja ujinga huo tena, kwani tumeshafinywa, mtu mzima ukifinywa, huona aibu,… eti jamani…leo iwe siku ya kusameheana na iwe hitimisho na ukurasa mpya uanze..’akasema mwenyekiti huku akimwangalia mume wa familia.

‘Hebu mwangalia mume wa familia alivyochongeka, ....ni taabu tupu, kwanini tufanye haya, tukijua kuwa ni makosa, tunamkomoa nani, ...baba, sasa ni wakati wako wa kurudisha mwili wako, ukae utulie ujipange vyema, muishi vyema wewe na mkeo wako na familia yenu kwa ujumla,...au sio, lakini sasa…’akasema na kutulia

‘Uamuzi wote upo mikononi mwa mke wako….’hapo akamgeukia mke wa familia.

Na mume wa familia akainua kichwa kidogo, hakusema neno

‘Kama ulivyoona hata mahakamani walikunyoshea kidole wewe, na kukupa onyo, na ulitakiwa ufungwe, lakini wakili wetu akafanya juhudi za ziada, akirejea maadili na tabia za familia kuu, matendo yetu mema ya kifamilia yakachukuliwa kukulinda wewe, ina maana kuachiwa kwako kunatokana na kumbukumbu za matendo yetu mema, maadili yetu mema yamukusaidia, sasa mimi kama mwenyekiti nikiwa hai sitakubali uadilifu wetu uporomoke tena, ...nawaomba kama wanafamilia tuitunze hiyo kumbukumbu,...’akasema mwenyekiti.

‘Nimeona niongee haya kabla ya mke wa familia, sijui yeye ana maamuzi gani, hatujui,…ila nina imani kuwa baada ya kipindi hicho kifupi alichoweza kukaa, na kipindi hicho kifupi ambacho mume wake alishikiliwa…yeye atakuwa ameweza kukaa na kutathimini, kama ulivyoomba yeye, na …’akatulia kidogo.

‘Natumai hutatuangisha kwa hilo..

‘Baada ya mume wako kutoka huko aliposhikiliwa, uliomba wewe na yeye make pamoja, myajadili maswala yenu..natumai mlifanya hivyo au sio, ...na kwahiyo wewe kama mdhulumiwa, unayo haki yako ya upendeleo…, na hatutapenda wanafamilia wengine waingilie kati hayo maamuzi yenu

Na maamuzi yenu yasije kuwadhulumu watu wengine, ...kama kuna mtu atadhulumiwa kwa maamuzi yao..basi kila mmoja anayo haki ya kusema,na kikao hiki ndicho halali cha kuyasikiliza hayo malalamiko ya mtu anayeona kadhulumiwa…msiogope kusema jamani, sisi hapa tupo tutaangalia haki iko wapi.

‘Mke wa familia, tunakuomba uondoe jaziba, najua umeumia sana, lakini yote ni maisha, kwenye wema, na wabaya wapo, na halikadhalika kwenye wabaya na wema hawakosekani, na mitihani hii inakuwa ngazi ya kutuvusha daraja fulani,…kwa wenye hekima watalielewa hilo, au sio…

Uliona pale mahakamani walisema nini…hawakutaka kuamua moja kwa moja japokuwa haki ilikuwa yako..mkataba wenu ulishahukumu..lakini bado wakasema tuwe na muda wa kutafakari, tuwe na muda wa kukaa kikao cha kifamilia,…sasa wewe, unayo haki, ya kuamua upendavyo..kwa vile wewe ndiye uliyedhulumiwa, na mkaaba wenu unakulinda kwa hilo..

‘Tunatarajia wewe utatoa maamuzi yako yenye hekima na busara,…haki ni yako, una haki ya kutumia mkataba wenu, au kutumia kauli yako mwenyewe, sisi kama wazazi tumeliongelea hilo, tukaona kwanini misisameheane mkayasahau yaliyopita na kuganga yajayo...’akasema mwenyekiti.

‘Nakumbuka kikao kilichopita tulimpa nafasi mlalamikiwa ajitetee, na kuelezea hisia zake, leo hatuna nafasi naye tena, leo ni siku ya mke wa familia kuongea yake na pia kutoa maamuzi yake, kwani imeonekana kweli kuwa mume wa familia ana makosa na mke wa familia ulitendewa isivyo haki, kwahiyo kwa upendeleo wewe mke wa familia una pewa nafasi mbili, ya kwanza ni kumsamehe mume wako....

‘Upo tayari kumsamehe mume wako…?’ akasema mwenyekiti kama ananiuliza, na mimi sikujibu kitu nikawa kimia tu, maana hakuna aliyejua nina nini moyoni mwangu,…

‘Usinijibu kwa sasa utajibu muda wako ukifika…’akasema mwenyekiti

‘Ila napenda niseme hivi….kusameheana ni wajibu wa kila mwanadamu, ni daraka kubwa ya ucha mungu…ukikosa na kukosewa hatuna budi kusameheana, ni vyema tujifunze hilo...’akatulia

‘Lakini yote ni maamuzi yako wewe mke wa familia,…kama utakubaliana nalo, basi sisi kama wanafamilia, tutawashikanisha mikono, na tutamaliza haya mambo kwa amani na salama hilo ndilo kama wazee wenu tunalihitajia na kulitarajia kutoka kwako wewe mke wa familia, ila sio kwamba tunakulazimisha ufanye hivyo maana una nafasi nyingine ya pili...’akasema mwenyekiti.

‘Nafasi yako ya pili, ambayo mimi kama mwenyekiti, sitaipendekeza sana, japokuwa nyie mlikubaliana kwenye makataba wenu iwe hivyo, ...kuwa atakayekiuka mambo fulani,…mambo mabaya yenye kuleta kashfa… ambayo wenzenu waliamua kuyatumia kisiasa, na hata kidini hayakubaliki,..na kwene famila kuu tumeyaanisha kama matendo yenye kuleta kashifa

‘Mhh…basi moja kwa moja ndoa inakuwa haipo…swali likaja je ni nani mwenye kuvunja ndoa…ni yoyote mke au mume…haya ni maswali manzito sana, na mume wa familia kasimamia hapo kuwa yeye ndiye ana haki yakuvunja ndoa…

Sasa mkataba wenu ulikuwa na maana gani,…mlikubaliana mbele ya wakili waliotambulikana, au sio na mola wenu ni shahidi…au sio…kwahiyo yakitendeka ya kuvunja ndoa, ndooa hapo inakuwaje…

‘Lakini hapo hapo tunaweza kurejea nafsi ya kwanza ya kusameheana,…kama mkoswaji, aliyekosewa, akaamua kusamehe..basi,…mambo yataendelea, na ndivyo tunavyotegemea hapa kwenye kikao hiki.

‘Tukumbuke jambo moja, sisi wanadamu wote ni wakosaji…hakuna mkamilifu, utamlaumu mwenzako kwa kosa hili kumbe na wewe una makosa mengne makubwa zaidi ya hayo unayomlaumu mwenzako au sio..kuna makosa mengi, sisi kama wanadamu tunayafanya kwa siri, sijui,…mimi sijui…mke wangu ananiamini sana kuwa sifanyi hivyo..hahaha....’akatulia mwenyekiti na kumwangalia mke wa familia.

‘Unapoteza muda bwana…’mke wa mwenyekiti akasema;

‘Sawa sawa, msaidizi wangu lakini ni wajibu wangu kuyaongea haya kama mzazi….maana hitimishi hili lisije kuwa ni mgogogo mwingine baadae…

Haya basi,..mimi naona nisipoteze muda, mke wa familia uwanja ni wako, ...’mwenyekiti akamwangalia mke wa familia.

************

Hapo mimi kama mke wa familia, kwanza nikasimama,…nikainamisha kichwa kidogo kutoa heshima kwa mwenyekiti..halafu nikageuka kumuangalia mume wangu..huku nikitafakari maneno ya mwenyekiti kuwa nina nafasi mbili, ya kwanza ni kusamehe, lakini ya pili ni kutumia mkataba wetu.

Kusamehe..yaha, yawezekana, moyoni sina kinyongi tena…lakini mkataba ulikuwa na maana gani…nifanyeje sasa…nikamuomba mola wangu anipe kauli yenye hekima na kulimaliza tatizo hili kabisa…

‘Naomba niongee nikiwa nimekaaa, ...mwenyekiti naomba kibali chako....’nikasema na mwenyekiti akatabasamu na kusema;

‘Nyie vijana bwana, mbona mnachoka mapema, haya wewe kaa tu, hata ukitaka lala, maana sote sasa hivi masikio na macho yetu ni kwako wewe….. sema yale yaliyo moyoni mwako, uwanja ni wako....’akasema mwenyekiti.

‘Nilitaka nisimame, lakini kama wenzangu walivyofanya kwa leo, nitaongea nikiwa hapa hapa, mtanisamehe kidogo, nipo kwenye wakati mgumu sana, namuomba mola wangu aniongoze tu..…’nikasema

‘Kwanza nimshukuru mwenyekiti kwa kunipa nafasi hii, ambayo, imekuwa kama vile mtu yupo kwenye chumba cha mtihani baada ya maandalizi ya muda mrefu. Ni kweli nimekuwa nikijianda kwa siku kadhaa nyuma hasa baada ya kikao kilichopita, ..ulikuwa ni wakati mgumu sana kwangu. Kama mke na kama mama wa watoto wawili….

‘Ni wakati mgumu maana kuna mambo mengi yalikuwa yakiendelea kichwani mwangu,..nikiwa sijui ya kesho yangu itakuwaje,

Je niamua nini, je hayo maamuzi yatakuwaje..

‘Haaah, …na leo ndio natakiwa kusema kile nilichokuwa nimejiandaa nacho, kiukweli hadi tunafika hapa bado mimi sijaweza kuwa na maamuzi ambayo ninaweza kusema ni sahihi kwangu…ndio ukweli wenyewe, utasemaje sasa, wakati …huna msaidizi..

Nilimuomba mungu wangu sana, na …akilini nikawa nawaza, ni kwanini najisumbua akili yangu wakati maamuzi tayari yalishajionyesha,…nilipoliwaza hilo, nikapumua, ni kweli mola ni wetu sote na kila kwenye shida, kila kwenye shinikizo la mawazo, mtegemee yeye, atakuongoza tu…

‘Nasema hilo kiukweli…maana maamuzi sio lazima mtu ayaongee, vitendo vitasadikisha hilo…ila kama alivyosema mwenyekiti, tunaomba sote mungu atupe hekima ili jambo hili liishe kwa amani na upendo, na mimi namuomba iwe hivyo....’nikageuka kumwangalia mume wa familia.

‘Pamoja na yote hayo, mume wa familia alipotoka rumande, huko alipokuwa ameshikiwa na polisi yeye na wenzake, maana imempita muda kidogo…, nilijaribu kukaa naye ili nione jinsi gani tutasaidiana kulitatua hili,...

‘Hili jambo, ni jambo gumu sana kuliamua peke yako, unaweza ukalitatua kwa jaziba, kwa hasira, mwisho wake ukaja kutulia ukaja kujijutia, na ni rahisi kuliongea kwa maneno ya haraka, lakini madhara yake ni makubwa, maana hili tatizo halinigusi mimi tu, linagusa kizazi changu ....ndio maana nimekuwa nikiliwazia sana.

‘Tulipoweka makubaliano, yetu, kila mmoja aliyapokea makubaliano yale ambayo yakaja kuwa mkataba wetu wa familia, …tuliyaweka kwa furaha tu.., na mimi sikutarajia kuwa mwenzangu angelikuja kuyafanya hayo aliyoyafanya,sikuamini..ndio maana wengine waliniona mimi kama mjinga….yanaonekana wazi machafu, lakini mimi nikawa nimeyafumbia macho…sikuamini…hamjui tu siku tunawekeana hayo makubaliano yetu ilikuwaje,

‘Kiukweli kwangu ilichukua muda sana kulikubali kichwani, inafikia hatua unaona kama unaishi na watu wawili tofauti, na kwa ujumla nimekwazika sana sana..sio siri, sijui nitakuja kumuamini nani katika dunia hii..

‘Wazazi wangu lazima niwaamini, nazungumzia, mume….’nikatulia

‘Kiukweli sikujua kuwa unaweza ukaishi na mtu, mkachangiana naye kila kitu, ukampa moyo wako wote, kumbe mwenzako hayupo nawe kabisa, kumbe mwenzako anaye anayempenda kwa dhati…, wewe upo kwa ajili ya kutumika tu...ni dhuluma ya hali ya juu…’nikatulia huku nikionyesha uso wa huzuni.

‘Nimejaribu kuongea na mwenzangu ili nione vipi tutasaidiana kwa hili, kama binadamu, sikutaka kuwe na unyonge, kuwa kwa vile mimi nina hali hii au ile, ...kwahiyo nilimtaka ajitoe, aseme anataka nini, atoe ukweli wake ulio moyoni mwake...lakini haikuwa kazi rahisi...’nikainama kama nasoma kwenye karatasi.

‘Haikuwa kazi rahisi ndio maana nasema kwanini niumize kichwa wakati …ukweli upo wazi…’ nikatulia.

‘Kwa ujumla kama mlivyoona, nia na malengo ya mwenzangu na mwenzake, ilikuwa ni kupata maisha mazuri..hiy ndio ilikuwa ndoto yao…wenyewe wamelibainisha hilo, kwa kauli yam dada, japokuwa mume wa familia, kwa nafasi yake hakutaka kuliweka hilo bayana…kiukweli hawakuoa au kuolewa kwa mapenzi ya dhati ...’nikatulia

‘Kwahiyo wakatumia hadaa, wakajipatia mume na mke, ambao wana kile walichokitaka…, lakini nafsini mwao bado kulikuwa na mapenzi ya mwenza wao, kama walivyoita wao, mpenzi wa asili. …unakuwa kama umelala na gogo au sio..

‘Nimeshasikia wengi wakisema waume au wake, wanaweza wakawa hivyo katika mapito ya maisha,..moyoni wanaoa tu , lakini wanakuwa na wapenzi wao wa asili, lakini siku zinavyokwenda, wanakuja kuyasahau hayo ya zamani, ya mapenzi yao ya asili…na wangi wamefanikiwa hivyo na maisha yamesonga mbele…, hilo lawezekana au sio…nikajiuliza kwanini sisi hilo lisifanikiwe...unaona eeh..’nikatulia

Sasa nilitarajia kwa mwenzangu kuwa huenda itakuwa hivyo,…ndio maana baada ya yeye kutoka huko rumande, nilipoongea naye akasema anahitaji nafasi ya pili,

‘Unahitajia nafasi ya pili kwa vipi…?’ nikamuuliza

‘Nahitajia kujirekebisha, …nimekosa basi, sasa unipe muda mwingine..’akasema

‘Kwani uliyofanya ulikosea,..au..?’ nikamuuliza

‘ndivyo ilivyoonekana, au sio..basi kwa vile ndio hivyo, nimeshajifunza, na mimi nipo tayari kuishi kama mume mwema. ..’ akaniambia hivyo.

‘Una uhakika na hilo…?’ nikamuuliza, kiukweli bado nilikuwa sina uhakika na hilo, japokuwa wazazi wangu wamenithibitishia hivyo, kuwa kwa mwanaume ikishatokea hivyo, basi hujifunza na hataweza kurudia makosa tena, ..mmh, ukishaumwa na nyoka kila ukiguswa na unyasi utashituka, huo ndio ukweli halisi kutoka moyoni...’nikageuka kumwangalia mume wa familia.

‘Mimi tukizidi kuongea nikamtolea mfano wa mpenzi wake wa asili ambaye kakiri makosa na kawa tayari kuchukua maamuazi magumu,...namsifu sana huyo mdada, ni mdada wa pekee sana…yeye amekomaa kiutu uzima, hongera zake na namuombea mola afanikiwa katika maisha yake..

Mimi nikamuuliza mwenzangu,

‘Unaona mwenzako alivyofanya, kaithibitishia dunia kuwa yeye yupoje, na ya kuwa yeye yupo tayari kusamehe kila kitu, kwa ajili yako, je wewe una msimamo gani,…?’ nikamuuliza

‘Msimamo gani…si nimeshakuambia, haya yote yamefanyika kwa chuki tu, mimi bado nasema hivi ndoa yangu haitavunjika kwa lolote lile…’akasema

‘Sasa ndoa huvunjwa kwa kosa gani..?’ nikamuuliza

‘Kosa hata liweje, mwenye mamlaka ya kuvunja ndoa ni mwanaume…’akasema

Unajua huyu mtu hadi hapo hakuwa amenielewa…nini lengo langu la maswali hayo yote,nilimuuliza maswali hayo kimtego kuona moyoni mwake yupoje..

Sawa anakiri kuwa kakosea, lakini kwanini aliyafanya hayo makosa, kajibu vipi…

‘Mim niliyafanya hayo kama mume wa familia, nikiwa na lengo jema la familia yangu…niliwajibika kama mume wa familia, kiukweli majibu haya yalinivunja nguvu...’

Mke wa familia akatulia halafu akawaangalia wajumbe na kuendelea kusema;

‘Hebu angalieni hilo jibu katikati ya mstari kwa hekima..kweli mtu baada ya kukosea,angelitoa kauli hiyo, kuwa aliyafanya hayo japokuwa ni makosa, lakini aliyafanya hayo kama mume wa familia, ..

Haaah.....nikaona bado kumbe mwenzangu anaona kuwa alichofanya ni sahihi,na kwahiyo hali hiyo huenda inaweza ikatokea tena....’kama mume wa familia..si ndio hivyo maana yake…au nimuulize tena hapa mbele yenu asema ni kwanini aliyafanya hayo makosa..’nikasema

‘Hapana..huo sio muda wake tena, huu ni muda wako wa kutoa maamuzi..’akasema mwenyekiti.

Najua na siwezi kumuuliza hayo maswali mbele yenu tena,maana majibu yake yameshapigiwa mstari…..mwenye akili anaweza kuyatathimini, hata kwa akili ndogo tu…

Kiukweli mkiishi sana, ndani ya ndoa, mnajenga udugu, ni zaidi ya udugu, mnakuwa kitu kimoja, na swala la kuachana ni gumu sana, hata kama itakuwa ni kwa jaziba…sio rahisi kuchukua hatua hiyo…

Na mimi nimeliwazia sana hilo…unajua unapokosewa nijuavyo mimi, yule mkosaji ndiye anatakiwa kufanya juhudi za kulimalizia hilo tatizo,…ni hekima au sio…sasa nyie kama wajumbe mngelipenda kuniuliza swali kama hilo moyoni, je mume wangu tokea muda huo aliwahi kuifanya hiyo juhudi…

‘Huyu hapa muulizeni.’nikasema na hapo mume wa familia akataka kuongea lakini mimi sikumpatia nafasi, nikaendelea kuongea…

Tutaendelea na sehemu hii ...kidogo tu, ili siku isiidhe bure, tutakuja kwenye hitimisho la isa chetu mola akipenda.

WAZO LA LEO: Maamuzi ya hekimakwenye matatizo, huhitajia muda, huhitajia msaada wa yule aliyetuumba, sio kwa akili tu ya kibinadamu. Wengi wetu hukimbilia kutoa maamuzi yao, kwa jaziba,…au kuwa ‘usomi’ walio nao…lakini baadae wanakuja kukiri kuwa walifanya makosa.

Subira ni muhimu sana kwenye matatizo,…
 
SEHEMU YA 125 ......... MWISHO PART 1/2


‘Kama ni kweli, mtu umekosea ulitakiwa kukiri kosa na kuomba msamaha jamani au sio…?’ nikawauliza wajumbe wengi wao wakatikisa kichwa kukubaliana na mimi..

Mume wa familia akawa bado kainamisha kichwa chini...

‘Lakini hilo halikuwahi kutokea hadi tunafika hapa, ina maana kazi yetu yot hapa hakiweza kufanikiwa…umeona hata hayo maswali niliyokuwa nikimuuliza yalikuwa ni namna ya kumzindua, lakini yeye, aliona kama ninamkera,…’nikageuka kumuangalia.

Bado alikuwa kainamisha kichwa chini...

‘Sasa..labda ni mimi ndiye niliyekosea, ni mimi ndiye natakiwa kuhangaika, kumuomba msamaha…au wajumbe nimekosea, je ni nani anastahili kumbembeleza mwanzake, kwa hali kama hii,…ni mkosaji au ni yule aliyekosewa...?’nikawa nimeuliza hivyo, lakini sikutaka jibu la mtu nikasema

‘Mimi kwa uoni wangu naona bado kuna tatizo, na huenda hilo ni tatizo sugu...nakiri kusema hivyo,…mungu anisamehe tu…’nikainama kidogo.

'Unamuuliza mtu swali kwanini ulifanya hivyo, makosa kama hayo... anakujibu nilifanya hivyo kama mume wa familia katika kuhakikisha familia yangu inakuwa salama,…na nilifanya hivyo kama kuwajibika,....hivi hayo makosa yalikuwa na muenendo huo….sawa labda...yapo, ...mengine utasingizia kuwa alifanya hivyo kwa kulazimishwa, labda kwa vile…lakini yaangalie hayo makosa, na muda yaliyofanywa…

‘Sasa kiukweli kwa majibu hayo, ilinifanya nifikirie mara mbili je ni nini mstakabali wa maisha bora ya mume na mke mwema...hivi nifanye nini mimi...unajua ni kazi kubwa sana kuchukua maamuzi hayo magumu!

‘Je…, ni, nini mstakabali wa watoto wangu...watakuwa wakiuliza baba yupo wapi...lakini je wataishije..watajifunza nini,, ili wawe na maisha bora, tabia njema,..ili waje kuiga tabia ya wazazi wao..’hapo nikageuka kumuangalia mume wa familia ambaye kwa muda huo alikuwa bado kainamisha kichwa chini, lakini sasa alikuwa akiniangalia kwa kujiiba.

‘Je maisha mema,…ndio hayo ya kutumia ubabe, uwongo, hadaa, ulevi... na ukikosa hutaki uambiwe umekosa, badili yake unatafuta visingizio...na zaidi hutaki kukiri kosa, …..hapana hatuendi hivyo, mimi sikulelewa hivyo...’nikamwangalia mwenyekiti, na mwenyekiti alikuwa katulia akijifanya anaandika andika.

‘Wazazi wangu nawashukuru sana kwa hekima zenu, kwakweli najisifia kwa kuwa na wazazi kama nyie, kwani mnafahamu jinsi gani ya kuishi na watu, kwani baada ya haya yote nilitarajia mungelikuwa na hasira na kuniambia kuwa mimi nimejitakia,…’nikatulia tena nikiwaangalia wajumbe.

‘Ni kweli kwa haya nimejitakia, mwenyewe, wema wangu ndio umeniponza…kwani mlishanikanya lakini sikuwasikia..nikajiona nimekuwa, nikajiona naweza kujibea mimi mwenyewe..sasa muda umefikia .., nibebe mzigo wangu mwenyewe, lakini baada ya yote haya mumekuwa mstari wa mbele, mkiniomba haya tuyamalize kwa amani, tusameane....ikibidi turejeane...kama mke na mume...haya nilikubaliana na hayo mawazo yenu, je ..mume yupo tayari kwa hilo…

‘Nimewaelewa sana, na mimi kama binadamu nahitajika kujirudi, kusamehe na kuangalia kuwa kweli kuna kuteleza, kuna kukosea,..na mkijitambua kama wazazi, kama mke na mume kama binadamu mwenye utashi, mnaweza mkayasahihisha makosa yenu mkaendelea mbele..nimelikubali hilo, ...’nikatulia.

Wajumbe wakajikuta wakipiga makofi, sikuelewa wanapiga makosa kwa lipi hasa, lakini sikuwajali kwa muda huo, …mwenyekiti alikuwa akiniangalia tu, mama alikuwa kainamisha kichwa chini…

‘Kabla ya kutoa maamuzi yangu, mimi nimefikiri sana, nikaona kuna haja ya kufanya yafuatayo..’nikasema hivyo na hapo mume wa familia akainua kichwa kuniangalia…Nilitulia kwa muda,…mpaka watu wakafikiria nimeshindwa cha kuongea..

‘Kwa vile mume wa familia lengo lake kubwa ni mali, lengo lake kubwa ni kupata utajiri, lengo lake ni kubwa ni kuwa na hali nzuri, basi, mimi kwa ridhaa yangu mimi mwenyewe nimekubali kumuachia kampuni yake, kwa asilimia mia moja…’nikasema hivyo

‘Yeye ...achukue hisa zote, na amilikishiwe moja kwa moja kama kampuni yake binafsi, …. Mimi sitakuwa na hisa tena kwenye kampuni hiyo, ina maana ni mali yake moja kwa moja...hilo mimi nimeliamua kwa moyo wangu wote, kuonyesha mapenzi yangu kwake..na hili wazazi wangu naomba mnisaidie hata kama kuna madeni, myasamehe…’nikasema na kumuangalia mwenyekiti.

Mwenyekiti akatabasamu kidogo, akawaangalia mawakili, lakini hakusema neno.

‘Kwa kufanya hivyo, sasa yeye ni tajiri, kwani ana kampuni ambayo ni yake, ambayo itakuwa haina madeni, na madeni yake anayodaiwa mimi nitajitolea kuyalipa, ina maana madeni ya kampuni hiyo yatahamia kwangu, unataka nini tena wewe mwanaume...’nilimuona mwenyekiti akiniangalia kwa macho makali hapo.

Nakumbuka wazo kama hilo niliwahi kuongea na wazazi wangu wakanipinga sana, kuwa kwa kufanya hivyo namdekeza mume, lakini mimi nikaona ndio njia pekee ya kumsaidia mume w familia, ili afikie malengo yake na huenda akajirudi na kufanya zaidi ya hapo.

‘Mimi nitabakia na kampuni yangu na hisa za mume wangu zitaondolewa kwa vile nimeshamkabidhi kampuni yake awe yeye ndiye mumiliki, na mimi sitajihusisha na kampuni yake tena

‘Ila kama akitaka msaada kwangu,kwa ridhaa yake yake mwenyewe nipo tayari kumsaidia…lakini sasa..

Katika hilo, wapo watu wa karibu yake, watu waliopigana naye bega kwa bega, hao hawezi kuwaacha, lakini hayo ni kwa utashi wake..anaweza kuwauzia wenzake hako hao hisa kama washirika wenza…

‘ni vizuri kufanya hivyo, ili kuonyesha wito wema, nakushauri ufanye hivyo ili kuonyesha ukomavu, na ubinadamu, au sio…watu hao ni aliyekuwa rafiki yangu,... na pia amuuzie, mpenzi wake wa asili baadhi ya hisa, hili ni pendekezo langu ndio maana nikaamua kuyachukua mdeni yote ili muweze kuanza kwa pamoja.

‘Nwaombe mfanya kazi hiyo kwa pamoja na kwa bidii kubwa,..nina imani kuwa mtafanikiwa,…nawafahamu wote kuwa ni wachapakazi…hodari…, hii itawasaidia wote, na ile ndoto yao ya kupata utajiri itakuwa imekamilika,..natumai wakiwa pamoja wataweza kufanikisha hili jambo, na ndio njia mojawapo ya kusaidiana..

‘Mimi nimeona tusaidiane kwa hilo, ili kila mwenye nacho amsaidie na mwenzake, kwani huenda haya yote yasingelitokea kama watu tungelipendana, wale walio nacho japo kuwa kidogo, wawasaidie wale wasio nacho, na kupandishana, katika namna ya kupeana majukumu, sio kupeana tu kama zawadi...ingelikuwa hivyo, nina imani dunia hii ingelikuwa ya upendo na amani..

‘Lakini pamoja na yote hayo, nafahamu kuna watu hawatosheki, nafahamu mtaka nyingi nasaba, anaweza akakosa yote, kama bado mume wa familia hajatosheka na hilo…’ nikatulia kidogo

Mimi nilimuuliza swali kubwa, je yeye anataka nini…hakunielewa nilikuwa na maana gani, nilitaka awe muwazi tu….hakuweza kunijibu, ila mimi nimeona ni kitu gani anakitaka, sasa je hilo hajatisheka nalo…

‘Kama hajatosheka na hili sijui mimi nitamsaidiaje, mimi kwa mtizamoo wangu, kama yeye hatariziki na hilo, itabidi twende mahakamani,…itapibidi turudi mahakamani ili sasa sheria ichukue mkondo wake,.. ili haki yake ipatikane, anayoitaka yeye,..

Na ikiwa hivyo basi mkataba wetu upo wazi utasimama hayo yote,..mkataba wetu ni ushahidi tosha, mengi tuliyaficha ficha ili kesi ibakia huko kwa wauaji watu, lakini haya yetu tuliona tuje tuyamalize hapa nyumbani..

Sasa kama mume wa familia hajarizika na hilo, basi mimi sitarudi nyuma tena, ...mkataba utafanya kazi yake na yeye hatakuwa na haki ya kupata kitu chochote, sasa ni uamuzi wake...’nikasema na kumwangalia mwenyekiti.

Mwenyekiti akatulia kwa muda halafu akaniuliza, ...’mbona hatujakuelewa, hatujasikia maamuzi yako, au hayo ndio maamuzi yako ya mwisho..., ?’

**********

‘Nilisema kabla sijatoa maamuzi yangu,nilitaka niyaweke hayo wazi, nilitoa hayo kama utangulizi, kabla sijatoa uamuzi wangu, ...nimefikiria sana…

Kwanza…nielewe wazi, moyoni nimeshasamehe yote yaliyotokea, na walionikosea nimeshawasamehe, akiwemo mume wangu, rafiki yangu na wengineo ....kama binadamu yeye anastahili kusamehewa, natumai hatarejea makosa kama hayo tena.

Niliposema hivyo mwenyekiti akatabasamu, mama ndiye aliinua kichwa akaniangalia kwa macho ya mshangao…

‘Kama alivyosema mwenyekiti, kusamehe ni wajibu wangu, ni hilo nimelitimiza, na nilishamwambia mwenzangu kuwa sina kinyongo nayeye tena.., lakini nataka kuyasema haya kama binadamu wa kawaida..

‘Baada ya yote hayo na kuyapima yote kwa makini zaidi, mimi nimegundua mengi, ambayo yatanifanya nitoe maamuzi yangu kama binadamu, natumai mtanielewa, kwa hayo nitakayo yasema....’nikatulia na watu wakaguna, kukawa kimiya.

‘Unajua kuna kitu kimoja nimekiwaza sana…ndoa ni ya mke na mume, ni mafungamano yenye usawa, kila mmoja anawajibika kutegemeana na hali yake..na nafsi ikubaliane na hilo..kama nafasi haitaki huwezi kulamisha, au sio..lakini kama unaweza ukasema nitajitahidi basi, pambana na nafsi yako..mungu atakusaidia,...

‘Nilishaongea na mwenzangu na kumtaka asome katiba yetu vyema, ili sije akasema mimi nilikuja kubuni Katiba nyingine, lakini alikataa..hilo.

‘Yeye alikuwa kaninunia tu, na kubakia kuniangalia kwa macho ya hasira na chuki,na alipoanza kuongea alikimbilia kunilaumu mimi na wazazi wangu kuwa ndio tumesababisha haya yote, hadi akawekwa ndani, kwa kosa ambalo hakulifanya, na aliyofanya yeye, alikuwa akiyafanya kwa minajili ya kuilinda familia yake, alijitolea muhanga kwa ajili ya familia…ni sawa, kama mlivyoona au sio kwa hilo namshukuru sana.

‘Lakini hawezi kututupia sisi lawama mimi na wazazi wangu....jamani hivi ni sisi tuliofanya hivyo, au ni matendo yao mabaya... je kwa hayo aliyoyatenda ni nani angelistahili kumkasirikia mwenzake...hapo mimi sikumuelewa...’nikatikisa kichwa.

‘Ina maana kweli mtu hajajifunza kwa hayo yaliyotokea, kuwa yeye ndiye mkosaji, yeye ndiye aliyestahili kuomba msamaha, na kunyenyekea kwangu, na kwa hawo walioathirika kutokana na matendo yake machafu.

Hivi kama mzazi, angelifurahia mtoto wake afanyiwe hivyo, au hata hilo la kumbaka mtoto wa kazi ni mbinu za marehemu…, kamuharibia mtoto wa watu mipangilio yake ya maisha...hilo halioni, na lo hilo ni kosa langu.

Haya labda..kama anavyodai labda, mimi sikuweza kumtosheleza…...yote kwake anaona ni kuwa hay a aliyoyatenda kama mume wa familia,..yeye anaona alivyotenda ni sawa tu kama anavyodai kuwa alifanya hayo akijua anawajibika kama mwanaume,labda kwa vile alikuwa akitafuta mtoto wa kiume, lakini kawapata wangapi, mbona alikuwa bado hajatosheka

‘Kwa mtizamo huo ninakuwa na mashaka, ,...msahamaha upo pale pale, nimeshamsamehe…lakini…’nikatulia kidogo

‘Huenda mwenzangu bado haajtosheka, huenda mwenzangu bado anahitaji muda wa kujirusha na kila mwanamke anayempenda, huenda nafsi yake ilikuwa haijatulia, ndio hivyo tena, yeye alinioa tu kwasababu kuna kitu alikitaka,…mali,

Lkini mali haiji hivi hivi, inabidi tufanyie kazi, ndivyo nilivyokuwa nafanya mimi, nilijitahidi kumjenga afahamu hivyo, natumai atayakumbuka maadili yangu kwenye kazi zake.., akiwa kama kiongozi mkuu, atajua kwanini nilikuwa namfanyia hivyo, akiwa sasa hamtegemei mtu atakuja ni kwanini nilikuwa nafanya hivyo....’nikamwangalia na yeye akawa ananiangalia kwa macho ya dharau hivi.

‘Sasa mimi nimeona nimpe kile alichokuwa akikitaka, natumai moyo wake utarizika, na huenda akatulia, ..huenda, akawa mume mwema, na kuweza kujenga familia yake kwa amani na upendo, maana watu wa namna hii hawatosheki bwana, lakini sasa atafanya hivyo akiwa anataka nini tena,...’nikatikisa kichwa kama kusikitika.

‘Mimi nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kutimiza wajibu wangu,sikuwahi kuvunja masharti makubwa ya ndoa hata siku moja, ina maana mimi nilikuwa mjinga, au sikuwa na vishwawishi vya hapa na pale…ina maana mimi sikuwa na tamaa ya kimwili,..

Wapo watu walikuwa wananikera, lakini mimi nilifahamu kabisa kuwa ni mwanandoa, na ndoa ina masharti yake, ...nikayatimiza, ina maana mimi nilikuwa sina hisia za kibinadamu kweli, ina maana mimi nimeumbwa kwa jiwe, hapana sio kweli hata mimi kama binadamu hali kaam hiyo ilikuwa ikinishika, lakini niliweza kuitawala nafasi yangu.

‘Kwakweli kila nikiliwazia hilo ninaumia sana, kwa ujumla nimekwazika kupita kiasi, nimezalilika, hasa pale ninapoambiwa sikuweza kutimiza wajibu wangu ndio maana mwenzangu akafanya hayo...

‘Jamani..hamfahamu jinsi gani mwanamke anavyojisikia pale mume wake anapotembea na wanawake wengine wakati yeye ni mke wa ndoa, inaumiza mtu kisaikolojia, unajiuliza mawali mengi, hivi mimi nina kasoro gani, hivi..hivi...unaumia sana, lakini ni nani atalifahamu hilo...’nikasema kwa machungu.

‘Lakini mungu ni mkubwa ukweli mara nyingi una nguvu, ukweli ukadhihiri, ukweli ukajileta, na mambo sasa yapo hadharani, kumbe hayo waliyapanga hata kabla hawajaingia kwenye ndoa, walichokuwa wanakitafuta ni sababu tu,...na sababu ikapatikana,…tunabakia kumsingizia marehemu…

‘Sawa mimi nakubali nifanyeje sasa…au sio.. ndiooo, kama binadamu hata mimi nilikuwa na madhaifu yangu, kama alivyodai, kuwa mimi mara nyingi sikuwa karibu naye, kutimiza wajibu wangu wa kindoa

Lakini hilo lilikuwa swala la kuongea, mimi ningelimuelewa au sio....hakuniambia, hakulalamika mbele yangu…mume na mke ni kuambizana, kubembelezana, ..ina leta raha zake…, akafanya aliyoyafanya kwa wale wa chapu chapu, wasiohitajia hayo, pesa ikaongea au sio.....lakini hicho ni kisingizio tu, walishayapanga hayo kabla, wakishirikiana na mwalimu wao...wameshajieleza hayo, ushahidi upo…

‘Udhaifu wangu, haukuwa wa kuvunja masharti makubwa ya ndoa, ni yale ya kibinadamu na kwenye mkataba tuliyaanisha hayo, yapo mapungufu ya kibinadamu, yanasameheka,....sio hayo aliyoyafanya yeye, ya kukiuka miiko ya ndoa, na kwenda kuzini nje, hadi kupata watoto, hawo watoto wanadai haki yao, kwanini walizaliwa hivyo, na wengine wanatelekezwa

Haya mnayaona mitaani au sio..haya ni kwasababu ya tamaa ya watu kama hawa wasio na maadili mema, hawa watu tutaishi nao mpaka lini, kwanini kusiwe na njia ya kuwawajibisha, eti jamani mimi hapo nakosea, ni lazima wawaji-...’nikasema na kumwangalia binti wa hiari wa wazee wangu, aliyekuwa mfanyakazi wangu wa ndani, alikuwa bado hajaondoka. Alikuwa analia…

************

‘Na nimesahau jambo moja la muhimu sana, huyu binti wa hiari, nimeamua kuwa nitamuajiri mimi kwenye kampuni yangu, nitaangalia jinsi gani ya kumsaidia,kabla hajapata hiyo ajira.

‘Naamua kuchukua dhima hiyo, kwa vile mimi ndiye niliyekwenda kumchukua kwa wazazi wake, yeye alikuwa katika mikono yangu na yote yalitokea kwenye nyumba yangu, mimi ndiye nabeba dhamana hiyo, mimi mwenyewe nitamsomesha na nina imani baada ya miaka mitatu atakuwa tofauti...namjenga rafiki mwingine mpya

‘Mimi...sitachoka kusaidia watu pale inapowezekana, nina imani baada ya muda huo, hatakuwa huyu binti tena....’nikasema.

‘Baada ya kusema hayo, ... ..., kama ilivyoanishwa kwenye mkataba wetu wa hiari, na kutokana na ushahidi uliotolewa mimi nimeona ndoa yetu ifikie kikomo na kila mmoja aangalie ustaarabu mwingine, kwani hata bila kauli yangu hiyo ndoa ilishavunjika, au sio jamani…?’ akawa kama anauliza

‘Ndio hivyo hata kidini, kaulizeni mtaambiwa,..maana mkataba tulisaini wenyewe kwa hiari zetu tukiwa na akili timamu,…tukakubaliana mtu akazini…na ushahidi ukapatikana, adhabu yake ni nini… mungu ni shahidi yangu kwani kanisaidia kutoa ushahidi…, ni dhahiri kuwa ndoa haipo tena...

‘Mwenyekiti alisema kama mtu hajatenda hiyo dhambi ajitokeze, haya mimi hapa najitokeza sijawahi kuifanya dhambi,...mungu ni shahidi yangu, na hata kama watu waliniona nikiwa na docta, tulikuwa naye tukiongea tu, mimi na yeye hatukuwahi kuvunja amri hiyo kwenye mkataba wangu,...kwahiyo mimi nimetimiza wajibu wangu,…

Hapo mimi nitasemaje nawaombeni mnisaidia hapo…ni kweli mimi nilimpenda mume wangu lakini je kuna upendo wa sehemu moja….atasema ananipenda, je ni kweli ananipenda, upendo wa kuigiza, hapana asema ukweli wake tu,..na ukweli upi tena,...naombeni sheria ifuate mkondo wake....

Na naombeni mnielewe, Maamuzi yangu ya kuachana na mume wangu, ni kuonyesha upendo wangu kwake, kuwa mimi najali hisia zake,...kuwa yeye ana mpenzi wake wanayependana naye sana, ..mpenzi wake wa asili…

Najua hata alipo anatamani awe naye, lakini kutokana na nakama za kimaisha, walishindwa, sasa wanazo mali, sasa wao ni matajiri, wanaweza kuishi kwa raha, nafiki ndoto yao sasa imetimia, au sio wenzangu...sasa wana mali, ...kwanini nisiwape nafasi hiyo,sitaweza kuwadhulumu kwa hilo, ndoa yangu na mume wa familia imekwisha, na nashukuru mungu kwa yote hayo, na sio nasema hivyo kuwa nina kinyongo tena, hapana nimeshawasamehe...

‘Ninachokifanya hapa ni kuwa sitaki kuwatendea dhuluma kwa vile walikuwa na hali hii au ile, nimechukua maamuzi haya magumu, kwa vile nampenda sana mume wangu, na nataka arikie na nafasi yake...’nikatulia kidogo.

‘Kama mlivyoona, mimi nilikuwa na mume ndani, nikijua kuwa mwenzangu yupo na mimi kumbe alikuwa akinivunga, na kunipaka mafuta kwa mgongo wa chupa....sasa muda umefika, yeye na mchumba wake wa asili wapo huru, baada ya taratibu zote za kuvunja ndoa yangu, talaka na kila kitu, wao watakua huru kuoana...hakuna kizuizi hapo,...’nikasema na kumwangalia aliyekuwa mke wa docta.

‘Lile swala la kuwa eti kwasasa kajifunza, hatarudia tena, mimi bado linanitia mashaka, na ninaona nisitumie mwanya huo kuwaharibia upendo wao na mpenzi wake wa asili, nilishaongea na mpenzi wake huyo na tumekubaliana mambo fulani fulani, ..

'Kwa ujumla mimi sioni kwanini wasioane, wanahitaji nini tena, sioni kwanini mpenzi wake huyo aende akaanza maisha ya kipeke yake huko kijijini, akae hapa, wafanye kazi, tumeshaliongea hilo na yeye japokuwa hakukubali moja kwa moja, lakini natumai wakikaa na mwenzake, watakubaliana kuhusu hilo..’nikasema na kugeuka kumwangalia mume wa familia halafu aliyekuwa mke wa docta.

Docta alikuwa kashika shavu utafikiri hayupo kwenye kikao, naona alikuwa akiumia sana moyoni.

‘Sasa kazi ni kwenu wapendwa..ila cha muhimu, nawashauri tena na tena, kazi kwanza, hayo mengine baadaye, ni muhimu sana hilo, muhangaike, ili muweze kuuendeleza huo utajiri kwani haukuja kirahisi hivyo, unahitajika kuwajibika, msilale, fanyeni kazi kwa bidii, nina imani mtafanikiwa, na kama mkihitaji ushauri wangu mimi nipo, tutasaidiana pale mtakaponihitajia, lakini kwa nia ya kutoa ushauri tu.

‘Ama kwa yule aliyeitwa rafiki yangu, mimi sina kazi naye tena , nilichofanya kwake ni kumsaidia, na kwa vile keshakuwa na anaweza kujichukulia maamuzi yake mwenyewe, basi, ....naona nimuache, kama nilivyoshauri, yeye apewe hisa kwenye hiyo kampuni,wanaweza kujiunga kwa pamoja wakajenga kampuni yao ikawa yenye nguvu.

Mimi nina imani nguvu hizo zikukutana kwa pamoja, kutakuwa na maendeleo makubwa sana..kwasababu nyote mnafahamiana, au sio...yeye sasa ana uwezo huo , hata wa kujiajiri yeye mwenyewe...sina wasiwasi na yeye, ...na nimemwambia kama atahitajia msaada kwangu mlango upo wazi

‘Hayo ndio maamuzi yangu, na sina zaidi naomba mawakili wetu wayaweke hayo sawa, na taratibu zote za kutalikiana zifanyike kwa amani, nataka hili zoezi lifanyike kwa amani ili baadaye tukikutana tukutane kama marafiki, hakuna chuki wala kununiana, au sio jamani…

‘Hayo ndio maamuzi yangu na hakuna kurudi nyuma, nawaomba wazazi wangu walipokee hilo , wakijua kuwa mimi sasa sio mtoto mdogo tena....’nikasema nikiwaangalia mawakili wetu na wazazi wangu, nilimuona mama akipitisha mikon usoni na kujifuta machozi....

‘Na kwa hivyo basi, ili kuweka mambo sawa, na kumhakikishia mume wa familia kuwa mimi sina kinyongo na yeye tema, nawaomba mawakili, wafanye taratibu za kisheria kuziondoa hisa zangu kwa kampuni ya mume wangu na kumumilikisha yeye, ...na pia waziondoe hisa za mume wangu kwenye kampuni yangu, na madeni ya kampuni y amume wangu yahamishiwe kwangu..

Na kwahiyo mimi nitamiliki kampuni yangu peke yangu, na yeye na wasaidizi kama watakubaliana wataangalia ni nani apate kipi ...nafahamu mume wa familia atakuwa na hisa kubwa kama mumiliki, ..wengine watakuwa na hisa zao ndogo ndogo, lakini sitawasaidia kwa hilo, hilo wakubaliane wao wenyewe...

‘Na kwa vile mume wangu ndiye mkosaji, mali nyingine alizozikuta zitabakia kama zilivyokuwa, kama alivyozikuta, ni mali yangu na watoto wangu ...ama kwa nyumba, ile nyumba,…nyumba aliyokuwa akikaa kwa sasa baada ya kutoka kuumwa na kifungoni , ile ni mali ya kampuni yake, basi itakuwa ni mali yake, sina haja nayo, ...’niliposema hivyo, mume wa familia akainua uso na niliona ukikunjuka na zile hasira alizokuwa nazo usoni zikayeyuka..

Akatabasamu…

‘Mnaona wenyewe, ni nini kilichokuwa kikitafutwa, natumai keshakipata, mimi namtakia maisha mema, na hili liwe fundisho kwake, na kwa wenzake,....mwenyekiti mimi naona nimemaliza....’nikasema huku machozi yakinilenga lenga. Mume wa familia alikuwa kavaa miwani, naona ni kwa ajili ya aibu ya hayo yaliyotokea.

*************
Ikawa kuna kuongea, kufurahi kucheka, baadae mwenyekiti akapiga makofi na kusema;

‘Basi sisi kama wazazi, kama mumeriziana hivyo, natumai tulimalize hivyo,… au mume wa familia una la kuongea, je hujarizika bado?....maana bado wewe ni mume wa familia hadi hapo sheria itakapochukua mkondo wake...au nimekosea?’ akauliza mwenyekiti akiwaangalia mawakili,..

Mume wa familia akawa kimiya kwa muda, lakini baadaye akasema;

‘Sina la kuongea ndugu mwenyekiti…, nitaongea nini wakati maamuzi yameshapita....nimerizika…zaidi sina kwakweli..’akasema hivyo na kukaa kimiya huku akiwa kainamisha kichwa na ile miwani aliyovaa huwezi hata kufahamu anafikiria nini

Leo mume wa familia hakuvaa kama kawaida yake, .. leo alikuwa kava kinyumbani zaidi, kawaida yake kwenye vikao kama hivyo huwa anavalia suti safi..na tai shingni, huwa anajipenda sana…na hupenda kujionyesha kuwa yeye ni bosi fulani hivi, lakini leo,…akafika na t-shirt,…na suruwali ya jeans..alivalia kinyumbani zaidi. Nahisi alitarajia kuwa leo anakosa kila kitu.

‘Lakini ni vyema tukasikia kauli yako kama mume wa familia, hata kama mwenzako ameshaamua hivyo, je umerizika, muhimu ni hapo.. ...upo tayari kuendesha hiyo kampuni mwenyewe. Swala la talaka, mlishaongea wewe nay eye au sio.., na hapa ni kama taarifa tu, ....sasa hebu tuambie na wewe una kauli gani...’akasema mwenyekiti.

Hapo mume wa familia akainua uso na kusema….

‘Labda niongee tu, kwa vile mnataka kusikia kauli yangu..’akasema hivyo.

‘Mimi…, nasema hivi kama binadamu nina mapungufu yangu, hayo yaliyotokea ni kweli niliyafanya, lakini kipindi nayafanya nilijua natimiza wajibu wangu, hilo siwezi kuliacha kulisema maana ndio ukweli wenyewe, ulivyo kuwa..ndivyo nafsi yangu ilikuwa ikinituma hivyo…

‘Ndio wakati mwingine, nilizidiwa na kuyafanya hayo yasiyofaa, ni kweli ni hulka, siwezi kuikataa. Wakati unafanya unaona ni sahihi, ila matokea yake ndio yanakupa fundisho.....lakini nimejifunza, na nilikuwa tayari kujirudi,…nilishaahidi iwe hivyo, lakini mwenzangu hataki,....nitafanya nini sasa…

‘Sikuweza kujibishana naye, maana utasema nini, wakati mwenzako kashika mpini,..ni haki yake aamue hivyo, huenda tangu mwanzo alitaka iwe hivyo, lakini hakukuwa na mwanya huo,…aah, ndio mawazo yangu, si mumetaka niongee…’akasema hivyo aliposikia watu wakiguna.

‘Ndio hivyo… sasa mwanya umepatikana, na katimiza dhamira yake, sawa.....mimi nasema hivi kwa vile kaamua hivyo,…na kiukweli moyo wangu ulikuwa haujarizika, mnafahamu ni kwanini..lakini nianyeje, .. na iwe hivyo tu…, kama ningekuwa na njia nyingine ya kumshawishi kuwa sitarudia tena ningelifanya hivyo, lakini sina,...sina..japokuwa mke bado nampenda…hamjui tu..

‘Ni kweli, ...nilikuwa na hasira sana, nikiona nasota jela, ...mimi sijaua, mimi nilijitolea muhanga kwa ajili ya watu wengine,..nilikuwa sina jinsi, marehemu alishaniweka kati..nisamehewe tu, na yeye asamehewe huko alipo…ilikuwa niamua familia yangu au mimi…nilikuwa sina jinsi, nikaona ni bora nijitolee mhanga …sasa ni nani angeliamini hivyo, eeh..kiukweli inauma sana.....na ...sawa sitaki kulalamika sana na kwa vile yeye keshahitimisha, basi sina jinsi..

‘Kwa vile keshamaliza, na maamuzi hayo ni hitimisho…, mimi nimekubaliana na maamuzi yake, nitajitahidi kufanya yale yote yanayostahili niyafanye, na kwa vile tuna mafungamano ya watoto, mimi na yeye bado tutakuwa karibu, hadi hapo atakapoona yeye, au hali ikisema hivyo...natumai hatanifukuza nikifika kuwaona watoto wetu...wale bado ni kuinganishi chetu…nawapenda sana watoto wangu…

‘Nimekubaliana na yeye juu ya watoto kuwa waendelee kuwa kwenye mamlaka yake, kwa vile kaona kuwa yeye anaweza kuwalea katika malezi bora, yeye kaona wakikaa na mimi labda wataharibika , labda wataniiga mimi na tabia zangu mbaya…mmh,...

‘Hilo kiukweli nalikana,..sio kweli kuwa mimi ni mbaya kiasi hicho, inapofikia kwenye malezi ya watoto…mimi kama mzazi nitajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kuwalea watoto kwenye maadili mema….hata hivyo, mimi sikutaka kupingana naye sana juu ya hilo, kwa vile kwa kufanya hivyo tunaweza kuwaathiri watoto wetu kisaikolojia,...nawaombea sana wapate malezi bora wawe kama mama yao…

‘Sawa,mimi nimekubali, kwa vile nawapenda sana watoto wetu, na nia yangu ni wao waishi maisha mema, yasiyokuwa na tabia mbaya kama za kwangu..nimekubaliana na mawazo yake kuwa huenda nitaoa,..na hajui huyo mke nitakaye muoa,…atakuwaje…anaweza asiwapende watoto…mimi sijui hilo kwa kweli…na mimi nisingelikubali…hatahivyo sawa…hamna shida.

‘Ni kweli hata mimi nimeliona hilo, ...mimi kama mzazi nawapenda sana watoto, nisingelikubali mtu awatese, lakini kwanini tugombane kwa hilo, basi nimewaacha watoto wakae naye, sina kinyongo kwa hilo…kabisa kabisa…kwani nitakwenda wapi, bado nipo kwenye jiji hili, tutazidi kuwa pamoja tu.

‘Ama kwa kampuni…nashukuru sana kwa uamuzi wake huo..mzigo mnzito umeshaondolewa, madeni…kiukweli yalikuwa mzigo mnzito sana…

‘Hata hivyo, bado hata mimi,..nitajitahidi kuyalipa, sitaweza kuwamtumpia mzigo weote yeye peke yake…ndio maana nasema., mimi nitajitahidi kuiendesha hiyo kampuni kwa juhudi kubwa sana

‘Ni sawa…mimi nitakaa na wenzangu, kama alivyopendekeza yeye, mke wa familia, kuwa nishirikiane nao,…nitashirikiana na rafiki yake, kwani hata kabla , yeye alishakuwa msaada mkubwa kwangu… inabidi nifanye hivyo kwa vile pia ana damu yangu, napia eeh, …mmh, nitamshirikisha,na,.. ..na....’hapo akasita huku akimgeukia mpenzi wake wa asili kwa aibu, na mimi nikasema;

‘Mpenzi wako wa asili....mke mtarajiwa’nikasema na watu wakacheka, na yeye akainama chini kwa kutahayari, lakini akaendelea kuongea kwa kusema;

‘Na yeye pia ataingizwa kwenye kampuni, kwani anaweza…yeye na rafiki wa mke wa familia walikuwa wakifanya shughuli zao kwa pamoja…kwahiyo kwa pamoja, sote tutasaidiana..sijakaa nao, ila baada ya hapa tutakaa pamoja na kuona ni nini cha kufanya, natumai, hata wao wamejifunza mengi, na kwahiyo hatutafanya makosa ..kampuni hiyo itaimarika na kuendelea kama kawaida...hilo ninawaahidi.

‘Kiukweli mimi nimejifunza mengi , ni kweli namshukuru mke wa familia kanisaidia sana,...tena sana,...na kwa hivi sasa ninaweza kuiendesha hiyo kampuni bila ya kusaidiana na yeye, lakini kwa vile na wenzangu wana uzoefu wa kikazi, na wana haki hiyo, ...sitawatupa, nitakuwa na wao bega kwa bega...’akasema huku akiinua kichwa na kumwangalia mwenyekiti.

‘Na pia nawashukuruni sana wazazi, wakwe zangu kwa kunipigania na kunijali,..nafahamu kama ingelifuatwa sheria basi ningelikuwa sina changu tena...

‘Kiukweli sikutegemea kabisa kuwa mngelinifikiria na kunitetea hadi hatua hii ya mwisho, nilishawaona nyie ni maadui zangu, haah..kweli nimeamini kuwa nyie ni wazazi wenye hekima, sitawatupa, na sitawasahahu katika maisha yangu yote, nyie moyoni kwangu ni wazazi wa kweli...’akasema akimwangalia mama na baba yangu.

‘Hata hivyo sina budi kukiri kuwa nimekosa, nimesikia kila mmoja akitaka mimi nikiri hivyo,… ni kweli moyoni nakubali hivyo, lakini mara nyingi kutoa kauli inakuwa na ugumu fulani kwa vile wakati mwingine unahisi hivyo kuwa hujakosa..ndio hivyo, niseme huo ukweli.

‘Sasa….’hapo akatoka na kusimama mbele ya watu, akapiga magoti..

‘Hii naitoa kutoka moyoni, kuwa mimi ni mikosaji,nimewakosea sana..hasa mke wangu, hasa wazazi wangu, na jamii kwa ujumla..naowaombeni sana mnisamehe kwa makosa hayo…sijui nifanye nini ili mjue kuwa mimi nimekosa na nahitaji msamaha wenu..nikifika hapa..aah, sijui nilitaka mke wangu,..lakini keshaamua tena nifanyeje…’hapo akashika kichwa

‘Oh…, sitaweza kuongea zaidi ya hapa…, ahsanteni sana...’akasema mume wa familia huku akionyesha huzuni fulani kama anataka kulia.

‘ Inatosha…kweli hapo nimeamini kuwa umekosa, na sisi , …mimi kwa niaba ya wote tumekusamahe……kama hakuna muongeaji, labda tufunge kikao,..’akasema mwenyekiti, wakati huo mume wa familia bado kapiga magoti.

***********

‘Mwenyekiti samahani kidogo naomba nifanye tendo hili kabla hatujafunga hiki kikao...’nikasema na kwa haraka nikatoka pale nilipokuwa nimekaa na kumsogelea mume wa familia,…nikamuinua maana alikuwa bado kapiga magoti.

Na yeye akawa kama kashikwa na butwaa, nikamuashiria aliyekuwa mke wa docta aje, na yeye bila kinyongo akasogea pale nilipokuwa, kwanza nilichofanya ni kumkumbatia mume wa familia, na nikawambia;

‘Ahsante kwa yote, mimi kwa moyo mkunjufu.. nimekusamehe, na nakutakia maisha mengine mema, ..’na yeye kwanza alisita kunishika na mikono yake, ikawa inatetemeka hivi..baadaye akainua mikono na kunishika tukakumbatia kwa muda, halafu tukaachana.

Baada ya tendo hilo,…mimi nikamsogelea aliyekuwa mke wa docta, na kumshika mkono, nikasema;

‘Nakuomba tafadhali uje hapa…’nikasema, alipofika huyo, aliyekuwa mke wa docta, nikamsogelea mume wangu na kusema;

‘Mume wangu kama nilivyokuomba…naomba utimize ile ahadi yenu, mliyowekeana kule kijijini, wewe na mpenzi wako wa asili… mpange siku gani mtafunga ndoa halali, ....sina shaka na uchumba wenu.., maana ilivyo, moyoni siku zote mlikuwa wachumba, au sio, sasa wadhihirishieni uma kuwa kweli mnapendana, kwa kukumbatiana...’nikasema

Kwanza iliwashika kama butwaa…wakawa wamesimama huku wakiangaliana kwa hali ya kutahayari kidogo, na baadaye, wakasogeleana na kukumbatiana, huku machozi yakiwatoka, kilichofuata hapo ni...vigelegele na shangwe vikatanda.

Baadaye na mimi nikamkumbatia aliyekuwa mke wa docta, na tukachekeana, nikampongeza, halafu ndio nikamgeukia mume wa familia,...nikamshika mkono na kumkaribisha kifuani kwangu, tukakumbatiana, kumbatio la mwisho, kwa amani na kuagana, huku machozi yakinitoka, ilikuwa kumbatio la kwaheri.

Ni heri iwe hivyo..

Kulikuwa hakuna njia nyingine, ilibidi hayo yafanyike kwa masilahi ya wote, na namshukuru mungu, kuwa tulifikia muafaka, kwani baada ya kikao hicho, na kumbatio hilo la mwisho kama mume na mke wa familia, mawakili walifanya kazi yao vyema, ndoa ikavunjwa, talaka ikatayarishwa, na ikawa mwisho wa ndoa yangu na mume wa familia, yeye akaanza maisha yake na mimi maisha yangu.


MWISHO
 
SEHEMU YA 126 .........MWISHO PART 2/2



NB: Mume wa familia kama ilivyotarajiwa baada ya miezi mitatu walifunga ndoa na mpenzi wake wa asili, ndoa tuliyoisimamia mimi na docta na wazazi wangu, na ilifana kwa kweli, ...mimi nikawa best woman wa mke wake, na docta akawa best man wake...

Sio siri, yaliyopangwa na mungu hayapingiki, baada ya mvutano, na ushawishi mwingi wa docta, nilikubali turejeane urafiki wetu, na sisi mapenzi yetu ya asili yakarejea, nikakubali ombi lake kuwa tufunge ndoa, ahadi ikatimia, lakini ni baada ya miaka kama miwili hivi ya mvutano…

Nikaona haina shida…kwanini tujivunge…tukafunga ndoa, na sisi tukawa mke na mume.

Na aliyekuwa rafiki yangu, yeye aliendelea kumlea mtoto wake, na alisema hataki kuolewa tena, sijui kwanini, ...

Pengine hajapata anayemtaka, yote maisha,..yeye anadai alichokitaka keshakipata, yaani mtoto, na mdogo wake aliyekuwa mume wa familia yangu, alihamia Kenya na kuanzisha maisha yake huko, na yule mfanyakazi wa ndani sasa hivi ni mmoja wa mabosi ndani ya kampuni yangu..huwezi amini ukiutana naye …anamiliki gari lake na nyumba yake mwenyewe..

‘Hicho ndicho kisa changu mpendwa...’ akamaliza mdada


WAZO LA LEO: Mkioana na bahati mbaya ikafikia hatua ya kutalikiana na juhudi zote za kusuluhishwa zikashiniakana, basi achaneni kwa amani, kuliko kuishi huku mkiumia,fanyeni hivyo kwa amani na upendo, kwa masilahi ya watoto wenu, na mahusiano mema, ili mje kutembeleana kama marafiki wa zamani kwa upendo na furaha.

Natoa wazo hili sio kwamba napenda mawaza ya talaka, ila wakati mwingine inabidi iwe hivyo, kwani kuna mengine hayavumiliki, na hatuwezi kujidanganya kuwa tutaishi hivyo hivyo tu, ya mungu mengi, huwezi kujua ni nini kakupangia badili yake,hatuwezi kulazimisha kitu ambacho hakitakuwa na amani kwetu, tukaishi kwa maumivu na masononeko.

Japokuwa kiukweli,kuachana si kuzuri, hasa mnapokuwa na watoto, mkifikia kuachana basi peaneni mikono na muombeni mungu wenu, kila mtu aje kufanikiwa katika maisha mengine…mola anajua zaidi.


MWISHO



Madame S
 
NAWASHUKURU WOTE WALIKUWA NAMI TOKA MWANZO WA KISA HIKI, MUNGU AWABARIKI SANA, NINGEPENDA KUSIKIA MAONI YENU. TUPO PAMOJA,....


Mwisho wa kisa hiki ndio mwanzo wa kisa kingine.
💥 💥 💥 💥
kisa kipya kinachoitwa NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU

Kwa kubonyeza hapa chini:

Ndoa ilivyoteteresha imani yangu (Kisa Cha Kweli)
 
aisee asante sana bwana makabrasha yan umenikosha moyo hatimae tumeimaliza yan mimi sjui kaka ningekua na subra hio kusubiria maushahidi kweli kila mtu na moyo wake tukatane kule kina erica
 
aisee asante sana bwana makabrasha yan umenikosha moyo hatimae tumeimaliza yan mimi sjui kaka ningekua na subra hio kusubiria maushahidi kweli kila mtu na moyo wake tukatane kule kina erica

Sawa mkuu, karibu..
 
Back
Top Bottom