Mkulima awahamasisha Wasukuma kumkabili Bashe anguko la bei ya Pamba

Mkulima awahamasisha Wasukuma kumkabili Bashe anguko la bei ya Pamba

Joined
Jan 30, 2023
Posts
74
Reaction score
80
MTANZANIA Mzalendo, Thomas Nkola maarufu Mkulima kutoka Kanda ya Ziwa ametoa wito kwa wakulima wote wa zao la Pamba kuandaa mashambulizi ya kumkataa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwa kuua zao la Pamba kwa kumtuhumu kuwa ni mnunuzi mkubwa wa zao hilo akishirikiana na baadhi ya wabunge.

Kupitia Mitandao mbalimbali ya kijamii Nkola amepaza sauti za wakulima masikini wa Pamba ambao hawana uwezo wa kujitetea kutokana na umasikini wao akiwataka kuunganisha nguvu kumuangusha Bashe ambaye ameangusha bei ya Pamba kutoka Shilingi 2,000 kwa kila hadi Shilingi 1,000 na kuwafanya wakulima hao kudidimia kwenye umasikini huku yeye akitajirika.

Amewataka wasukuma kuacha unyonge na kutumia vizuri nguvu waliyonayo kujitetea kumkabili Bashe.
 
Wakulima wapiganie HAKI zao kwasababu kile chama ambacho kilianzishwa kwa ajili ya kuwatetea kimekuwa chama cha mafisadi na wala RUSHWA watekaji na wauaji.
 
Back
Top Bottom