Mkulima wa Tanzania vs Kenya

Mkulima wa Tanzania vs Kenya

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Nina rafiki zangu wanalima chai wilaya ya Rungwe, walikuwa wanalalamika bei ya chai ipo chini ukilinganisha na Kenya. Wanasema kilo moja wanauza 228Tshs, hawakusema bei ya Kenya ikabidi nitafiti. Nimeona msimu wa 2013/2014 kilo ilikuwa usd 35cents ambayo kwa sasa nikama Tsh 600!

Na hapo imepungua, msimu wa nyuma ilikuwa US 50cents. Najiuliza ni kwanini hawa wa Tanzania wanapunjwa hivi?

Mwenye habari tafadhali..
 
CCM wakale wapi?

Viongozi wa ccm walipora mashamba ya wakulima ya chai Usambara (Yamerudishwa)

Viongozi wa ccm walipora mashamba ya wakulima wa chai ya Lupembe (Kesi isiyoisha ipo mahakama kuu)
 
Tatizo la bei ndogo siyo kwenye zao la chai pekee. Ni mazao yote ya biashara, ndiyo maana wakulima wa kahawa wa Kagera huvuka mpaka na kwenda kuuza kahawa Uganda ambapo bei ni kubwa. Ushuru na makato mengine mengi ndiyo yanayowaumiza sana wakulima, pesa wanayolipwa ni robo ya dhamani halisi ya mazao wanayopeleka sokoni. Mara nyingi serikali huwakopa wakulima na hawalipwi kwa wakati.
 
CCM wakale wapi?

Viongozi wa ccm walipora mashamba ya wakulima ya chai Usambara (Yamerudishwa)

Viongozi wa ccm walipora mashamba ya wakulima wa chai ya Lupembe (Kesi isiyoisha ipo mahakama kuu)

CCM wamekufanyaje mkuu!
 
Nadhani chai ya kenya ipo demanded sana ndo maana bei ipo juu
 
Back
Top Bottom