Mkulo apasua jipu

Mkulo apasua jipu

Mpe cha Kaisari kilicho cha Kaisari. Kila kitu kilipiwe kodi tu.
 
Mkandara,
Utadhani ulikuwepo kwenye fikra zangu. Kila kitu ulichosema ndicho nilichofikiria mimi.
Huwezi kubadilisha sheria just because a few individuals misused that law. Kuna vyombo vya sheria vya kuwakabili. Kwa nini havifanyi kazi yao?

Ndugu yangu Jasusi, tuna vyombo vya sheria Tanzania!? au kuna vyombo vinavyofanya USANII WA HALI JUU huku vikataka vionekane machoni mwa Watanzania kama ni vyombo vya sheria. Tungekuwa na vyombo vya sheria ambavyo vinatenda kazi zao kama inavyotakiwa basi hawa mapapa wa mafisadi wangeshakuwa history katika anga za kisiasa Tanzania, lakini hadi hii leo bado wanapeta tu pamoja na ushahidi chungu nzima dhidi yao.
 
Kama anavyosema Askofu Kilaini kama una utitiri wa taasisi za kidini na asasi za kiraia ambazo baadhi yao zinatumia vibaya misamaha ya kodi, basi serikali inayozisajili ndo izidhibiti, sasa sioni tena haja ya viongozi wa kidini na asasi za kirai kupiga makelele wakati serikali imeanza kuchukua hatua hizo, na msimamo wa seikali naona upo wazi katika maeneo ambayo yatafutiwa misamaha ya kodi.
 
Kama anavyosema Askofu Kilaini kama una utitiri wa taasisi za kidini na asasi za kiraia ambazo baadhi yao zinatumia vibaya misamaha ya kodi, basi serikali inayozisajili ndo izidhibiti, sasa sioni tena haja ya viongozi wa kidini na asasi za kirai kupiga makelele wakati serikali imeanza kuchukua hatua hizo, na msimamo wa seikali naona upo wazi katika maeneo ambayo yatafutiwa misamaha ya kodi.

Junius,
Naona hujaelewa rafiki yangu. Mkullo amefuta sheria kwa kulalamika kuwa baadhi ya makanisa yameitumia vibaya. Kama waliovunja sheria hawajachukuliwa hatua na serikali na badala yake serikali inafuta sheria kwa sababu kuna walioitumia vibaya kinachoonekana hapa ni kwamba serikali haijafanya kazi yake kuhakikisha sheria inafuatwa. It is that simple.
 
Jasusi,

Unajua mkuu wangu wananchi wenyewe wanashindwa kuona pale serikali inaposhindwa kufanya kazi zake kisha wanailaumu serikali hiyo hiyo bila kuwaelezea ni wapi wanakosea..

Hakuna kanisa wala msikiti unaoendesha shughuli zake bila kutegemea misaada..hawa sii wafanyabiashara unless mnataka kusema dini ziwe biashara pia.

Sasa unapoondoa msamaha wa kodi iwe import au vyovyote vile kwa sababu wana abuse msamaha huo basi hata makusanyo ya fedha za kanisa/misikiti (sadaka) zilipiwe kodi.. kwani nako makanisa na misikiti zinatumika nje ya vyombo hivi.

Hao Bakwata wamewaibia waislaam fedha kibao kwa mamillioni lakini huwezi kuviadhibu vyombo vyote vya jumuiya za kidini kwa ushenzi wa chombo hiki..huu ndio mtindo unaotumika Tanzania kila siku ktk maamuzi mengi yaani tunatafuta shortcut..

BoT wameiba fedha wanaondolewa viongozi bila kuadhibiwa wanaletwa wengine walioiba NSSF... Mabadiliko wanayofanywa ni BoT kutoshughulika na fedha za EPA tena..ila bank ya .... ambayo viongozi wake baadhi wametoka BoT..Helooo!

Sasa kwa mnaosema NGOs walipie ushuru je mko tayari mashirika haya kutoza ada na kuuza nguo kwa watoto Yatima.. Mlipe entrance fee kila unapokwenda kusali kanisani/misikitini ili kufidia gharama za kodi walizolipa...besides, hili jukumu ni la nani haswa kila mmoja wetu akijikata kivyake itakuwaje?
 
mi nadhani serikali iko sahihi kuondoa misamaha kwenye vyombo vya dini,na im of the opinion kwamba sio tu watu wachache bali taasisi hizo zinajua zinavyonufaika na hiyo misamaha kwa maslahi ya wachache ndani yake,bora serikali ikusanye hela zote ili tujue zinakopotelea kuliko hali ilivyo kumbe zingine zinazama kwa watu waliojificha kwenye kivuli cha taasisi za dini!tutakuja ona mambo mengi ili wanajf tupate uwigo wote wa watu wanaobomoa uchumi wa tz.serikali isiishie hapo tu iingie ndani ya TRA ili hela zote ziwe accounted maana nina uhakika 20% bado zinazama ndani ya TRA yenyewe jamaa wote wako fit kinoma kiuchumi.
 
..................Waziri huyo alitoa mfano wa moja ya madhehebu lililoagiza mabati 4,000 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa likatumia mabati 200 tu na mengine mmoja wa viongozi wa kanisa hilo akaenda kuyauza kwa bei ya soko. Pia alitoa mfano wa madhehebu ya dini ambayo yaliagiza tani 5,000 za sukari kutoka Malawi kwa ajili ya kituo cha watoto yatima, lakini tani tano tu zilienda Singida kwenye kituo hicho na tani zingine zilizobaki zilikwenda Makambako na kufungwa kwenye mifuko na kuwauzia wananchi.

Katika kuelezea namna baadhi ya watu wanavyonufaika na misaada hiyo, alitoa mfano wa kiongozi mmoja wa kidini aliyeagiza magari kwa ajili ya kanisa lakini akayatumia magari hayo kwa kuanzisha kampuni ya kitalii (tour operator) kwa ajili ya kukodisha kibiashara. Alitoa mfano wa taasisi zisizokuwa za kiserikali (NGOs) kuwa kuna zinazotumiwa na wafanyabiashara kuagiza vifaa mbalimbali sio kwa ajili ya matumizi ya kijamii bali kibiashara...................

halafu tunasema kuwa eti tuna Waziri wa fedha!!..............na eti kwa majigambo ansema kuwa Wataalamu ndio wamemshauri hivyo......eti na hao ndio wataalamu washauri wa Waziri............yaani nachoka kabisa
 
mawaziri wa tanzania ni afueni hata wakanyamaza na wasijibu hoja! manake mkulo kazidi kulikoroga
hivi kwa kuwa watu wachache wanavunja sheria ndio wahukumiwe wote!
ukiwauliza hao walovunja sheria mliwachukulia hatua gani, hamna jibu
kwa namna hii tanzania haiwezi kuendelea hata kidogo
 
Mkulo kachemsha katika kujibu hoja. Madhehebu yote ya dini yamelalamikia tatizo hili la kuondolewa msamaha,cha ajabu ni kuwa kawashambulia wakristu.

Ndo maana siku zote nasema serikali ya kikwete imejaa udini zaidi na lengo ni kuwakomo wakristu walokwisha endelea. Mwisho wakristu wataacha kupiga kura wawaachie waislamu waendeshe nchi watakavyo.

JK angalia sana utaipeleka nchi pabaya.
 
Kama serikali iko makini hivi kupitisha uamuzi wa jumlajumla ( blanket decision) pale kosa linapotendeka, nadhani madhambi mengi yanayotendwa na watu mbalimbali ndani na nje ya serikali yangepungua kama siyo kuisha kabisa.Huwa najiuliza, serikali kwa mfano haijaona upotevu mkubwa wa rasilimali unaosababishwa na watendaji wabovu? Mbona hakuna hatua za haraka bali kuunda tume kila kukicha kufanya uchunguzi ambao hata matokeo yake ni vigumu kuyaona?
Anyway, siye yetu macho.
 
halafu tunasema kuwa eti tuna Waziri wa fedha!!..............na eti kwa majigambo ansema kuwa Wataalamu ndio wamemshauri hivyo......eti na hao ndio wataalamu washauri wa Waziri............yaani nachoka kabisa

Ogah ndugu yangu, ile ni takataka siyo waziri, Kuna mtu humu ndani alipendekeza aitwe ABUNWASI! nadhani alikuwa sahuhu kabisa. Yaani yeye waziri anawafahamu watu waotumia fursa ya misamaha ya kodi vibaya tena kwa ushahidi wa wazi then anashindwa kuchukua hatua!! kwanini?
Mimi naenda mbaali zaidi,.. naamini vita dhidi ya ufdisadi ndiyo iliyowaponza watu wa dini, ni katika kuwa tetea mafisadi serikali imeamua kukomoa kwamba hata hata watu wa dini wanaopiga vita ufisadi nao ni mafisadi!
Na ninaamini ushauri huu umetolewa na Rostam akishirikiana na mashoga zake pamoja na UWT.
 
kwanini wasi set affodable tax ambayo kila mtu ataweza lipa bila kukocomplain? wabunge, wafanyakazi wa serikali nao walipe kodi tu
 
wao wanakampenia udini zaidi.Huyu hana tofauti saaana na Megji katika kubwatuka bila kutumia akili.Naanza kupata wasiwasi na elimu yake huenda ni ya madrasa pekee.

Hawezi kunyambua mambo na kuangalia na wakati.Tusubiri mwakani atafanyiwa kama Megji. Kwanza hakuna mtu corrupt kama Mkulo. Fikiria alivyokuwa NSSF aliyoyafanya hadi akaombwa a resign. Sasa kaja kupewa fadhila kwa sababu za Vijiwe na udini pamoja na ndugu yake Mataka.

Tunaomba TAKUKURU wafuatilie record za huyu Mkulo waweke hadharani, Mtashangaa......!!!!!
 
hapa ndio viongozi wetu wanaposhangaza.kuna makampuni makubwa mengi wananjia zao za kukwepa kodi na serikali inajua, hao hawasumbuliwi.Lakini mtu wa chini wao ndio wanajiona kila siku ndio mzuri kwa kumbana inapokuja swala la kodi.


ukiziba mwanya mmoja kati ya mianya kumi,ni hatua moja katika kuelekea uzibaji wa mianya yote.
 
Ogah ndugu yangu, ile ni takataka siyo waziri, Kuna mtu humu ndani alipendekeza aitwe ABUNWASI! nadhani alikuwa sahuhu kabisa. Yaani yeye waziri anawafahamu watu waotumia fursa ya misamaha ya kodi vibaya tena kwa ushahidi wa wazi then anashindwa kuchukua hatua!! kwanini?
Mimi naenda mbaali zaidi,.. naamini vita dhidi ya ufdisadi ndiyo iliyowaponza watu wa dini, ni katika kuwa tetea mafisadi serikali imeamua kukomoa kwamba hata hata watu wa dini wanaopiga vita ufisadi nao ni mafisadi!
Na ninaamini ushauri huu umetolewa na Rostam akishirikiana na mashoga zake pamoja na UWT.
Mkuu unashangaa nini katika hilo? Muungwana mwenyewe alishasema anawafahamu wala rushwa kwa majina,alichukua hatua gani? Wauza unga anawafahamu,amechukua hatua gani? kule bandarini nako kasemaje? mbona kimya?
Hapa ni kuzugana tuu, Ukweli utendaji wa serikali yetu ni kama wa kiuenda wazimu hivi. Kwamba kumfahamu tuu mhalifu hata kama humchukulii hatua zozote basi umetimiza wajibu wako kama kiongozi na unayo haki ya kujisifu kwa utendaji huo.
Ila katika hili, wataucheza muziki wake.
 
Apa tusimlaumu Mkulo ni serikali nzima hasa tuanze na JK bse Mkulo ni chambo tuu.
Huwezi tatua tatizo kwa kulikimbia,kama watu walitumia mianya ya taasisi za dini kufanya mambo yao serikali imechukua hatua gani?
Si shangai maamuzi ya serikali yetu ndo yalivyo
 
swala la kodi ni lazima kwa kila taasisi iwe serikali, mashirika ya umma, makanisa,misikiti,NGO, Mashirika ya dini, viongozi wa serikali n.k tunalipa wananchi tulio na kipato cha chini halafu wenye vipato vikumbwa wanasamehewa.. wote tulipe kodi period!!! kama serikali inafahamu mashirika ambayo yalikiuka sheria za ulipaji au utozwaji kodi basi sheria na ichukue mkondo wake.

Ni kweli kodi ni lazima lakini nadhani mchango wa mashirika ya dini hasa kwenye sector ya afya na elimu hakuna mtanzania mwenye akili timamu anaweza kulipuuzia hili. Hii tabia ya serikali kugeneralize mambo ni aibu na inabidi iachwe mara moja. Kama kuna watu walikuwa wanaabuse walishindwa vipi kuwachukulia hatua? Kwanini kuwaadhibu mamilioni ya watu kwa sababu ya watu wachache tu? huu si uvivu wa kudeal na mambo? Halafu huyu mwandishi naye mnafiki eti "Apasua jipu" Mbona mimi sioni jipu hapa zaidi ya kurahisisha mambo kwa gharama ya watanzania maskini? Halafu cha ajabu hawakutaka mjadala kwenye hili ila misamaha ya kodi ya mafuta kwa makampuni ya madini wanataka mjadala? Hivi hii serikali ni ya wawekezaji au ya watanzania? Anyway ipo siku.
 
Huu ni ujinga mtupu. Ukwepaji wa kodi kwa baadhi ya mashirika ya dini ni jambo lililokuwa wazi, tena katika instance fulani wao mawaziri wamehusika sana kushirikiana nao.
Sasa leo ndio anajifanya amelielewa hili na kutaka kuwa victimize wote? kama anawajua waliokosea hatua hakuchukua kwa hiyo anakuja kushitaki kwetu ili sisi ndio tuwaadhibu?
Bla bla bla bla nyingine ya mawaziri kanjanja!
 
Ukiacha ishu ya misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini, suala kubwa zaidi ni 'incompetence' ya hali ya juu sana na usanii wa serikali katika kusimamia sheria na katika utekelezaji wa program zake za misamaha ya kodi. Hii ndo inapelekea watu kuona kodi kama "gharama isiyokua na manufaa yoyote na inapaswa kukwepwa kwa namna yoyote ile". Hii inapelekea 'tax compliance' kua chini mno.

Katika hali ya kawaida, kila mtu na taasisi inapaswa kulipa kodi ili serikali iweze kuondesha shughuli zake muhimu kwa jamii kama ujenzi wa miundombinu, upatikanaji wa nishati kwa bei nafuu, kuhakikisha wananchi na mali zao wapo salama, nk. Kama hizi huduma muhimu kwa wananchi zinakosekana, basi hata hiyo misamaha ya kodi inakua haina maana na haiwanufaishi walengwa kama inavyotarajiwa. Kuna maana gani kutoa msamaha wa kodi kwa taasisi za kidini kama hazipati umeme na barabara ni mbovu mpaka hazipitiki? Zitatoa huduma ya aina gani? Wangapi hapa wataenda kufungua biashara Somalia hata wakiahidiwa misamaha ya kodi?

Nchi zilizoendelea kila mtu analipa kodi. Kodi ni muhimu kwa maendeleo. Lakini muhimu zaidi ni serikali iliyo makini katika kuikusanya na kuitumia kwa manufaa ya wananchi wake wengi.
 
wao wanakampenia udini zaidi.Huyu hana tofauti saaana na Megji katika kubwatuka bila kutumia akili.Naanza kupata wasiwasi na elimu yake huenda ni ya madrasa pekee.

Hawezi kunyambua mambo na kuangalia na wakati.Tusubiri mwakani atafanyiwa kama Megji. Kwanza hakuna mtu corrupt kama Mkulo. Fikiria alivyokuwa NSSF aliyoyafanya hadi akaombwa a resign. Sasa kaja kupewa fadhila kwa sababu za Vijiwe na udini pamoja na ndugu yake Mataka.

Tunaomba TAKUKURU wafuatilie record za huyu Mkulo waweke hadharani, Mtashangaa......!!!!!


Huwezi kuona udini bila ya wewe kuwa mdini kwanza! Unadai Mkulo kapewa fadhila kwa sababu ya vijiwe vya udini, je Mattaka nae kapewa kwa "vijiwe" vya udini?

Acha kupanda mbegu ya udini kwa ku pick and choose
 
Back
Top Bottom