Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkandara,
Utadhani ulikuwepo kwenye fikra zangu. Kila kitu ulichosema ndicho nilichofikiria mimi.
Huwezi kubadilisha sheria just because a few individuals misused that law. Kuna vyombo vya sheria vya kuwakabili. Kwa nini havifanyi kazi yao?
Kama anavyosema Askofu Kilaini kama una utitiri wa taasisi za kidini na asasi za kiraia ambazo baadhi yao zinatumia vibaya misamaha ya kodi, basi serikali inayozisajili ndo izidhibiti, sasa sioni tena haja ya viongozi wa kidini na asasi za kirai kupiga makelele wakati serikali imeanza kuchukua hatua hizo, na msimamo wa seikali naona upo wazi katika maeneo ambayo yatafutiwa misamaha ya kodi.
..................Waziri huyo alitoa mfano wa moja ya madhehebu lililoagiza mabati 4,000 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa likatumia mabati 200 tu na mengine mmoja wa viongozi wa kanisa hilo akaenda kuyauza kwa bei ya soko. Pia alitoa mfano wa madhehebu ya dini ambayo yaliagiza tani 5,000 za sukari kutoka Malawi kwa ajili ya kituo cha watoto yatima, lakini tani tano tu zilienda Singida kwenye kituo hicho na tani zingine zilizobaki zilikwenda Makambako na kufungwa kwenye mifuko na kuwauzia wananchi.
Katika kuelezea namna baadhi ya watu wanavyonufaika na misaada hiyo, alitoa mfano wa kiongozi mmoja wa kidini aliyeagiza magari kwa ajili ya kanisa lakini akayatumia magari hayo kwa kuanzisha kampuni ya kitalii (tour operator) kwa ajili ya kukodisha kibiashara. Alitoa mfano wa taasisi zisizokuwa za kiserikali (NGOs) kuwa kuna zinazotumiwa na wafanyabiashara kuagiza vifaa mbalimbali sio kwa ajili ya matumizi ya kijamii bali kibiashara...................
halafu tunasema kuwa eti tuna Waziri wa fedha!!..............na eti kwa majigambo ansema kuwa Wataalamu ndio wamemshauri hivyo......eti na hao ndio wataalamu washauri wa Waziri............yaani nachoka kabisa
hapa ndio viongozi wetu wanaposhangaza.kuna makampuni makubwa mengi wananjia zao za kukwepa kodi na serikali inajua, hao hawasumbuliwi.Lakini mtu wa chini wao ndio wanajiona kila siku ndio mzuri kwa kumbana inapokuja swala la kodi.
Mkuu unashangaa nini katika hilo? Muungwana mwenyewe alishasema anawafahamu wala rushwa kwa majina,alichukua hatua gani? Wauza unga anawafahamu,amechukua hatua gani? kule bandarini nako kasemaje? mbona kimya?Ogah ndugu yangu, ile ni takataka siyo waziri, Kuna mtu humu ndani alipendekeza aitwe ABUNWASI! nadhani alikuwa sahuhu kabisa. Yaani yeye waziri anawafahamu watu waotumia fursa ya misamaha ya kodi vibaya tena kwa ushahidi wa wazi then anashindwa kuchukua hatua!! kwanini?
Mimi naenda mbaali zaidi,.. naamini vita dhidi ya ufdisadi ndiyo iliyowaponza watu wa dini, ni katika kuwa tetea mafisadi serikali imeamua kukomoa kwamba hata hata watu wa dini wanaopiga vita ufisadi nao ni mafisadi!
Na ninaamini ushauri huu umetolewa na Rostam akishirikiana na mashoga zake pamoja na UWT.
swala la kodi ni lazima kwa kila taasisi iwe serikali, mashirika ya umma, makanisa,misikiti,NGO, Mashirika ya dini, viongozi wa serikali n.k tunalipa wananchi tulio na kipato cha chini halafu wenye vipato vikumbwa wanasamehewa.. wote tulipe kodi period!!! kama serikali inafahamu mashirika ambayo yalikiuka sheria za ulipaji au utozwaji kodi basi sheria na ichukue mkondo wake.
wao wanakampenia udini zaidi.Huyu hana tofauti saaana na Megji katika kubwatuka bila kutumia akili.Naanza kupata wasiwasi na elimu yake huenda ni ya madrasa pekee.
Hawezi kunyambua mambo na kuangalia na wakati.Tusubiri mwakani atafanyiwa kama Megji. Kwanza hakuna mtu corrupt kama Mkulo. Fikiria alivyokuwa NSSF aliyoyafanya hadi akaombwa a resign. Sasa kaja kupewa fadhila kwa sababu za Vijiwe na udini pamoja na ndugu yake Mataka.
Tunaomba TAKUKURU wafuatilie record za huyu Mkulo waweke hadharani, Mtashangaa......!!!!!