MKURABITA! Historia za Kweli jinsi wadau(Tz) walivotoka kiuchumi. Ngombe 1 mpaka kumiliki Ranch!

lara 1

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2012
Posts
15,700
Reaction score
29,164
IGWEEEEEEEEEEEEEE

Ile vita yangu na mkakati wa kutokomeza umasikini wa fikra na mawazo mgando unaendelea! Leo tunaanza episode 1.

Bwana X (Amegoma nisimtaje jina) ni muajiriwa wa wizara ya Y, tangia mwaka 90 na kitu. Bwana X alihamishwa kikazi tokea huku Dsm kwenda kibaha picha ya ndege katikati ya miaka ya tisini. Asili yake ni Singida. Mkewe ni mwalimu. Wizarani ni mtu wa kati mwenye cheo cha ofisa.

Baada ya kufika kibaha picha ya ndege miaka hio ya 90, bwana X alinunua ngombe mmoja Frishian(Sijui kama nimepatia) jike na kuanza kumfuga ili apate kujikimu kiuchumi. Enzi za mkapa mambo yalikuwa tight si mchezo. Kama ujuavyo hizi ngombe za broiler zinazaliana sanaaa. Basi ngombe akazaa jike, na ndama akazaa jike, na yule mkubwa akazaa jike tena. Akawa ana ng'ombe 4, majirani wakaanza kupiga makelele kuhusu hygene.

Bwana X akaenda kibahaa ndani ndani huko akanunua heka 60 kipindi hiko ni miaka ya mwnzoni mwa 2000, aliuziwa heka 10,000 ilikuwa pesa mingi coz kibaha viwanja vilikuwa 70,000. Akahamishia ng'ombe zile kule na kuajiri watu toka singida wakae hukohuko coz majani yalikuwa rahisi pia kupata. Akaanza kufuga na kuku za kienyeji, bata na mbuzi.

Mpaka kufikia 2003 bwana X alikuwa anakamua lita 60 asubuhi na jioni kila siku. Akanunua na pickup ya kusambazia maziwa huku dar. Akanunua na generator ili maziwa yawe fresh mda wote. Bwana X alijituma kushika tenda za kusupply maziwa wizara nyingi sana na makampuni mengi tu, na sababu ya stability sio rahisi kumnyanganya tenda.

Hadi kufikia 2010 bwana X alikuwa na Ngombe zipatazo 100 na zaidi (Walizaa wengine alienda kuongezea Momela Morogoro walikuwa na best breed) za kisasa na anakamua si chini ya lita 300 asubuhi na 300 jioni. Pia ana supply mbuzi hapo machinjioni, bata na kuku wa kienyeji na mayai yake hoteli mbalimbali za kitaliii. Lita saivi inauzwa wastani wa 800. Piga mbesa yake kwa siku. Si chini ya 1mill/day as profits. Kazi gani utalipwa 1mill/day labda mkurugenzi wa nini sijui.

Kifupi bwana X ni millionea. Anamiliki karanch chake. Na faida aliyopata kubwa ni kusomesha wanae U.S.A bila stress yoyote kwa ufahari, Hoteli kadhaa, na mali kibao haipendezi mimi kuzianika hapa. Ni mambo binafsi ya mtu (Chezeya TRA nyie)

Sio kwamba kwake ilikuwa tambarare, noooo! Ali persvere na kujicommit kuhakikisha anafanikisha azma yake. Akavuka vkwazo na sasa anakula kuku kwa mrija.

Wakazi wa kibahaa picha ya ndege, maili moja hapo na jirani nazani mwamjua uzuri huyu mjasiria mali wenu.! Supplier mkubwa wa maziwa Na mnisaidie kuprove kuwa he made things happen na sijatunga.

So wale wa mikoani kazi kwenu.
 
nasubili wale waliobisha katika thread ya kuzungusha ela badala ya kujenga nyumba waje hapa...nitarudia tena kwa mwendo huu wa wadau kama wewe,sitoweza kufa maskini...napata elimu ya kufungua macho yangu kuona fursa mbalimbali kabla umri haujapigiwa kipenga....kiukweli tatzo letu watanzania especially vijana katika swala la kutafuta pesa hatujui,tunapenda showoff za masimu makubwa,magari ya mikopo na kupambalika na kubatalika kwa sana kumbe huku ndo unazidi kujichimbia kwenye shimo la umaskini,tufanye investment wabongo na umaskin tutausikia 2 kwenye majukwaa ya siasa lasivyo tutakwishaaa....

Over n out.
 

Na tunapenda kuonekana tuna pesa kuliko wenye pesa halisi.
Ongezea na signature yangu hapo chini!
 
Kupanga ni kuamua, lara 1 unaogopa kuweka mali nyingine kisa TRA huo ni ushahidi tosha kwamba kuna utapeli mwingi, dhuluma na ukandamizaji ulifanyika kulimbikiza hivyo alivyopata. Kuna watu wanapenda kuongelea mafanikio lakini ukweli unabakia kuwa markets nchini bila hujuma huwezi kuwa mega-enterpreneur. Kama mafanikio yanacost dhuluma na fitina lets stay in the middle class.
 
Last edited by a moderator:

ooh wamekuja hao..
 
Last edited by a moderator:
Agricultural products, na Income generated from Biological Assets hazina ushuru kwa Tanzania, Unless zimefanyiwa further processing. TRA hatuhusiki hapa.
 
Angalia shilling elfu kumi kama unayo hapo utaona signature yangu....

"Ukitafiti fursa za kiuchumi zilizopo ndani ya Tanzania, hautailaumu tena serikali bali utajilaumu wewe mwenyewe"

That's my signature and it's what i meant!
 
Reactions: LJJ
Agricultural products, na Income generated from Biological Assets hazina ushuru kwa Tanzania, Unless zimefanyiwa further processing. TRA hatuhusiki hapa.

nimefurahi sn mkuu kusema wazi manake hapa topic ingebadilika na kuwa ukwepaji kodi, kudanganyana na kutiana ujinga
 

Copy,
Tembelea mlimani city, na maeneo mbalimbali ya kumbi za starehe!
OVER
 
Bado sijakupata alaf nikishatembelea huko inakuwaje yaan..dadavua vizuri.

Roger,
Ukishatembelea ndio utaona vijana wengi tunavyojidanganya kwa anasa za muda mfupi na kujisahau kwamba kila hela tunayoipata sasa hivi tunatakiwa tu invest wisely.

Watu wameingia kwenye madeni yasiyo na ulazima kisa, kutaka kuonekana wapo kwenye chati hata kama uhalisia hauko hivyo matokeo yake topiki kama hizi zikija unakua na chuki binafsi na kuona kama haiwezekani kumbe ni kushindwa kutoa vipaumbele kwenye vipato na matumizi yetu.

Over
 

Usijidanganye kila mtu anajua siri ya jinsi alivyopata hela,hata sie uwa tunajidanganya mtaani kwamba bakharesa alianza kushona viatu magomeni,Siri anaijua mwenyewe na si lara 1 take it from me,matajiri wengi wanajua take-off yao ya jinsi walivyopata hela sie wa nje tunaona zile vibizna vyake lkn hauwezi jua labda kafukia sana miguu ya albino(Kova sorry sio uchochezi huu).
 
Last edited by a moderator:
lara 1 naona umeamua kumuunga mkono bwana ruge na kampeni yake ya twenzetu ili kutumia fursa kupitia mkurabita na mkukuta pia andaa mchakato ambayo sio mtambuka ili target zifike haraka
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…