MKURABITA!!!!!! Mchawi Wa Maendeleo Yako Ni Wewe Mwenyew ( Burning the bridge na Kuamua Kuwa Tajiri)

kweli kabisa uko sahihi lazima ujitoe unapofanya kitu chochote chenye gharama lazima ikugharimu
 

Hapo usiguse Lara,...maumivu yake usisimuliwe!
 
sijui kwa nini hii thread haijapata wachangiaji wa kutosha.
Bid up LARA
 
Lara1 naona siku hizi ushakuwa mjasilia mali
 
mm nilipomjua lara1 na mathread yake lizani ni lishangingi fulani hivi, sasa nilipoona ule uzi wake wa mwanzo episode 1, nikajiuliza kulikoni tena... sasa tena na tena nazidi kubadili kabs mtizamo wangu juu ya lara1.

hongera san lara1 na ubarikiwe na huu uzi
 
So inspirational lara 1. Ni kweli unayosema. Binafsi nimeanza kuona mafanikio ktk project yangu ya ku design logo na today I just got payed advance na client wangu yuko London. Na I have 2 projects na mteja wangu mwingine ambaye yuko Palestina. Ni kwa sababu nili burn the bridge. Nakesha nikifanya kazi na sina muda hata kidogo Wa kukaa maskani. Ukimuomba Mwenyezimungu kisha uka believe in yourself kisha ukafanya kazi kwa bidii utafanikiwa maana kazi ni ibada na Mola hamtupi Mja wake
 
Last edited by a moderator:
sijui kwa nini hii thread haijapata wachangiaji wa kutosha.
Bid up LARA
Maneno haya yanawachoma watu wengi, uchomaji wa madaraja ndo unafanya wasichangie sana mana bado hawana alternatives.

Zaidi ya reality hii nadhan tungeenda mbele na kuelezana alternatives. For instance nnapoamua kuchoma daraja, niipigane vipi vita hiyo. Labda pale wizara ya kilimo kuna fursa hii na hii, Pale wizara ya kazi na vijana kuna fursa hii na hii, pale sido may be kuna hili na hili, pale wanasupport vikundi or individuals etc.

Wapo wengine wasiojua hata pa kuanzia ingawa in the real sense wana wish kuchoma madaraja yao, wapo wengine ambao madaraja yao yalishaungua siku nyingi, yan wanasubiria tu adui afike kummaliza, coz hawana alternatives au hawajui wap pa kuanzia.

So tu my opinion, nadhan ipo haja ya kusaidiana kuainisha fursa mbalimbali ambazo zinatolewa na serikali au zilizopo ktk kufikia malengo. I know serikali yetu ina mipango mingi mizuri kuwezesha vijana kujikwamua. Na njia nyepesi katika kupata information hizo tembelea mabanda mbalimbali wakati wa 77, utajifunza mengi mengi sana ambayo yanaweza kukumotivate uchome daraja na kupambana.
 
Suala la kuchoma madaraja kama ulivyoliita ndilo linalowaumiza na kuwafanya wafe masikini baadhi ya watumishi wa kada fulani, mfano walimu wa shule za msingi na sekondari. Kuna kijanaamejikongoja akasoma masters, alipomaliza akarudi kwa mwajiri wake, basi ana mwaka wa tano sasa anaendelea kushika chaki kijijini. Analalamika eti hawa,pandishi cheo. Kwa hiyo yeye aliongeza elimu ili apate cheo. Pamoja na masters yake amekuwa mvivu wa kufikiri na mgumu wa kuvunja madaraja. Naamini angechukua maamuzi magumu sasa hivi angekuwa mbali sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…