Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
IGWEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!
Episode 3.
Historia ya Burning the bridge concept!!!!!!!!!!!!!!
Wakati wa vita kuu vya pili vya dunia, katika moja ya uwanja wa vita, jeshi la Manazi wa Kijerumani lilikuwa likipambana na jeshi lingine na wakawa wamezidiwa nguvu vibaya mno! Wakaanza kurudi nyuma baada ya kupewa cha mtemakuni! Kamanda wa Manazi wale wa Kijerumani akaona ishakuwa soo, sasa ikambidi afanye maamuzi magumu!
Ili warudi kijiji kinachofuata ilibidi wavuke daraja ambalo chini kuna mto mkbwa na mamba wengi! Sasa kama mjuavyo madaraja mengi miaka hio ya 40 yalikuwa ya mbao! Kamamnda wa Kinazi akafanya maamuzi magumu ya kuliwasha moto kwa bomu daraja! Kisha akatoa angalizo na muongozo.
Hakuna tena daraja wala hakuna jinsi yoyote ya kurudi nyuma zaidi, hapo kinachobidi ni either wapambane waende mbele ama wazembee waje wamalizwe na jeshi lingine wachukuliwe mateka au wajitose mtoni waliwe na mamba! There is only 1 way out! Either take the way or perish! Walipambana hadi wakashinda na kusonga mbele.
Sasa hata sisi wengi wetu kwenye maisha yetu kilicho katikati yetu na mafanikio yetu ni sisi wenyewe na woga wetu ama kurizika. Inatupasa kuburn madaraja yaliyo kati yetu na umasikini wetu na kuamua iwe isiwe siwezi kurudi nilikotoka au kubaki hapa nilipo!!!!!!!!! Period
Burning the bridge inahusisha Kufanya maamuzi magumu ya kudhubutu ama kujitosa mzimamzima bila kugeuka nyuma! Hapa ndipo ugumu ulipo! Na wengi hapa ndipo wanapoishia na ndoto kubakia ndoto bila kutekeleza. You realy need bigger balls here!
1.Upo kazini unasema nitaacha kazi nisimamie biashara kikamilifu ama nisimamie kampuni yangu kikamilifu. Nitaacha! Nitaacha! Mpaka unastaafu. Hukudhubutu kuburn the bridge!
2. Nitaanza mitihani ya bodi, nitaanza nitaanza! Mpaka unazeeka majukumu yanakuzidi ndo basi tena.
3. Nitaanzisha biashara, nitaanzisha nitaanzisha mpakaaaa!!!!!!!! Huanzi chochote!
Wengi wetu hapa ndo shughuli ilipo. Kama umekosa internal force ya kufanya kitu basi tafuta external force iwe kama push!!!!!!! Kama ni mitihani ya bodi funga macho kalipe ada! Trust me utapata tu appettite ya kusoma. Kama ni biashara piga simu kwa dalali akutafutie fremu, kama ni kampuni kaisajili. You have to start some where!
ITS EITHER NOW OR NEVER!!!!!!!!!! Jiulize mara ngapi umeahirisha!!!!!!! What makes you think kama hukuanza jana, kesho utaanza!!!!!!!!!!!
Remember
IN THIS LIFE WE GET FEW CHANCES AND IF YOU DONT GRAB THEM TIGHTLY BY THE BALLS YOU WILL END UP WONDERING HOW YOU BECAME SECOND RATED IN LIFE!!!!!!!!!!!!
Sasa the few chances are wearing down. School tick, Job tick, Good salary tick. Who knows how many chances are left?
Maneno haya yanawachoma watu wengi, uchomaji wa madaraja ndo unafanya wasichangie sana mana bado hawana alternatives.sijui kwa nini hii thread haijapata wachangiaji wa kutosha.
Bid up LARA