Mkurugenzi abanwa kwa kugoma kumlipia Makamu wa Rais malazi

Mkurugenzi abanwa kwa kugoma kumlipia Makamu wa Rais malazi

Maoni ya Celina Kombani kwenye Magazeti ya Tanzania leo kuhusu nani hasa wa kulaumiwa kwenye suala hili yanaonyesha dhahiri namna anavyokiri kwamba tunajua namna serikali yetu inavyoendeshwa. Hongera wana JF. Lakini baada ya kukiri asingeishia hapo. Kwani Katibu Mkuu Kiongozi Bw Luhanjoa hajaachia ngazi hadi leo. Huyu kwa mujibu Sheria ya utumishiwa Umma Na. 8 ya 2002 ndiye Mkuu wa Utumishi wa Umma na Katibu wa Baraza la Mawaziri. Na isitoshe masuala ya usalama na uendeshaji wa ofisi binafsi za viongozi wakuu wa nchi yetu yako chini yake. Haya yanatokea hataki hata kuwaomba radhi wananchi waliomchagua Rais (Makamu aligombea kwa tiketi moja na Rais wetu). Hivi leo kweli Kamati za Maadili alizounda zitamwadhibu nani ikiwa kama yeye mwenyewe na timu yake wanatenda dhambi kama hii halafu wanamlaumu DED. Kama hataadhibiwa kwa hili basi tuamini kuwa nchi yetu haiendeshwi kwa misingi ya utawala bora. Nashindwa kuelewa hivi makamu kafanyiwa hivi kwa sababu ni mkimya sana au kwa sababu ni Mzanzibari? Puuh!
 
Bluray,
Mkuu shukran sana kwa maelezo yenye mwanga na kina cha uhakika..
Kitu kimoja tu ambacho napenda unifahamu. naelewa sana sheria na taratibu zinazotakiwa ktk sifa za tawala zetu kimaandishi lakini kilichonipa shida mimi zaidi ni kuelewa taratibu zinazotumika ziku zote..
Ikiwa Kiwete anapotembelea wilaya hulipiwa na wilaya husika, ikiwa Makamu wa rais anapotembelea wilaya hulipiwa gharama hizo... Je, nini matokeo ya mfarakano huu! Kumbukeni tu nchi yetu inaongozwa kiholela, kuna mambo mengi sana nchini yanafanyika bila hata aibu, acha kutembelea wilaya hata huku Ulaya wanapokuja ni kutumbua tu, hakuna hata mtu mmoja mwenye fikra za maslahi ya Taifa. Utaonekana mjinga na mwenye wazimu kwani sheria ya nchi yetu iko mikononi mwa watu...
Hivyo swala zima ni lazima litazamwe kwa mapana yake...Fedha inaliwa vibaya sana tena pengine na baadhi ya watu ambao wamo humu humu JF wanapo kwenda mikoani..Swala sio nani analipa isipokuwa ufujaji wa mfuko wetu iwe bajeti ni ya wilaya au taifa bado ni fedha za wananchi..Hizo millioni kwa msafara wa siku moja umekataliwa na mkurugenzi huyu lakini ukweli ni kwamba bado zitalipwa from somewhere..Ukiacha kutoa fedha mfuko wa nyuma ukatoa toka mfuko wa mbele au ktk shati lako bado maumivu ya matumizi mabaya ni yale yale...Ndizo guards nazotaka tuziweke..
 

Nashindwa kuelewa hivi makamu kafanyiwa hivi kwa sababu ni mkimya sana au kwa sababu ni Mzanzibari? Puuh!

"Makamu kafanyiwa hivi," kafanyiwa na nani?

Yeye VP Shein ndio kawafanyia wenzake vibaya. Yeye ndio alitakiwa kulipa. Waziri wa TAMISEMI, ofisi ya Waziri Mkuu, kasema: "Ndiyo maana rais anapokuwa kwenye ziara huenda na vyakula vyake," alisema Kombani.

Kwa hiyo, ni Shein mwenyewe ndio kala, kalala, na msafara wake, wamekunywa, wamekula, labda wakafungiwa na kufungiwa take-out, wakaondoka bila kulipa.

Halafu hii inakuonyesha kwamba, Mkuu wa Wilaya hajui taratibu za matumizi ya pesa, Makamu wa Rais hajui taratibu za fedha, au anajua lakini hajali (si ziara yake ya kwanza hii). Yeye huwa anakwenda tu sehemu na misafara mirefu, analala, anahutubia, anakula, anaondoka, hajui, hajali, haimuhusu, nani atalipa. Mpaka Waziri anakupa ujumbe hadharani, Makamu wa Rais beba chakula chako? Shame on Shein.
 
SAKATA la halmashauri ya Karatu, kugomea kulipia malazi ya Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein na ujumbe wake limechukuwa sura mpya baada ya aliyekuwa kaimu mkurugenzi wakati wa ziara hiyo, Majid Myao kutakiwa kutoa maelezo.


Myao aliitwa na mkuu wa wilaya ya Karatu, Mathew Sedoyeka hivi karibuni ili akatoe maelezo juu ya suala hilo hasa kutokana na halmashauri hiyo kugoma kulipa kiasi cha Sh2milioni ambazo ni malipo ya kulala siku moja na chakula kwa ujumbe huo, katika hoteli ya Bougain Villea ya mjini Karatu.


Kwa mujibu wa maelezo ya maandishi ya Myao, yaliyopo katika barua yake ya Machi 3, 2009 yenye kumbukumbu namba kdc/ded/cv.3/1/121, Myao amejitetea kuwa uamuzi wa kutolipiwa ziara hiyo, umetokana kamati ya fedha ya madiwani kukataa kuidhinisha fedha hizo.


Alisema kutokana na kutoidhinishwa malipo hayo, aliona angekiuka sheria namba tisa ya mwaka 1982 ambayo inahusu masuala ya matumizi ya fedha za halmashauri na maamuzi ya kamati ya fedha.


“Kama mimi ningetoa malipo hayo ni wazi ningekiuka sheria za serikali za mitaa hasa ikizingatiwa madiwani katika kikao chao halali ndio waligomea,”alieleza Myao.


Akizungumzia sakata hilo, mbunge wa jimbo la Karatu, Dk Wilbroad Slaa alisema ni halali kwani walikuwa hawana bajeti ya malipo hayo na aliomba mtendaji yoyote wa halmashauri hiyo asiwajibishwe kwa suala hilo.

Source:Mwananchi


Pongezi madiwani wa Karatu kwa kukataa matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.Hizi ziara za Viongozi wa kitaifa zinapaswa kutengewa bajeti na ofisi zao na si kutumia fedha za halmashauri kwa ziara za viongozi wa kitaifa.

Jamani ninavyoelewa safari za makamu na viongozi wa serikali kuu zinagaramiwa na serikali kuu, kwani makamu alialikwa na halmashauri ya karatu? Hivi Tanzania tuna viongozi au ndo maana hata wenye ubongo wana hamia kwenye SIHASA(SIASA).
 
Back
Top Bottom