Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kampuni kubwa za Kichina zinazojihusisha na uzalishaji wa saruji zimeibuka kuwa tishio kubwa kwa wazalishaji wa ndani katika Afrika Mashariki. Kwa kutumia mitaji mikubwa na mbinu za ushindani wa bei, kampuni hizo zinaelezwa kupunguza nafasi ya kampuni za ndani kukua na kuhimili ushindani, Ameeleza Mkurugenzi Mtendaji wa Amsons Group, Edha Nahdi.
Kwa mujibu wa Edha Nahdi, amesema kampuni yake inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa makampuni makubwa ya Kichina. Kampuni hizo zina mitaji mikubwa na uwezo wa kuwekeza kwa kiwango kikubwa, jambo linalofanya iwe vigumu kwa wazalishaji wa ndani kushindana.
Katika jitihada za kupanua biashara, ameeleza kuwa Amsons Group ilihusika katika ununuzi wa Bamburi Cement ya Kenya kwa gharama ya TZS bilioni 500 ($182 milioni). Ingawa walifanikiwa kupata hisa hizo, mchakato huo ulikuwa na ushindani mkali kutoka kwa kampuni za Kichina ambazo zilionyesha nia ya kununua Bamburi ili kuendelea kutawala soko la saruji Afrika Mashariki.
“Kampuni za Kichina zina uwezo wa kushusha bei ya bidhaa kwa muda mrefu ili kuwatoa wazalishaji wa ndani sokoni,” ameeleza Nahdi akiongeza kuwa kwa kampuni za China, uwekezaji wa mamia ya mabilioni ya shilingi ni kama "pesa ya kuchezea" (Mickey Mouse money), hivyo wanapata faida hata kwa kutumia mbinu za bei za chini ili kutawala soko.
Mbali na Kenya, Amsons pia inapanua uwekezaji wake Tanzania kwa kufungua viwanda viwili vipya vya saruji ili kukabiliana na ushindani huo. Kampuni hiyo pia imewekeza zaidi ya TZS bilioni 812 ($320 milioni) kuboresha uzalishaji wa klinka katika kiwanda cha Bamburi kilichopo Mombasa, ili kuongeza uwezo wa uzalishaji na kupunguza utegemezi wa malighafi kutoka nje.
Aidha, amesema Uganda pia imekuwa uwanja wa ushindani mkali kati ya kampuni za ndani na wawekezaji wa kigeni. Mnamo Machi 2024, Bamburi Cement iliuza hisa zake 70% katika Hima Cement kwa Sarrai Group na Rwimi Holding kwa TZS 214 bilioni ($84 milioni). Amsons inafuatilia kwa karibu soko la Uganda kwa lengo la kufanya uwekezaji wa muda mrefu.
Nahdi anasema kuwa, ili wazalishaji wa ndani waweze kushindana na kampuni za Kichina, kunahitajika ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali. Pia, kampuni za ndani zinapaswa kuungana na kuwekeza kwa pamoja badala ya kushindana, ili kuimarisha uthabiti wao sokoni.