LGE2024 Mkurugenzi, Dionis Myinga afafanua ushindi wa Wilfred Ritte (CHADEMA) licha ya kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha Uchaguzi wa Uenyekiti wa Kijiji

LGE2024 Mkurugenzi, Dionis Myinga afafanua ushindi wa Wilfred Ritte (CHADEMA) licha ya kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha Uchaguzi wa Uenyekiti wa Kijiji

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Dionis Myinga ambaye pia ndiye aliyekuwa Msimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa wilayani humo amesema kuwa aliyekuwa Mgombea wa Uenyekiti wa kijiji cha Usari kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo @chadematzofficial Wilfred Ritte alishiriki kugombea na kushinda kihalali katika uchaguzi huo.

Myinga ameeleza hayo kutokana na kusambaa kwa taarifa mitandaoni zikidai kuwa mgombea huyo ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa kijiji hakushiriki kugombea kihalali na kwamba imekuwaje ameshinda kutokana na kuwekewa pingamizi.

Msimamizi huyo amesema kuwa baada ya Mgombea huyo kwa tiketi ya CHADEMA kuwekewa pingamizi alikata rufaa ambayo alishinda na kuruhusiwa kwa mujibu wa sheria kugombea.

Jambo TV imezungumza na Katibu wa CHADEMA wilaya ya Hai, Joseph Ntele kama chama hicho kina mtambua Mwenyekiti huyo ambapo amesema kuwa, "Mchakato wa uchaguzi Jimbo la Hai ulinajisiwa na kuhusu Mwenyekiti huyo kuwa na baraka za Chama au kutokuwa nazo ni suala ambalo ni lakuketi kama Kamati tendaji ya Chama na kisha tutatoa msimamo wetu."
 
Back
Top Bottom