Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Baada ya Mdau wa JamiiForum.com kueleza kuwa hadi leo Januari 21, 2025, Wakazi wa maeneo ya Isyesye hapa Jijini Mbeya hawajapata maji kwa wiki moja, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya (MBEYA UWSA) imefafanua kuwa kuna mgawo na pia uzalishaji haukidhi mahitaji ya Mkoa.
Kusoma hoja bofya hapa ~ Uongozi wa Mkoa wa Mbeya unaendelea kudhibiti Kipindupindu lakini Wakazi wa Isyesye hatuna Huduma ya Maji kwa wiki sasa, hii inarudisha nyuma juhudi
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya (MBEYA UWSA), CPA.Gilbert Kayange anasema:
Uwezo wetu wa kuzalisha maji haujakidhi mahitaji ya Wananchi ambapo kwa sasa tunahudumia kwa kutoka asilimia 58 kwa siku, kunapokuwa na uwezo mdogo maana yake lazima kutakuwa na mgawo wa maji.
Kuna maeneo yanaweza kuwa na mgawo mkali na wengine wa kawaida, ndio maana kuna Mradi wa Mto Kiwira unaotarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja na nusu, ukikamilika utasaidia sana kuondoa adha hiyo ya uhaba wa maji.
Mradi huo pia ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha maji Lita takribani Milioni 117 kwa siku, hivyo utakidhi mahitaji kwa kuwa ukijumlisha na huu uzalishaji uliopo sasa hivi inamaanisha tutakuwa na uwezo wa kuzalisha maji na kuhudumia kwa Wananchi wa Mbeya kwa zaidi ya miaka 20 ijayo.
Changamoto nyingine ni kuwa kuna wakati tunaweza kuwa na breakdown ya mitambo, inapotokea hivyo inaweza kuathiri huduma ya maji kwa baadhi ya Watu.
Hata sasa kuna changamoto ya Mitambo kuunguzwa na umeme, tangu juzi mafundi wetu wanapambana ili uzalishaji urejee.
Hilo eneo la Isyesye wanapolalamikia kukosa maji, miaka mitatu iliyopita hali ilikuwa mbaya zaidi, leo hii wanasema siku kadhaa hawana maji, lakini wakati huo ilikuwa kawaida kwao kukosa maji kwa miezi kadhaa.
Kilichosaidia hadi huduma zikawafikia ni mradi uliokamilika na kugharimu Tsh. Milioni 950, ulipunguza ukali wa kukosa huduma za maji na ndio maana sasa hivi ikitokea wamekosa basi inakuwa ni kwa siku kadhaa.